Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mst.
Thomas Mihayo (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.
Hamisi Kigwangalla kuhusu Maonesho
ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 kabla ya kuzindua maonesho hayo
katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye (wa tatu kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kilifair Promotion, Tom Kunkler (kushoto).
Na Hamza Temba-WMU-Moshi
.......................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa
wito kwa taasisi za Serikali, jamii, sekta binafsi na wadau kwa pamoja
kushirikiana kuendeleza utalii katika maeneo yao ili sekta hiyo iweze kunufaisha
zaidi taifa kwa kiwango kinachostahiki kuliko ilivyo hivi sasa.
Ametoa wito huo juzi katika uwanja wa Chuo Kikuu
cha Ushirika mjini Moshi wakati akifungua maonesho ya kimataifa ya utalii ya Karibu/Kili
Fair 2018 ambayo yameshirikisha makampuni na wadau wa utalii zaidi ya 350
kutoka nchi zaidi ya 12 duniani huku na kuvutia watu zaidi ya 4,000
kuyatembelea.
Amesema ushirikiano huo utaiwezesha sekta hiyo kuongeza mchango
wake katika uchumi wa Taifa ambao kwa sasa ni takriban asilimia 17.2 ya pato la
Taifa, zaidi ya asilimia 24 ya mapato yote ya fedha za kigeni sambamba na zaidi
ya asilimia 10 ya ajira zote nchini.
Amesema mchango huo bado ni mdogo ukilinganisha na aina na idadi
ya vivutio vilivyopo hapa nchini.
Dkt. Kigwangalla amesema Serikali ya awamu ya tano imeshaanza
kuchukua hatua mbalimbali zitakazosaidia kuboresha sekta hiyo ikiwemo ujenzi
unaoendelea wa reli ya kisasa ya Standard Gauge, ujenzi wa Terminal 3 katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Saalam na uboreshaji wa
Shirika la Ndege la ATCL.
Pamoja na hayo amesema Serikali kupitia wizara yake inaendelea
na mpango wa kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini ili kuongeza idadi ya
watalii na mapato ambapo Mapori matano ya Akiba mkoani Kagera na Geita
yatapandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa (Burigi, Biharamulo, Kimisi, Ibanda
na Rumanyika).
"Napenda kumshukuru sana Mhe. Rais, Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kuridhia mapendekezo yetu ya kupandisha hadhi Mapori matano ya
Akiba kuwa Hifadhi ya Taifa ambayo itaitwa Chato National Park, 'Tunatake pia advantage'
ya uwepo wa uwanja wa ndege wa Chato ambao unajengwa katika kiwango cha kutua
ndege kubwa zitakazowawezesha watalii kufika katika hifadhi hiyo" amesema
Dkt. Kigwangalla.
Amesema hatua hiyo itafungua utalii wa kanda ya Kaskazini
Magharibi tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo ni kanda ya kaskazini pekee
inayofanya vizuri zaidi kwenye sekta hiyo. Amesema mpango huo unakwenda
sambamba na kufungua utalii wa kanda ya kusini ambapo mradi wa Kusimamia
Maliasili na Kuendeleza Utalii Kanda ya Kusini (REGROW) upo katika hatua ya utekelezaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha
Mdachi amesema Serikali kupitia bodi hiyo itaendelea kushirikiana na
wadau kutangaza utalii wa Tanzania katika maonesho mbalimbali ya ndani na
nje ya nchi sambamba na kuwashirikisha kunadi kauli mbiu mpya ya utalii wa
Tanzania, "Unforgettable, Tanzania".
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na
Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema kamati hiyo itaendelea
kutoa ushirikiano kwa Serikali na wadau hususan katika eneo la mabadiliko na
maboresho ya sheria za kusimamia sekta hiyo iweze kuondokana na changamoto
zilizopo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akijaribu
kuendesha baiskeli maalum ambayo hutumika kwenye utalii wa baiskeli kwenye
maeneo mbalimbali ya hifadhi nchini baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa
ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Devotha Mdachi wakiwa katika meza kwenye hafla ya ufunguzi wa maonesho hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa
Jimbo la Mtama, Nape Nnauye kabla ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa
ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la
Mtama, Nape Nnauye, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilifair Ltd,Tom Kunkler, Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mkurugenzi wa Karibu Fair, Dominick Shoo na viongozi wengine wa Serikali na sekta
binafsi wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa
ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa
Jimbo la Mtama, Nape Nnauye kwenye eneo la mfano wa kilele cha Uhuru cha mlima
Kilimanjaro baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili
Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi,
Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye na viongozi
wengine wa Serikali na sekta binafsi wakiwa kwenye eneo la mfano wa kilele cha
Uhuru cha mlima Kilimanjaro baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa
ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Waziri Kigwangalla akisalimia baadhi waoneshaji katika banda la utalii wa kiutamaduni kwenye maonesho hayo.
Waziri Kigwangalla akiangalia moja ya gari la kitalii la wazi katika maonesho hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya
gari maalum la kusafirisha watalii ambalo limebuniwa hapa nchini na kampuni ya
Hanspaul Automechs Ltd ya Jijini Arusha baada ya kufungua Maonesho ya Utalii ya
Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika
mjini Moshi mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa Kampuni hiyo, Satbir
Singh Hanspaul.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la
Mtama, Nape Nnauye (kulia) kwenye moja gari maalum la kifahari la kusafirisha
watalii ambalo limebuniwa hapa nchini na kampuni ya Hanspaul Automechs Ltd ya
Jijini Arusha baada ya kufungua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili
Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Waziri Kigwangalla akipanda gari maalum la kusafirisha watalii katika maonyesho hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa wizara hiyo, Deogratious Mdamu wakiwa ndani ya gari hilo maalum la kusafirisha watalii kwenye maonyesho hayo.
Waziri Kigwangalla akiwa amejilaza kwenye moja ya kitanda maalum katika hema la kitalii katika maonesho hayo.
Waziri Kigwangalla akiteta jambo na Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Jorg Herera katika moja ya chumba maalum cha wazi cha kitalii katika maonesho hayo.
Waziri Kigwangalla, Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Jorg Herera na viongozi wengine wakishuka kutoka kwenye chumba hicho cha wazi cha kitalii katika maonesho hayo.
Waziri Kigwangalla akiwa kwenye banda la Bodi ya Utalii na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa bodi hiyo, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (kushoto), Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Devotha Mdachi (wa pili kushoto), wafanyakazi wa bodi hiyo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilifair Promotion Tom Kunkler.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki
kupekecha mti maalum uliokuwa ukitumika enzi za mababu kwa ajili ya kufua moto
katika Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 yanayoendelea katika
uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la
Mtama, Nape Nnauye (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Longido, Dkt. Steven Kiruswa
(wa pili kulia) wakishiriki kucheza ngoma za kimasai na kikundi cha ngoma cha
kabila hilo baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair
2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
No comments:
Post a Comment