slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Monday, November 6, 2017

"SIWEZI KUJARIBIWA NA SIWEZI KUCHEZEWA, SIKO HAPA KWA BAHATI MBAYA". DK. KIGWANGALLA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Hamdun Mansur (katikati) na Afisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Ndugu Bajuta wakisoma ramani ya Pori Tengefu Loliondo na mpaka wake na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Ngorongoro muda mfupi kabla ya kuaza ziara ya kukagua maeneo hayo jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu Loliondo jana mkoani Arusha jana, pamoja na mambo mengine alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara hiyo, Prof. Alexander Songorwa kwa tuhuma za rushwa na kuhujumu jitihada halali za Serikali za kumaliza mgogoro huo. Aliagiza Mkurugenzi huyo afikishwe TAKUKURU kwa uchunguzi wa tuhuma hizo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu Loliondo jana mkoani Arusha jana.
Dk. Kigwangalla (kulia) akimuhoji mmoja ya wananchi jamii ya wafugaji alipotembelea Pori Tengefu Loliondo jana.
Waziri Kigwangalla (kushoto) akioneshwa  mpaka wa Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Pori Tegefu Loliondo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Hamdun Mansuri wakati wa ziara yake ya kukagua iwapo mifugo inaingizwa katika hifadhi ya Serengeti kama ilivyoripotiwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari. 

Saturday, November 4, 2017

DK. KIGWANGALLA ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA ZIWA MANYARA NA KUKAGUA SHUGHULI MBALIMBALI ZA UHIFADHI NA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akisalimiana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Manyara, Noelia Myonga alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Noelia Myonga (wa pili kushoto) kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akizungumza na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Noelia Myonga alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na  Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Noelia Myonga alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Noelia Myonga kuhusu hifadhi hiyo alipoitembelea jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiongozwa na Mhifahdi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Noelia Myonga kwenda kuangalia kivutio cha Maji ya Moto ya Asili ndani ya hifadhi hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akigusa maji ya moto ya asili ambayo ni kivutio cha kipekee cha utalii kilichopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. Maji hayo yanakadiriwa kuwa na nyuzi joto 80 ambapo imeelezwa kuwa baadhi ya watalii huweza kuchemsha mayai katika maji hayo. Nyuma yake anayeshuhudia ni Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Noelia Myonga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akionyeshwa maeneo ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara na Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Noelia Myonga alipoitembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa ‘Lodge’ ya AndBeyond Lake Manyara Tree, Mei Saimon (kulia) kuhusu ‘lodge’ hiyo ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa ‘Lodge’ ya AndBeyond Lake Manyara Tree, Mei Saimon (kulia) kuhusu mazingira ya nje ya ‘lodge’ hiyo ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. 
 Waziri, Dk. Kigwangalla akikagua miundombinu ya lodge hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akikagua mazingira ya Lodge’ ya AndBeyond Lake Manyara Tree ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. Kulia kwake ni Meneja wa hoteli hiyo, Mei Saimon. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya miundombinu ya kupumzikia wageni katika Lodge’ ya AndBeyond Lake Manyara Tree ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. Kulia kwake ni Meneja wa hoteli hiyo, Mei Saimon. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya miundombinu ya kupumzikia wageni katika Lodge’ hiyo ya AndBeyond Lake Manyara Tree ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara. Kulia ni Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Noelia Myonga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia waliosimama) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Nyumba ya Kulala Wageni ya AndBeyond Lake Manyara Tree Lodge ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara wakati alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. 
Simba katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Baadhi ya miundombinu ya daraja katika hifadhi hiyo ambayo huwarahisishia watalii kuona wanyamapori mbalimbali.
Pundamilimilia
Ndege na nyati katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Ndege aina mbalimbali wanapatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Mtoto wa Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Baadhi ya Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)

Friday, November 3, 2017

DK. KIGWANGALLA AAGIZA RASIMU YA SERA MPYA YA TAIFA YA MISITU IKAMILIKE NDANI YA MWEZI HUU WA NOVEMBA KUWEZESHA UPATIKANAJI WA SHERIA NA KUNUNI MPYA ZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA SEKTA HIYO

Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasili katika ukumbi wa Hoteli ya Morena mjini Dodoma jana kwa ajili ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.

Na Hamza Temba - WMU
............................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza kukamilishwa haraka kwa rasimu mpya ya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 2016 ili kuwezesha upatikanaji wa Sera, Sheria na Kanuni mpya za usimamizi wa rasilimali za misitu nchini kwa ufanisi zaidi.

Ameagiza wataalamu wa Wizara hiyo kukamilisha rasimu hiyo mwezi huu wa Novemba na iwasilishwe kwake mapema mwezi ujao (Desemba) ili aweze kupata ushauri zaidi wa wataalamu wengine huru kabla ya kuwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri na baadaye kutungiwa Sheria na Kanuni za utekelezaji.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana mjini Dodoma wakati akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa misitu iliyolenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.

“Natoa agizo mchakato huu ukamilike ndani ya mwezi huu wa 11, tarehe moja mwezi wa 12 mlete rasimu ambayo nyie wataalamu mmeridhika nayo, muiwasilishe kwangu mimi na Mhe. Naibu Waziri, na siku hiyo mtakayoiwasilisha kwetu mniletee timu ya wataalamu watakaonishauri kwenye maeneo mbalimbali.

“Pamoja na hao wataalamu washauri nataka watu wengine huru wahusike kwenye kunishauri, ili nipate picha ya watu wengine huru kabla hatujatengeneza andiko ambalo tutalipeleka kwenye kikao cha baraza la Mawaziri, waje wanishauri maeneo yanayotaji maboresho, kuongeza ubunifufu au kukazia zaidi”. Aliagiza Dk. Kigwangalla.

Alisema amelazimika kuharakisha zoezi hilo ili Sera hiyo ikamilike haraka iweze kushughulikia changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo ongezeko la watu linalosababisha misitu mingi kuteketezwa kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kupitia shughuli za kilimo na uanzishwaji wa makazi mapya.

Alisema pamoja na misitu kuonekana inachangia kidogo kwa asilimia 3.5 kwenye pato la taifa, bado mchango wake ni mkubwa kuliko inavyochukuliwa hivi sasa. Alisema tafiti zilizofanywa awali hazikuzingatia mambo muhimu ikiwemo mchango halisi wa misitu kwenye upatikanaji wa maji ambayo huzalisha umeme, hunywesha mifugo na wanyamapori, matumizi ya majumbani na kilimo cha umwagiliaji.

Alisema ili kupata mchango halisi wa misitu kwenye uchumi mpana wa taifa letu, Wizara yake imeshaandaa andiko maalum kwa ajili ya kuendesha utafiti mkubwa wa kubaini mchango huo na kazi inayofanyika hivi sasa ni ya utafutaji wa fedha kutoka kwa wadau mbalimbali kufanikisha utafiti huo.

Akizungumzia Uhifadhi Shirikishi Jamii, Dk. Kigwangalla alisema kwa zaidi ya asilimia 32 ya maeneo yote nchini yamehifadhiwa kisheria, hivyo njia rahisi ya kuyalinda ni kupitia ushirikishwaji wa wananchi. “Bila kufanya hivyo hatuwezi kusema tuna askari wa kutosha kulinda misitu yote, mbuga zote za wanyama au mapori yote tengefu nchini.

“Lakini nje ya maeneo hayo kuna maeneo ya vijiji ambayo pia yamehifadhiwa, yote haya huwezi kusema utayalinda kirahisi sana bila ushiriki wa wananchi, kuwaleta wananchi kwenye uelewa wa pamoja, kwamba tunahifadhi kwa faida yao.

“Tuwaelimishe, kwa mfano usipohifadhi misitu kiwango cha mvua kitashuka, usalama wa chakula utaathirika, upatikanaji wa maji safi na salama utaathirika, upatikanaji wa umeme nao pia utaathirika, hivyo tunahifadhi kwa faida ya jamii kwa ujumla”. alisema Dk. Kigwangalla.

Awali akiwasilisha mada kuhusu hali ya sekta ya misitu nchini, Prof. Romanus Ishengoma wa Chuo Kikuu cha Sokoine - SUA alisema changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo ni ukataji holela wa miti ambapo takwimu za NAFORMA zinaonyesha kuwa Tanzania inapoteza hekta 372,000 za misitu kwa mwaka.

Alisema changamoto nyingine ni uchomaji moto misitu, uvunaji wa mkaa, uingizaji mifugo kwenye maeneo ya hifadhi, kukosekana kwa mpango bora wa matumizi ya ardhi, utegemezi uliokithiri kwenye mazao ya misitu, uanzishwaji wa makazi mapya na utegemezi wa nishati ya kuni. Alisema changamoto hizo zinahitaji Sera madhubuti za kukabiliana nazo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa alisema, Rasimu hiyo ya Sera mpya ya Misitu itakamilika kwa wakati kama alivyoelekeza Waziri Kigwangalla na kwamba maoni yote ya wadau yatazingatiwa katika Rasimu hiyo.


Warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika mjini Dodoma iliandaliwa kwa ushirikiano wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Shirika la Uendelezaji wa Nishati Endelevu za Kisasa Tanzania (TATEDO), Kundi la Uhifadhi wa Misitu Tanzania (TFCG), Wizara ya Maliasili na Utalii na Ubalozi wa Switzerland nchini. 
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza wakati wa ufunguzi wa  warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiteta jambo na Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo. 
Baadhi ya wajumbe walioshiriki warsha hiyo wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal Briquettes ltd, Abdala Seushi kuhusu nishati mbadala ya mkaa mkombozi wa afya na mazingira muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal Briquettes ltd, Abdala Seushi kuhusu majiko banifu ya mkaa muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza katika warsha hiyo.
Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli akizungumza katika warsha hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) akipokea zawadi ya nishati mbadala ya mkaa mkombozi wa afya na mazingira kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal Briquettes ltd, Abdala Seushi (wa tatu kushoto) muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa. 
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo. 
 Prof. Romanus Ishengoma wa Chuo Kikuu cha Sokoine - SUA akiwasilisha mada kuhusu hali ya sekta ya misitu nchini katika warsha hiyo.
Picha ya pamoja.
Meza kuu, Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Uhifadhi wa Misitu Tanzania, Charles Meshak (wa pili kushoto), Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Doto Biteko (kulia).
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandhishi wa habari muda mfupi baada ya ufunguzi wa warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.