slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Sunday, June 11, 2017

KATIBU MKUU, WIZARA YA MALIASILI, MEJA JENERALI GAUDENCE MILANZI AFUNGA MAFUNZO YA JESHI USU KWA ASKARI WA TAWA KATIKA PORI LA AKIBA RUGWA

NA TWAHA TWAIB - TAWA
................................................................

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ni mamlaka iliyoanzishwa kwa Amri ya Serikali na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali Na.135 la tarehe 9 Mei, 2014. Uanzishwaji wa Mamlaka hii ni utekelezaji wa kifungu cha 8 cha Sheria ya kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009.Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu,  Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.na Walimu wa mafuzo hayo kutoka Marekani waliyochuchuma.


 Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, askari wa TAWA waliohitimu mafunzo ya Jeshi Usu na wakufunzi wa mafunzo hayo kutoka jeshi la Marekani. Mafunzo hayo yalifanyika katika Pori la Akiba Rugwa.
Mamlaka ya Wanyamapori imeanza kazi rasmi tarehe 1/Julai/2016. Makao makuu yake kwa sasa yapo Morogoro katika jengo la Taasisi ya utafiti wa mazao ya misitu (TAFORI). Majukumu ya TAWA ni kusimamia na kulinda wanyamapori wote waliyopo maeneo ya  nje za Hifadhi za Taifa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongororo.

Wizara  ya Maliasili kupitia  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imetoa mafunzo ya kijeshi ya kukabiliana na Ujangili wa wanyamapori kwa Askari wanyamapori wapatao 75 kutoka katika Mapori ya Akiba Rungwa, Ugala na vikosi Dhidi ya ujangili vya Manyoni na Arusha.Mafunzo hayo yalifanyika  katika Pori la Akiba Rungwa/Muhesi/Kizigo, yakiendeshwa na askari wa jeshi la Marekani. Mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mej.Generali Gaudence S. Milanzi  akifuatana na Mkurugenzi Mkuu wa TAWA  Bw. Martin Laibooki, Mkurugenzi uzuiaji ujangili wa TAWA Bw. Faustin Masalu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya wanyamapori Bw. Canisius Karamaga, muwakilishi wa ubalozi wa Marekani ambaye ni Mwambata wa jeshi la Marekani hapa nchini Tanzania Liutenat Colonel Michael Lee, na wawakilishi wa mashirika ya wafadhili wa mafunzo hayo wawili kutoka mashirika tofauti, Bw. Aaron Nicholas toka Shirika la ‘ Wildlife Conseration Society- WCS) na Bw. Trevor Johnes toka shirika la uhifadhi la ‘STEP’.  Aidha kulikuwa na wawakilishi wengine kutoka mkoa wa Singida wakiwepo  muwakilishi wa RC na RPC. 
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto) akisalimia na mwambata wa jeshi la Marekani nchini Tanzania Liutenant Colonel Micheel Lee kwenye Pori la Akiba Rungwa wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi amewataka wahitimu wa mafunzo hayo  waliyopata kukabiliana na vitendo vya ujangili kwa kuwakamata majangili na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

alitoa nasaha hizo wakati akifunga mafunzo ya  watumishi wa wizara , Aidha alishuhudia mafunzo ya vitendo yalitoendeshwa kwenye makao makuu ya Pori la Rungwa kama picha hapo chini zinavyoonyesha.
Afisa wanyamapori Bw.Baraka Baragae akielezea vitendo vya mafunzo vinavyoendelea hapo chini na jangili amekamatwa.


Askari wa TAWA akionesha kwa vitendo namna ya kupambana na jangili wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akiwa na baadhi ya wahitimu hao.


Wahitimu wa mafunzo hayo wakisoma risala yao kwa mgeni rasmi, Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi. 
Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Martin Loibooki (kushoto)  akizungumza na baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo kupata maoni yao.
Mafunzo hayo yalianza Machi 27 hadi Juni 5, mwaka huu 2017 kwa maofisa 75 . Mafunzo waliyojifunza yalijikita kwa masomo yafuatayo; Upelelezi, Huduma ya kwanza,mbinu za kufanya doria, mazoezi ya viungo,usomaji wa ramani, GPS, ushirikishaji jamii katika uhifadhi na matumizi ya siraha.

Katika kushirikiana na Serikali ya Marekani kupitia mashirika ya WCS na STEP wamesaidia  vifaa mbalimbali katika Mapori ya Akiba ya Rungwa/Muhesi/Kizigo vifaa hivyo ni pamoja na magari manne, tractors 2, mafuta ya magari.

Katibu Mkuu akionyeshwa baadhi ya magari aina ya L/Cruiser yaliyonunuliwa na Serikali ya Marekani. Kushoto kwake anashuhudia Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Bw. Martin Loibooki 
Katibu Mkuu aliwaeleza wahitimu kuwa,yeye binafsi natambua kuwa mafunzo haya hayakuwa rahisi kwenu haswa ukizingatia wengi wenu kama siyo wote, hii ndiyo mara yenu ya kwanza kupata mafunzo kama haya,lakini kwa dhamira nzuri na yenye mtazamo chanya mliyokuwa nayo imepelekea wote kumaliza salama. Ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatasaidia kuimarisha nidhamu kwenye maeneo yetu  ya kazi katika kipindi hiki tunachojianda kuingia katika mfumo wa kiutendaji wa jeshi usu.

