slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Sunday, July 22, 2018

WAZIRI KIGWANGALLA AAGIZA UJENZI WA VIWANDA VIDOGO VYA ASALI KWA WILAYA ZOTE ZA MIKOA YA TABORA NA KATAVI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri kukagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana. Ameigiza Halmashauri ya wilaya hiyo kukamilisha taratibu za Tathmini ya Athari za Kimazingira (EIA) ili Serikali ifanye uamuzi wa kuendelea au kusitisha mradi huo. Wengine kwenye msafara huo ni Naibu Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda (wa nne pichani ).

.............................................................

*Ahamasisha kilimo cha Korosho kama zao mbadala la kuinua uchumi na uhifadhi wa mazingira

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ameuagiza Mfuko wa Ruzuku wa Misitu Tanzania (TAFF) kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuanzisha mradi wa viwanda vidogo vya kusindika na kufungasha asali katika mikoa ya Tabora na Katavi ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kujenga uchumi wa viwanda.

Ametoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mtakuja wilaya ya Skonge mkoani humo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake.

Alisema kwa kiwango kikubwa wananchi wa mikoa hiyo wamekuwa wategemezi kwenye zao moja tu la tumbaku ambalo sio rafiki kwa mazingira kwakuwa miti mingi hukatwa kwa ajili ya kukausha zao hilo jambo ambalo ni muhimu sasa kuwekeza zaidi kwenye mazao mengine ikiwemo viwanda vya kusindika na kufungasha asali ili kuongeza uzalishaji, ubora na hatimaye kuongeza kipato na faida zaidi.

"Mwaka huu ule mfuko wa misitu, kwa kiasi kikubwa tuamue tuwekeze ukanda huu wa magharibi  ambapo kuna zaidi ya asilimia 60 ya misitu yote hapa nchini, na tuanze kwa kujenga kiwanda kimoja katika kila wilaya, ikiwemo Nzega, Skonge, Uyui, Tanganyika, Mlele, Mpanda na Kaliua.

"Tuwawezeshe wananchi wajiunge katika vikundi, tuwagawie mizinga ya kisasa, wafuge nyuki kisasa, warine asali kisasa, wakisharina wapeleke kwenye viwanda, ifungashwe kisasa, ipate bei kubwa, na mwisho wa siku wataona faida ya kuwa na misitu.

"Hapo tutakuwa tumewasaidia, watapa kipato mbadala lakini watakua wakali sana kwa watu wanaoharibu misitu na tutatengeneza jeshi kubwa la wananchi la ulinzi wa misitu yetu, hivyo nataka mradi huu uanze mara moja bila kusuasua ili na sisi tuchangie jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. " alisema Dk. Kigwangalla.

Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla amewashauri wananchi wa mikoa hiyo kuanzisha kilimo cha korosho kama zao jingine mbadala la kuongeza kipato na kunusuru misitu badala ya kujikita kwenye zao moja la tumbaku ambalo ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa misitu ya mikoa hiyo.

Amesema ni muhimu walau kwa kila kaya moja kuanza kwa kupanda ekari moja ya mikorosho ili kuongeza zao jingine mbadala la biashara ambalo lina tija zaidi kiuchumi na kiuhifadhi wa mazingira. 

"Kilimo cha tumbaku sio rafiki kwa mazingira tumejaribu kuleta mabani banifu yanayotumia kuni chache,  tumejaribu kuwashawishi wananchi wapande miti lakini tumechemsha, miti mingi imeendelea kukatwa misitu nayo inateketea siku hadi siku, ni lazima tutafute mbinu mbadala ya kukabiliana na changamoto hii, na hii ni kupitia zao hili la korosho" alisema Dk. Kigwangalla.

Amesema tafiti zinaonyesha kuwa zao la korosho katika mikoa hiyo lina uwezo wa kustawi zaidi na kuzalisha mara mbili kuliko mikoa ya kusini ambayo inasifika zaidi kwa uzalishaji huo hapa nchini.

Aidha ameziagiza halmashauri zote za mikoa hiyo kufanya utaratibu wa kupata mbegu na miche ya zao hilo mapema iwezekanavyo kwa ajili ya kuwagawia wananchi kabla ya msimu wa mvua kuanza na wataalamu wa kilimo wawaelimishe wananchi njia bora ya kupanda na kutunza miche hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri alisema kiwango cha mvua kwa mwaka katika wilaya hiyo kimeshuka na kufikia 600mm kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri kukagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana. Ameigiza Halmashauri ya wilaya hiyo kukamilisha taratibu za Tathmini ya Athari za Kimazingira (EIA) ili Serikali ifanye uamuzi wa kuendelea au kusitisha mradi huo. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda (wa nne).
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akipiga jaramba alipokuwa akikagua  eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani Skonge jana. Anayefuata ni Naibu Waziri TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda, Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri na viongozi wengine wa wilaya hiyo. Ameiagiza Halmashauri ya wilaya hiyo kukamilisha taratibu za Tathmini ya Athari za Kimazingira ili Serikali ifanye uamuzi wa kuendelea au kusitisha mradi huo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akipiga jaramba alipokuwa akikagua  eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani Skonge jana. Kulia ni Naibu Waziri TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akiongoza kupiga jaramba alipokuwa akikagua  eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani Skonge jana. Wengine pichani ni Naibu Waziri TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda (Nyuma Katikati). Ameiagiza Halmashauri ya wilaya hiyo kukamilisha taratibu za Tathmini ya Athari za Kimazingira ili Serikali ifanye uamuzi wa kuendelea au kusitisha mradi huo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana. Kulia kwake Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri na Naibu Waziri TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda (wa pili kulia). Ameigiza Halmashauri ya wilaya hiyo kukamilisha taratibu za Tathmini ya Athari za Kimazingira ili Serikali ifanye uamuzi wa kuendelea au kusitisha mradi huo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana. Anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAWA, Mabula Misungwi, Naibu Waziri TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda na viongozi wengine wa wilaya hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana. Anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAWA, Mabula Misungwi, Naibu Waziri TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda na viongozi wengine wa wilaya hiyo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa wilaya ya Skonge wakati wa ziara yake wilayani humo jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtakuja katika wilaya ya Skonge mkoani Tabora baada ya kukagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtakuja katika wilaya ya Skonge mkoani Tabora baada ya kukagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana.

Friday, July 20, 2018

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DK. HAMISI KIGWANGALLA ATEMBELEA PORI LA AKIBA MASWA

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mandhari ya Pori la Akiba Maswa lililopo wilaya ya Meatu mkoani Simiyu wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani humo jana. Kushoto ni Mkuu wa Kanda wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Serengeti, Johnson Msella.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia akioneshwa ramani ya Pori la Akiba Maswa na Meneja wa pori hilo, Lusajo Masinde (kushoto kwake) wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya eneo la "camp" ya kitalii katika Pori la Akiba Maswa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua  mandhari ya Pori la Akiba Maswa lililopo wilaya ya Meatu mkoani Simiyu wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani humo jana. 
 Muonekano wa baadhi ya twiga katika Pori la Akiba Maswa wakati wa ziara ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla katika pori hilo jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mandhari ya Pori la Akiba Maswa lililopo wilaya ya Meatu mkoani Simiyu wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani humo jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mandhari ya Pori la Akiba Maswa lililopo wilaya ya Meatu mkoani Simiyu wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani humo jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa Pori la Akiba Maswa na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Makao wakiangalia mandhari ya Pori la Akiba Maswa lililopo wilaya ya Meatu mkoani Simiyu wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani humo jana. (Picha zote na Hamza Temba- Wizara ya Maliasili na Utalii)

AGIZO ALILOTOA WAZIRI KIGWANGALLA MKOANI SIMIYU, LIPO LA KUMTAKA MUWEKEZAJI KUSALIMISHA HATI YA KIWANJAWaziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa muwekezaji wa hoteli ya kitalii ya Kijereshi Tented Camp kurudisha kwa Kamishna wa Ardhi hati miliki ya kipande cha ardhi chenye ukubwa wa hecta 464 kilichopo ndani ya pori hilo kwakuwa ni batili.
Aidha, amewapa siku 45 wananchi wanaoishi kinyume cha Sheria ndani ya eneo la kinga (bufer zone) za Pori la Akiba Kijereshi kuondoka kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuanza operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu.

Thursday, July 19, 2018

WAZIRI KIGWANGALLA AWAPA NOTISI YA SIKU 45 WALIOVAMIA PORI LA AKIBA KIJERESHI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya Pori la Akiba Kijereshi na Meneja wa pori hilo, Dianna Chambi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu. Alitoa siku 45 kwa wananchi wote waliovamia kingo/bafa za hifadhi hiyo kuondoka kwa hiari yao. Kulia ni Mkuu wa Kanda wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Serengeti, Johnson Msella.

Na Hamza Temba-Simiyu
.........................................................

*Atoa miezi mitatu kwa Muwekezaji kurudisha Serikalini hati miliki ya kipande cha ardhi kilichopo ndani ya Pori hilo

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewapa siku 45 wananchi wanaoishi kinyume cha Sheria ndani ya kingo (bufer zone) za Pori la Akiba Kijereshi kuondoka kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuanza operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu. 

Ametoa agizo hilo jana alipotembelea pori hilo katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu ikiwa ni muendelezo wa ziara zake mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake.

Baada ya kushuhudia makazi na shughuli nyingine za kibinadam ndani ya pori hilo, Dk. Kigwangalla aliamua kutoa agizo hilo na kusema kuwa sheria za uhifadhi wa wanyamapori haziruhusu vitendo hivyo ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa kisheria pamoja na kingo zake (buffer zone) ambazo ni mita 500 kutoka kwenye mpaka halisi wa eneo la hifadhi.

"Mpaka itakapofika tarehe 31 mwezi ujao (Septemba) wananchi wote hawa wawe wameshaondoka eneo hili kwa hiari yao wenyewe, muwatangazie na mpime eneo hili vizuri muweke alama ili wajue ni wapi wanatakiwa kuondoka.

"Na ikifika tarehe 1 Septemba kama kuna watakaokuwa wamekaidi agizo hili, basi mfanye oparesheni maalum muwaondoe na msafishe kila kitu, ni lazima ifike mahali kila mmoja aheshimu sheria za nchi" alisema Dk. Kigwangalla kuuagiza uongozi wa pori hilo.

Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa muwekezaji wa hoteli ya kitalii ya Kijereshi Tented Camp kurudisha kwa Kamishna wa Ardhi hati miliki ya kipande cha ardhi chenye ukubwa wa hecta 464 kilichopo ndani ya pori hilo kwakuwa ni batili.

Aimesema pori hilo lilianzishwa mwaka 1994 wakati muwekezaji huyo anadai kumilikishwa eneo hilo mwaka 1995 jambo ambalo haliwezekani mtu binafsi kupewa hati ya kumiliki eneo lililopo ndani ya eneo jingine tena hifadhi.

Aidha, amemtaka pia muwekezaji huyo kuheshimu sheria na taratibu za uwekezaji katika eneo hilo ikiwemo kulipa ada na tozo mbalimbali.
 
Pori la Akiba Kijereshi lenye ukubwa wa kilomita za mraba 65.72 linasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA na lilipandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba mwaka 1994 kwa Tangazo la Serikali Na. 215 la terehe 10 Juni, 1994 na hiyo ni kutokana na umuhimu wake kiuchumi na kiikolojia hususan katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa Meneja wa Pori la Akiba Kijereshi, Dianna Chambi (wa pili) kuhusu wananchi waliovamia hifadhi hiyo alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu.  
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la hoteli ya kitalii ya Kijereshi Tented Camp iliyopo ndani ya Pori la Akiba Kijereshi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu, ametoa miezi mitatu kwa mmiliki wa hoteli hiyo kurudisha hati miliki ya kiwanja chenye hekta 464 kilichopo ndani ya pori ya pori hilo kwa kamishna wa ardhi kwakuwa ni batili na aendelee kutoa huduma kwa kuzingatia sheria na taraibu za uwekezaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua koki ya maji katika eneo la hoteli ya kitalii ya Kijereshi Tented Camp iliyopo ndani ya Pori la Akiba Kijereshi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu, ametoa miezi mitatu kwa mmiliki wa hoteli hiyo kurudisha hati miliki ya kiwanja chenye hekta 464 kilichopo ndani ya pori hilo kwa kamishna wa ardhi kwakuwa ni batili na aendelee kutoa huduma kwa kuzingatia sheria na taraibu za uwekezaji. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alipowasili mkoani humo jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya eneo la kingo/bafa la Pori la Akiba Maswa ambalo limevamiwa na wananchi kwa ajili ya shughuli kilimo alipolitembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Kulia kwake ni Mbunge wa Itilima, Njaru Silanga na Meneja wa Pori hilo, Lusajo Masinde.

Tuesday, July 17, 2018

DK. KIGWANGALLA AAGIZA KATIBU WA UVCCM TARIME KUKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA YA KUIKASHIFU SERIKALI

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima mtego wa misumari uliotegwa na watu wasiojulikana kwa lengo la kuzuia msafara wake wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.

Tarime - Mara
.......................................................
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameliagiza Jeshi la Polisi wilaya ya Tarime mkoani Mara kumkamata na kumfungulia mashtaka Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya hiyo, Newton Mongi na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Richard Tiboche kwa tuhuma za kuikashifu Serikali na kuchochea mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi ya Serengeti na vijiji jirani.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana majira ya saa tatu usiku baada ya kuhitimisha ziara yake wilayani humo iliyolenga kutafuta suluhu ya mgogoro uliodumu kwa miongo kadhaa kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani ikiwemo kijiji cha Kegonga.

Akiwa njiani majira ya saa tatu za usiku kwenye gari la wazi baada ya kukagua eneo hilo la mpaka kwa zaidi ya masaa sita, Waziri Kigwangalla na msafara wake walikuta lundo la mawe yakiwa barabarani ndani ya eneo la hifadhi hiyo, hali iliyosababisha taharuki kubwa na msafara wake kushuka na kuanza kuondoa mawe hayo ili kupata njia ya kupita.

Wakati zoezi hilo likiwa  linaendelea, Kiongozi huyo wa UVCCM alisikika akiituhumu Serikali kwa kuweka mawe hayo na kwamba hayakuwekwa na wananchi wa eneo hilo, jambo lililozua mshangao mkubwa  kwa viongozi wa Serikali waliokuwepo katika msafara huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.

Mkuu huyo wa mkoa alisema tukio hilo sio la mara ya kwanza na kwamba limewahi kuripotiwa mara nyingi na uongozi wa hifadhi hiyo kuwa wananchi wa vijiji jirani hujaza mawe barabarani kwa ajili ya kuzuia magari ya doria ili waweze kulisha mifugo yao ndani ya hifadhi hiyo. Alisema hata msafara wa tume ya Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda iliyoundwa na CCM hivi karibuni kufuatilia mgogoro katika eneo hilo nao ulizuiliwa kwa mawe barabarani.

Imedaiwa pia kuwa kwa nyakati tofauti viongozi hao wamekuwa wakiwatolea viongozi wa Serikali maneno ya kejeli pamoja na kuwakwamisha kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi ipasavyo.

Awali, kabla ya tukio hilo la mawe barabarani moja ya gari lililokuwa likiongoza msafara huo lilipata pancha baada ya kukanyaga misumari iliyokuwa imetengwa kwenye moja ya barabara zinazoingia na kutoka ndani ya Hifadhi ya hiyo ya Serengeti.

Waziri Kigwangalla alisikitishwa na kitendo hicho ambacho alikielezea kuwa sio cha kiuungwana kwa kuwa kinalenga kudhoofisha juhudi za Serikali kumaliza mgogoro huo kwa faida ya pande zote.

"Mimi ni Muislam, nimesikia kwa masikio yangu na wala sijaambiwa na mtu yeyote na siwezi kumsingizia mtu, nimeshangazwa sana na kiongozi tena mtendaji wa chama tawala anawezaje kuitukana Serikali, na hapa sisi tumekuja kuwahudumia wananchi" alisema Dk. Kigwangalla kwa masikitiko makubwa.

Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa wananchi wote waliovamia ndani ya Hifadhi ya Serengeti na eneo la wazi (buffer zone) ambao wanaendesha shughuli zao ikiwemo kilimo, ufugaji na makazi kuachia maeneo hayo kwa hiari yao wenyewe, na kwamba muda huo ukipita wataondolewa kwa nguvu na chochote kitakachokutwa ndani ya eneo hilo kitatekezwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumzia kuhusu suluhu ya mgogoro huo wa mpaka amesema, Serikali itaunda timu ya wataalam kutoka wizarani kwake, wizara ya ardhi, uongozi wa mkoa wa Mara na wilaya ya Tarime ambao watashirikiana na watu wengine huru watakaochaguliwa na wananchi wa vjiji husika wakiongozwa na mbunge wao, John Heche ambao watakuwa na uelewa wa kusoma ramani na kutafsiri mipaka ili kushirikiana kuhakiki mipaka halisi ya eneo hilo na kufikia muafaka.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kushoto) na viongozi wengine wa mkoa huo wakiangalia mawe yaliyowekwa njiani kuzuia msafara wake kutoka ndani hifadhi ya Serengeti na watu wasiojulikana wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi hiyo na vijiji jirani jana usiku.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake  ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge wa Tarime John Heche wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa eneo lenye mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro huo mkoani Mara jana. Katikati aliyeinama ni Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake  ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake  ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisoma taarifa mbalimbali kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani vya wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wakati wa ziara yake  ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya vijiji na hifadhi hiyo jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche.

Sunday, July 15, 2018

DK. KIGWANGALLA AAGIZA MBINU HII MPYA ITUMIKE KUDHIBITI TEMBO WAHARIBIFU BUNDA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akijibu kero mbalimbali za wananchi katika kijiji cha Mariwanda kata ya Hunyari wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Lydia Bupilipili na Mbunge wa Bunda Vijijini, Bonafasi Mwita Getere (kulia). 

Na Hamza Temba, Bunda, Mara
.........................................................................

Kilio cha muda mrefu cha wananchi wa wilaya ya Bunda hususan katika ukanda unaopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuhusu wanyamapori waharibifu jamii ya Tembo kuvamia makazi yao na  mashamba kinaelekea kupata ufumbuzi wa kudumu.
Hatua hiyo inakuja kufuatia agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuanzisha mradi wa ufugaji nyuki kwa vijiji kumi vinavyopakana na hifadhi hiyo ili watumike kama uzio wa kudhibiti wanyamapori hao.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mariwanda, kata ya Hunyari wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani humo. 
"TANAPA wakishirikiana na TFS waje waanzishe mradi wa ufugaji nyuki wa kisasa katika vijiji vyote 10 vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa Serengeti, waje wahamasishe uundwaji wa vikundi, wafundishe namna ya kuweka mizinga ya kisasa na namna ya kufuga nyuki na kuvuna, na mwisho wa siku wananchi wapate faida ya kuzuia wanyamapori kuvamia mashamba na makazi yao pamoja na kuvuna asali itakayowatengenezea kipato mbadala" ameagiza Dk. Kigwangalla. 
Akielezea mbinu hiyo mpya inavyofanya kazi Dk. Kigwangalla amesema, wataalamu ndani ya wizara yake wameeleza kuwa mbinu hiyo ya kuweka mizinga ya nyuki kuzunguka maeneo ya mashamba na makazi ya wananchi itasaidia kudhibiti Tembo  kwakuwa huogopa sana nyuki na endapo wakisikia tu harufu yake huwa vigumu kusogelea maeneo hayo.
Awali akiwasilisha malalamiko kwa niaba ya wananchi wa vijiji hivyo, Mbunge wa Bunda Vijijini, Bonifasi Mwita Getere alisema kwa muda mrefu sasa wananchi hao wamekuwa wakipata madhara ya kuvamiwa na Tembo ambao hula mazao yao mashambani na hata majumbani, kuwajeruhi wananchi na wengine kupoteza kabisa maisha.
Baraka Abdul ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mariwanda wilayni humo alisema, mbinu zinazotumika kufukuza Tembo hivi sasa ikiwemo kupiga makelele na madebe na kutumia tochi za mwanga mkali zimekua hazisaidii, hivyo ameiomba Serikali kuongeza idadi ya askari na vituo katika maeneo yanayoathirika zaidi na matukio hayo.
Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ametoa onyo kali kwa wananchi wanaofanya vitendo vya ujangili na uingizaji mifugo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuwataka kuacha mara moja kwakuwa wakikamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kutaifishwa mifugo yao kwa mijibu wa kifungu cha 111 Na. 5 cha Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 2009.
Katika hatua nyingine, ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kupitia eneo la mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Bufer Zone) kuanzia Ghuba ya Speke hadi kwenye mpaka na nchi ya Kenya, wabaini mipaka halisi na ramani na kuainisha mahitaji ya wananchi na changamoto zilizopo na hatimaye kuwasilisha kwake mapendekezo ya kuondoa changamoto zilizopo.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na uongozi wa wilaya ya Bunda alipowasili wilayani hapo jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza uongozi wa wilaya ya Bunda ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Lydia Bupilipili (kulia kwake) wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kutatua changamoto za uhifadhi wilayani humo jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kata Nyatwali wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za uhifadhi katika wilaya ya Bunda mkoani Mara jana. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Martin Loibooki na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili (wa pili kulia). 
Mwananchi wa kata Nyantwali akitoa maoni yake kwa Waziri Kigwangalla.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bukore wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za uhifadhi katika wilaya ya Bunda mkoani Mara jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini, Bonifasi Mwita Getere muda mfupi baada ya kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Bukore wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za uhifadhi katika wilaya ya Bunda mkoani Mara jana.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mariwanda  wakati ziara ya Waziri Kigwangalla wilayani humo.
Baraka Abdul, mkazi wa kijiji cha Mariwanda akiwasilisha maoni yake kwa waziri Kigwangalla katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.
Dk. Kigwangalla akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mariwanda.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akijibu akifafanua jambo katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Mariwanda kata ya Hunyari wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dk. James Wakibara akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mariwanda wakimasikiliza Waziri Kigwangalla (hayuko pichani) wakati wa mkutano wa hadhara kijijini hapo.