Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania Bara na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Zanzibar zimeweka mkakati wa pamoja wa kuimarisha ushirikiano wa usimamizi wa maliasili, malikale na kuendeleza utalii kwa maslahi ya pande zote za Muungano.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi baada ya mkutano wa pamoja wa wizara hizo uliofanyika hivi karibuni katika Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo wa siku moja uliongozwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Joseph Meza.
Akifungua Mkutano huo wa siku moja, Maj. Gen. Milanzi alisema pamoja na Wizara hizo kutokuwa za muungano imekuepo haja kubwa ya kukutana kwa ajili kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha sekta ya maliasili na utalii na kukabiliana na changamoto zinazogusa sekta hiyo katika Muungano.
"Tumejadiliana kuona ni namna gani tunaweza kushirikiana kwenye masuala mbalimbali ya biashara ya mazao ya misitu, biashara ya Wanyamapori inayohusiana na mikataba ya CITES na mikataba mingine ya ndani na ya Kimataifa.
"Tumekubaliana pia kuhuisha sheria zinazokinzana katika usimamizi wa sekta tunazozisimamia ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza katika utekekezaji na hivyo kuathiri Muungano wetu," alisema Maj. Gen. Milanzi.
Alisema katika mkutano huo wa siku moja wataalamu kutoka pande zote za Muungano waliagizwa kuwasilisha mapendekezo ya namna bora ya kuendesha biashara ya mazao ya misitu na kupendekeza utaratibu wa kufanya biashara kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zilizopo.
Alisema kupitia mkutano huo Wizara hizo zimeunda kamati maalum ya kuratibu utekelezaji wa maazimio ya pamoja ya kuimarisha usimamizi bora wa sekta hizo na utatuzi wa changamoto zilizopo kwa kuandaa mapendekezo ya kimkakati ya muda mfupi na mrefu.
"Kamati hiyo itaongozwa na Afisa Mipango Mkuu Msaidizi kutoka Idara ya Misitu na Maliasili Zisizorejesheka (DFNR), Saleh Kombo Khiari na Mchumi kutoka Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Maliasili na Utalii, Mugure Wambura," alisema Milanzi.
Mbali na hayo alisema kutakuwepo na vikao mbalimbali vya kuimarisha Muungano kupitia Wizara hizo katika ngazi ya wataalamu, Makatibu Wakuu na Mawaziri ambapo kikao kingine kinatarajiwa kufanyika kabla ya tarehe 30 Machi, 2018.
Serikali italipa fidia na vifuta jasho kwa vitongoji ambavyo
vipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Pori la Akiba Mkungunero ili
viweze kupisha maeneo hayo yaendelee kuhifadhiwa kwa mujibu wa sheria.
Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.
Hamisi Kigwangalla katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha
Kimotorok katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ambao ulihudhuriwa pia na
Wakuu wa Wilaya za Simanjiro, Kiteto na Kondoa.
Alisema fidia hiyo italipwa kwa vitongoji viwili vya kijiji cha
Irkishbo vya Maasasi na Lumbenek vilivyopo katika Wilaya ya Kiteto mkoani
Manyara ambavyo vilikutwa ndani ya Pori la Akiba Mkungunero wakati pori hilo
linaanzishwa mwaka 1996 kwa Tangazo la Serikali Na. 307.
"Tutafanya tathmini, tutawaomba wananchi mshirikiane na
Serikali ili muweze kulipwa fidia mpelekwe maeneo mengine, jukumu letu sisi ni
kugharamia zoezi la tathmini na kulipwa fidia ili muweze kuondoka katika maeneo
haya ya hifadhi," alisema Dk. Kigwangalla.
Alisema kwa upande wa baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kimotorok
ambao wameanzisha makazi kimakosa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na
Pori la Akiba Mkungunero hawatalipwa fidia na badala yake watafanyiwa tathmini
na kulipwa kifuta jasho na kupelekwa maeneo mengine.
"Kimsingi ukimkuta mtu yupo katika eneo lako hupaswi kulipa
fidia, hapa tumekuwa waungwana na kutumia roho ya kibinadamu, vinginevyo
tungeweza kusema leo hapa tusione mtu na tungevunja kwa sababu ni eneo halali
la hifadhi na hairuhusiwi kwa mujibu wa sheria mtu kuishi ndani ya hifadhi.
"Kwa sasa hatutatumia nguvu, lakini tukikamilisha zoezi la
tathmini tukalipa watu fidia yao, tutatoa muda maalum wa watu kuondoka na watu
watapaswa kuondoka, ilimradi tutajiridhisha kwamba tulimtendea haki kila
mwananchi anayeishi katika eneo hili," alisema Dk. Kigwangalla.
Akizungumzia moja ya zahanati iliyojengwa ndani ya kitongoji
hicho cha Kimotorok ambayo nayo itabomolewa baada ya zoezi la kulipa vifuta
jasho, aliiagiza TANAPA kujenga zahanati nyingine katika eneo jipya
litakalopangwa Halmashauri husika kwa ajili ya wananchi hao kuhamia.
Alisema zoezi la tathmini pamoja na wananchi kulipwa fidia na
vifuta jasho linatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi tisa ijayo
kuanzia mwezi Machi, 2018.
Akizungumzia hatma ya makazi mapya kwa wananchi watakaondolewa
kwenye maeneo hayo ya hifadhi, Dk. Kigwangalla ameziagiza Halmashauri husika za
Kiteto, Kondoa na Simanjiro kupanga maeneo mengine mbadala ya kuwahamishia
wananchi hao punde baada ya kulipwa fidia zao.
Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za
Taifa linalosimamia Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori inayosimamia Pori la Akiba Mkungunero kusaidia jamii jirani na
maeneo hayo ya hifadhi kwa kuweka mpango bora wa matumizi ya ardhi, kuendeleza
eneo la malisho na kuchimba mabwawa ya maji ya kunywesha mifugo ili kujenga
misingi ya urafiki na ujirani mwema.
Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla amefuta mipaka ya Jumuiya
ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makame ambayo imeingia kimakosa ndani ya Pori la
Akiba Mkungunero na kumuagiza Meneja wa Pori hilo, Emmanuel Bilaso kuweka
ulinzi mkali katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula alisema
watasimamia utekelezaji wa maagizo hayo ya Serikali ili kuhakikisha mgogoro huo
wa muda mrefu unapatiwa ufumbuzi.
Katika ziara hiyo ya siku moja Mkoani Manyara, Waziri
Kigwangalla alitembelea na kukagua eneo la Ranchi ya Manyara ambayo pia ni
sehemu ya mapito ya wanyamapori, eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya Burunge, Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Pori la Akiba
Mkungunero ambapo alitoa maelekezo mbalimbali ya kuboresha maeneo hayo.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya
Taifa ya Tarangire, Herman Batiho kukakua maeneo hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua changamoto
za uhifadhi mkoani Manyara.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire
na viongozi wa hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua
changamoto za uhifadhi mkoani Manyara jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Herman Batiho kukakua maeneo ya mapito ya wanayamapori na mipaka ya hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua changamoto za uhifadhi mkoani Manyara jana.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana Mkuu wa Wilaya ya Kondoa,
Sezaria Makuta wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua changamoto za
uhifadhi katika Kijiji cha Kimotorok mkoani Manyara jana. Wanaoshuhudia kushoto
Mkuu wa wilaya ya
Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magesa.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na viongozi wa TANAPA alipotembelea
Hifadhi ya Taifa ya Ausha jana na kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi
hususan maeneo yenye migogoro kwa lengo la kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua mazingira ya Hifadhi ya Taifa ya
Arusha alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali
za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa lengo la kuyatafutia ufumbuzi wa
kudumu. Katikati ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa
TANAPA, Martin Loibooki na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga (kulia).
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia moja ya eneo lenye mgogoro ndani
ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha alipotembelea hifadhi hiyo jana na kukagua
shughuli mbalimbali za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuyatafutia
ufumbuzi wa kudumu. Katikati ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za
Taifa TANAPA, Martin Loibooki na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga (kulia).
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkurugenzi wa Uhifadhi wa
Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA, Martin Loibooki alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha jana na
kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi
hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Kulia
ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga.
Picha ya pamoja Waziri Kigwangalla na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA.
