slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Tuesday, August 29, 2017

PROF. MAGHEMBE ATEMBELEA OFISI ZA KIKOSI DHIDI YA UJANGILI KANDA YA KASKAZINI NA CITES JIJINI ARUSHA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimsikiliza Afisa Wanyamapori Mwandamizi, Segolin Tarimo alipotembelea ofisi za CITES Jijini Arusha jana.
Waziri wa Maliasili, Prof. Maghembe akizungumza na uongozi wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) alipotembelea na kuona shughuli za kikosi hicho Jijini Arusha jana.
Baadhi ya viongozi wakuu wa KDU Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Mhe. Waziri, Prof. Jumanne Maghembe (hayupo pichani). 
Baadhi ya watumishi wa KDU Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Waziri, Prof. Jumanne Maghembe alipotembelea ofisi zao jana mkoani Arusha.
Mkutano ukiendelea jana katika ofisi za KDU Kanda ya Kaskazini kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii ,Prof. Jumanne Maghembe na watumishi kikosi hicho.

Thursday, August 24, 2017

TANGAZO.............


NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI, DKT. ALOYCE NZUKI AFUNGUA WARSHA YA KUKUSANYA MAONI YA WADAU WA KANDA YA KATI KWA AJILI YA KUPITIA UPYA SERA YA TAIFA YA UTALII YA MWAKA 1999 MJINI DODOMA

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania mjini Dodoma leo. 

Dkt. Nzuki amesema ipo haja sasa kwa Sekta za Umma kuona umuhimu wa kuwekeza moja kwa moja katika biashara ya utalii nchini hususani katika huduma za malazi na usafiri ili kuiwezesha Serikali kupata mapato ya moja kwa moja na kuongeza zaidi kwenye pato la taifa. 

Alisema kwa kuimarisha usafiri wa anga kutawezesha usafiri wa watalii moja kwa moja kutoka kwenye soko na kuwaleta nchini huku wakilipia gharama zote hapa nchini tofauti na hivi sasa ambapo baadhi ya makampuni ya nje hulipwa fedha kiasi nje ya nchi na hivyo kuikosesha Serikali mapato kupitia ushuru unaotozwa na TRA. 

Alisema sio lazima Serikali iwe inasimamia moja kwa moja utoaji wa huduma hizo kwa kuwa upo uwezekano wa kutumia makampuni makubwa hata ya nje ya nchi kuja kuendesha huduma hizo kwa ufanisi zaidi hapa nchini.  
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) na wadau wengine wa sekta ya utalii wakimsikiliza Prof. Raphael Mwalyosi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kulia) wakati akiwasilisha mada kuhusu Hoja ya Marekebisho ya Sera ya Utalii ya Mwaka 1999 katika warsha ya kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya kupitia upya Sera hiyo iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania mjini Dodoma leo.
Kamu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deograsias Mdamu akizungumza katika warsha ya siku moja ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania mjini Dodoma leo. 
Picha ya pamoja ya Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (katikati waliokaa) na wadau wa sekta ya utalii katika warsha ya siku moja ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania mjini Dodoma leo.
Baadhi ya wadau wa sekta ya utalii wakisikiliza moja ya mada katika warsha ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta hiyo kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania mjini Dodoma leo. 
 Baadhi ya wawezeshaji wa hafla hiyo ambao ni Maafisa Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakisikiliza moja ya mada katika warsha hiyo. 
Baadhi ya wadau wa warsha hiyo wakisikiliza hotuba ya ufunguzi ya Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki. 
 Baadhi ya wadau wa warsha hiyo.
Baadhi ya Washiriki wa warsha hiyo kutoka Mikoa ya Kanda ya Kati iliyofanyika mjini Dodoma. 
HOTUBA YA UFUNGUZI YA NAIBU KATIBU MKUU, WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, DKT. ALOYCE NZUKI

