slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Saturday, June 30, 2018

DK. KIGWANGALLA AHITIMISHA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA KIMONDO DUNIANI MKOANI SONGWE

Na Hamza Temba-Songwe
................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa wito kwa wadau wa utalii wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuweka juhudi za pamoja na kushirikiana na Serikali katika kuendeleza na kutangaza vivutio vya utalii vya kanda hiyo ili viweze  kunufaisha zaidi wananchi na Taifa kwa ujumla.

Ametoa wito huo jana wakati akihitimisha kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika eneo la Kimondo cha Mbozi kwenye kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.

Amesema mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ina vivutio vingi vya utalii ambavyo bado havijaendelezwa vya kutosha na kutangazwa vizuri kama vile vya nyanda ya kaskazini ikiwemo vivutio vya mambo ya kale, wanyamapori na tamaduni mbalimbali.

Amesema mpango wa Serikali wa maendeleo wa miaka mitano umeelekeza kuwepo kwa shughuli za utalii zitakazoenda sambamba na kuinua maisha ya wananchi, hivyo ametoa rai kwa idara ya mambo ya kale na utalii, na taasisi za wizara yake kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Songwe  kupanga namna ya kuendeleza eneo la kimondo cha Mbozi kwa kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi zitakazowainua wananchi wa eneo hilo kupitia utalii.

Amesema Serikali kupitia Wizara yake imeanza kuchukua hatua ya kufungua utalii wa kanda hiyo ambapo imesaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia kwa ajiri ya Mradi wa Kusimamia maliasili na Kuendeleza Utalii Kanda ya Kusini (REGROW).

Pamoja na kanda hiyo amesema Serikali pia inafungua utalii wa kanda ya Kaskazini Magharibi ambapo tayari mapori matano ya akiba yameshatangazwa kupandishwa hadhi ya kuwa Hifadhi za Taifa, huku ujenzi unaendelea wa uwanja wa ndege wa kisasa wa Chato ukitarajiwa kuchagiza maendeleo ya hifadhi hizo.

Dk. Kigwangalla pia ametoa wito kwa wadau wa kanda hizo kutumia fursa hizo kuwekeza katika sekta ya utalii ikiwemo ujenzi wa mahoteli ya kitalii, biashara ya kusafirisha watalii na huduma nyingine mbalimbali katika sekta hiyo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema wizara yake inaendelea na mikakati mbalimbali ya kutangaza vivutio vya utalii nchini ambapo mwezi Septemba kila mwaka utakuwa na mwezi maalum wa kuadhimisha utamaduni wa Mtanzania ili kukuza utalii wa kiutamaduni.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa amesema mkoa wake umedhamiria kutangaza vivutio vya utalii mkoani humo kupitia njia za matamasha, michezo mbalimbali na kuwashirikisha wadau. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati), Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga (kushoto kwake), Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Galawa (kulia kwake) na viongozi wengine mkoani humo wakiangalia Kimondo cha Mbozi wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndolezi wilaya Mbozi mkoani Songwe wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kuhusu Kimondo cha Mbozi kutoka kwa mkuu wa kituo hicho, Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Filmerick Basange wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Galawa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akinasisha sumaku kwenye Kimondo cha Mbozi wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Kutoka kushoto nyuma yake ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Galawa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chuku Galawa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Wa tatu kushoto Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa wakijaribu kahawa ya asili inayozalishwa mkoani humo kwenye maonesho wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa wakijaribu maziwa ya mtindi yanayozalishwa mkoani humo kwenye maonesho wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa wakishiriki kucheza ngoma wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, akipata maelezo kuhusu vinyago vya kiutamaduni vinavyoelimisha jamii kutoka kwa mmoja ya waoneshaji wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa (kulia kwake). 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wakati wa kuhitimisha maadhimisho hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga (kushoto kwake), Mkuu wa Mkoa wa Songwe (kulia kwake), Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela na viongozi wengine wakishiriki kukata utepe kama ishara kuzindua maonesho ya Karibu Kusini yatakayofanyika mwezi Septemba mwaka huu, mkoani Iringa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa cheti maalum cha wizara cha kutambua mchango wake wa kuhamasisha na kuendeleza shughuli za utalii mkoani humo. Kushoto anaeshuhudia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Japhet Hasunga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga wakinyoosha mikono huu kama ishara ya kuwakaribisha wananchi katika maonesho ya Karibu Kusini yatakayofanyika mwezi Septemba, mkoani Iringa mda mfupi baada ya kuyazindua wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. 

Wednesday, June 27, 2018

DK. KIGWANGALLA APOKEA TAARIFA YA AWALI YA KAMATI YA KOVA KUHUSU TUHUMA ZA MAUAJI YA TEMBO


VIDEO
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya Tembo katika Ikolojia ya Ruaha-Rungwa ambazo ziliripotiwa na kituo cha habari cha ITV-London mwaka 2017, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma hizo, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova ofisini kwake Jijini Dodoma. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Japhet Hasunga na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Iddi Mfunda (kulia). Tuhuma hizo ziliwahusisha watumishi wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Duniani (UNDP) kupitia mradi wa SPANEST waliokuwa wakiufadhili.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) na Naibu Waziri, Japhet Hasunga (katikati) wakipokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya Tembo katika Ikolojia ya Ruaha-Rungwa ambazo ziliripotiwa na kituo cha habari cha ITV-London mwaka 2017, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma hizo, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova ofisini kwake Jijini Dodoma. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) na Naibu Waziri, Japhet Hasunga (wa pili kulia) wakipokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya Tembo katika Ikolojia ya Ruaha-Rungwa ambazo ziliripotiwa na kituo cha habari cha ITV-London mwaka 2017, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma hizo, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova ofisini kwake Jijini Dodoma. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, Julius Kibebe, Kresensia Swai na Emmanuel Musamba (kushoto). 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Iddi Mfunda taarifa hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa mapendekezo ya kamati hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wajumbe wa kamati maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma za mauaji ya Tembo ambazo ziliwahusisha watumishi wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Duniani (UNDP) kupitia mradi wa SPANEST waliokuwa wakiufadhili. (Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii).

Tuesday, June 26, 2018

DK. KIGWANGALLA AFUNGUA WARSHA YA KITAIFA YA WADAU WANAOPINGA VITENDO VYA UHALIFU DHIDI WANYAMAPORI NA MISITU NCHINI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua warsha ya kitaifa ya siku moja ya wadau wanaopinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. Warsha hiyo imelenga kujadili na kuainisha mahitaji na vipaombele katika sekta ya mahakama na mashtaka kwa ajili ya kudhibiti uhalifu huo.  
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Iddi Mfunda (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga (wa pili kulia) na Mkuu wa ofisi wa Shirika la Ufuatiliaji wa Wanyamapori (TRAFFIC), Julie Thomson (kulia) wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa warsha ya kitaifa ya siku moja ya wadau wanaopinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. 
 Baadhi ya wadau wa kitaifa walioshiriki hafla hiyo wakiimba wimbo wa Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua warsha ya kitaifa ya siku moja ya wadau wanaopinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. 
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na wadau wa kitaifa wa kupinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini.

Sunday, June 24, 2018

DK. KIGWANGALLA AELEZA MSIMAMO WA TANZANIA ULIVYOPENYA KWENYE ITIFAKI YA UTALII NA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI YA EAC



TANZANIA YAWEKA MSIMAMO MKALI KWENYE ITIFAKI YA UTALII NA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI YA EAC


Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Mambo ya Kale wa Uganda, Ephraim Kamuntu (katikati) na wawakilishi wa Mawaziri wa Utalii wa Burundi, Kenya na Rwanda wakisaini Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) katika ukumbi wa EAC Jijini Arusha. 

Na Hamza Temba-Arusha
..............................................................
Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) imezua mjadala mzito na mabishano makali katika Mkutano wa Nane wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo uliofanyika Jijini Arusha juzi.

Mvutano huo ulisababishwa na hoja iliyowasilishwa na Tanzania ambayo ilitaka kuboreshwa kwa kifungu cha nne cha itifaki hiyo ambacho kinazitaka nchi wanachama kutangaza eneo lote la jumuiya ya Afrika ya Mashariki kama kituo kimoja cha safari za utalii duniani.

Tanzania ikiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, ilipinga vikali na hatimaye ikagoma kusaini itifaki hiyo ambayo imejadiliwa kwa zaidi ya miaka saba mpaka pale mapendekezo yake yalipoingizwa kwenye kifungu hicho.

Kifungu hicho kilikuwa kinasema, "Every Partner State shall market and promote the Community as a single tourist destination", (Kila nchi mwanachama itatangaza jumuiya kama kituo kimoja cha safari za utalii (duniani)).

Tanzania ikapendekeza kwenye kifungu hicho uongezwe mstari unaosema, "while maintaining country identites" (huku kila nchi mwanachama ikibaki na utambulisho wake halisi).

Mapendekezo hayo ya Tanzania yaliungwa mkono na Burundi na kupingwa vikali na nchi za Kenya, Uganda na Rwanda ambazo zilisema hakuna madhara yeyote ya kutobadilisha kifungo hicho. Nchi ya Sudan Kusini haikuweza kushiriki mkuatano huo.

Licha ya majadiliano makali yaliyosababisha mkutano huo  kumalizika majira ya saa nne za usiku badala ya saa 12 jioni kwa mujibu wa ratiba ilivyopangwa, wajumbe hao walikubali mapendekezo ya Tanzania na hatimaye itifaki hiyo ikasainiwa.

Awali itifaki hiyo ilijadiliwa kwenye vikao vya wataalam wa jumuiya hiyo na Makatibu Wakuu, siku tatu kabla ya kuwasilishwa kwenye Baraza hilo la Mawaziri.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema Tanzania ililazimika kuweka msimamo huo ili kuepuka madhara ya nchi nyingine kutangaza vivutio vyake kuwa viko nchini kwao kama ambavyo nchi ya Kenya imewahi kutangaza mlima Kilimanjaro upo kwao.

Aidha, alisema msimamo huo pia ulilenga kulinda maslahi ya Tanzania kwakuwa ni nchi pekee yenye vivutio vingi na ambayo imehifadhi ardhi yake kwa zaidi ya asilimia 32 ukilinganisha na nchi nyingine wanachama, mfano Kenya ambayo imehifadhi takriban asilimia 7 tu ya ardhi yake.

Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Ibara ya 115 (1-3) na Ibara ya 116 unaeleza kuwa jumuiya inaweza kuanzisha sera, mikakati na mbinu mbalimbali za kufanya shughuli za utalii na usimamizi wa wanyamapori kwa pamoja, huku kila nchi ikiruhusiwa kubaki na usimamizi, mikakati na sera zake kadri inavyoona inafaa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Mambo ya Kale wa Uganda, Ephraim Kamuntu (katikati) na wawakilishi wa Mawaziri wa Utalii wa Burundi, Kenya na Rwanda wakisaini Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) katika ukumbi wa EAC Jijini Arusha. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasilisha mapendekezo ya Tanzania kwenye kifungu cha nne cha Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika Mkutano wa Nane wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki.
Baadhi ya wajumbe wa Tanzania walioshiriki mkutano huo.

Friday, June 22, 2018

DK. KIGWANGALLA ATIMUA WAVAMIZI KWENYE PORI LA AKIBA SWAGASWAGA


Video
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana, alipotembelea kijiji hicho kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga. 

Na Hamza Temba-WMU-Chemba, Dodoma
.......................................................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wananchi waliovamia Pori la Akiba Swagaswaga na kuendesha shughuli zao ikiwemo kilimo, makazi na ufugaji ndani ya pori hilo kinyume cha Sheria waondoke mara moja kwa hiari yao kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Ametoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Handa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua mgogoro wa ardhi kwenye hifadhi hiyo wilayani humo.

"Tunawapa siku 30 muanze kutoka wenyewe, baada ya siku 30 tunatoa notisi ya siku nyingine 30 za kutumia nguvu, kwahiyo kuanzia sasa hivi anzeni kujipanga wenyewe na kuondoka wakati Halmashauri ikifanya tathmini ya maeneo ya vijiji ambavyo ni halali ya kuwagawia kwa wale watakaopenda kupewa maeneo huko", alisisitiza Dk. Kigwangalla.

Alisema sheria za uhifadhi haziruhusu mtu yeyote kuingia ndani ya maeneo ya hifadhi na kuendesha shughuli za kibinadamu na kwamba kufanya hivyo ni kudharau Sheria na Malmlaka zilizopo.

Alisema kwa upande wa wananchi wa kijiji cha Handa ambacho kilianzishwa kimakosa ndani ya pori hilo wataendelea kubaki mpaka pale wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Tamisemi na Ardhi zitakapoamua hatma yao ikiwemo ama kulipwa fidia kupisha eneo hilo au waendelee kubaki na mipaka ya hifadhi isogezwe.

Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kujenga miundombinu ya kuvuta maji kutoka katika chemchem iliyopo ndani ya hifadhi hiyo na kuyasogeza kwenye makazi ya wananchi ili kulinda chanzo hicho kwa kuzuia uharibifu unaofanywa na wananchi wanaofuata huduma katika eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga alisema atasimamia ipasavyo maagizo yaliyotolewa na Dk. Kigwangalla na kwamba endapo wanavamizi hao walioingia ndani ya pori hilo kinyume cha sheria watakaidi agizo hilo atatoa notisi ya siku 30 na hatimaye kuwaondoa kwa nguvu ili kupisha eneo hilo liendelee kuhifadhiwa.

Kwa upande wake mbunge wa Chemba, Juma Nkamia alimshukuru Dk. Kigwangalla kwa kutembelea eneo hilo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo na kuwataka wananchi kutii sheria na kuepuka kuvamia maeneo yaliyohifadhiwa kisheria ili kuepuka usumbufu na mamlaka zinazosimamia eneo hilo.

Viongozi wengine walioongozana na Dk. Kigwangalla katika utatuzi wa mgogoro huo ni Mbunge wa Hanan'g, Dk. Marry Nagu, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Jackson Masaka, na viongozi wengine wa Chama na Serikali wa wilaya za Chemba na Mkalama.

Kijiji cha Handa kilisajiliwa tarehe 16 Agosti, 2004 kikiwa na ukubwa kilomita za mraba 72.23 na vitongoji vitano, vinne kati yake vikiwa ndani ya Pori la Akiba Swagaswaga. Vitongoji hivyo ambavyo ni Ilala A, Ilala B, Mbugani na Mnang'ana vina ukubwa wa kilomita za mraba 7.85 na kaya 1,169 zenye watu zaidi  ya 5,291.

Pori la Akiba Swagaswaga lilianzishwa kwa Tangazo la Serikali namba 72 la tarehe 21 Februari, 1997 likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 871. Pori hilo lipo katika wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma na wilaya ya Singida Vijijini mkoani Singida.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana, alipotembelea kijiji hicho kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia akizungumza katika mkutano huo katika kijiji cha Handa wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alipotembelea kijiji hicho jana kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga. 
Mbunge wa Hanan'g, Dk. Marry Nagu akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya Chemba na Mkalama wakikagua mpaka wa Pori la Akiba Swagaswaga ambalo lina mgogoro na kijiji cha Handa alipotembelea eneo hilo jana katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma kwa ajili ya kutatua mgogoro huo. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia, Mbunge wa Hanang, Dk. Marry Nagu, Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Jackson Masaka, na viongozi wengine wa wilaya ya Chemba na Mkalama wakiangalia ramani ya mpaka Pori wa Pori la Akiba Swagaswaga alipotembelea eneo hilo jana kwa ajili kutatua mgogoro wa hifadhi na vijiji.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya Chemba na Mkalama wakikagua mpaka wa Pori la Akiba Swagaswaga ambalo lina mgogoro na kijiji cha Handa alipotembelea eneo hilo jana katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma kwa ajili ya kutatua mgogoro huo. 
  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alipotembelea kijiji hicho jana kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga. 
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alipotembelea kijiji hicho jana kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga.

Friday, June 8, 2018

KIGWANGALLA AFUTURISHA WABUNGE DODOMA, ASISITIZA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO WA KITAIFA

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.  Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimkaribisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai nyumbani kwake kwa ajili ya kujumuika na wabunge wengine kwenye hafla ya futari aliyoiandaa kwa ajili yao nyumbani kwake Jijini Dodoma.

..........................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefuturisha wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika makazi yake yaliyopo Area D Jijini Dodoma.

Futari hiyo ilihudhauriwa na wabunge mbalimbali wa chama tawala CCM na wa vyama vya upinzani wakiongozwa na Spika, Job Ndugai na Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson.

Dkt. Kigwangalla aliwashukuru wabunge wote waliohudhuria hafla hiyo na kusema kuwa imelenga kudumisha upendo, mshikamano na umoja wa kitaifa uliopo baina ya wabunge hao bila ya kujali mipaka ya vyama vyao hususan katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

"Nimefarijika sana kuwapokea waheshimiwa wabunge wenzangu hapa nyumbani kwangu, ninawashukuru sana kwa kuja maana shughuli ni watu, tuliandaa futari nyingi kwa ajili ya wabunge wote, sasa msingefika tungepata mtihani ni wapi pa kuipeleka. 

"Hafla kama hii ya Iftar inatuunganisha sisi sote bila kujali dini zetu, inajenga na kudumisha upendo, mshikamano na umoja wetu wa kitaifa bila kujali mipaka ya vyama vyetu" alisisitiza Dkt. Kigwangalla. 

Alisema zamani kulikuwa na utamaduni wa watu kufuturu nje ya nyumba zao ili wapita njia au majirani wakikuta wanafuturu nao wanajumuika, "Siku hizi tumeanza kufuturia ndani kila mtu na familia yake, basi siku moja moja kama hivi inatokea tunaamua kuukumbuka utamaduni wetu na kualikana kufuturu pamoja" alisema. 

Kwa upande Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alikua mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, Job Ndugai alimpongeza na kumshukuru Dkt. Kigwangalla kwa kuandaa hafla hiyo na kusema kuwa inajenga mshikamano baina ya wabunge bila kujali itikadi za vyama na dini zao. 
 Mbunge wa Viti Maalum, Janeth Massaburi akimuombea dua  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla katika hafla ya futari aliyoiandaa jana kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.  Hamisi Kigwangalla akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson kwanye hafla ya futari aliyoiandaa kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.  Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Mama Salma Kikwete kwenye hafla ya futari aliyoiandaa kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (wa tatu kulia) akizungumza na baadhi ya wabunge kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla nyumbani kwake jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.  Hamisi Kigwangalla akizungumza na wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao aliwaalika kwenye futari ya pamoja nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Mbunge wa Vunjo, James Mbatia akichukua futari katika hafla ya kufuturu iliyoandaliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma.
 Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hillal akisalimiana na mbunge wa Vunjo, James Mbatia katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma. Kushoto ni Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.  Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliowaalika kujumuika naye kwenye futari ya pamoja nyumbani kwake Jijini Dodoma.

DKT. NZUKI AIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA UNWTO-AFRIKA NCHINI NIGERIA

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akisalimiana na Waziri wa Utalii wa Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa barani Afrika (UNWTO), Mhe. Najib Balala walipokutana kwenye semina wakati wa mkutano wa kimataifa wa kujadili takwimu za utalii kama kichocheo cha maendeleo barani Afrika jijini Abuja nchini Nigeria Juni 4-6,2108. Dkt. Nzuki amemuwakilisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla katika mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akiwa na Waziri wa Utalii wa Zambia, Mhe. Charles Banda katika mkutano huo.