Waziri wa Malisili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA, Martin Loibooki kuhusu Kreta ya Hifadhi ya Ziwa Manyara muda mfupi kabla ya kuhitimisha ziara yake katika hifadhi hiyo jana jioni. (Picha na Hamza Temba-WMU)
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameuagiza uongozi wa Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania TFS kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo
la chanzo cha maji ya mto zigi kilichopo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia
Amani kwa ajili ya kulinda chanzo hicho.
Dk.
Kigwangalla ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea eneo la chanzo hicho na
kukuta uharibifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuchimba
madini ya dhahabu katika eneo hilo la hifadhi kinyume cha sheria
"Nimeagiza
watu wa TFS wajenge kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hili, na waweke
walinzi wetu wa kudumu hapa badala ya kutegemea kufanya patrol (doria) na kuondoka,
kwasababu eneo hili wananchi wanaamini lina madini ya dhahabu kwahivo kila siku
wataendelea kuja kujaribu kuvuna dhahabu kutoka hapa.
"Kwasababu
sisi kazi yetu ni kuhifadhi Maliasili ambayo tumepata kama urithi wa nchi yetu,
niwahakikishie kwamba tutaimarisha ulinzi kwa kuanzisha kituo cha ulinzi hapa
ili askari wawe wanabadilishana na kudhibiti kabisa uharibu ambao umekuwa
ukifanyika, kwasababu maji yanayotoka katika chanzo hiki yanakwenda kunywesha
Muheza yenyewe na wilaya wa Tanga, tukiharibu hapa yatakosekana maji safi na
salama" alisema Dk. Kigwangalla.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala huyo, Prof. Dos Santos Silayo alisema
pamoja na eneo hilo kwa sasa kuwa linalindwa na askari wa Suma JKT
watahakikisha ulinzi unakuwepo muda wote kwa kutekeleza agizo hilo la Waziri la
kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu ili askari wawepo katika eneo hilo muda
wote.
"Lengo
letu ni kuhakikisha kwamba wananchi hawaingii ili tusiwe tunawashtukiza
kuwakamata na kwachukulia hatua, lazima tuwe watu wa kuzuia uhalifu usitokee,
nia yetu ni kuwa na kituo mara moja kama alivyoelekeza Mhe. Waziri na hili
jambo tumelichukua kama maelekezo na tutalitekeleza kwa nguvu kabisa,"
alisema Prof. Dos Santos Silayo.
Awali
Dk. Kigwangalla alitembelea kikundi cha wafugaji wa vipepeo katika Tarafa ya
Amani ambao waliiomba Serikali ifungulie vibali vya kusafirisha bidhaa hiyo nje
ya nchi, aliahidi kuyafanyia kazi maombi yao huku akiwataka kutumia fursa ya
ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya
Mazingira Asilia Amani.
Akiwa
mkoani Tanga alitembelea pia Kituo cha Mambo ya Kale cha Mapango ya Amboni na
kusema Wizara yake itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya
Kale ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini viweze kuchangia zaidi
kwenye pato la Taifa.
Katika
ziara hiyo ya siku moja mkoani Tanga alitembelea pia shamba la miti ya Mitiki
Longuza, Makumbusho ya Shaban Robert na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia vipepeo katika moja
shamba la wafugaji katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana. Mbali na biashara
ya kuuza vipepeo hao nje ya nchi aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya
ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia
watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea zawadi ya pambo la
vipepeo kutoka kwa mmoja wa wafugaji Asina Athumani muda mfupi baada ya kukagua
shamba la vipepeo katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka
wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa
maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisaidia baadhi ya watu kupanda
mlima baada ya kukagua chanzo cha maji cha Mto Zigi ambacho kipo ndani ya
Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani wilayani Muheza mkoa wa Tanga. Ameiagiza TFS
kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hilo linalovamiwa na wananchi
kwa madai ya kuchimba madini ya dhahabu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya shamba la vipepeo
katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka wafugaji hao kutumia
fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia
watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani tofauti na hivi sasa
wanapotegemea soko la kuuza nje ya nchi. Kulia ni Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi
Rajabu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa
Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana
Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo
vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi
Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kuhusu kivutio cha
utalii cha umbo la asili la ramani ya Afrika alipotembelea mapango hayo jana
Jijini Tanga.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo
kuhusu asali inayozalishwa na Wakala huyo kupitia shamba la Miti Sao Hill muda
mfupi kabla ya kuikabidhi kwa Asha Shaban ambaye ni dada yake na aliyekuwa
mshairi na mwandishi mashuhuri wa riwaya Shaban Robert alipotembelea makumbusho
ya mwandishi huyo Jijini Tanga jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Asha Shaban ambaye
ni dada yake na Shaban Robert aliyekuwa mshairi na mwandishi mashuhuri wa
riwaya zawadi ya asali inayozalishwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS
kupitia shamba la Miti Sao Hill alipotembelea makumbusho ya mwandishi huyo
Jijini Tanga jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kukagua Kituo cha Mapango
ya Amboni wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Tanga jana ambapo alisema
Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili
vichangie zaidi kwenye pato la Taifa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo ya namna ya
kupanda miti ya Mitiki kutoka Meneja wa shamba la Miti Longuza alipotembelea
shamba hilo jana wilayani Muheza Mkoani Tanga.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wafanyakazi wa
Hifadhi ya Taifa Mkomazi alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Tanga.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi kuanzisha mchakato wa kisheria wa kupandisha
hadhi Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wamimbiki kuwa Pori la Akiba ili
iweze kuhifadhiwa vizuri baada ya kushindwa kujiendesha.
Ametoa
agizo hilo leo mkoani Pwani baada ya kutembelea eneo la Jumuiya hiyo wakati wa
ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi katika eneo hilo ambalo ndani
yake pia kuna mapito ya wanyamapori.
Dk.
Kigwangalla amechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa
jumuiya hiyo ikiwemo tuhuma walinzi wake kutoka katika vijiji vinavyounda jumuiya kujihusisha
na vitendo vya ujangili. Hata hivyo alipokea ombi la Mwenyekiti wa Jumuiya
hiyo, Omari Tofiki ambaye aliiomba Serikali ichukue jukumu la kulinda hifadhi
hiyo kwa asilimia 100.
"Sisi
kama jamii tumeshindwa, tunaomba msaada wa Serikali, itusaidie kuondoa hawa
wavamizi na ikiwezekana ichukue jukumu la kulinda hifadhi hii kwa asilimia
100," alisema Tofiki.
Alisema
jumuiya hiyo ambayo ni muunganiko wa vijiji 24 inakabiliwa na changomoto kubwa
ya ujangili uliokithiri ambao umepelekea kuuwawa kwa wanyamapori zaidi ya
asilimia 90 ya waliokuwepo tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo mwaka 1997.
Alisema
changamoto nyingine ni kukosekana kwa muwekezaji na mapato ya kujiendesha,
uvamizi wa mifugo ndani ya hifadhi hiyo na majungu yanayosababishwa na baadhi
ya wananchi na viongozi wanaonufaika na vitendo vya ujangili na uharibifu wa
hifadhi hiyo.
Dk.
Kigwangalla alisema jumuiya hiyo imefeli katika kila eneo jambo ambalo
linalazimu kuanzishwa kwa mchakato wa kuirudisha Serikalini ili iweze kuhifadhiwa
vizuri. Alitoa wito kwa viongozi wa Wilaya na vijiji kuanza kuwaelimisha
wananchi juu ya umuhimu wa kupandishwa hadhi jumuiya hiyo kwa faida ya pande
zote.
"Nimepokea
maombi mengi ya kuongeza idadi ya wanyamapori katika hifadhi ya Saadan, tatizo
kubwa hapa ni kwamba wanyamapori wanapotoka nje ya hifadhi hiyo na kupita
kwenye eneo la Wamimbiki wanavunwa na majangili ambao wengi wao wanasuply
(wanasambaza) nyamapori Jijini Dar es Salaam," alisema Dk. Kigwangalla
akielezea umuhimu wa kupandishwa hadhi hifadhi hiyo.
Kwa
upande wake Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania TAWA, Abraham Julu amesema Serikali imekuwa ikisaidia
katika ulinzi wa eneo la jumuiya hiyo kwa kushiriki kwenye doria mbalimbali
ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia kuondoa makazi ndani ya hifadhi hiyo.
