slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Friday, March 31, 2017

PUBLIC NOTICE FOR GRADING OF ACCOMMODATION FACILITIES IN ARUSHA AND MANYARA REGIONS (PHASE I)

The United Republic of Tanzania
MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM
NOTICE FOR GRADING OF ACCOMMODATION FACILITIES IN ARUSHA AND MANYARA REGIONS (PHASE I)
All owners and operators of accommodation facilities in Arusha and Manyara Regions are hereby notified that the Ministry of Natural Resources and Tourism shall conduct Grading task of all registered accommodation facilities in Arusha and Manyara Regions. To this effect, the Ministry gives thirty (30) days notice, from the date of issuance of this notice, for the owners and operators of accommodation facilities in Arusha and Manyara Regions to make the necessary preparations for a smooth and efficient run of the ensuing task.

TO ACCESS the Criteria for Grading and the list for essential items as documents to be used during assessment CLICK HERE

This notice is given in consideration of Sections 10 (1), (3), 17, 53 (1) (b) and (c), 46 (1) (a) and (f) of the Tourism Act, No. 29 of 2008; and Regulation 5 of the Tourism (Fees and Charges) of 2015 (GN.267).

Issued by:
PERMANENT SECRETARY
MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM
MPINGO HOUSE – 40 JULIUS NYERERE ROAD
15472 – DAR ES SALAAM
TEL: +255 22 2864271/ 2864230


ISSUED ON 31st MARCH, 2017

Thursday, March 30, 2017

WIZARA YA MALIASILI KWA KUSHIRIKIANA NA MRADI WA SPENEST YAENDESHA MAFUNZO YA UTALII NA UKARIMU, SERIKALI YAANDAA KANUNI KUVIBANA VYUO VYA UTALII KUTOA HUDUMA BORA

Image may contain: 3 people, people standing, people sitting and indoor
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (wa pili kulia) akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu kwa watoa huduma za Utalii na Ukarimu Mkoani humo ambayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Mradi wa SPANEST. 
Image may contain: 3 people, people sitting and people standing
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii wa Wizara ya Maliasili, Paskasi Mwiru (wapili kushoto) akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza kufunga mafunzo hayo. 

Picha ya pamoja.

................................................................

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa kanuni ambayo itavibana vyuo vinavyofundisha utalii na ukarimu ili viweze kuzalisha wataalamu wenye ubora.

Kanuni hiyo itasaidia kuthibiti utitiri wa vyuo vilivyoanzishwa nchini huku vikiwa vimejikita kupata faida wakati wahitimu wanaozalishwa kupitia vyuo hivyo wakiwa ni wa viwango vya chini.


Kufuatia hali hiyo hata wataalamu watakaozalishwa kupitia vyuo hivyo watasimamiwa lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa kwa watalii zinakidhi viwango vinavyokubalika.


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza aliyasema hayo jana mjini Iringa wakati akifunga mafunzo ya ukarimu na utalii yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu kwa wahudumu wa hoteli na migahawa kwa kuratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Mradi wa SPANEST.

‘’Wale wamiliki wa hoteli wenye tabia ya kuajiri ndugu zao wasio kuwa na ujuzi wowote huu ndo utakuwa mwisho wao,kama kuna yeyote anayetaka kufanya kazi katika tasnia hii ni lazima aende shule’’. Alisisitiza Masenza.

Akitaja sababu ya Nyanda za juu kusini kutembelewa na watalii wachache licha ya kuwa na vivutio lukuki, alisema wahudumu nao wamekuwa kikwazo kwani baadhi yao hawana elimu kabisa.

Akitoa takwimu za mwaka 2015, Mkuu wa Mkoa alisema ni asilimia nne tu ya watalii 764,837 toka nje ya nchi na asilimia nane tu ya watalii 641, 114 wa ndani waliotembelea vivutio vya mikoa ya kusini huku idadi kubwa iliyobaki wakitembelea vya kaskazini.

