Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 25 Mei, 2016 limekubali kupitisha bajeti
ya Wizara ya Maliasili ikiwa na makadirio ya mapato na matumizi ya jumla ya Sh.
135,797,787,000 kwa mwaka 2016/2017. Kati ya fedha hizo, Sh. 118,051,105,000 ni
kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Sh. 17,746,682,000 ni kwa ajili ya Miradi
ya Maendeleo. Fedha za Matumizi ya Kawaida zinajumuisha Sh. 59,592,676,000 za
Mishahara ya watumishi na Sh.58,458,429,000 za Matumizi Mengineyo. Fedha za
Miradi ya Maendeleo zinajumuisha Sh. 15,746,682,000 fedha za nje na
Sh.2,000,000,000 fedha za ndani.
Waziri wa
Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (Mb) akijibu hoja mbalimbali za
wabunge wakati wa kuwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara (2016/2017) katika
bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 24-25 Mei, 2016.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne
Maghembe (Mb) na Naibu Waziri, Eng. Ramo Makani (Mb) wakipongezwa na baadhi ya
wabunge ndani ya ukumbi wa bunge baada ya kujibu hoja mbalimbali na kufanikisha
kupitishwa kwa bajeti ya Wizara.
Picha ya
pamoja kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (Mb),
Naibu Waziri, Eng. Ramo Makani (Mb), Katibu Mkuu, Maj. Gen. Gaudence Milanzi,
Naibu Katibu Mkuu, Angelina Madete, Vingozi wa Idara na Vitengo pamoja na Viongozi
wa Taasisi mbalimbali za Wizara hiyo muda mfupi baada ya Bajeti ya Wizara
kupitishwa na Bunge tarehe 25 Mei, 2016 nje ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma.