slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Monday, May 30, 2016

BAJETI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII (2016/2017) YAPITISHWA NA BUNGE

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 25 Mei, 2016 limekubali kupitisha bajeti ya Wizara ya Maliasili ikiwa na makadirio ya mapato na matumizi ya jumla ya Sh. 135,797,787,000 kwa mwaka 2016/2017. Kati ya fedha hizo, Sh. 118,051,105,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Sh. 17,746,682,000 ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Fedha za Matumizi ya Kawaida zinajumuisha Sh. 59,592,676,000 za Mishahara ya watumishi na Sh.58,458,429,000 za Matumizi Mengineyo. Fedha za Miradi ya Maendeleo zinajumuisha Sh. 15,746,682,000 fedha za nje na Sh.2,000,000,000 fedha za ndani. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (Mb) akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kuwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara (2016/2017) katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 24-25 Mei, 2016.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (Mb) na Naibu Waziri, Eng. Ramo Makani (Mb) wakipongezwa na baadhi ya wabunge ndani ya ukumbi wa bunge baada ya kujibu hoja mbalimbali na kufanikisha kupitishwa kwa bajeti ya Wizara.

Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (Mb), Naibu Waziri, Eng. Ramo Makani (Mb), Katibu Mkuu, Maj. Gen. Gaudence Milanzi, Naibu Katibu Mkuu, Angelina Madete, Vingozi wa Idara na Vitengo pamoja na Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Wizara hiyo muda mfupi baada ya Bajeti ya Wizara kupitishwa na Bunge tarehe 25 Mei, 2016 nje ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma.

Wednesday, May 18, 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MAJ. GEN. GAUDENCE MILANZI AONGOZA MKUTANO WA 23 CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA HIYO

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati),  Naibu Katibu Mkuu Angelina Madete (kulia) na Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii Wilfred Msemo (kushoto) wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jana tarehe 17 Mei, 2016 katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, tawi la Bustani, Jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza wakati akifungua Mkutano wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Jijini Dar es Salaam. 

Katika salamu zake amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuhakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao katika kutekeleza lengo kuu la Wizara ambalo ni kuendeleza uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Kukuza Utalii nchini. 

Amewataka watumishi wote wa Wizara kuwa waadilifu, wabunifu, kufanya kazi kwa ushirikiano, kuepuka vitendo vya rushwa na makundi yasiyokuwa na tija kwa Wizara na Serikali kwa ujumla. 

Alionya kuwa, Mtumishi yeyote atakeenda kinyume cha sheria na taratibu hatosita kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kuachishwa kazi ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano ya "HAPA KAZI TU"

Maj. Gen. Milanzi alimuwakilisha Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ambaye yupo Mkoani Dodoma kwa ajili ya majukumu mengine ya Kiserikali (Bunge la bajeti).
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii wakiimba wimbo wa kuashiria umoja wa wafanyakazi (Solidarity Forever). 
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo wakiimba wimbo wa umoja wa wafanyakazi "Solidarity Forever"