Alisema
eneo hilo ni muhimu sana kwa uhifadhi wa wanyamapori kwa kuwa ni moja ya eneo
la mazalia ya wanyamapori na shoroba nne (mapito ya wanyamapori)
zinazounganisha hifadhi ya Taifa ya Saadan, Mikumi na Pori la Akiba la Selous.
Katika
hatua nyingine baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan, Dk. Kigwangalla
ameuagiza uongozi wa TANAPA kupitia hifadhi hiyo kwa kushirikiana na uongozi wa
Wilaya ya Bagamoyo na vijiji kuweka utaratibu maalum utakaowawezesha wananchi
kupita katika barabara zilizopo ndani ya hifadhi hiyo kwa ajili ya shughuli za
kijamii ikiwemo kuwatengenezea vitambulisho maalum.
Ametoa
agizo hilo kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwake na Mbunge wa Jimbo la
Chalinze, Ridhiwan Kikwete kuwa wananchi wake wanazuiliwa kutumia barabara hizo
kwa madai ya kushiriki kwenye vitendo vya uharibifu wa hifadhi hiyo. Amewataka pia viongozi wa hifadhi hiyo ya pekee barani Afrika ambayo ipo katika fukwe za bahari ya Hindi kuwa wabunifu zaidi kwa kuanzisha bidhaa mpya za utalii ikiwa ni pamoja na kutangaza fursa zilizopo. Alisema hifadhi hiyo ambayo ipo karibu na Jiji la Dar es Salaam na Tanga ni fursa nzuri kwa watalii kutumia ukaribu huo kuweza kuwaona wanyamapori mbalimbali wakiwemo Simba, Twiga na Tembo pamoja na utalii wa fukwe.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa Jumuiya
ya Hifadhi ya Wanyamapori Wamimbiki wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua
migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la Jumuiya ya
Hifadhi ya Wanyamapori Wamimbiki wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua
migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wafanyakazi wa
Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya hifadhi katika
wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa
TANAPA, Martin Loibooki.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mazingira ya Hifadhi
ya Taifa ya Saadan na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Stephano Msumi wakati wa
ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani Jana. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la
Chalinze, Ridhiwan Kikwete wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya hifadhi kwenye
Hifadhi ya Taifa ya Saadan katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana.
Katikati ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA, Martin Loibooki.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mazingira ya fukwe ya
Hifadhi ya Taifa ya Saadan na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete
wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani Jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa bodi
hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.
Waziri
wa Maliasili na Utaliii, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo Februari 20, 2018,
amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Makao makuu ya Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) Jijini Dar es Salaam na kuitaka kufanya kazi kwa kasi na ubunifu
zaidi.
Akizungumza
na viongozi wa Bodi hiyo, Dkt. kigwangalla amewataka kuongeza kasi zaidi katika
kutangaza Utalii wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuanzisha studio ya kimataifa
ya kutangaza vivutio vya Tanzania ndani na nje ya nchi kwa kutumia lugha
mbalimbali za Kimataifa.
Aidha,amewataka
kuharakisha zoezi la uwekaji wa mabango yanayotangaza Utalii wa Tanzania katika
viwanja vya ndege hususani uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar
es Salaam (JNIA).
Hata
hivyo amewataka pia kujikita zaidi katika matumizi ya mitandao ya kijamii kwa
kuhakikisha inahuishwa mara kwa mara.
Pamoja
na hayo, ameiagiza bodi hiyo, kushirikisha wadau mbalimbali wanaotoa huduma za
Utalii ikiwemo madereva taxi na Marubani kwa kuwapa elimu ya kutangaza
utambulisho wa Tanzania kupitia Utalii na vivutio vilivyopo.
Akiwa
katika ofisi hizo ndani ya jengo la Utalii House, alikagua ofisi mbalimbali za
bodi hiyo pamoja na zile za Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na
kupata maelezo machache kutoka wa maafisa wa Shirika hilo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa bodi
hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi hiyo, Devetha Mdachi kukagua mazingira ya ofisi hiyo mapema
leo tarehe 20 Februari, 2018.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi hiyo, Devetha Mdachi kukagua mazingira ya ofisi hiyo mapema
leo tarehe 20 Februari, 2018.
Picha
ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na uongozi
wa bodi hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20
Februari, 2018.