slider gif
kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ
Friday, December 8, 2017
Tuesday, December 5, 2017
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, JAPHET HASUNGA ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KITULO, MAARUFU KAMA BUSTANI YA MUNGU
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Veronika Kessy wakiangalia maua ya asili ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii katika hifadhi ya Taifa ya Kitulo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Hifadhi hiyo ni maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo hayapatikani kwengineko duniani. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa wenyeji kama 'BUSTANI YA MUNGU'.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Makete, Veronika Kessy (kulia) na baadhi ya viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo wakiangalia maua ya asili ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii katika hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Hifadhi hiyo ni maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo hayapatikani kwengineko duniani.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa nne kulia), akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Veronika Kessy (wa tatu kulia) na baadhi ya viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Hifadhi hiyo ni maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo hayapatikani kwengineko duniani.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Makete, Veronika Kessy na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kitulo, Pius Mzimbe wakiangalia maporomoko ya maji ya Mwakipembo ambayo ni kivutio cha utalii ndani ya hifadhi ya Kitulo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Pamoja na kivutio hicho hifadhi hiyo ni maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo hayapatikani kwengineko duniani. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa wenyeji kama 'BUSTANI YA MUNGU'.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akipata maelezo kuhusu maporomoko ya maji ya Mwakipembo ambayo ni kivutio cha utalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Kitulo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Pius Mzimbe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Makete, Veronika Kessy. Pamoja na kivutio hicho hifadhi hiyo ni maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo hayapatikani kwengineko duniani.
Muonekano mwanana wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo. Hifadhi hii ina aina zaidi ya 350 za maua huku aina 35 yakiwa ndwele na hupatikana katika hifadhi hiyo pekee duniani. Vivutio vingine vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ni Maporomoko ya maji, ndege aina mbalimbali ambao wengine huama kutoka ulaya wakati wa baridi, wanyamapori aina Swala, Mbega na Nsya. Hata hivyo katika kutimiza mkakati wa Wizara kuboresha vivutio vya utalii, hifadhi hiyo ipo katika maandalizi ya kuanzisha makazi ya Pundamilia na wanyama wengine. Awamu ya kwanza ya kuhamisha pundamiliz 25 kutoka hifadhi ya taifa ya mikumi inatarajiwa kukamilika mwishoni mw mwaka huu. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa wenyeji kama 'BUSTANI YA MUNGU'.
Aina mojawapo ya ua ambalo hupatikana katika hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo, Pius Mzimbe (kushoto) akimuonyesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) sehemu ya eneo lililochaguliwa ndani ya hifadhi hiyo kwa ajili ya kuanzisha makazi ya Pundamilia 25 watakaohamishwa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Mikumi. Alisema kabla ya mwaka huu kuisha Pundamilia hao watakuwa wameshahamishiwa eneo hilo. Huo ni mkakati wa wizara na Serikali katika kuboresha vivutio vya utalii nchini ili kuongeza idadi ya watalii na mapato.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisalimiana na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo alipowasili makao makuu ya hifadhi hiyo yaliyopo Makete mkoani Njombe jana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo makao makuu ya hifadhi hiyo yaliyopo Makete mkoani Njombe. Amewaaka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na ubunifu, kujiepusha na vitendo vya rusha, kuweka mikakati wa kudhibiti mifugo kuingia hifadhini na sio kusubiri iingie na kuanza kutangaza kuikamata au kuitaifisha, kupunguza malalamiko ya wananchi jirani na hifadhi hiyo, kuongeza idadi ya mapato ya hifadhi na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo. (Picha na Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii)
ALICHOSEMA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, JAPHET HASUNGA BAADA YA KUTEMBELEA MAPOROMOKO YA MTO KIMANI KATIKA PORI LA AKIBA MPANGA KIPENGELE
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akionyeshwa njia ya kuelekea kwenye maporomoko ya maji ya mto Kimani na Kaimu Meneja wa Pori la Akiba la Mpanga Kipengele, Stanslaus Odhiambo (katikati) alipotembelea maporomoko hayo katika Wilaya ya Makete Mkoani Njombe. Maporomoko hayo ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii katika pori hilo yana urefu wa mita zaidi ya 70. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akionyeshwa maporomoko ya maji ya mto Kimani na Kaimu Meneja wa Pori la Akiba la Mpanga Kipengele, Stanslaus Odhiambo (katikati) alipotembelea maporomoko hayo jana katika Wilaya ya Makete Mkoani Njombe. Maporomoko hayo ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii katika pori hilo yana urefu wa mita zaidi ya 70. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune kwenda eneo la maporomoko ya maji ya mto Kimani ambayo yapo ndani ya Pori la Akiba la Mpanga Kipengele katika Wilaya ya Makete Mkoani Njombe. Maporomoko hayo ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii katika pori hilo yana urefu wa mita zaidi ya 70.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akiangalia maporomoko ya maji ya mto Kimani alipotembelea Pori la Akiba la Mpanga Kipengele katika Wilaya ya Makete Mkoani Njombe. Maporomoko hayo ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii katika pori hilo yana urefu wa mita zaidi ya 70.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, David Kanyata (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa Pori la Akiba la Mpanga Kipengele alipotembelea maporomoko ya maji ya mto Kimani ambayo yapo ndani ya pori hilo katika Wilaya ya Makete Mkoani Njombe. Maporomoko hayo ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii katika pori hilo yana urefu wa mita zaidi ya 70.
Maporomoko ya Maji ya Mto Kimani ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele katika Wilaya ya Makete mkoani Njombe. Maporomoko hayi yana urefu wa mita zaidi ya 70.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune wakiangalia moja fuvu la mnyamapori katika moja ya pango ambalo ambalo Chief Mkwawa alilitumia kujificha wakati wa vita na wakoloni alipotembelea Pori la Akiba la Mpanga Kipengele katika Wilaya ya Makete Mkoani Njombe.
Picha ya pamoja. (Picha na Hamza Temba)
Sunday, December 3, 2017
IJUE BARABARA YA LAMI AMBAYO NI KIVUTIO CHA UTALII NCHINI, SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA YA KIVUTIO HICHO
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akiongozwa na Meneja wa shamba la Miti Kawetire, Arnorld Shoo kukagua moja ya eneo katika shamba hilo ilipopita barabara ya lami ambayo ipo juu zaidi ya nyingine nchini ikiwa na urefu (Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa wa bahari wakati wa zaira yake ya kikazi jana mkoani Mbeya. Alisema Serikali itaboresha mazingira ya eneo hilo ili yatumike kama kivutio cha utalii nchini.
Bofya kitufe cha PLAY kuangalia VIDEO
Na Hamza Temba, Mbeya
........................................................
Serikali imesema
itaboresha mazingira ya kivutio cha utalii cha barabara ya lami ambayo ipo juu
zaidi kutoka usawa wa bahari kuliko barabara zote nchini ili kupanua wigo wa
vivutio vya utalii na kuongeza idadi ya watalii na mapato.
Hayo yameelezwa jana na
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga baada ya kutembelea shamba
la miti la Kawetire wilayani Mbeya na kujionea sehemu ya barabara ya lami
inayopita katikati ya shamba hilo katika mlima Kawetire kwenye safu za milima
ya Mbeya.
Eneo hilo la barabara hiyo
ambayo hupitisha magari kutoka Jijini Mbeya kwenda katika Wilaya ya Chunya na
Mikoa ya Singida na Tabora lina urefu (Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa wa
bahari katika Latitude 08’ 35 S na Longitude 33’ 25 E.
“Hatutaki ule utalii
wa kutegemea wanyamapori pekee, hii sasa ni sehemu ya aina nyingine ya utalii
ambayo ni lazima tuiboreshe tuweke kibao kizuri tuweke mazingira mazuri pamoja
na kukitangaza ili watanzania na watalii kutoka nje waweze kutembelea hapa,”
alisema Hasunga.
Alisema ili kufikia
lengo liliwekwa na Serikali la kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni mbili
mwaka 2020 na milioni 8 mwaka 2025 vivutio vyote vya utalii vilivyopo nchini
vitatambuliwa, kuimarishwa na kuviwekea miundombinu itakayowavutia watalii
kuvitembelea.
Aidha aliuagiza
uongozi wa shamba hilo kushirikiana na wakala wa huduma za barabara –Tanroads
katika kuboresha mazingira yanayozunguka eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka
bango la kisasa la kutambulisha eneo hilo, kujenga bustani na maeneo rafiki ya
kupumzikia kwa ajili ya kuwavutia watalii kutembelea eneo hilo na kupiga picha.
Mbali na kivutio hicho
aliuagiza uongozi wa shamba hilo kutobomoa majengo ya kale yaliyotumiwa na
wakoloni katika shamba hilo na badala yake yatumike kwenye utalii wa mambo ya
kale sambamba na utalii wa misitu ya kupandwa inayopatikana pia katika shamba
hilo.
Hata hivyo alisema
kupitia mradi wa REGROW wa kuendeleza utalii kanda ya kusini Serikali imepokea
mkopo wa masharti nafuu wa dola za Kimarekani milioni 150 sawa za zaidi ya
bilioni 340 za kitanzania kutoka benki ya dunia kwa ajili ya kusaidia kuboresha
miundombinu ya vivutio vya ukanda huo.
Kwa upande wake Meneja
wa shamba hilo, Arnorld Shoo alisema eneo hilo la barabara limekuwa ni kivutio
cha kipekee cha utalii katika shamba hilo ambapo pia hupata mapato kupitia watu
na vikundi mbalimbali ikiwemo wanakwaya na wanafunzi ambao hufika eneo hilo kwa
ajili ya kupiga picha za kumbukumbu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) na Meneja wa shamba la Miti Kawetire, Arnorld Shoo wakiangalia bango linaloonesha eneo katika shamba hilo ilipopita barabara ya lami ambayo ipo juu zaidi ya nyingine nchini ikiwa na urefu (Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa wa bahari wakati wa zaira yake ya kikazi jana mkoani Mbeya. Alisema Serikali itaboresha mazingira ya eneo hilo ili yatumike kama kivutio cha utalii nchini.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA ATOA MIEZI MITATU WANANCHI WALIPWE FIDIA WAPISHE ENEO LA HIFADHI
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na watumishi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengele alipotembelea makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wangin'ombe mkoani Njombe. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, David Kanyata na Kaimu Meneja wa pori hilo, Stanslaus Odhiambo.
Na Hamza Temba, Mbarali - Mbeya
.......................................................................................
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ametoa miezi mitatu kwa uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kukamilisha malipo ya fidia ya shilingi milioni 771.6 kwa kaya 308 za Kitongoji cha Machimbo ili ziweze kupisha eneo la hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele.
Naibu Waziri Hasunga ametoa agizo hilo jana katika mkutano wa hadhara baada kutembelea kitongoji hicho katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutatua migogoro kwenye maeneo ya hifadhi mkoani humo.
“Kaimu Mkurugenzi (TAWA) kama unavyoona wananchi hawa wapo tayari kupisha eneo hili la hifadhi, wanachosubiri ni malipo yao ya fidia, naagiza mpaka ifikapo mwezi Februari mwakani (2018) wawe wameshalipwa fidia zao, na ikiwezekana hata ndani ya mwezi Januari wawe wameshalipwa,”alisema Hasunga.
Awali akiwasilisha taarifa ya pori hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, David Kenyata alisema wakati pori hilo linaanzishwa mwaka 2002 kwa Tangazo la Serikali Na. 483 wananchi wa kitongoji hicho na vitongoji vingine walikuwa ndani ya eneo hilo la hifadhi.
Alisema mazungumzo yalishafanywa kupitia vikao halali vya uongozi wa viijiji na halmashauri ambapo wananchi hao waliridhia kulipwa fidia ili kuachia maeneo hayo ya hifadhi.
Alisema sababu kubwa ya kuanzishwa kwa pori hilo ni pamoja na kuhifadhi vyanzo vya maji yanayotiririka kwenda mto Ruaha na kwenye mabwawa ya kidatu na mtera yanayotumika kuzalisha umeme nchini.
Akizungumzia malipo ya fidia kwa vijiji na vitongoji vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo alisema kijiji kimoja kilishalipwa mwaka 2015 jumla ya shlingi milioni 500 na vijiji vilivyosalia vitalipwa kwa awamu ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 fedha zimetengwa kwa ajilia ya kulipa wananchi wa kitongaoji cha Machimbo ambao tayari walishafanyiwa uthamini mwaka 2015.
Awali akizungumza na watumishi wa Pori hilo katika ofisi zao zilizopo Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, Naibu Waziri Hasunga aliwataka watumishi hao kuongeza nguvu na ubunifu kwenye kuzuia mifugo isiiingie hifadhini badala ya kusubiri iingie ndipo waikamate na kuitoza faini au kuitaifisha.
“Nyie ni watalaamu, tumieni mbinu na ubunifu wenu wote muhakikishe mnazuia mifugo isiingie hifadhini, sitaki kusikia mmekamata au mmetaifisha mifugo hifadhini, hiyo siyo sifa, sifa ni kuzuia isiingie kabisa, na nitawapima kwa hilo,” alisema Hasunga.
Aidha aliwataka watumishi hao kuimarisha uhifadhi shirikishi, kujiepusha na vitendo vya rushwa, kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kuongeza ubunifu utakaowezesha ongezeko la mapato ya Serikali.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo aliwatembelea wananchi wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji katika Skimu ya Igomelo ambao awali waligomea zoezi la uwekwaji wa vigingi vya mpaka kwenye eneo lao na Pori la Akiba la Mpanga Kipengele kwa hofu ya kupoteza maeneo hayo.
Hata hivyo baada ya kuwaelimisha kuwa lengo la zoezi hilo ni kuiwezesha Serikali kufanya uamuzi wa mwisho wa kumaliza migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu baina ya vijiji na maeneo ya hifadhi nchini wananchi hao walielewa na kuahidi kushirikiana na mamlaka husika kukamilisha zoezi hilo kwa muda uliopangwa.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Pori hilo, Stanslaus Odhiambo alisema pori hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uwepo wa vijiji na vitongoji 13 ndani ya pori hilo, uchomaji moto maeneo ya hifadhi, ukataji miti hovyo, ujangili na uhaba wa vitendea kazi.
Pori la Akiba la Mpanga Kipengele lina ukubwa wa Kilometa za mraba 1574.25 katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya na Wilaya za Wanging’ombe na Makete Mkoani Njombe.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (waliokaa mbele katikati) akizungumza na watumishi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengele alipotembelea makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wangin'ombe mkoani Njombe.
Baadhi ya watumishi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengele wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (hayuko pichani).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akisalimiana na Kaimu Meneja wa Pori la Akiba la Mpanga Kipengele, Stanslaus Odhiambo muda mfupi baada ya kuwasili makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.
Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Machimbo wapatao kaya 308 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ambaye aliwatembelea jana na kuagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania iwalipe fidia ya shilingi milioni 771.6 kabla ya Februari, 2018 ili wapishe eneo la Hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele alipowatembelea.
Saturday, December 2, 2017
DK. KIGWANGALLA ATOA SIKU 30 KWA WAMILIKI WA MAGOGO YALIYOKAMATWA BANDARINI DAR KUJITOKEZA
Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam
.............................................................................
.............................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Kigwangalla, amefanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar es Salaam ambapo ameagiza Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii atangaze kujitokeza kwa wamiliki wa magogo 938 yaliyokaa bandarini kwa zaidi ya miaka 10. Kama wamiliki wasipojitokeza, magogo hayo yatakuwa mali ya Serikali.
Aidha Dkt. Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wamiliki wa makontena 55 yanayodaiwa kuingizwa nchini kutoka Zambia kujitokeza na kuwasilisha nyaraka zao zenye kuthibitisha kama kweli yalivunwa nchini Zambia na yalivunwa wapi na kwa vibali gani vya nchi hiyo. Pia kufuatilia nyaraka za kuingiza ndani ya Tanzania. Ameagiza kitengo cha kuzuia ujangili kifuatilie kubaini uhalisia na uhalali wa taarifa hizo vinginevyo yatakuwa mali ya Serikali.
Dkt. Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo kufuatia uwepo wa taarifa za uvunaji holela wa magogo nchini, ambapo kuna taarifa kuwa kuna wafanyabiashara wa kigeni wanagawa vifaa vya kuvunia bure kwa ahadi ya kuuziwa mzigo na wahusika, pia uwepo wa taarifa kwamba kuna baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanatoa vibali na kugonga nembo kinyume cha taratibu za kisheria. Hali inayotishia usalama wa raslimali adimu ya misitu yetu ya asili.

Dkt. Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo kufuatia uwepo wa taarifa za uvunaji holela wa magogo nchini, ambapo kuna taarifa kuwa kuna wafanyabiashara wa kigeni wanagawa vifaa vya kuvunia bure kwa ahadi ya kuuziwa mzigo na wahusika, pia uwepo wa taarifa kwamba kuna baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanatoa vibali na kugonga nembo kinyume cha taratibu za kisheria. Hali inayotishia usalama wa raslimali adimu ya misitu yetu ya asili.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangallaakitoa maagizo kwa uongozi wa bandari ya TPA.


Baadhi ya magogo hayo yaliyokutwa katika makontena bandarini hapo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakiwa katika eneo la bandari ya nchi kavu ya Malawi Cargo. wakati wa kukagua magogo hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya mbao zilizokutwa bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya mbao zilizokutwa bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa nyaraka ya idadi ya makontena katika eneo la Malawi Cargo.
Zoezi la ukaguaji likiendelea
Baadhi ya magogo yaliyokutwa bandarini hapo.
Subscribe to:
Posts (Atom)