HOTUBA YA KAIMU MKURUGENZI IDARA YA UTALII, DEOGRASIAS MDAMU

Tuesday, August 22, 2017

ZIARA YA KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, MAJ. GEN. GAUDENCE MILANZI MKOANI RUVUMA

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akisalimiana na viongozi wa Kijiji cha Likuyu Sekamaganga alipotembelea Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii - Likuyu Semaganga mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto) akikagua bwalo la chakula la Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii - Likuyu Semaganga kilichopo Mkoani Ruvuma. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexandre Songorwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mhe. Luckness Amlima.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa tatu kulia) akikagua vitalu vya miche ya miti katika mradi wa Panda Miti Kibiashara unaosimamiwa na Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu akizungumza na Wahifadhi na Askari wa Wanyamapori wa Pori la Akiba la Liparamba, mkoani Ruvuma ambao walikuwa katika Kituo cha Doria cha Mpepai (Mpepai Game Post).
Katibu Mkuu (wa pili kulia) na Lt.Gen. Mstaafu Samwel Ndomba wakishuka kutoka moja ya Vivutio vya Utalii Ndani ya Bustani ya Wanyama ya Lugali, wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.

Thursday, August 17, 2017

TAARIFA KWA UMMA JUU YA ZOEZI LA KUONDOA MIFUGO NA MAKAZI NDANI YA HIFADHI YA TAIFA SERENGETI NA KWENYE MPAKA WA PORI TENGEFU LOLIONDO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TAARIFA KWA UMMA

ZOEZI LA KUONDOA MIFUGO NA MAKAZI NDANI YA HIFADHI YA TAIFA SERENGETI NA KWENYE MPAKA WA PORI TENGEFU LOLIONDO

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngorongoro, kwa kushirikisha Hifadhi ya Taifa Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, inaendesha zoezi la kuondoa mifugo na makazi ndani ya hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo.

Zoezi hilo lililoanza tarehe 10  Agosti 2017  litadumu kwa siku kumi na nne na linashirikisha Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ngorongoro, Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa Serengeti na Hifadhi ya eneo la Ngorongoro.

Zoezi hilo linalenga kunusuru uhifadhi ndani ya hifadhi, ndani ya Pori Tengefu Loliondo, na ndani ya mfumo ikolojia wa Serengeti na pia kunusuru utalii katika mfumo ikolojia huo.

Aidha, hatua hii ya kuondoa makazi na mifugo kutoka katika maeneo ya mipaka ya Pori Tengefu Loliondo kutaongeza uhakika wa kupatikana malisho ya mifugo wakati wa kiangazi kwa kuwa hakutakuwepo na makazi ndani ya Hifadhi na ufugaji holela.

kimsingi zoezi hili linaendana na wito wa Serikali wa kuondoa mifugo ndani ya maeneo yote yaliyohifadhiwa nchini.

Katika kutekeleza zoezi hili, Mkuu wa Wilaya  Ngorongoro, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ngorongoro Bwana Rashidi Taka, alitoa maelekezo yafuatayo:

1. Zoezi litafanyika ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo. Kwa upande wa mpaka wa Pori Tengefu Loliondo zoezi litaanzia kaskazini hadi kusini urefu wa kilometa 90, na upana wake utakuwa kilometa 5. Kwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti litafanyika upande wa mashariki kuanzia milima ya Kuka (kaskazini) hadi kigingi na. SNP 9 (kusini); 

2. Maboma yatakayokutwa ndani ya hifadhi yatateketezwa kwa moto na watu watakaokutwa na mifugo watachukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kupelekwa mahakamani;

3.  Maboma yaliyoko ndani ya mpaka wa Pori Tengefu Loliondo -  kwenye mpaka na ndani ya kilometa tano - wataondolewa ili warudi vijijini. Eneo hilo litabaki kwa ajili ya malisho na si kwa ajili ya makazi.  Uwepo wa makazi kwenye mpaka wa Hifadhi ya Taifa Serengeti umekuwa kichocheo kikubwa cha mifugo kuingizwa hifadhini.

Zoezi hili linalenga kuondoa changamoto kubwa ya mifugo kuingizwa Hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo, kupambana na uvamizi mkubwa uliofanywa na wahamiaji haramu kutoka nchi jirani na kunusuru vyanzo vya maji kutokana na mifugo kulishwa kwenye vyanzo vya maji na hivyo kusababisha vyanzo hivyo kuharibika na kukosekana kwa maji kwa ajili ya mifugo na wanyamapori.

Hadi sasa zoezi hili la kuondoa mifugo na makazi ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo linaendelea vizuri likihusisha kuchoma moto maboma yote yaliyoachwa na wafugaji walioondoka wakati wa zoezi.

Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuufahamisha umma kuwa hakuna watu wanaopigwa katika zoezi hili.

Pia, Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuutaarifu umma kuwa habari zinazosambazwa mitandaoni ni upotoshaji wa ukweli wenye nia ovu ya kujenga chuki dhidi ya Serikali  kwa wananchi wa Loliondo na maeneo yanayopitiwa na zoezi hilo.

Aidha, Wizara ya Maliasili na Utalii, inapenda kuweka bayana kuwa, taarifa za kupigwa risasi Pormoson Losso mwenye umri wa miaka 23, mkazi wa Ololosokwan zilitolewa tarehe 8 Agosti 2017 na hazihusiani na zoezi tajwa kwani tukio hilo  lilitokea siku tano kabla ya kuanza zoezi la kuondoa mifugo na makazi ndani ya hifadhi wakati zoezi hili lilianza kutekelezwa Jumapili tarehe 13 Agosti 2017.

Hata hivyo Serikali inawapongeza wananchi wengi miongoni mwa wafugaji kwa kuunga mkono zoezi hili na kwa ushirikiano wanaotoa.
Serikali inatoa onyo kwa yeyote anayejihusisha na upotoshaji wa ukweli kuhusu zoezi hili lenye nia njema linalolenga kunusuru hifadhi, kuacha mara moja ili kujiepusha na hatua za kisheria zitakazochukuliwa pindi atakapobainika.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

17/08/2017

Tuesday, August 15, 2017

ZIARA YA MANAIBU WAZIRI WATATU UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE NA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA

Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (wa nne kulia) na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Edwin Ngonyani (wa tano kulia) wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Uzingatiaji wa Viwango wa Mamlaka ya Viwanja wa Ndege, Paul Rwegosha wakati wa ziara yao ya pamoja ya kukagua maeneo ya kuingilia wageni wa kimataifa hususan watalii katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam kwa ajii ya kubaini changamoto na kuziboresha ikiwa ni pamoja na kuziba mianya ya mapato ya Serikali yanayotokana na watalii wanaoingia nchini.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akizungumza katika kituo cha "terminal III" cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam kinachoendelea kujengwa wakati wa ziara ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni (wa tatu kulia) na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) kwa ajili ya kukagua maeneo ya kuingilia wageni wa kimataifa hususan watalii katika uwanja huo kwa ajii ya kubaini changamoto na kuziboresha ikiwa ni pamoja na kuziba mianya ya mapato ya Serikali yanayotokana na watalii wanaoingia nchini.
 Mkuu wa Kitengo cha Uzingatiaji Viwango wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, Paul Rwegasha, akifafanua jambo wakati wa ziara iliyojumuisha  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani(kushoto), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wapili kushoto)  na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia).Lengo la ziara hiyo ni kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu,Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.
Meneja Huduma za Abiria wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Damas Temba, akielezea jinsi huduma ya kukagua mizigo inavyofanyika katika sehemu ya mizigo wakati wa ziara ya Manaibu Waziri, Mhandisi Hamad Masauni (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi), Mhandisi Ramo Makani(Wizara ya Maliasili na Utalii) na Mhandisi Edwin Ngonyani(Wizara ya UIjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano), ikiwa na lengo kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu, Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.
Meneja Mradi Ujenzi wa Uwanja Mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Ray Blumrick, akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kumaliza kutembelea ujenzi huo.Lengo la ziara hiyo ni kukagua kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu, Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.
Naibu Mkurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania, Lazaro Twange (katikati), akiwaonyesha ramani ya bandari ya Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani(kulia) na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ziara ya viongozi hao lengo ikiwa ni kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu, Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.
Naibu Mkurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania, Lazaro Twange,  akifafanua jambo kwa  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani(wapili kulia) na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (kulia), wakati wa ziara ya viongozi hao, lengo ikiwa ni kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu, Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Polisi Bandarini,Matanga Mbushi.

Friday, August 4, 2017

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, PROF. JUMANNE MAGHEMBE AFANYA MABADILIKO MADOGO YA UONGOZI KWA BAADHI YA IDARA NA TAASISI ZA WIZARA HIYO

Image may contain: text
Image may contain: text

MHANDISI MAKANI ASISITIZA UHIFADHI SHIRIKISHI WA MALIASILI ZA TAIFA

Niabu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mshiri wilayani Moshi ,alipotembelea kijiji hicho kusikiliza Changamoto zinazo wakabili hususani katika eneo la Nusu Maili lililopo chini ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Mkazi wa Kijiji cha Mshiri akiwaslisha hoja yake kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani.

NA HAMZA TEMBA -WMU
...............................................................................

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo makani amesema  jukumu la uhifadhi wa Maliasili za taifa sio la Serikali pekee kwakua Maliasili hizo ni urithi wa taifa na kila mwananchi anapaswa  kujua kuwa ana jukumu la kulinda urithi huo kutokana na umuhimu wake kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Makani amesema hayo juzi wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mshiri, Jimbo la Vunjo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo kwa ajili kuona changamoto za uhifadhi na kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.

Alisema askari pekee na mitutu ya bunduki haitoshi kulinda maliasili hizo kutokana na ukubwa wa maeneo yaliyopo ukilinganisha na rasilimali zilizopo. "Maliasili hizi zipo kwa faida ya kila mwananchi, tunawaomba muendelee kuiunga mkono Serikali katika kulinda Maliasili tulizonazo, tunahitaji kufanya uhifadhi shirikishi, utalii uimarike na nchi yetu ipate mapato zaidi tuweze kufikia uchumi wa kati", alisema Makani.

Akitaja miongoni mwa faida hizo, Makani alisema maliasili za misitu husaidia upatikanaji wa mvua, kuweka mazingira bora kwa ajili ya kilimo na upatikanaji wa hewa safi. Kwa upande wa faida za kiuchumi alisema sekta hiyo kupitia utalii inachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimi 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Betrita Loibooki alisema hifadhi hiyo imejenga mahusiano mazuri na wananchi wa vijiji jirani na kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kukabiliana na ujangili ambapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita hakuna tukio lolote la ujangili wa tembo lililoripotiwa katika hifadhi hiyo.

Betrita alisema katika kutekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la uwekaji wa vigingi vya mipaka kwenye maeneo ya hifadhi ili kuepuka migogoro na wananchi alisema jumla vigingi 290 vimewekwa kwa ushirikiano na wananchi kuzunguka hifadhi hiyo kwa urefu kwa kilomita 123 sawa na asilimia 100 ya lengo lililokusudiwa.


Kwa upande wa Wananchi wa kijiji hicho cha Mshiri ambacho kinapakana na Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro waliiomba Serikali iwalegezee masharti waweze kuingia na waume zao pamoja na vijana wao wa kiume katika eneo la Nusu Maili lililopo ndani ya hifadhi hiyo waweze kusaidiana kazi ya kukata majani ya mifugo na kuokota kuni.

Akitoa ombi hilo mbele ya Mhandisi Makani, mkazi wa kijiji hicho, Theresia Mtui alisema wanawake wa vijiji jirani na hifadhi hiyo wanaruhusiwa kuingia ndani ya eneo hilo kwa ajili ya kukata majani ya mifugo na kuokota kuni kavu lakini wanaume hawaruhusiwi.

Alisema wapo tayari kuhifadhi na kulinda mlima huo “Tunaomba mturuhusu na mtupe angalao miaka miwili au mitatu ya majaribio muone tutakavyolinda msitu huu”, alisema Mtui.

Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Estomi Benjamin Moshi alisema “Ombi letu turuhusiwe kuingia na kukata majani tu katika eneo hili, tupo tayari kuilinda hifadhi hii kwa taratibu tutakazopewa”.

Akijibu ombi hilo Naibu Waziri Makani alisema, ombi hilo litaenda kufanyiwa kazi kwa ushirikiano kati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wakuu wa Wilaya zinazozunguka eneo hilo la hifadhi ambazo ni Moshi, Rombo, Hai na Siha, Wizara ya Maliasili na Utalii na TANAPA ambapo wananchi watapewa mrejesho wa ombi lao hilo.

Sheria za uhifadhi zinakataza mtu yeyote kuingia na kulisha mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa kisheria ikiwa ni pamoja na shughuli nyingine za kibinadamu, kutokana na umuhimu wa eneo hilo kwa wananchi wanaolizunguka na katika jitihada za Serikali kujenga uhifadhi shirikishi, Mwaka 2014 Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kilimanjaro iliruhusu wanawake pekee kuingia ndani ya eneo hilo umbali wa mita 800 kutoka kwenye mpaka wa hifadhi hiyo kwa ajili ya kukata majani ya mifugo na kuokota kuni, wanaume walizuiliwa kutokana na kujihusisha na uharibifu wa eneo hilo. 

Nae mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia alisema ili uhifadhi uimarike ni lazima uwepo ushirikiano wenye tija kwa Serikali, Wananchi na Hifadhi huku akitoa rai ushirikiano huo uimarishwe kwa maslahi ya pande zote.

Wednesday, August 2, 2017

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, MHANDISI RAMO MAKANI AKAGUA SHUGHULI ZA UTALII NA MFUMO WA UKUSANYAJI MAPATO KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO

Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kushoto) akizungumza na watalii kutoka Marekani wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame ndani ya Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro jana. Alipowauliza watalii hao ni wapi walipata habari za mlima huo, walijibu kuwa kila mtu anajua kuhusu mlima Kilimanjaro!. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kushoto) akizungumza na watalii kutoka Marekani wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame ndani ya Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro jana. Alipowauliza watalii hao ni wapi walipata habari za mlima huo, walijibu kuwa kila mtu anajua kuhusu mlima Kilimanjaro!. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba, Mhifadhi Mkuu wa KINAPA, Betrita Loibooki na nyuma yake ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia.

Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi (wa pili kulia) namna mfumo wa ukusanyaji mapato unavyofanya kazi katika Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo, James Mbatia.
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (kulia kwake), Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga (kushoto) na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (kulia).
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kulia) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo James Mbatia (wa tatu kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga (kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Mtango Mtahiko (kulia), Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (wa pili kulia) na Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi.  
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo James Mbatia (wa nne kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (kulia), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Mtango Mtahiko (kushoto), Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (wa pili kushoto) na Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi (wa pili kulia).  
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia (kulia) na Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akisikiliza na kujibu kero mbalimbali za wapagazi wanaopandisha mizigo ya watalii katika mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana
 Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, Betrita Loibook (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na mtalii (katikati) pamoja na mhifadhi wa hifadhi hiyo wakati wa ziara hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, Betrita Loibook akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahifadhi, mtalii na waongoza watalii.

Tuesday, August 1, 2017

MHANDISI MAKANI ASISITIZA UTALII WA MISITU YA ASILI NCHINI KAMA CHANZO MUHIMU CHA KUONGEZA PATO LA TAIFA NA JAMII KWA UJUMLA


Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akijibu kero mbalimbali za uhifadhi kwa wananchi wa Kijiji cha Shume Nywelo, Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi wilayani humo jana. 

NA HAMZA TEMBA - WMU
.........................................................................................
Katika kuhakikisha sekta ya utalii nchini inaendelea kukua kwa kasi, Serikali imesema itaimarisha utalii wa Misitu ya Asili nchini iweze kutoa mchango mkubwa kwenye pato la taifa tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo hutegemea zaidi utalii wa wanyamapori.

Hayo yamesemwa jana wilayani Lushoto na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja wilayani humo kwa ajili ya kutatua migogoro mbalimbali ya uhifadhi.

Alisema sekta ya utalii nchini imekuwa ikitegemea sana wanyamapori na kusahau vivutio vingine kama vile misitu ya asili ambayo ndani yake kuna mimea na viumbe hai mbalimbali adimu duniani na ambavyo hupatikana Tanzania pekee.

“Tumezoea zaidi utalii wa wanyamapori, utalii wa misitu unaweza kuzidi hata wa wanyamapori, kwenye misitu yetu ya asili tunajivunia mimea adimu ya asili na viumbe hai mbali mbali kama vile ndege, vyura, vipepeo, mijusi nakadhalika, tunachotakiwa kufanya ni kutunza misitu yote ya asili, tuiboreshe na kuitangaza ili kupata watalii wengi zaidi na pato la taifa liendelee kukua”, alisema Makani.

Kwa mujibu wa tovuti ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Tanzania ina jumla ya Hifadhi za Misitu ya Asili 100, idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na hifadhi za taifa ambazo zipo 16 pekee, idadi hiyo kubwa pamoja na upekee wake inatoa fursa pana ya kuendeleza sekta ya utalii nchini.

Akizungumzia mafanikio, Makani alisema sekta hiyo inachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni. Alisema pamoja na faida hizo, sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uharibifu wa misitu ya asili ambayo ni muhimu kutafutiwa suluhu ya kudumu ili kunusuru misitu hiyo.

“Ni lazima tutafute njia endelevu ya ulinzi wa misitu, hatuwezi kuwa na askari wa kutosha, walinzi na mitutu, njia sahihi ni ulinzi shirikishi, tuwaelimishe wananchi umuhimu wa misitu na tuwaeleze watanufaikaje, tofauti na zile faida za ujumla za upatikanaji wa mvua na hali nzuri ya hewa, hii itasaidia sana kuwaleta karibu kwenye uhifadhi wa pamoja”, alisema Makani.

Akizungumza na wananchi wa kijiji Nywelo wilayani humo kuhusu mgogoro wa mpaka baina ya kijiji hicho na shamba la miti Shume, Makani alisema tatizo lililopo ni uelewa tofauti kuhusu mpaka huo baina ya pande hizo mbili,  hivyo akuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kutuma wataalamu wa upimaji waliopima eneo hilo awali waje wafanye uhakiki wa mpaka huo kwa kushirikisha uongozi wa wilaya, halmashauri na kijiji hicho ili kuondoa tofauti hizo na kumaliza mgogoro huo ndani ya wiki mbili zijazo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Januari Lugangika alisema wilaya yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali za uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti ya asili, uchimbaji wa madini kwenye maeneo ya hifadhi, uchomaji moto misitu na uhaba wa watumishi.

Katika ziara yake hiyo wilayani Lushoto, Naibu Waziri Makani alitembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Magamba na Shamba la Miti la Shume, alifanya pia vikao vinne vya ndani na mkutano mmoja wa hadhara ambapo alijibu kero mbalimbali za wananchi.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kushoto) akisikiliza moja ya kero kuhusu uhifadhi kutoka kwa Abunio Abraham Shangali (wa pili kulia) ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Shume Nywelo, Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga jana wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi wilayani humo. 
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akizungumza na viongozi wa kikundi cha uhifadhi na utalii cha Friends of Usambara kilichopo Lushoto Mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi wilayani humo jana.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Januari Sigareti Lugangika katika kijiji cha Shume Nywelo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi wilayani humo jana.
Muwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Mwalimu Elias Mkwilima akijibu baadhi ya hoja katika mkutano huo uliofanyika katika kijiji cha Nywelo jana wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga.