slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Tuesday, June 27, 2017

WANAWAKE WAWEKA REKODI YA KUCHEZA SOKA KATIKA KILELE CHA UHURU,MLIMA KILIMANJARO

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii-Kanda ya Kaskazini.
.........................................................................................................................

Wachezaji 30 wa timu za soka za mataifa mbalimbali wameshiriki kuweka rekodi ya kwanza Duniani kwa kucheza mchezo wa kirafiki katika mlima Kilimanjaro ,umbali mita 5731 kutoka usawa wa bahari.

Rekodi nyingine iliyowekwa ni ile ya mwamuzi wa kike wa Tanzania anayetambulika na Shirikiho la Soka Duniani (FIFA) Jonesia Rukyaa  kuchezesha mchezo huo  wa dakika 90 uliomalizika kwa sare ya bila kufungana .
Kundi la Wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa zaidi ya 20 walioshiriki kuweka rekodi ya kucheza soka katika eneo la kreta lililopo katika kilele cha Uhuru.
Baadhi ya wachezaji walioshiriki mchezo wa soka katika Kilele cha uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrta Loibook akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini ,Devota Mdachi walipowapokea wachezaji wa timu za taifa za wanawake wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Mwika.
Mhifadhi Mkuu KINAPA,Betrita Loibook pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii,Geofrey Tengeneza wakifurahia mara baada ya wachezaji wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani kuweka rekodi ya kucheza mpira katika kilele cha Uhuru .
Wachezaji wa timu za Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya utalii pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Timu za Gracier fc na Volcano fc zikijiandaa kwa mchezo wa kirafiki katika eneo la Kreta,kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakiweka pozi la picha katika Kreta ya Uhuru katika kilele cha Uhuru juu ya Mlima Kilimanjaro.

Thursday, June 22, 2017

WAZIRI WA MALIASILI, PROF. JUMANNE MAGHEMBE AMUAGA NA KUMSHUKURU BALOZI WA UJERUMANI NCHINI ANAYEMALIZA MUDA WAKE, EGON KONCHANKE

 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Juni, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Waziri Maghembe alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano na misaada mbalimbali aliyoitoa, yeye binafsi na nchi yake katika kusaidia kuendeleza sekta ya uhifadhi nchini.
Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (katikati) akifurahia zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori alivyopewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 juni, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi.  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 juni, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Martin Loibooki.
 Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous mkoani Morogoro.
Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kulia) akimkabidhi Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe zawadi ya picha ya kumbukumbu ambayo ilipigwa wakati wawili hao wakitua kwa ndege katika uwanja wa ndege wa Matambwe, Selous, Kwa mujibu wa balozi huyo siku hiyo haikuwa rahisi kwa ndege hiyo kutua kwa kuwa mvua zilikuwa zinanyesha. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)

HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA KWA MAENDELEO ENDELEVU...

TANAPA, TTB, NCAA NA TBC WAINGIA MAKUBALIANO YA KUANZISHA CHANNEL YA UTALII

Image may contain: 8 people, people sitting
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa pamoja jana wamesaini makubaliano ya kuanzishwa kwa Chaneli maalum ya Utalii itakayohusika na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa soko la ndani na nje ya nchi.

Makubaliano hayo yametiwa saini na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (wa pili kulia), Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Devota Mdachi (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dk. Ayub Rioba (wa kwanza kulia) na Kaimu Mhifadhi wa NCAA Asangye Bangu (wa pili kushoto).
Image may contain: 6 people, people smiling, indoor

Sunday, June 18, 2017

WAZIRI MAGHEMBE AZINDUA MRADI WA BIL. 47 WA UHIFADHI NA MAENDELEO YA IKOLOJIA YA PORI LA AKIBA LA SELOUS (SECAD)

NA HAMZA TEMBA - WMU
..............................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe kwa kushirikiana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Konchanke amezindua Mradi wa Uhifadhi na Maendeleo ya Ikolojia ya Pori la Akiba la Selous SECAD (Selous Ecosytem Conservation and Development Program) ambao umefadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania, mradi huo utatekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, WWF (World Wildlife Fund) na FZS (Frankfurt Zoological Society).

