slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Friday, September 29, 2017

PROF. MAGHEMBE ATOA WITO KWA WANANCHI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA VITA DHIDI YA UJANGILI

Na Hamza Temba-WMU
...............................................................
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe jana tarehe 29 Septemba, 2017 amefungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na Serikali katika kupambana na Majangili kwa kutoa taarifa za siri zitakazoweza kuwaibaini na kuchukuliwa hatua.

“Ili kulinda uwepo wa rasilimali za utalii zilizopo kwa vizazi vya sasa na vijavyo, ni lazima wananchi kushirikiana pamoja na Serikali katika mapambano dhidi ya ujangili, mkiona mtu ananyemeleanyemelea huko porini tuambieni tutamshukia kama mwewe, hizi rasilimali na zetu sote” alisisitiza Prof. Maghembe.

Alisema changamoto ya ujangili bado ipo katika baadhi ya maeneo hapa nchini, alitaja maeneo hayo kuwa ni upande wa Pori la Rugwa na Selous karibu na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo watu huingiza mifugo hifadhini kwa kisingizio cha kutafuta malisho wakati huo huo wakifanya uhalifu wa kuua tembo.

Prof. Maghembe alifungua maadhimisho hayo pamoja na Maonesho ya Karibu Kusini na maonesho ya wajasiariamali wa viwanda vidogo SIDO yaliyoshirikisha wajasirimali kutoka mikoa ya nyanda zajuu kusini kwa lengo la kuonesha bidhaa zao zitakazoweza kutumiwa na watalii pamoja na watoa huduma hiyo. 

Akifungua maadhimisho hayo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Prof. Maghembe alisema, kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu kwa upande wa Siku ya Utalii Duniani ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo wakati ile ya Maonesho ya Karibu Kusini ikiwa ni “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.

Alisema sekta ya utalii imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi kwa kuchangia asilimia kubwa ya mapato ya Serikali, kuongeza ajira, kipato cha jamii na kuchochea ukuaji wa sekta zingine. 

"Utalii ndio ndio sekta pekee inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha za kigeni kwa asilimia 25, Aidha, inachangia asilimia 17.5 ya pato la taifa na asilimia 11 ya ajira zote nchini" alisema prof. Maghembe. 

Alisema mapato yanayotokana na utalii yameongezeka kutoka Dola za Kimarekani milioni 1,353.29 mwaka 2011 hadi Dola za Kimarekani milioni 2,131.57 mwaka 2016.

Alisema mchango huo umechagizwa na ongezeko la watalii kutoka nje ya nchi ambao waliongezeka kutoka 867,994 mwaka 2011 na kufikia 1,284,279 mwaka 2016.

Hata hivyo, alisema mafanikio hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na juhudi za Serikali katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali, utangazaji, mazingira bora ya uwekezaji na ushirikiano madhubuti baina ya sekta ya umma na binafsi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani alisema Serikali imekusudua kuhakikisha kuwa utalii wa nyanda za juu kusini unakua juu zaidi uweze kutoa mchango stahiki kwenye pato la taifa. Alitoa wito kwa wananchi kutunza vivutio vya utalii vilivyopo, kuhifadhi mazingira na kupiga vita ujangili.

"Kwa upande wa sekta binafsi na wananchi kwa ujumla natoa witoe washirikiane na Serikali kuweka mazingira bora na ya kuvutia katika maeneo yenye vivutio  vya utalii ikiwemo hoteli za kisasa kwa ajili kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi kutembelea vivutia hivyo" alisema Mhandisi Makani.

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina masenza alisema katika kuunga mkono azma ya Serikali ya kukuza na kufungua utalii wa Nyanda za Juu Kusini Serikali ya mkoa wake kwa kushirikiana na wadau wa utalii wameandaa Mpango Makakati wa kukuza sekta hiyo mkoani humo. Mpango huo umezinduliwa jana na Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe.

