Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi
Ramo Makani (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii wakati wa ziara yao ya kikazi katika eneo la Jumuiya
ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wami Mbiki/Ushoroba mkoani Morogoro ambayo iliyolenga
kubaini changamoto mbalimbali za uhifadhi kwa ajili ya kuishauri Serikali namna
bora ya kukabiliana nazo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii wakimsikiliza Afisa Wanyamapori Mkuu wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Leonard Mayeta (wa nne kulia) wakati
akitoa maelezo kuhusu Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wami Mbiki/Ushoroba
wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye hifadhi hiyo ambayo ililenga kubaini changamoto
mbalimbali za uhifadhi kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana
nazo.
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara na Utalii wa
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi akiwasilisha
taarifa ya mamlaka hiyo kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Dkt. James Wakibara
mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii baada ya kutembelea eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wami Mbiki mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi
Ramo Makani (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),
Prof. Dos Santos Silayo (wa tatu kulia) wakiongoza Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kupanda mlima katika Hifadhi ya
Mazingira Asilia Uluguru mkoani Morogoro wakati wa ziara yao iliyolenga kubaini changamoto
mbalimbali za uhifadhi kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana
nazo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akizungumza na Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati wa ziara yao ya
kikazi katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru mkoani.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia
Uluguru, Cathbert Mafupa (kushoto) akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu Hifadhi hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Utalii, Mary Chatanda (wa tatu kushoto) akizungumza kutaka
ufafanuzi wa baadhi ya mambo kuhusu Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru wakati
wa ziara ya kamati kwenye hifadhi hiyo. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo
Makani (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa
nne kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu, Prof. Dos Santos
Silayo (wa pili kulia).
Wajumbe wa Kamati wakikagua eneo la Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru mkoani Morogoro wakati wa ziara yao ya kikazi ya kuangalia changamoto mbalimbali za uhifadhi zinazoikabili hifadhi hiyo kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana nazo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akiongoza Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kutembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia
Uluguru.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na
Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) na Wajumbe wa Kamati hiyo wakitembelea eneo la Hifadhi ya Mazingira Asilia
Uluguru.
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mtango Mtahiko (kulia) ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo kwenye ziara hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) akiwasilisha taarifa ya
taasisi hiyo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii baada
ya kutembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru mkoani Morogoro jana wakati
wa ziara ya kamati hiyo iliyolenda kubaini changamoto mbalimbali za uhifadhi katika
hifadhi hiyo kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana nazo.
No comments:
Post a Comment