slider gif
kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ
Sunday, July 3, 2016
Saturday, July 2, 2016
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YANYAKUA TUZO MBILI KATIKA MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM 2016 - SABASABA
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akikabidhi tuzo mbili za ushindi ilizoshinda Wizara yake katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwa viongozi wa Kamati ya Maonesho ya Wizara hiyo jana tarehe 01 Julai, 2016 katika viwanja vya Sabasaba. Tuzo hizo ni Mshindi wa Kwanza katika kundi la Wizara na Taasisi za Serikali na Mshindi wa pili katika kundi la Mshindi wa Jumla wa Maonesho hayo. Tuzo hizo zilikabidhiwa na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame aliyekuwa Mgeni Rasmi akiongozana na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa tano kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waoneshaji wa Wizara yake muda mfupi baada ya kupokea tuzo mbili za ushindi katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam jana tarehe 01 Julai, 2016 katika viwanja vya Sabasaba. Tuzo hizo ni Mshindi wa kwanza katika Kundi la Wizara na Taasisi za Serikali na Mshindi wa Pili katika Kundi la Mshindi wa Jumla.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa tano kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waoneshaji wa Wizara yake muda mfupi baada ya kupokea tuzo mbili za ushindi katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam jana tarehe 01 Julai, 2016 katika viwanja vya Sabasaba. Tuzo hizo ni Mshindi wa kwanza katika Kundi la Wizara na Taasisi za Serikali na Mshindi wa Pili katika Kundi la Mshindi wa Jumla.
Baadhi ya Waoneshaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakifurahia ushindi wa tuzo hizo. Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ni moja ya mabanda yanayovutia zaidi katika Maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu 2016, kwa kuwa na mchanganyiko wa mambo mbali mbali yanayoelimisha kuhusu uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Utalii. Katika banda hilo zipo pia fursa za kuwaona wanyama hai kama vile Simba, Nyati, Chui, Mamba, Ndege mbalimbali n.k. Kwa upande wa Utalii wa Ndani zipo fursa za kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa gharama nafuu ya Tsh. 10,000 kwa watoto na Tsh. 20,000 kwa watu Wazima ikiwa ni nauli ya kwenda na kurudi, Aidha kwa wale watakaopenda kulala itawagharimu Tsh. 50,000.
Baadhi ya Waoneshaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakifurahia tuzo hizo katika banda la Wizara hiyo.
Taswira ya tuzo hizo.
Monday, June 27, 2016
TAARIFA KWA UMMA
Wizara ya Maliasili na Utalii itashiriki katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 8 Julai, 2016 katika viwanja vya Mwalimu Julius. K. Nyerere, Dar es Salaam.
Wizara itakuwa na washiriki kumi na sita (16) ambao ni Idara pamoja na Taasisi zake mbalimbali. Idara zitakazoshiriki ni Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale na Misitu na Nyuki.
Kwa upande wa Taasisi ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chuo cha Taifa cha Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) na Vyuo vya Wanyamapori (Mweka, Pasiansi na Likuyu Semaganga).
Taasisi nyingine ni Vyuo vya Misitu na Nyuki (Olmotonyi, FITI Moshi na Chuo cha Nyuki Tabora), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Wakala wa Mbegu za Miti, Taasisi ya Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Washiriki wote hao watakuwa kwenye banda moja la MALIASILI, Wizara inawakaribisha wananchi wote kwenye banda hilo waweze kujionea na kuelimika na mambo mbalimbali yanayohusu Utalii, Ufugaji wa Nyuki, Uhifadhi wa Misitu, Malikale na Wanyamapori.
Aidha, Wizara itatoa punguzo kwa watanzania kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa gharama nafuu. Safari ya kwenda na kurudi kwa watoto itakua Tsh. 10,000 na watu wazima Tsh. 20,000. Safari ya kulala itakuwa Tsh. 50,000.
Pia katika maonesho hayo itakuwepo fursa ya kuwaona wanyamapori hai mbalimbali kama vile Chui, Nyoka, Ndege wa aina mbalimbali pamoja na SIMBA.
Kaulimbiu ya Maonesho hayo mwaka huu inasema “Tunaunganisha Uzalishaji wa Masoko”
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Maliasili na Utalii
27 Juni, 2016.
27 Juni, 2016.
Thursday, June 16, 2016
MKURUGENZI WA IDARA YA UTAWALA NA RASILIMALI WATU (DARHM) WIZARA YA MALIASILI, SAID A.S MSAMBACHI ASTAAFU RASMI UTUMISHI WA UMMA, AACHA WOSIA KWA WATUMISHI WA WIZARA HIYO
Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Utawala na
Rasilimali Watu Wizara ya Maliasili na Utalii, Said Msambachi akizungumza na watumishi wa Idara ya Utawala (hawako
pichani) katika ukumbi wa Ngorongoro alipowaaga rasmi jana tarehe 16 Juni, 2016 kwa kukamilisha safari
yake ya utumishi wa umma. Amewaasa watumishi wote wa wizara kuimarisha
ushirikiano kazini, kufanya kazi kwa bidii, kuwa wabunifu, kupendana, kusalimiana, kudumisha uaminifu, utii wa amri halali za
viongozi, uadilifu, usawa, usiri wa taarifa za serikali, kuwahi kazini na
kujiendeleza kielimu. Amewaasa pia kujiepusha na vitendo vya
rushwa, majungu, uchochezi, chuki, ubaguzi na upendeleo wa aina yeyote.
Kikao kikiendelea katika ukumbi wa Ngorongoro.
Picha ya pamoja.
Friday, June 10, 2016
SERIKALI YA TANZANIA NA ZAMBIA ZASAINI MAKUBALIANO YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA MAZAO YA MISITU NA MAGOGO KUPITIA MIPAKA YA NCHI HIZO
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi (katikati) akisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya
Tanzania na Zambia, jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa
mazao ya misitu hususan magogo katika mipaka ya nchi hizo mbili. Wanaoshuhudia kulia ni
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili, Gladynes Mkamba na
Kaimu Mtendaji Mkuu TFS, Richard Kamwenda (kushoto). Waliosimama kulia ni
Mwanasheria wa TFS, David Mung’ong’o na Mwanasheria wa Wizara ya Maliasili, Stephen
Mwamasenjele.
Katibu Mkuu
Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia,
Trevor Kaunda akisaini makubaliano hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi
ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakibadilishana hati ya makubaliano
waliyosaini kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao
ya misitu hususani magogo katika mipaka ya nchi hizo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi akizungumza katika hafla fupi ya kuweka makubaliano kati ya Serikali
ya Tanzania na Zambia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa
usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo katika mipaka ya nchi hizo. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,
Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda. Maj. Gen. Milanzi alisema kuwa ushirikiano huo utaleta tija katika udhibiti wa biashara haramu ya uvunaji na usafirishaji wa magogo kutoka katika nchi hizo kwenda nchi nyingine kupitia mipaka ya nchi hizo na bandari ya Dar es Salaam. Aliwataka watanzania wanaojihusisha na biashara haramu ya uvunaji na usafirishaji wa magogo nje ya nchi waache mara moja kwani Serikali imejipanga kuhakikisha wanakamatwa na sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi
ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakiteta jambo wakati
wakikagua Makontena 103 ya magogo (nyuma pichani) yaliyokamatwa hivi karibuni
katika bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini Zambia na DRC. Makatibu Wakuu hao
wamesaini makubaliano ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji
wa mazao ya misitu hususani magogo kwenye mipaka wa nchi hizo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi
ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakiangalia sehemu ya magogo
yaliyokamatwa hivi karibuni katika bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini
Zambia na DRC. Makatibu Wakuu hao wamesaini makubaliano ya kukabiliana na
changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususani
magogo kwenye mipaka wa nchi hizo.
...........................................................................................
...........................................................................................
Serikali ya Tanzania na
Zambia zimesaini makubaliano ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa
usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo katika maeneo ya mpakani kwa
lengo la kulinda misitu na kuimarisha uhifadhi katika nchi hizo.