Awali, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii wa Wizara ya Maliasili, Paskasi Mwiru alisema serikali imeamua kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watoa huduma baada ya kubaini baadhi ya vyuo vinavyotoa mafunzo ya ukarimu na utalii nchini, vinayatoa chini ya kiwango.

Kwa kupitia mafunzo hayo, alisema watoa huduma wanapewa mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji wa huduma ya chakula na vinywaji, upishi na namna ya kukuza huduma ya malazi ili kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa katika sekta ya ukarimu na utalii katika mikoa ya kusini ambayo ipo chini.

Kwa kupitia mafunzo hayo, jumla ya wahitimu 80 kati ya zaidi ya 100 waliojitokeza wamefanikiwa kuhitimu na kutunukiwa vyeti walivyokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Mradi wa SPANEST umechangia zaidi ya asilimia 75 ya gharama zote za kuendesha mafunzo hayo lengo likiwa ni kushirikiana na Serikali katika kukuza na kuendeleza utalii katika Kanda ya Kusin.

Thursday, March 2, 2017

TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA WANYAMAPORI DUNIANI LEO

MTI MREFU ZAIDI BARANI AFRIKA WAGUNDULIKA KATIKA HIFADHI YA MLIMA KILIMANJARO

Mti mrefu Afrika wagunduliwa katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania
Wanasayansi wanasema kuwa wamegundua kile wanachoamini kuwa ni mti mrefu zaidi barani Afrika. Mti huo uko bonde moja lililo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika eneo la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Wanasayansi kutoka chuo cha Bayreuth nchini Ujerumani, wanasema wanaamini kuwa mti huo unaopatikana karibu na mlima Kilimanjaro ndio mrefu zaidi barani Afrika.
Mmoja wa wanasayansi hao alisema kuwa aliona mtu huo miaka 20 iliyopita, lakini ni hadi hivi majuzi wakitumia vifaa maalum walifaulu kupima urefu wake.
Mti huo kutoka familia ya 'Entandrophragma excelsum' una urefu wa mita 81.
Wanasayansi nchini Tanzania bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu ugunduzi huo.
Wanasayansi waliogundua mti huo sasa wanataka ujumuishwe kwenye kumbukumbu ya miti isiyo ya kawaida duniani. (SOURCE: BBC SWAHILI)

Wednesday, March 1, 2017

USAFIRISHAJI MKAA WILAYA MOJA HADI NYINGINE WAPIGWA MARUFUKU

Image may contain: one or more people, sky and outdoor
SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imepiga marufuku kusafirisha mkaa kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine, kwa lengo la kukabiliana na tatizo kubwa la ukataji wa miti unaendelea hali inayochangia kukosekana kwa mvua katika maeneo mengi nchini.
Waziri wa wizara hiyo, Profesa Jumanne Maghembe amewaagiza maofisa misitu wa wilaya zote nchini, wasitoe vibali vinavyoruhusu mkaa kusafirishwa kutoka nje za wilaya zao na pia wakamate mfanyabiashara yoyote yule atakayethubutu kusafirisha mkaa kwenda wilaya nyingine.
Akizungumza jana katika siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 110 ya Vita vya Maji Maji na uzinduzi wa Makumbusho ya hayati Rashidi Kawawa, yaliyofanyika wilayani Songea mkoani Ruvuma, Profesa Maghembe alisema mkaa utakaozalishwa katika wilaya utumike ndani ya wilaya hiyo hiyo hakuna kusafirishwa kwenda nje.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara yake kwa vyombo vya habari, Profesa Maghembe alisema kutokana na matumizi makubwa ya mkaa ndani na nje ya nchi, akitolea mfano Mkoa wa Tanga ambako mkaa wake umekuwa ukisafirishwa Zanzibar na hatimaye kupelekwa nchi za Uarabuni, ambako kumekuwa na soko kubwa la mkaa kutoka Tanzania, umechangia idadi kubwa ya miti kukatwa kutokana na hali hiyo athari zimeanza kujitokeza katika mikoa ya kaskazini.
“Kama serikali hatuwezi kukaa kimya huku tukiacha hali hii ikiendelea, ni lazima tuchukue hatua madhara ya kutopata mvua ya kutosha yanayotokea kwa sasa katika mikoa hiyo na baadhi ya maeneo ya mengi nchini yanasababishwa na miti mingi kukatwa bila kufuata utaratibu,” alibainisha Profesa Maghembe.
Aidha, alisema licha ya biashara hiyo ya uuzaji mkaa kufanywa ndani na nje ya nchi, watu wanaojihusisha na uchomaji wa mkaa wamezidi kuwa watu maskini kwa vile wafanyabiashara wamekuwa wakiwalangua kwa bei ndogo huku wao wakiuuza kwa bei kubwa sokoni halafu wahusika wakizidi kutumbukia kwenye hali umaskini na ndio waathirika wakubwa ukame na pale mvua inapokuwa hainyeshi.
Miongoni mwa mikoa ambayo itaathirika na uamuzi huo wa serikali ni Jiji la Dar es Salaam, ambalo limekuwa likitegemea mkaa kutoka nje ya mkoa huo.
Nchini Tanzania zaidi ya ekari 370,000 za misitu huharibiwa kila mwaka, kiwango kikubwa kwa matumizi ya nishati, kwa mujibu wa Wakala wa Misitu yenye mamlaka ya kuangalia matumizi mbalimbali ya misitu.
Mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam inaongoza kwa matumizi ya mkaa kama chanzo kikuu cha nishati kwa matumizi ya majumbani, huku Mkoa wa Simiyu ukiwa na idadi ndogo zaidi ya matumizi ya nishati hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya mgawanyo wa kijamii na kiuchumi iliyotolewa mwaka jana na Ofisi ya Takwimu Nchini (NBS), Dar es Salaam ndiyo inayoongoza kwa matumizi ya mkaa, japokuwa mkoa huu una vyanzo mbalimbali ambavyo ni rafiki wa mazingira.
Matumizi makubwa ya mkaa katika mikoa hiyo, umesababisha kichocheo cha ukataji wa miti katika mikoa mingine na inakadiriwa kuwa karibu hekta 300,000 hadi 400,000 za misitu ya asili huharibiwa kila mwaka kutokana na utengenezaji mkaa.
Ripoti hiyo iliyochapishwa na NBS imeonesha kwamba zaidi ya asilimia 73 (familia nane kati ya 10) wanatumia mkaa kama chanzo cha nishati kwa ajili ya kupikia.
Katika hatua nyingine, Profesa Maghembe ameiomba Serikali ya Ujerumani irudishe kichwa cha aliyekuwa Kaimu Nduna, Songea Mbano aliyenyongwa na kisha kukatwa kichwa katika vita vya Majimaji na baadaye kuzikwa kwenye kaburi la pekee yake katika eneo ambalo mashujaa wenzake wapatao 66 walinyonyongwa na kuzikwa katika kaburi moja.
Amemwambia Balozi wa Ujerumani, Egon Kochanke katika maadhimisho hayo kuwa ni muda muafaka sasa kukirudisha kichwa hicho kwa kuwa shujaa huyo hakuwa raia wa Ujerumani alikuwa Mwafrika hivyo ni vyema kichwa chake kikarudishwa katika ardhi yake.
Awali, wakati akizindua nyumba ya Makumbusho ya Rashidi Mfaume Kawawa (Simba wa Vita), aliishukuru familia yake kwa kukubali kukabidhi nyumba ya Bombambili Songea kwa Wizara ya Maliasili na Utalii itakayotumika kuhifadhi historia ya maisha yake, kumbukumbu za kazi na mchango wake katika kulitumikia Taifa.
Pia aliwataka Watanzania kumuenzi Mzee Kawawa kwa kuwa maisha yake yote aliyatoa kwa kuwatumikia Watanzania bila kujali itikadi zozote.