Wafanyakazi wa Huduma za Misitu nchini TFS,
Wakiwaonesha wadau Mazao Mbalimbali yatokanayo na misitu ambayo ni mazuri kwa
ajili ya kuimarisha afya ya Mwanadamu |
Meneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini, Mariam Kobelo akieleza huduma za kitalii zilizopo ndani ya Hifadhi za Misitu zilizo chini ya TFS |
Afisa Misitu Mwandamizi , Anna Lawuo Akizungumza
na Waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mazao yatokanayo na misitu
nchini |
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetoa wito kwa watanzania kutembelea Maeneo yaliyohifadhiwa ili kuweza kujionea namna ikolojia na uhifadhi katika misitu hiyo ilivyo na faida kwa viumbe hai na Wanadamu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Afisa Misitu Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS),Arijanso Mlog katika Onesho la Kimataifa la Utalii lijulikanalo kama Swahili International Tourism Expo (SITE) linaloendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mlog amesema kuwa watu wanapaswa kutemblea misitu hii ili waweze kujionea na kujifunza umuhimu wa ikolojia katika hifadhi.
"Ni vyema watu wakaja wakatembelea hifadhi ya misitu ya Amani waweze kujionea namna Misitu iliyopakana na makazi ya watu na maporoko ya maji ambayo hayakauki muda wote na kujionea maua ambayo yanaaminika katika imani kuwa ndio yalitumika wakati wa kristo na watu husafiri kutoka sehemu mbalimbali kuyafuata kutoka maeneo ya mbali"amesema Mlog.
Kwa upande wake, Meneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini, Mariam Kobelo amewataka wdau mbalimbali kutembelea banda lao lililopo katika Onesho La Kimataifa la Utalii la SITE linaloendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam ili kujionea huduma zitolewazo na TFS na kujua wapi wanaweza kutembelea kwa ajili ya mapumziko yao.
Mariamu amesema kuwa Misitu inayohifadhiwa na TFS ina upekee sana , Hivyo ametoa wito kwa wanafunzi, wanasayansi na wanataaluma mbalimbali kuwa wanaweza kwenda ili kuweza kufanyia tafiti, Mapumziko kwa wana ndoa pia wanaweza kwenda kutembea na familia zao .
No comments:
Post a Comment