Akizungumza katika hafla iliyofanyika jana, Matambwe na Tagalala Selous, Mkoani Morogoro, Waziri Maghembe alisema Serikali ya Ujerumani kupitia benki ya KFW imechangia Euro Mil. 18 (sawa na Shilingi Bil. 45.124) katika mradi huo wa miaka mitano huku mashirika ya WWF (World Wildlife Fund) na FZS (Frankfurt Zoological Society) yakichangia Euro laki 4 kila moja (sawa na Shilingi bil. 2.005) katika mradi huo. Pamoja na uzinduzi huo alizindua pia Mpango Kazi wa Dharura wa kuendeleza pori hilo.

"Mradi huu ni muhimu sana kwakua utasaidia kuongeza nguvu kwenye jitihada zetu za kuendeleza na kuimarisha hifadhi ya pori hili la Selous ikiwemo upatikanaji wa vitendea kazi muhimu pamoja na kutuongezea nguvu kwenye mapambano dhidi ya ujangili", alisema Prof. Maghembe.

Alisema jitihada ambazo Serikali imeshazifanya katika pori hilo ni pamoja na kuimarisha doria za ndege zenye rubani na zisizo na rubani (drones), kutoa mafunzo ya jeshi usu kwa askari, kuongeza maaskari pamoja na vitendea kazi ambapo katika mwaka ujao wa fedha Serikali itatoa magari mengine 15 kusaidia pori hilo.

"Pamoja na jitihada hizo tunawekeza dola za kimarekani Milioni 156 (sawa na Shilingi bilioni 349.441) kwa ajili ya kuboresha pori hili (Selous), Ruaha, Mikumi, Rungwa na Kitulo kuhakikisha watalii wanatembelea maeneo haya na kuondoa kile kikwazo cha wao kutotembelea hifadhi za kusini, hiyo inaenda sambamba na kuimarishwa kwa shirika la ndege la Serikali la Air Tanzania na kuondoa changamoto iliyokuwepo ya usafiri wa anga", alisema Prof. Maghembe. 

Akizungumzia changamoto ya ujangili katika pori hilo alisema Serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na tatizo hilo ambapo majangili wengi wameshakamatwa katika maeneo ya Tunduru, Namtumbo na maeneo ya katikati ya Selous. Alisema changamoto hiyo bado ipo katika maeneo ya Mkoa wa Ruvuma ambapo imeripotiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo kuwa kuna upatikanaji wa silaha za kivita kutoka nchini Msumbiji ambazo zinapatikana kwa watu kubadilishana na magunia ya mchele changamoto ambayo inaendelea kufanyiwa kazi.

Wakati huo huo, Prof. Maghembe akijibu swali aliloulizwa na wanahabari kuhusu hatua iliyofikiwa juu ya kauli aliyoitoa bungeni hivi karibuni ikiwa na dhamira ya kuunganisha taasisi zote za uhifadhi nchini alisema, tayari ameshaunda kamati ya watu sita ikiongozwa na Mkuu wa Chuo cha Wanyamapori Mweka, Prof. Japhary Kidegesho kwa ajili kuangalia namna bora ya kutekeleza azma hiyo. "Tayari kamati hiyo imeshaanza kazi na itaonana na wadau mbalimbali kupata maoni yao na katika kipindi cha mwezi na nusu watatuletea ripoti", alisema.

Kwa upande wake Balozi Konchanke alimuahakikishia Prof. Maghembe kuwa Serikali ya Ujerumani itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili hifadhi hiyo ikiwemo ubovu wa miundombinu na uvamizi  pori hilo kwa faida ya jamii kwa ujumla. Aidha, alitoa wito kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kubuni mbinu mpya za kukabiliana na changamoto zilizopo.

Meja Jenerali Gaudence Milanzi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, alisema "Serikali kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi imefanya kazi kubwa kuhakikisha Selous inaondolewa katika orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyopo hatarini kutoweka,  hiyo ni pamoja na kunzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyanapori Tanzania TAWA, kuanzishwa kwa mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na ujangili na miradi mbali ikiwemo huu wa SECAD uliozinduliwa leo ambayo kwa kiasi kikubwa imeasaidia katika kuendesha hifadhi zetu pamoja na kusaidia kwenye mapambano dhidi ya ujangili".

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, TAWA, Martin Loibooki aliishukuru Serikali ya Ujerumani kwa mradi huo na kusema kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto mbalimbali katika pori hilo ikiwemo ya uhaba wa vitendea kazi, miundombinu ya barabara na ujangili na hivyo kuifanya hifadhi hiyo iendelee kuwa miongoni mwa maeneo ya urithi wa dunia.

Pori la Akiba la Selous ni hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania ikiwa ukubwa wa Kilomita za mraba 50,000. Hifadhi hiyo ambayo ipo katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma ina vivutio vingi vya utalii huku ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara, ujangili, rasilimali watu na vitendea kazi. 
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akipokelewa jana katika uwanja mdogo wa ndege wa Matembwe uliopo Selous na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Martin Loibooki (wa pili kushoto) alipowasili kwa ajili ya hafla hiyo. Nyuma yake anayeshuka kwenye ndege ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa (kushoto).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana katika kituo cha Tagalala, ndani ya Pori la Akiba la Selous Mkoani Morogoro.
Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Konchanke akizungumza katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza katika hafla hiyo jana.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Prof. Faustin Kamuzora akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali Mstaafu, Hamis Semfuko akizungumza katika hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Martin Loibooki akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana, Tagalala, Selous.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizindua Mradi wa Uhifadhi na Maendeleo wa Ikolojia ya Pori la Akiba la Selous (SECAD) ambao umefadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika hafla iliyofanyika jana Matambwe, Selous Mkoani Morogoro. Wanaoshudia kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani, Egon Konchanke, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustin Kamuzora.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara hiyo, Prof. Alexander Songorwa Mpango Kazi wa Dharura wa Kuendeleza Pori la Akiba la Selous baada ya kuuzindua sambamba na mradi wa Uhifadhi na Maendeleo ya Ikolojia ya Pori la Akiba la Selous (SECAD). Kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani, Egon Konchanke, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustin Kamuzora, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Martin Loibooki na Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Dembe. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) na  Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Konchanke wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari sita aina ya Land Cruiser ambayo ni sehemu ya Mradi aliouzindua wa Uhifadhi na Maendeleo ya Ikolojia ya Pori la Akiba la Selous (SECAD).
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akijaribu moja ya gari baada ya uzinduzi wa magari sita aina ya Land Cruiser ambayo ni sehemu ya Mradi huo.
 Magari sita aina ya Land Cruiser yaliyotolewa na Serikali ya Ujerumani kama sehemu ya mradi wa SECAD.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira Prof. Faustin Kamuzora (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali Mstaafu, Hamisi Semfuko (kulia).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Mghembe (kushoto) akipokea zawadi ya picha yenye ujumbe wa Mashujaa wa Kuokoa Selous kutoka kwa Mkurugenzi wa Afrika wa WWF Ujerumani, Philipp Goltenboth (kulia). Anaeshuhudia katikati ni Mkurugenzi Mkaazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusaru.
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Mghembe (wa tatu kushoto), Balozi wa Ujerumani, Egon Konchanke (wa pili kushoto) na viongozi wengine wakuu wa Wizara na Taasisi pamoja na washiriki wa hafla hiyo. Nyuma yao ni ziwa Tagalala ambalo ni sehemu ya kivutio cha utalii ndani ya hifadhi hiyo. 
 Baadhi ya watumishi wa Pori la Akiba la Selous wakiwa katika hafla hiyo.
Taswira mwanana ya baadhi ya Twiga ndani ya Pori la Akiba la Selous.

Wednesday, June 14, 2017

WIZARA MALIASILI KUPITIA BODI YA UTALII TTB YATOA SEMINA KWA WABUNGE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA PIC MJINI DODOMA

NA HAMZA TEMBA - WMU
.................................................................................
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania TTB, imefanya semina ya mafunzo ya siku moja kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kwa lengo la kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu majukumu ya taasisi hiyo ambayo imefanyika jana mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani na Katibu Mkuu, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.

Akizungumza katika semina hiyo, Meneja wa Huduma za Utalii wa taasisi hiyo, Philip Chitaunga alisema bodi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1993 ilipewa jukumu la jumla la kukuza sekta ya utalii nchini ikiwemo kutumia mbinu mbalimbali za utangazaji, kuhamasisha uendelezaji wa mazao ya utalii na miundombinu yake, kufanya tafiti za masoko na utalii kwa ujumla pamoja na kuhamasisha uelewa wa watanzania kufahamu umuhimu na faida za utalii.

Alisema taasisi hiyo imefanya juhudi mbalimbali za kutangaza utalii wa Tanzania nje ya nchi ikiwemo kuratibu ziara za waandishi wa habari za kitalii, kuweka matangazo katika magazeti ya utalii ya kimataifa, kushiriki katika maonesho ya utalii ya kimataifa na kutangaza kupitia Televisheni za kimataifa kama CNN ya Marekani.

“Jitihada zingine tulizofanya ni kutumia balozi zetu nje ya nchi na mabalozi wa utalii wa hiari yaani 'Goodwill Ambasadors', kutumia mitandao ya kijamii na matangazo kwenye vyombo vya usafiri vya umma ambapo mwaka 2008 hadi 2009 tulitangaza kwenye mabasi 124 jijini london Uingereza, taxi 100, treni mbalimbali na katika uwanja wa ndege wa Heathrow” alisema Chitaunga.

Alisema jitihada za hivi karibuni za kutangaza utalii zimefanyika kupitia michezo ya Ligi Kuu ya Uingereza ikiwemo timu za mpira wa miguu za Seattle Sounders na Sunderland, kupitia majarida, CD na filamu fupi kwa lugha mbalimbali kama Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswahili. Pia, kupitia tovuti maalum ya utalii ya taifa (www.tanzaniatourism.gotz), App kwenye ‘Smart Phones’ na kufanya ziara za utangazaji wa utalii yaani Roadshows katika nchi za China, Afrika ya Kusini, bara la Ulaya, Amerika na Australia.

Kwa upande wa jukumu la kuhamasisha utalii wa ndani, Chitaunga alisema bodi imetekelza jukumu hilo kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari nchini pamoja na mitandao ya kijamii, kushiriki katika maonesho mbalimbambali ya ndani ya nchi kama vile Sabasaba na Kili Fair, kuhamasisha wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo, kuendesha matangazo mbalimbali ya Radio na TV na kuweka mabango maeneo mbalimbali ikiwemo ya mpakani na kwenye viwanja vya ndege.

Aliseme katika kuhamasisha utalii wa ndani, siku za hivi karibu TTB imeingia makubaliano na chama cha wenye mabasi nchini TABOA ambapo filamu mbalimbali zinazohamasisha utalii wa ndani zitaoneshwa katika mabasi zaidi ya 300 ya mikoani.

Akizungumzia kuhusu mafanikio, alisema taasisi hiyo imechangia ongezeko la idadi ya watalii wa kimataifa nchini kutoka 230,166 mwaka 1993 na kufikia 1,284,279 mwaka 2016. Aidha, mapato yameongezeka kutoka Dola za Kimarekani Milioni 146.84 na kufikia Dola za Kimarekani Milioni 2,132 huku sekta hiyo ya utalii ikichangia asilimia 17.5 ya pato la taifa.

Alisema mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na Tanzania kupata umaarufu mkubwa zaidi duniani ambapo mitandao na kampuni mbalimbali za safari za kitalii ikiwemo Safari Bookings, Fox News.com na New York Times zimeitambua kama eneo bora la utalii barani Afrika. Aidha, Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti zimetambuliwa kama miongoni mwa maajabu saba barani Afrika huku kampuni ya World Travel Awards ikiutambua Mlima Kilimanjaro kama kivutio bora zaidi barani Afrika.

“Baadhi ya watu maarufu duniani kutembelea Tanzania kama vile Oprah Winfrey, Bill Gates, Will Smith, Roman Abramovic, David Beckham, Moussa Sissoko na Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel, Ehud Barak ni sehemu pia ya viashiria vya mafanikio kwa taasisi yetu kutangaza utalii wa Tanzania nje ya nchi”, alisema Chitaunga.

Aliongeza kuwa, watu maarufu kuja kuandaa filamu zao Tanzania ni sehemu ya mafanikio ya kutangaza utalii wa Tanzania nje ya nchi, “Watu mashuhuri saba kutoka China hivi karibuni wameandaa filamu itakayorushwa katika Anhui TV inayotazamwa na watu zaidi ya milioni 800 duniani” alisema.

Katika jitihada za kutangaza utalii wa Tanzania kupitia shirika la ndege la Air Tanzania Chitaunga alisema, “TTB sasa inaandaa gazeti la Air Tanzania litakalojulikana kama Safari Njema kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania na vivutio vyake pamoja na kuimarisha usafiri wa anga kupitia shirika hilo la Umma”.

Alisema pamoja na mafanikio hayo, bodi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu hafifu katika baadhi ya maeneo ya vivutio vya utalii, changamoto ambayo imeanza kufanyiwa kazi na Serikali ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, uimarishaji wa viwanja vya ndege na kuimarisha shirika la ndege la Air Tanzania.

Alisema changamoto nyingine ni ufinyu wa bajeti ya utangazaji, hofu ya matukio ya ugaidi na mlipuko wa magonjwa katika bara la Afrika, upungufu wa vyumba vya malazi katika baadhi ya maeneo yenye vivutio vya utalii, mtazamo hasi kuwa Tanzania ni ghali na mtazamo kuwa jukumu la utangazaji na uendelezaji utalii ni la Wizara na Taasisi zake pekee. Alisema changamoto zote hizo zinafanyiwa kazi ikiwemo kuhamasisha wawekezaji kuwekeza katika sekta ya utalii na watanzania kuona umuhimu wa utalii na kuutangaza pamoja kuwatoa hofu watalii na kuwawekea mazingira bora na rahisi ya kutembelea Tanzania.

Akizungumzia mipango ya baadaye ya taasisi hiyo, Chitaunga alisema ni pamoja na kutafsiri tovuti ya utalii ya Taifa katika lugha ya Kijerumani, Kichina na Kiswahili, kuendeleza juhudi za kufungua masoko mapya ya utalii kama vile China, Israel, Urusi na India, kuimarisha utangazaji wa utalii kupitia TEHAMA, kuongeza idadi ya mabalozi wa hiari katika masoko mahususi ya utalii, uwekaji wa mabango, tafiti za masoko mapya ya utalii na kuandaa filamu mpya za kuitambulisha Tanzania ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Albert Obama aliipongeza Wizara na TTB kwa semina hiyo pamoja na jitihada wanazozifanya za kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi na kutaka juhudi zaidi ziongezwe huku baadhi ya wabunge waliochangia wakiitaka Serikali iongeze uwekezaji katika bajeti ya utangazaji ili taasisi hiyo iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Naye Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani alisema ushauri uliotolewa na wabunge hao utafanyiwa kazi na hoja zote zilizowasilishwa zitajibiwa kwa maandishi huku Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akihitimisha kwa kusema kuwa Wizara imepiga hatua kubwa ya kukabiliana na ujangili ndani na nje ya maeneo ya hifadhi nchini. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kushoto) akizungumza jana mjini Dodoma katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu majukumu ya bodi hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Albert Obama. 
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto) akizungumza jana mjini Dodoma katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu majukumu ya bodi hiyo. Katikati ni Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Albert Obama.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Albert Obama (kulia) akizungumza jana mjini Dodoma katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu majukumu ya bodi hiyo. Katikati ni Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi. 
Meneja wa Huduma za Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Chitaunga (kushoto) akiwasilisha mada ya jumla kuhusu shughuli za taasisi hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia bodi hiyo mjini Dodoma jana. 
Meneja wa Huduma za Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Chitaunga (kushoto) akiwasilisha mada ya jumla kuhusu shughuli za taasisi hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia bodi hiyo mjini Dodoma jana. 
 Meneja wa Huduma za Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Chitaunga (kushoto) akiwasilisha mada ya jumla kuhusu shughuli za taasisi hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia bodi hiyo mjini Dodoma jana. 
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiangalia video zilizoandaliwa na TTB kwa ajili ya kutambulisha utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili kupitia bodi hiyo mjini Dodoma jana.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) na Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Lulida akichangia jana mjini Dodoma katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu majukumu ya bodi hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katika semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili kupitia Bodi ya Utalii Tanzania mjini Dodoma jana.
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Geofrey Meena akifafanua jambo katika semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili kupitia Bodi ya Utalii kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu majukumu ya bodi hiyo.

Sunday, June 11, 2017

SERIKALI YABAINI MBINU MPYA INAYOTUMIWA KUTAKATISHA FEDHA HARAMU KUPITIA MIFUGO INAYOINGIZWA KWENYE MAENEO YA HIFADHI NCHINI – PROF. MAGHEMBE

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.  Alimueleza balozi huyo kuwa Serikali imebaini na itakomesha ujanja unaofanywa na wafanyabiashara haramu wa kutakatisha fedha kwa kununua makundi makubwa ya mifugo na kuyachunga kwenye maeneo ya hifadhi nchini na baadae kuyauza kwa faida kwenye minada.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimkabidhi Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke majarida mbalimbali enye taarifa za vivutio vya Tanzania ofisini kwake mjini Dodoma. (Picha na Hamza Temba - WMU)