Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na
Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja
ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya
Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania mjini Dodoma
leo.
Dkt. Nzuki amesema
ipo haja sasa kwa Sekta za Umma kuona umuhimu wa kuwekeza moja kwa moja katika
biashara ya utalii nchini hususani katika huduma za malazi na usafiri ili
kuiwezesha Serikali kupata mapato ya moja kwa moja na kuongeza zaidi kwenye pato la
taifa.
Alisema kwa kuimarisha usafiri wa anga kutawezesha usafiri wa watalii
moja kwa moja kutoka kwenye soko na kuwaleta nchini huku wakilipia gharama zote
hapa nchini tofauti na hivi sasa ambapo baadhi ya makampuni ya nje hulipwa
fedha kiasi nje ya nchi na hivyo kuikosesha Serikali mapato kupitia ushuru
unaotozwa na TRA.
Alisema sio lazima Serikali iwe inasimamia moja kwa moja
utoaji wa huduma hizo kwa kuwa upo uwezekano wa kutumia makampuni makubwa hata
ya nje ya nchi kuja kuendesha huduma hizo kwa ufanisi zaidi hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na
Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) na wadau wengine wa sekta ya utalii wakimsikiliza
Prof. Raphael Mwalyosi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kulia) wakati
akiwasilisha mada kuhusu Hoja ya Marekebisho ya Sera ya Utalii ya Mwaka 1999
katika warsha ya kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya kupitia upya Sera hiyo iliyoandaliwa
na Wizara hiyo kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania mjini
Dodoma leo.
Kamu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya
Maliasili na Utalii, Deograsias Mdamu akizungumza katika warsha ya siku moja ya
kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya
Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania mjini Dodoma
leo.
Picha ya pamoja ya Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (katikati waliokaa) na wadau wa sekta ya
utalii katika warsha ya siku moja ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya
utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa
na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho
la Vyama vya Utalii Tanzania mjini Dodoma leo.
Baadhi ya wadau wa sekta ya utalii wakisikiliza moja
ya mada katika warsha ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta hiyo kwa ajili ya
kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya
Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Vyama vya Utalii
Tanzania mjini Dodoma leo.
Baadhi ya wawezeshaji wa hafla hiyo ambao ni Maafisa Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakisikiliza moja ya mada katika warsha hiyo.
Baadhi ya wadau wa warsha hiyo wakisikiliza hotuba ya ufunguzi ya Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki.
Baadhi ya wadau wa warsha hiyo.
Baadhi ya Washiriki wa warsha hiyo kutoka Mikoa ya Kanda ya Kati iliyofanyika mjini Dodoma.
HOTUBA YA UFUNGUZI YA NAIBU KATIBU MKUU, WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, DKT. ALOYCE NZUKI
HOTUBA YA KAIMU MKURUGENZI IDARA YA UTALII, DEOGRASIAS MDAMU
No comments:
Post a Comment