Katibu Mkuu aliwaeleza wahitimu kuwa Wizara inatambua mchango wa TAWA tangu kuanzishwa katika kukabiliana na ujangili. Kuanzia mwezi Julai 2016 jumla ya majangili 3,185 wamekamatwa, kati ya hao 1539 wamefikishwa mahakamani,  na siraha 270 na risasi 1058 zimekamatwa. Aidha askari wametegua mitego 3,273 ya kuua wanyamapori. Nawapongeza sana TAWA.

Alimalizia hotuba yake kwa kuipongeza Serikali ya Marekani na Mashirika yasiyo ya kiserikali ya WCS na STEP kwa mchango wake katika uhifadhi.
Katibu Mkuu akisalimiana na Mratibu wa shirika la STEP Bw.Travor Johnes
Katibu Mkuu akisalimiana na Mratibu wa Shirika la WCS Bw. Aaron Nicholaus 
KATIBU MKUU AKISALIMIANA MA MKUFUNZI WA MGAMBO WILAYA YA MANYONI BW. Lala Awe Silago
Mkurugezi Msaidizi kutoka Idara ya Wanyamapori Bw. Canisius Karamaga(Mwenye koti nyeusi) alimwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori


Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akisaini kitabu cha wageni.

Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Bw.Martin Loibooki alimueleza mgeni rasmi kuwa Katibu  lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kuongoza watumishi walio chini yao ambao wengi ni askari.wakati wahitimu hawa wengi wao hawajapata mafunzo ya kijeshi tangu wamalize elimu yao ya chuo kikuu. Bw.loibooki alisema majukumu waliyopewa ni makubwa ambayo lengo lake ni kuwaanda kuwa wahifadhi wakuu na baadaye. Hivyo ni vyema wakatambua kuwa baada ya mafunzo haya wanajukumu yanawasubiri mbele yao.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Bw. Martin T.Loibooki, alianza hotuba yake kwa kumshukuru Katibu Mkuu kukubali kuja kufunga mafunzo hayo ya Maafisa wanyampori

Bw.loibooki alielezea kidogo Mamlaka anayoisimamia kwa kuanza kusema, Mamlaka ilianzishwa na Serikali kama chombo cha utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa niaba ya Serikali chini ya uangalizi wa Serikali na  kuwa na mfumo unaonesha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi zaidi. Kama ilivyo kwa Mamlaka Serikali nyingine nchini, lengo la kuanzishwa TAWA ni kutekeleza majukumu ya Idara ya Wanyamapori hasa ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini. Majukumu ya TAWA ni kusimamia shughuli za utawala, ulinzi, usimamizi wa raslimali ya Wanyamapori katika maeneo yote nje ya Hifdahi za Taifa na Hifadhi ya Ngorongoro.

Akiitimisha hotuba yake Bw. Loibooki alizungumzia suala la ujangili kwa kusema, TAWA inaamini kwamba changamomoto za ujangili na uvunaji haramu wa misitu na matatizo mbalimbali yanayohikabili uhifadhi nchini hayawezi kutatuliwa kwa mfumo wa utendaji kazi wa kiraia. Hivyo, Wizara inakamilisha taratibu za kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka wa kiraia kwenda jeshi usu.Mabadiliko haya ya kimfumo ni matakwa ya Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009 ambayo imeanisha kwamba kutaundwa kikosi cha jeshi usu (Wildlife Protection Unit), ili kuhakikisha ulinzi kamili wa rasilimali katika maeneo yaliyohifadhiwa
Kaimu Mkurugenz Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),mARTIN loibooki akitoa hotuba yake wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo.
Bw. Loibooki alimueleza mgeni rasmi anawashukuru Serikali ya Marekani kupitia shirika lisilo la Kiserikali la WCS kwa kutoa mafunzo ya kikosi maalumu cha kukabiliana na ujangili kwa haraka zaidi kiitwacho ‘Rapid Response Team’ ambacho kimepatiwa vifaa ikiwepo magari ya doria kwenye Mapori ya Akiba ya Rungwa, Rukwa na Piti. WCS vilevile wanasaidia doria ya kutumia ndege katika kukabiliana na ujangili.Hapo chini ni baadhi ya kikosi hicho.

Mkurugenzi Mkuu akimuelezea  mgeni rasmi utendaji kazi wa kikosi hicho cha ‘Rapid Response Team’ kinavyofnya kazi
AFISA HABARI NA MAHUSIANO WA TAWA BW.TWAHA TWAIBU AIKWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KIKOSI CHA ‘RAPID RESPONSE TEAM’ RUNGWA

KAIMU MKURUGENZI MKUU BW.LOIBOOKI AKITELEMKA KWENYE UWANJA WA RUNGWA AMEFUATANA NA KATIBU MKUU.

1 comment:

  1. Wakufunzi kutoka America! Maelezo kidogo tafadhali. Imekuwaje tunatumia wakufunzi kutoka Jeshi la America?

    ReplyDelete