Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasili katika ukumbi wa Hoteli ya Morena mjini Dodoma jana kwa ajili ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera
mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha
sekta hiyo.
Na Hamza Temba - WMU
............................................................
“Natoa agizo mchakato
huu ukamilike ndani ya mwezi huu wa 11, tarehe moja mwezi wa 12 mlete rasimu
ambayo nyie wataalamu mmeridhika nayo, muiwasilishe kwangu mimi na Mhe. Naibu
Waziri, na siku hiyo mtakayoiwasilisha kwetu mniletee timu ya wataalamu watakaonishauri
kwenye maeneo mbalimbali.
Na Hamza Temba - WMU
............................................................
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza kukamilishwa haraka kwa rasimu mpya ya
Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 2016 ili kuwezesha upatikanaji wa Sera, Sheria
na Kanuni mpya za usimamizi wa rasilimali za misitu nchini kwa ufanisi zaidi.
Ameagiza wataalamu wa
Wizara hiyo kukamilisha rasimu hiyo mwezi huu wa Novemba na iwasilishwe kwake mapema
mwezi ujao (Desemba) ili aweze kupata ushauri zaidi wa wataalamu wengine huru kabla ya kuwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri na baadaye kutungiwa Sheria na Kanuni za
utekelezaji.
Dk. Kigwangalla ametoa
agizo hilo jana mjini Dodoma wakati akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa
misitu iliyolenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki,
pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
“Pamoja na hao wataalamu
washauri nataka watu wengine huru wahusike kwenye kunishauri, ili nipate picha
ya watu wengine huru kabla hatujatengeneza andiko ambalo tutalipeleka kwenye kikao
cha baraza la Mawaziri, waje wanishauri maeneo yanayotaji maboresho, kuongeza ubunifufu
au kukazia zaidi”. Aliagiza Dk. Kigwangalla.
Alisema amelazimika
kuharakisha zoezi hilo ili Sera hiyo ikamilike haraka iweze kushughulikia changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo ongezeko la watu linalosababisha misitu
mingi kuteketezwa kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kupitia
shughuli za kilimo na uanzishwaji wa makazi mapya.
Alisema pamoja na
misitu kuonekana inachangia kidogo kwa asilimia 3.5 kwenye pato la taifa, bado mchango
wake ni mkubwa kuliko inavyochukuliwa hivi sasa. Alisema tafiti zilizofanywa
awali hazikuzingatia mambo muhimu ikiwemo mchango halisi wa misitu kwenye
upatikanaji wa maji ambayo huzalisha umeme, hunywesha mifugo na wanyamapori,
matumizi ya majumbani na kilimo cha umwagiliaji.
Alisema ili kupata
mchango halisi wa misitu kwenye uchumi mpana wa taifa letu, Wizara yake imeshaandaa
andiko maalum kwa ajili ya kuendesha utafiti mkubwa wa kubaini mchango huo na kazi
inayofanyika hivi sasa ni ya utafutaji wa fedha kutoka kwa wadau mbalimbali
kufanikisha utafiti huo.
Akizungumzia Uhifadhi Shirikishi
Jamii, Dk. Kigwangalla alisema kwa zaidi ya asilimia 32 ya maeneo yote nchini yamehifadhiwa
kisheria, hivyo njia rahisi ya kuyalinda ni kupitia ushirikishwaji wa wananchi.
“Bila kufanya hivyo hatuwezi kusema tuna askari wa kutosha kulinda misitu yote,
mbuga zote za wanyama au mapori yote tengefu nchini.
“Lakini nje ya maeneo hayo
kuna maeneo ya vijiji ambayo pia yamehifadhiwa, yote haya huwezi kusema
utayalinda kirahisi sana bila ushiriki wa wananchi, kuwaleta wananchi kwenye
uelewa wa pamoja, kwamba tunahifadhi kwa faida yao.
“Tuwaelimishe, kwa mfano
usipohifadhi misitu kiwango cha mvua kitashuka, usalama wa chakula utaathirika,
upatikanaji wa maji safi na salama utaathirika, upatikanaji wa umeme nao pia utaathirika,
hivyo tunahifadhi kwa faida ya jamii kwa ujumla”. alisema Dk. Kigwangalla.
Awali akiwasilisha mada
kuhusu hali ya sekta ya misitu nchini, Prof. Romanus Ishengoma wa Chuo Kikuu cha
Sokoine - SUA alisema changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo ni ukataji
holela wa miti ambapo takwimu za NAFORMA zinaonyesha kuwa Tanzania inapoteza
hekta 372,000 za misitu kwa mwaka.
Alisema changamoto
nyingine ni uchomaji moto misitu, uvunaji wa mkaa, uingizaji mifugo kwenye
maeneo ya hifadhi, kukosekana kwa mpango bora wa matumizi ya ardhi, utegemezi
uliokithiri kwenye mazao ya misitu, uanzishwaji wa makazi mapya na utegemezi wa
nishati ya kuni. Alisema changamoto hizo zinahitaji Sera madhubuti za kukabiliana
nazo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa alisema, Rasimu hiyo ya Sera mpya ya Misitu itakamilika kwa wakati kama alivyoelekeza Waziri Kigwangalla na kwamba maoni yote ya wadau yatazingatiwa katika Rasimu hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa alisema, Rasimu hiyo ya Sera mpya ya Misitu itakamilika kwa wakati kama alivyoelekeza Waziri Kigwangalla na kwamba maoni yote ya wadau yatazingatiwa katika Rasimu hiyo.
Warsha hiyo ya siku moja
iliyofanyika mjini Dodoma iliandaliwa kwa ushirikiano wa Mtandao wa Jamii wa
Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Shirika la Uendelezaji wa Nishati
Endelevu za Kisasa Tanzania (TATEDO), Kundi la Uhifadhi wa Misitu Tanzania (TFCG),
Wizara ya Maliasili na Utalii na Ubalozi wa Switzerland nchini.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia)
akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha
ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga
kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto
na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto)
akiteta jambo na Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli muda mfupi
baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini
Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya
Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta
hiyo.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki warsha hiyo wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa
pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal
Briquettes ltd, Abdala Seushi kuhusu nishati mbadala ya mkaa mkombozi wa afya
na mazingira muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu
iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu
ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya
kuboresha sekta hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia)
akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal Briquettes ltd,
Abdala Seushi kuhusu majiko banifu ya mkaa muda mfupi baada ya kufungua warsha
ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga
kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto
na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara
hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza katika warsha hiyo.
Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli akizungumza katika warsha hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa
pili kushoto) akipokea zawadi ya nishati mbadala ya mkaa mkombozi wa afya na mazingira
kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal Briquettes ltd, Abdala Seushi (wa
tatu kushoto) muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu
iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu
ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya
kuboresha sekta hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa
Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia)
akizungumza na Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli muda mfupi
baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini
Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya
Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta
hiyo.
Prof. Romanus Ishengoma wa Chuo Kikuu cha Sokoine - SUA akiwasilisha mada kuhusu hali ya sekta ya misitu nchini katika warsha hiyo.
Picha ya pamoja.
Meza kuu, Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Uhifadhi wa Misitu Tanzania, Charles Meshak (wa pili kushoto), Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Doto Biteko (kulia).
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza
na waandhishi wa habari muda mfupi baada ya ufunguzi wa warsha ya siku moja ya wadau
sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho
ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati
mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
No comments:
Post a Comment