Kila mwaka nchi wanachama wa Shirika la Utalii Duniani huadhimisha Siku ya Utalii tarehe 27 Septemba kwa lengo la kuhanasisha umuhimu wa sekta hiyo katika kuleta maendeleo ya jamii, utamaduni, kukuza demokrasia, kutunza na kuhifadhi mazingira, kujenga uchumi na kuimarisha mahusiano ya kitaifa na kimataifa. Kilele cha Maadhimisho ni siku ya jumanne tarehe 2 Oktoba, 2017.
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (katikati),  Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) wakiimba wimbo wa Taifa katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe, akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 2, Oktoba. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani akizungumza katika maadhimisho hayo mkoani Iringa jana.
Mkuu wa Wilaya ya Iirnga, Richard Kasesela akiratibu shughuli nzima ya maadhimisho hayo.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mkakati wa Utalii wa Mkoa wa Iringa ambao umeandaliwa kwa lengo kuunga mkono azma ya Serikali wa kufungua utalii wa Nyanda za Juu Kusini katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Amina Masenza na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto), Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wa Serikali wakionesha Mkakati wa Utalii na Jarida la Iringa baada ya uzinduzi rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga akiwa na baadhi ya washiriki wengine kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo.
 Baadhi ya Machifu wa Iringa waliohudhuria ufunguzi wa maadhimisho hayo.
 Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatila ufungunguzi wake.
Sehemu ya washiriki wa maadhimisho hayo ya Wiki ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini. Nyuma yao ni mabanda ya maonesho hayo.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakielekea kukagua mabanda ya maonesho katika viwanja vya Kichangani Mkoani Iringa jana.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akipimwa afya katika banda la MSD wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. KKauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni  “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto), akikagua bidhaa za wajasiriamali wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa pili kushoto). 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza moja ya bidhaa za wajasiriamali wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatu kulia). Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), akikagua kifaa maalum cha kuwashia umeme katika banda la VETA wakati wa zoezi la kukagua mabanda kwenye Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (kushoto). 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto),  Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia kwake) wakipata maelezo katika banda la Sido kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini yanayoendelea Mkoani Iringa.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), akikagua gari maalum kwa ajili ya mafunzo katika banda la VETA wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Wanaoshuhudia pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatno kulia). 
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kulia kwake) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza wakikagua vifaa vya mfumo wa umwagiliaji vilivyotengenezwa na VETA katika maadhimisho hayo.
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), akisalimiana na Machifu wa Kabila la Wahehe katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akionesha picha za nyayo za Zamadamu wa Laetoli na Engaresero zilizogundulika Ngorongoro mkoani Arusha takribani miaka milioni 3.6 iliyopita kufuatia tafiti mbalimbali zilizofanyika kwa muda mrefu.
Katika maadhimisho hayo kuna fursa za kuwaona wanyamaori mbalimbali ikiwemo Simba kama wanavyoonekana kwenye banda lao maalum. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)

Thursday, September 28, 2017

PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA NCHI 21 DUNIANI KUJADILI UKUKUZAJI WA SEKTA YA UPANDAJI WA MITI KIBIASHARA

Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. Aliwataka wajumbe hao kujadili namna ya kuwawezesha wakulima wa miti wakati wanasubiri kuvuna mazao yao waweze kujishuulisha na kilimo cha mazao ya muda mfupi kwa kutumia mbinu bora za kisayansi ili waweze kujikimu kimapato.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
Baadhi ya wajumbe kutoka nchi 21 duniani wakifuatilia mkutano huo. Nchi hizo ni Burkina Faso, Chad, Ethiopia, Gambia,Ghana, Italy, Mali, Niger, Nigeria, Senegal, Sudan, Liberia, Cameroon, Swaziland, Finland, Zambia, Canada,Mozambique, Zimbabwe, Kenya na Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Steven Kebwe akizungumza katika mkutano huo. Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili na kuishauri dunia namna bora ya kutunza na kuendeleza misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho ikiwemo utekelezaji wa sheria za usimamizi wa misitu.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wajumbe kujadili kwa uwazi kuhusu mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto za sekta ya misitu na kwamba Serikali kupitia Wizara itapokea maoni na mapendekezo yao kwa ajili ya kuyafanyia kazi ili kuimarisha ustawi wa sekta hiyo. 
Waziri Maghembe akieleza jambo kwenye ka mkutano huo ambapo aliwataka wajumbe wajumbe wajadili namna bora ya kuwafundisha wakulima wa miti kufanya kilimo bora ikiwa ni pamoja na mafunzo uvunaji wa hewa ukaa ili kuwainua kimapato. Aliwataka pia kusaidia wakulima wa miti katika upatikanaji wa masoko ya uhakika.
  Prof. Maghembe akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana na baadhi ya viongozi waliondaa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika muda mfupi kabla ya kufungua mkutano huo wa siku mbili uliowashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
  Baadhi ya wajumbe walishiriki mkutano huo kutoka nchi 21 duniani.
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza na Mbunge kutoka Kenya, Chariti Katambi mkoani Morogoro jana baada ya kufungua mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro jana baada ya kufungua mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
Picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.

MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KUZINDUA MAKUMBUSHO MAPYA YA OLDUVAI NA ONESHO LA CHIMBUKO LA MWANADAMU TAREHE 03 OKTOBA, 2017 MKOANI ARUSHA

Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani Morogoro kuhusu uzinduzi wa Makumbusho Mapya ya Olduvai na Onesho la Chimbuko la Mwanadamu ambayo yatazinduliwa tarehe 03 Oktoba, 2017 na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Olduvai wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. 
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani Morogoro kuhusu uzinduzi wa Makumbusho Mapya ya Olduvai na Onesho la Chimbuko la Mwanadamu ambayo yatazinduliwa tarehe 03 Oktoba, 2017 na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Olduvai wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. (Picha na Hamza Temba - WMU)

Morogoro, Septemba 28, 2017
.........................................................................
Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya imekamilisha ujenzi wa Makumbusho mapya ya Olduvai ambayo yanaonesha Chimbuko la Binadamu (The Cradle of Humankind) katika Bara la Afrika.
Makumbusho hayo mapya pamoja na Onesho la Chimbuko la Binadamu, yatafunguliwa rasmi na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tarehe 03 Oktoba, 2017 katika eneo la Olduvai, ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Onesho hilo ni matokeo ya utafiti wa muda mrefu uliofanyika katika Bonde la Olduvai na Laetoli katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. Wananchi, viongozi mbalimbali wa kitaifa na Mabalozi wanatarajiwa kuhudhuria kwenye hafla hiyo.
Idadi kubwa ya vioneshwa katika Makumbusho hiyo, vilipatikana katika bonde la Olduvai na Laetoli nchini Tanzania kupitia utafiti wa kisayansi wa muda mrefu na vilikuwa vimehifadhiwa katika Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam. Vioneshwa hivi ni pamoja na masalia ya zamadamu, zana za mawe na masalia ya wanyama walioishi takribani miaka milioni 4 iliyopita.
Makumbusho hayo yamepangwa kuonesha sehemu kuu nne zinazowiana.  Sehemu ya kwanza inahusu ushahidi wa nyayo za zamadamu zilizongunduliwa huko Laetoli mwaka 1978 na mtafiti Dr. Mary D. Leakey.  Nyayo hizi ziliachwa na zamadamu anayeiitwa Australopithecus afarensis na ndio ushaidi usiopingika wa zamadamu kutembea wima kwa miguu miwili takribani miaka milioni 3.6 iliyopita.
Sehemu ya pili inahusu hadithi ya kusisimua ya kuwa binadamu (Genus Homo); ambapo kutakuwa na masalia ya zamadamu wanaoitwa Zinjanthropus au Paranthropus boisei na Homo habilis, zana za mawe za mwanzo zilizotumika (Oldowan) katika kujipatia chakula na ushahidi wa kale wa ulaji wa nyama katika historia ya mabadiliko ya binadamu, takribani miaka million 2 iliyopita.
Sehemu ya tatu inahusu maisha ya jamii ya Homo erectus.  Jamii hii ilikuwa inafanana zaidi na binadamu wa sasa kuliko jamii zilizotangulia. Kutakuwa na masalia zamadamu Homo erectus, zana za mawe (Acheulian) na ushahidi wa ulaji wa wanyama wakubwa kama vile Nyati na tembo katika historia ya mabadiliko ya binadamu, takribani miaka million 1.7 iliyopita.
Sehemu ya nne inaonesha kipindi cha mwanzo cha binadamu wa sasa (Homo sapiens) walioanza kutokea hapa Afrika miaka laki 2 iliyopita. Sehemu hii pia itaonesha mila na utamaduni wa makabila mbalimbali kama vile Wahadzabe, wamasai na Datoga.  Kutakuwa na mavazi ya asili ya jamii hizo, zana za kuwinda na vifaa mbalimbali wanavyovitumia katika maisha yao ya kila siku.
Wizara ya Maliasili na Utalii inawakaribisha wananchi wote kuhudhuria ufunguzi huo ambapo watapata pia fursa ya kutembelea vivutio vingine vilivyopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kujifunza na kufurahia urithi huu wa asili na kiutamaduni wa Taifa letu.
Imetolewa na;

Prof. Jumanne Maghembe
Waziri wa Maliasili na Utalii

Wednesday, September 27, 2017

PROF. MAGHEMBE AONGOZA MAADHIMISHO YA 87 YA SIKU YA TAIFA LA SAUDI ARABIA JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa la Kifalme la Saudi Arabia yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Prof. Maghembe alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kulia ni Balozi wa taifa hilo nchini Tanzania, Balozi Mohammed Bin Mansour Al Malik.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik (wa pili kulia) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakijiandaa kukata keki ya maadhimisho hayo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik (katikati) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakikata keki ya maadhimisho hayo.

Baadhi ya watoto wa Taifa la Kifalme la Saudi Arabia wakiinua bendera ya nchi hiyo kuashiria maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa hilo yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

Tuesday, September 19, 2017

CHUO CHA MISITU OLMOTONYI CHATAKIWA KUJIIMARISHA KITAALUMA - PROF. MAGHEMBE


Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimpa maelekezo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel (kushoto) ambayo inajenga mradi wa bweni na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Misitu Olmotonyi alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe kumaliza ujenzi wa mradi huo.

