slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Saturday, December 2, 2017

DK. KIGWANGALLA ATOA SIKU 30 KWA WAMILIKI WA MAGOGO YALIYOKAMATWA BANDARINI DAR KUJITOKEZA

Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam
.............................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Kigwangalla, amefanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar es Salaam ambapo ameagiza Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii atangaze kujitokeza kwa wamiliki wa magogo 938 yaliyokaa bandarini kwa zaidi ya miaka 10. Kama wamiliki wasipojitokeza, magogo hayo yatakuwa mali ya Serikali.
Aidha Dkt. Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wamiliki wa makontena 55 yanayodaiwa kuingizwa nchini kutoka Zambia kujitokeza na kuwasilisha nyaraka zao zenye kuthibitisha kama kweli yalivunwa nchini Zambia na yalivunwa wapi na kwa vibali gani vya nchi hiyo. Pia kufuatilia nyaraka za kuingiza ndani ya Tanzania. Ameagiza kitengo cha kuzuia ujangili kifuatilie kubaini uhalisia na uhalali wa taarifa hizo vinginevyo yatakuwa mali ya Serikali. 

Dkt. Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo kufuatia uwepo wa taarifa za uvunaji holela wa magogo nchini, ambapo kuna taarifa kuwa kuna wafanyabiashara wa kigeni wanagawa vifaa vya kuvunia bure kwa ahadi ya kuuziwa mzigo na wahusika, pia uwepo wa taarifa kwamba kuna baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanatoa vibali na kugonga nembo kinyume cha taratibu za kisheria. Hali inayotishia usalama wa raslimali adimu ya misitu yetu ya asili. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangallaakitoa maagizo kwa uongozi wa bandari ya TPA.Baadhi ya magogo hayo yaliyokutwa katika makontena bandarini hapo.Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakiwa katika eneo la bandari ya nchi kavu ya Malawi Cargo. wakati wa kukagua magogo hayo.Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya mbao zilizokutwa bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo.Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya mbao zilizokutwa bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo.Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa nyaraka ya idadi ya makontena  katika eneo la Malawi Cargo.Zoezi la ukaguaji likiendeleaBaadhi ya magogo yaliyokutwa bandarini hapo.

No comments:

Post a Comment