Makubaliano hayo
yalitiwa saini jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence
Milanzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili,
Ardhi na Hifadhi ya Mazingira ya nchini Zambia, Bw. Trevol Kaunda na kushuhudiwa na
Wajumbe kutoka Zambia na Tanzania.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari mara baada ya
kusaini makubaliano hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi alisema hatua hiyo
imefikiwa ili kukabiliana na changamoto mbali mbali zilizopo za uharibifu wa
misitu na usafirishaji wa mazao ya misitu na magogo kupitia mipaka ya nchi hizo.
Makubaliano hayo
yalifikiwa mara baada ya kumalizika kwa kikao cha siku tatu cha wajumbe kutoka
nchi hizo mbili cha kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta misitu
maeneo ya mpakani.
katika kikao hicho
Tanzania iliwakilishwa na wajumbe kutoka taasisi za Serikali ambazo ni Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya
Bandari (TPA), Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali na Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS).
Katika hatua nyingine
mara baada ya kusaini makubaliano hayo, msafara wa Makatibu Wakuu hao ulitembelea
Bandari ya Dar es Salaam kukagua shehena ya magogo yaliyokamatwa katika bandari
hiyo kuanzia mwezi Novemba mwaka jana kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.
Maj. Gen. Milanzi alisema
kuwa jumla ya makontena ya magogo hayo ni 103 ambapo makotena 56 yalikamatwa
kuanzia mwezi Novemba mwaka jana yakidaiwa kutoka nchini Zambia na makontena mengine
47 yaliyodaiwa kutoka DRC ambayo yamekamwatwa kuanzia mwezi Januari mwaka huu.
Akizungumza na
waandishi wa habari baada kukagua makontena hayo, Maj. Gen. Milanzi alisema
"Napenda kuwaasa wananchi wanaojihusisha na biashara hii haramu ya
kusafirisha magogo waache mara moja kwani inasababisha uharibifu mkubwa wa
misitu na endapo tutawakamata tutawachukulia hatua kali za kisheria”.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili, Ardhi na
Mazingira wa Zambia, Bw. Trevol Kaunda alisema kuwa “Ushirikiano baina ya pande
hizi mbili utaleta ufanisi katika suala la uhifadhi wa misitu yetu kwa kuwa
baadhi ya watu wamekuwa wakisafirisha magogo na mazao ya misitu kwa kutumia
njia danganyifu, umoja huu utatusaidia kuwabaini ni kuwachukulia hatua stahiki”.
Aliongeza kuwa
makubaliano hayo ni mwanzo mzuri wa kuweza kufanya kazi kwa ushirikiano na
Serikali ya Tanzania katika mpaka wa Tunduma ambako mazao ya misitu na magogo
toka nchini Zambia yamekuwa yakipitishwa kwenda bandari ya Dar es Salaam na
baadae nje ya nchi.
Akizungumzia hatima
ya magogo hayo Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za
Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Mohammed Kilongo alisema
kuwa “Wafanyabishara wote waliokamatwa na magogo haya wametakiwa kuleta
vielelezo halali vya uvunaji na usafirishaji wake jambo ambalo wameshindwa kutekeleza
mpaka sasa, muda tuliowapa ukiisha utaratibu wa kuwafungulia mashitaka utafuata
ili sheria ichukue mkondo wake”.
Sunday, June 5, 2016
MINISTER OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM PROF. JUMANNE MAGHEMBE MEETS AMERICAN JOURNALIST ROBERT ROSS
American Journalist Robert
Ross (RIGHT) handing over his book called "The Selous of Africa: A long Way from Anywhere" to the Minister of Natural Resources and Tourism, Hon. Prof. Jumanne Maghembe when visited his office recently. The book
contains more than 100,000 shots of fauna, flora and dramatic landscapes of
Selous Game Reserve. The book will be an important agent in promoting Tanzanian Tourism Worldwide.
Prof. Maghembe (left) perusing the book, Left is Dr. Ross. The book is published by Officina Libraria and distributed in the U.S. by ACC. It is available to buy now on Amazon. The book was launched by the Minister through his representative Deputy Permanent Secretary Eng. Angelina Madete on 3rd June, 2016, Slipway Hotel, Dar es Salaam.
Thursday, June 2, 2016
WAZIRI WA MALIASILI PROF. JUMANNE MAGHEMBE AIOMBA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KWA VITENDO KATIKA VITA DHIDI YA UJANGILI
Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kulia) akipokea
ndege maalum aina ya drones kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa
Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Marco Lambertini (wa tatu
kushoto) kwa ajili ya kusaidia doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili
katika pori la akiba la Selous. Wengine
katika picha ni kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa WWF - Tanzania, Amani Ngusaru, Meneja
wa Pori hilo la Akiba Selous, Mabula Misungwi, Mwenyekiti wa bodi ya
WWF - Ujerumani, Dkt. Valentin Von Moscow, Mkurugenzi Mtendaji WWF – Ujerumani,
Ebenhard Brandes na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kuzuwia Ujangili, Faustine
Ilobi Masalu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Viongozi
wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) na Viongozi wengine
wa Wizara wakipokea maelekezo kutoka kwa Mtaalam wa uendeshaji wa ndege maalum
aina ya drones na jinsi zinavyofanya kazi, Parmena Elisa, ndege hizo zilitolewa na Mfuko
wa WWF kusaidia doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili katika pori la
akiba la Selous jana tarehe 1 Julai, 2016 Matambwe Selous.
Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe akizungumza katika hafla ya
makabidhiano ya ndege maalum aina ya drones zilizotolewa na Mfuko wa WWF kusaidia
doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili katika pori la akiba la Selous. Wengine katika picha ni Mkurugenzi
Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF)
Dkt. Marco Lambertini (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji WWF – Ujerumani,
Ebenhard Brandes (kushoto).
Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na
Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Marco Lambertini (wa pili kushoto) akimkabidhi, Namsifu
Johannes Marwa (Mhifadhi Wanyamapori), Tuzo ya WWF ya Mhifadhi Bora kwa mchango
wake alioutoa katika kupambana na ujangili katika pori la akiba la Selous. Wanaoshuhudia
ni Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Mkurugenzi
Mtendaji WWF – Ujerumani, Ebenhard Brandes na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya
Kuzuwia Ujangili Wizara ya Maliasili, Faustine Ilobi Masalu (wa nne kushoto),
tuzo hiyo ilitolewa Matambwe Selous tarehe 1 Julai, 2016. 
Picha ya pamoja.
.....................................................................................................
.....................................................................................................
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Prof.
Jumanne Maghembe ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kuunga mkono juhudi za
Serikali katika kupiga vita ujangili kwa vitendo katika kuimarisha uhifadhi
nchini.
Prof.
Maghembe alisema hayo jana, Matambwe Selous, katika hafla fupi
ya makabidhiano ya ndege maalum 8 zilizotolewa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na
Mazingira Duniani (WWF) kwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Ndege
hizo ndogo aina ya drones ambazo hazitumii rubani na huongozwa na mitambo
maalum zitatumika katika pori la akiba la Selous kwa ajili ya kuimarisha ulinzi
wa Wanyamapori kwa kukusanya taarifa za kiitelijensia zitakazosaidia kukamatwa
majangili. Ndege hizo zina thamani ya dola za kimarekani 80,000 sawa na zaidi
ya Tsh milioni 172.
"Msaada
huu umekuja wakati muafaka ambapo Pori la Akiba la Selous linahitaji teknolojia
za kisasa katika kuimarisha mapambano dhidi ya ujangili ndani na kuzunguka
hifadhi hii" alisema Prof. Maghembe.
Alieleza
kuwa changamoto kubwa inayoikabidili hifadhi ya Selous ni ujangili ambao kwa
kiasi kikubwa umesababisha idadi ya Wanyamapori hususani tembo kupungua kwa kasi
kubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Alisema
kuwa takwimu zinaonesha kuwa mwaka 1986 idadi ya tembo katika pori hilo ilikuwa
50,000, idadi ambayo iliongezeka mwaka 2003 na kufikia 70,000 baada ya
Serikali ya Ujerumani kusaidia kuanzishwa kwa Mpango wa Kuendeleza Selous
(Selous Conservation Program) na Serikali ya Tanzania kukubali aslimia 50 ya
makusanyo yanayotokana na utalii yabaki kuendeleza uhifadhi katika pori hilo.
Alisema
kuwa baada ya mradi huo kuisha na mfumo wa “retention” kuondolewa na Serikali
hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi ambapo kati ya mwaka 2008 na 2011 vitendo
vya ujangili viliongezeka maradufu, sensa ya mwaka 2013 ilionesha idadi ya
tembo hao kupungua hadi kufikia 13,000.
Prof.
Maghembe aliongeza kuwa pamoja na hayo Serikali imejipanga kuhakikisha
Wanyamapori wanalindwa usiku na mchana na kwamba wale wote wanaojihusisha na
vitendo vya ujangili watakamatwa na kufikishwa mahamani ili sheria ichukue
mkondo wake.
"Hatutawavumilia
hawa watu wamalize wanyamapori wetu wote tulionao, tunawafuatilia usiku na
mchana na lazima tutawakamata" alisisitiza Prof. Maghembe.
Aliongeza
kuwa Serikali kwa kushirikiana na washirika wa uhifadhi imechukua hatua za
makusudi za kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kuanzishwa kwa mpango wa Kitaifa
wa Kukabiliana na Ujangili na Biashara Haramu ya Wanyamapori, mpango ambao
umekuwa na matokeo mazuri baada ya kuungwa mkono na washirika hao kwa kusaidia
fedha, vifaa na misaada mbalimbali ya kiufundi.
Aliongeza
kuwa sehemu ya mpango wa Serikali wa kukabiliana tatizo hilo ni kuanzishwa kwa
Jeshi Usu (Paramilitary) ambapo maeneo yote ya hifadhi nchini yatalindwa
kijeshi.
Prof.
Maghembe ameeleza kuwa pamoja na mambo mengine ili kukomesha ujangili ni lazima
mataifa yaliyoendelea ambayo ndiko yaliko masoko makubwa ya meno ya tembo na
bidhaa zake kusitisha kabisa uingizwaji wa meno hayo katika nchi zao ili
kukomesha biashara hii haramu.
“Kuna
nchi ambazo tayari zimechukua hatua ya kukataza kabisa uingizwaji wa meno ya
tembo nchini mwao, mfano Marekani, tunaiomba sana jumuiya ya kimataifa wakiwemo
marafiki zetu China na nchi nyingine wakatae kabisa uingizwaji wa meno haya
nchini mwao, hii itasaidia sana kukomesha biashara hii haramu” Alisema.
Katika
hatua nyingine Prof. Maghembe aliwataka wafugaji walioingiza mifugo katika
maeneo yote ya hifadhi nchini waondoe mifugo yao kwa hiari kabla ya
kushinikizwa kufanya hivyo na Serikali kwa mujibu wa sheria.
Sheria ya
Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 Ibara ya 18 (2) inasema “Si ruhusa mtu yeyote
kuingia na kulisha mifugo ndani ya Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na Ardhioevu”
Prof.
Maghembe alisema kuwa “mtandao wa ujangili unaanzia na watu wanaoingiza mifugo
ndani ya hifadhi, hivyo ni lazima sheria zifuatwe na waondoke mara moja,
watakaokaidi sheria itafuata mkondo wake na mifugo itakayokamatwa itataifishwa
na Serikali kwa mujibu wa sheria za nchi, sheria hizi hazina tofauti na sheria
zinazokataza watu wasijenge mabondeni au kwenye hifadhi za barabara”
Awali
akitoa taarifa, Meneja wa Pori hilo la Akiba la Selous Mabula Misungwi
alieleza baadhi ya changamoto kuu zinazoikabili hifadhi hiyo kuwa ni pamoja na ujangili, miundombinu mibovu ya barabara kwa ajili ya doria na vifaa
ikiwemo magari ya doria na nyumba za watumishi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa
wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Marco
Lambertini alisema kuwa ili kuimarisha Uhifadhi nchini ni lazima wananchi
waishi karibu na maeneo hayo na pia washirikishwe juu ya umuhimu wake ili wasaidie
kuyalinda kwa faida yao na taifa kwa ujumla.
Subscribe to:
Posts (Atom)