Na Hamza Temba - WMU
.................................................................
Chuo cha Misitu Olmotonyi kilichopo mkoani Arusha kimetakiwa kuboresha taaluma na mitaala ya kufundishia iweze kukidhi mahitaji ya jamii ya sasa na ijayo ikiwemo kujibu kero na changamoto zinazoikabili jamii hiyo.


Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipotembelea chuo hicho jana kwa ajili kukagua maendeleo yake na kuzungumza na waalimu pamoja na wafanyakazi ambapo pia alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayojengwa chuoni hapo ikiwemo ya bweni na ukumbi wa mihadhara.


Alisema Tanzania ya leo inahitaji wataalamu watakaojibu kero na kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya uhifadhi nchini ikiwemo ya uharibifu wa misitu kwa njia ya uchomaji wa mkaa, uvunaji haramu wa magogo na vitendo vya uingizaji wa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi nchini. 

"Ni lazima muwafundishe wanafunzi wenu uaminifu na uzalendo wa kutumia rasilimali za misitu kwa njia endelevu, muwafundishe uhifadhi zaidi na sio uvunaji pamoja kutumia sheria ipasavyo katika kulinda na kusimamia rasilimali hizi huku wakitambua kuwa rasilimali hizo zikitoweka hakuna maisha kutokana na umuhimu wake katika maisha ya binadamu" alisema Prof. Maghembe.

Pamoja na hayo, alikitaka chuo hicho kujiimarisha zaidi katika mafunzo kwa vitendo kufikia viwango bora vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na kuendeleza waalimu kitaaluma kwa kutumia fursa mbalimbali ikiwemo za mafunzo ya nje ya nchi kwa mfumo wa "Scholarships". 

Aidha, alikitaka pia chuo hicho kujikita zaidi katika utoaji wa huduma kwa jamii katika sekta ya misitu pamoja na kuanzisha na kuimarisha programu mbalimbali za utafiti ambazo pamoja na faida nyingine pia zitakitangaza chuo hicho ndani na nje ya nchi.

Katika hatua nyingine, Prof. Maghembe amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel kukamilisha haraka ujenzi unaoendelea wa jengo la bweni na ukumbi wa mihadhara chuoni hapo. Ujenzi huo upo chini ya mradi wa ECOPRC na jengo la bweni litakua na uwezo wa kuchukua wanafunzi 100 na ukumbi wa mihadhara wanafunzi 200. 

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Christognus Haule alisema, chuo hicho kinatoa mafunzo ya misitu na hifadhi ya mazingira kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada pamoja na mafunzo ya muda mfupi. Pia kinatoa huduma za ushauri na utafiti wa misitu na hifadhi ya mazingira.

Akizungumzia udahili wa wanafunzi chuoni hapo alisema umekua ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo katika mwaka wa fedha 2015/2016 idadi hiyo imeongezeka kutoka 499 na kufikia 595 mwaka 2016/2017. Alisema kwa mwaka ujao 2017/2018 wanategemea kupata wanafunzi wengi zaidi kufikia 650.

Chuo cha Misitu Olmotonyi ni chuo cha Serikali ambacho kilianzishwa mwaka 1937 na kinasimamiwa na Wizara ya Maliasili kwa ajili ya kutoa mafunzo ya misitu na hifadhi ya mazingira. Chuo hicho kwa sasa kina waalimu 21 wa ngazi tofauti.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel ambayo inajenga jengo la bweni na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Misitu Olmotonyi kuhusu maendeleo ya mradi huo alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe kumaliza ujenzi wa mradi huo. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Chuo cha Misitu Olmotonyi  Mkoani Arusha jana ambapo alitoa maelekezo mbalimbali na ushauri wa kuboresha chuo hicho. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Christognus Haule. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi Mkoani Arusha alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo jana ambapo alitoa maelekezo na ushauri wa namna ya kuboresha chuo hicho. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na waalimu na wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi mkoani Arusha jana . Kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Christognus Haule.

Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia waliokaa) na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi.

 Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia waliokaa) na baadhi ya waalimu wa Chuo cha Misitu Olmotonyi.
Ujenzi bweni la wanafunzi chuoni hapo ukiwa unaendelea chini ya mradi wa ECOPRC. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel (kulia) ambayo inajenga jengo la bweni na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Misitu Olmotonyi kuhusu maendeleo ya mradi huo alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe kumaliza ujenzi wa mradi huo.
Jengo la vukumbi wa mihadhara  (Lecture Theatre) ambalo linaendelea kujengwa chuoni hapo kupitia mradi mradi wa ECOPRC.


Baadhi ya waalimu na wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi wakisikiliza maelekezo mbalimbali kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (hayupo pichani) alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha.