Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Finland nchini, Pekka Hukka ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamejadili namna ya kuimarisha sekta ya misitu nchini ikiwemo kuwakaribisha wawekezaji kutoka Finland kuwekeza katika viwanda vya kuchakata mazao ya misitu pamoja na uzalishaji wa nishati mbadala.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akimsikiliza Balozi wa Finland nchini, Pekka Hukka (kulia) ofisini kwake leo mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Gaudence Milanzi.
Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson (katikati) akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali, Gaudence Milanzi (kushoto) akizungumza katika kikao hicho cha Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) na Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson leo mjini Dodoma. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)
No comments:
Post a Comment