slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Sunday, December 30, 2018




NAIBU WAZIRI MHE.KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI

NA LUSUNGU HELELA-MWANZA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu amewataka wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani  ya Hifadhi ya misitu ya Visiwa vya  Kome  na Maisome vilivyoko wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza kulipa tozo za serikali bila kulazimishwa.



Kauli hiyo ameitoa  wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya  Msitu wa Shigala ulioko Kome Mchangani ambayo ni kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.



Mbunge wa Jimbo la Buchosa Dkt. Charles Tizeba amemueleza  Naibu Waziri hiyo kuwa kumekuwepo na changamoto ya ulipaji  tozo kubwa hata kama mtu ana eneo dogo na ndipo wananchi walilazimika kugoma kulipa tozo hiyo kwa lengo la kupata msaada zaidi.



Amefafanua kuwa mtu anayemiliki hekari moja  anatakiwa kulipa Tsh.425,000 kwa mwaka lakini hata mtu anayemikili eneo dogo la mita 20 naye anatakiwa kulipa kama wa hekari moja  kitendo kilichowafanya wananchi hao kushindwa kulipa na kusubili maelekezo ya wizara husika.



Mmoja wa wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi hiyo,Juma Ramadhani amemwomba Naibu Waziri kuangalia upya sheria hiyo ili wananchi wapate nafuu ya kulipa na serikali iweze kupata mapato yake.



Kaimu Meneja wa TFS Kanda ya Ziwa, Thomas Moshi amesema kuwa tozo hizo zipo kwa mujibu wa sheria kinachotakiwa ni wananchi kulipa na siyo kugomea kulipa tozo hizo na wanapofanya hivyo wanakwenda kinyume na matakwa ya sheria ya hifadhi ya misitu.



Kanyasu amewahakikishia wananchi hao kuwa suala hilo atalipatia majibu kwa haraka lakini amewataka watu wanaomiliki hekari moja  kulipa tozo hizo kwa wakati na wale wenye maeneo madogo madogo wajiunge katika vikundi ili waweze kuilipa pesa hiyo



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akizungumza na  wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani  ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kuwa watalipa tozo za serikali bila kulazimishwa alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akizungumza na wananchi wa Jimboni kwake  kwenye mkutano wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wa   kutatua kero za  wananchi wanaoishi ndani ya  Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya  Kome Mchangani

Mwenyekiti wa Kijiji cha Buhama kata ya Buhama, Thomas Sabuni, akizungumza  na wananchi kwenye mkutano wa hadhara kabala ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ikiwa lengo  kutatua kero za  wananchi  wa Kisiwa hicho wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya  katika eneo la Kome mchangani
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akiteta jambo na Meneja wa Shamba la Buhindi , Ayoub Kigongwira wakati wa  mkutano wa hadhara uliofanyika katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Baadhi  ya wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu ndani  ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Buhama  wakati alipowasili katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wvuvi kwa ajili ya  kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiiangalia taarifa mara baada ya kukabidhiwa taarifa Mwenyekiti wa kijiji Buhama, Thomas Sabuni  wakati alipowasili katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wvuvi kwa ajili ya  kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo




Saturday, December 8, 2018

MHE KANYASU AENDESHA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA


 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ( wa pili kushoto)  akizungumza mara baada ya ibada iliyofanyika katika ya Kanisa la Wasabato la Geita kati wakati ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita


Baadhi ya waumini ibada wa Kanisa la Wasabato la Geita kati wakifuatilia ibada kabla  ya  harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita


 Mchungaji na  Mwenyekiti wa South Nyanza Conference, Sadoki Butoke akitoa mahubiri kwa  waumini waliojumuika katika ibada ya  harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa  Kanisa la Wasabato la Geita wakisikiliza mahubiri kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita
Baadhi ya wanakwaya wakiimba wakati wa mahubiri kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akivishwa skafu na wanafunzi wa Skauti kanisa la Wasabato la Geita Kati kabla  ya Naibu Waziri huyo kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja  na kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita mara baada ya kusomewa taarifa ya hali ya uhifadhi wa misitu na wanyamapori kabala ya kushirikia harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Afya