NAIBU
WAZIRI MHE.KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA
TOZO BILA SHURUTI
NA
LUSUNGU HELELA-MWANZA
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu amewataka wananchi
wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani ya Hifadhi ya misitu ya Visiwa vya Kome
na Maisome vilivyoko wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza kulipa tozo za
serikali bila kulazimishwa.
Kauli
hiyo ameitoa wakati alipokuwa
akizungumza na wakazi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Shigala ulioko Kome Mchangani ambayo
ni kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili
wananchi wa maeneo hayo.
Mbunge
wa Jimbo la Buchosa Dkt. Charles Tizeba amemueleza Naibu Waziri hiyo kuwa kumekuwepo na
changamoto ya ulipaji tozo kubwa hata
kama mtu ana eneo dogo na ndipo wananchi walilazimika kugoma kulipa tozo hiyo
kwa lengo la kupata msaada zaidi.
Amefafanua
kuwa mtu anayemiliki hekari moja
anatakiwa kulipa Tsh.425,000 kwa mwaka lakini hata mtu anayemikili eneo
dogo la mita 20 naye anatakiwa kulipa kama wa hekari moja kitendo kilichowafanya wananchi hao kushindwa
kulipa na kusubili maelekezo ya wizara husika.
Mmoja
wa wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi hiyo,Juma Ramadhani amemwomba Naibu
Waziri kuangalia upya sheria hiyo ili wananchi wapate nafuu ya kulipa na
serikali iweze kupata mapato yake.
Kaimu
Meneja wa TFS Kanda ya Ziwa, Thomas Moshi amesema kuwa tozo hizo zipo kwa
mujibu wa sheria kinachotakiwa ni wananchi kulipa na siyo kugomea kulipa tozo
hizo na wanapofanya hivyo wanakwenda kinyume na matakwa ya sheria ya hifadhi ya
misitu.
Kanyasu
amewahakikishia wananchi hao kuwa suala hilo atalipatia majibu kwa haraka
lakini amewataka watu wanaomiliki hekari moja
kulipa tozo hizo kwa wakati na wale wenye maeneo madogo madogo wajiunge
katika vikundi ili waweze kuilipa pesa hiyo
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji
mali ndani ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa
cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya
Uvuvi iliyopo wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza wakinyoosha mikono ikiwa ni
ishara ya kukubali kuwa watalipa tozo za serikali bila kulazimishwa alipofanya
ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Dkt. Charles
Tizeba akizungumza na wananchi wa Jimboni kwake
kwenye mkutano wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine
Kanyasu wa kutatua kero za wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi
iliyopo wilayani Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara
uliofanya Kome Mchangani
Mwenyekiti wa Kijiji cha Buhama kata ya Buhama,
Thomas Sabuni, akizungumza na wananchi
kwenye mkutano wa hadhara kabala ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ikiwa
lengo kutatua kero za wananchi
wa Kisiwa hicho wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa
hadhara uliofanya katika eneo la Kome
mchangani
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na
baadhi ya viongozi wa kijiji cha Buhama
wakati alipowasili katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wvuvi kwa
ajili ya kutatua kero zinazowakabili
wananchi wa maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment