slider gif
kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ
Tuesday, February 20, 2018
Friday, February 16, 2018
DK. KIGWANGALLA AMALIZA MGOGORO WA HIFADHI NA WANANCHI WILAYANI RUFIJI
Na Hamza Temba (WMU) - Rufiji, Pwani
.....................................................................
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya
miaka minne baina ya Hifadhi ya Msitu wa Utete maarufu kama Msitu wa Kale na vitongoji
vinavyopakana na hifadhi hiyo vya Siasa, Nyawanje, Kindwitwi na Utunge katika
wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.
Dk. Kigwangalla amemaliza
mgogoro huo kwa kumuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania,
Prof. Dos Santos Silayo kuunda timu ya wataalamu watakaoshirikiana na wataalamu
wa mkoa wa Pwani na wilaya ya Rufiji kwa ajili ya kufanya tathmini ya eneo
lenye mgogoro na kuanzisha mchakato wa kisheria wa kurekebisha mipaka ya eneo
hilo na hatimaye kuligawa kwa wananchi.
Dk. Kigwangalla ametoa
agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Utete,
wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua
migogoro baina ya hifadhi na wananchi mkoani humo.
“Nimejiridhisha kwamba
hakutokuwa na madhara yeyote yale, kama tutamega eneo la msitu wa Hifadhi
kidogo ambalo wananchi wamekuwa wakilima miaka yote hii na kulirusha kwa
wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo kuliko kuendelea kulihifadhi wakati
wananchi wanakosa mahala pa kupata riziki yao.
“Naagiza Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, uunde timu ya wataalam waje
washirikiane na wataalam wa mkoa na wilaya, wafanye tathmini kwenye lile eneo
ambalo wananchi wamekuwa wakilima kabla hata msitu haujawa ‘gazzeted’
(haujatagazwa) kuwa hifadhi ili muone ni kwa kiasi gani mnaweza mkamega eneo na
kulirudisha kwa wananchi ili waweze kuendelea na kilimo,” aliagiza Dk.
Kigwangalla.
Ameagiza pia kamati
hiyo ifanye tathmini ya eneo la chemchem ambalo ni sehemu ya hifadhi hiyo ambalo
limevamiwa kwa kiasi kikubwa na makazi ya wananchi ili waweze kurekebisha
mipaka yake na hatimaye wananchi wabaki na eneo lao la makazi na eneo litakalobakia
liendelee kuhifadhiwa.
“Kamati hiyo pia ije
ifanye tahtmini inawezaje kuhamisha mipaka ya hifadhi ili kupisha zile nyumba
ambazo zimeshajengwa pale kwa sasa na hapo sasa wananchi wawe hawana mgogoro na
hifadhi, waishi kwenye eneo lao na waiache hifadhi upande wa pili, lakini sasa
waishi kwa mujibu wa sheria kuliko ilivyo hivi sasa tunavyowachukulia kama
wavamizi;” alisema Dk. Kigwangalla.
Aidha Dk. Kigwangalla
ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kutafuta eneo mbadala la
msitu ambalo ni mali ya vijiji likabidhiwe kwa Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania ili liweze kuhifadhiwa ikiwa ni fidia ya eneo hilo la Hifadhi ya Msitu
wa Utete litakalokabidhiwa kwa wananchi kwa ajili ya kilimo na makazi.
Mbali na maagizo hayo Dk.
Kigwangalla ameagiza pia wananchi waliolima kwenye bonde katika Hifadhi hiyo
wasiondolewe katika msimu huu wa kilimo wakati zoezi la uwekaji wa mipaka
likiwa linaendelea.
Hifadhi ya Msitu wa
Utete ilianzishwa kwa tangazo la Serikali Na. 1cap 132p 1351 la tarehe 1
Oktoba, 1957 ikiwa na jumla ya ekari 2,346. Desemba 2015 msitu huo ulipimwa
tena na kuchorewa ramani.
Wananchi wanaozunguka
hifadhi hiyo wamedai kuwepo katika baadhi ya maeneo hayo ya hifadhi hata kabla
ya kuanzishwa kwa hifadhi hiyo, hivyo wameiomba Serikali iwamegee maeneo katika
hifadhi hiyo ili waweze kuendeleza shughuli zao za kilimo na makazi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kuhusu kivutio cha utalii cha Chemchem
ya Maji ya Moto yanayofikia nyuzi joto 75 katika Msitu wa Hifadhi wa Chemchem wakati
wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika
Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akijadili jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya
Rufiji, Rajab Mbonde na Mbunge wa Rufiji, Mohammed Mchengerwa kuhusu mgogoro wa
mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa Utete na vijiji jirani wakati wa ziara yake ya kutatua
migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi wilayani humo mkoani Pwani jana
ambapo alitoa maelekezo kadhaa ya kufanywa ili kumaliza mgogoro huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rufiji,
Rajab Mbonde kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa Utete na vijiji
jirani wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya
hifadhi wilayani humo mkoani Pwani jana ambapo alitoa maelekezo kadhaa ya kufanywa
ili kumaliza mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Rufiji, Mohammed Mchengerwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Utete katika wilaya ya Rufiji
Mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa Utete na vijiji
jirani wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya
hifadhi wilayani humo mkoani Pwani jana ambapo alitoa maelekezo kadhaa ya kufanywa
ili kumaliza mgogoro huo.
Baadhi ya wananchi walioshiriki mkutano huo.
Baadhi ya wananchi walioshiriki mkutano huo.
Wednesday, February 14, 2018
Hifadhi ya Mikumi yaiomba Serikali kuchepusha barabara ya lami inayopita ndani ya Hifadhi hiyo
Na Hamza Temba-WMU-Morogoro
................................................................
Serikali inafikiria namna bora ya kubadilisha uelekeo wa eneo la kilometa hamsini za barabara ya lami inayopita ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi au kutoza kodi ya utalii kwa watu wanaotumia barabara hiyo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazosabishwa na barabara hiyo kwenye uhifadhi.
Serikali inafikiria namna bora ya kubadilisha uelekeo wa eneo la kilometa hamsini za barabara ya lami inayopita ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi au kutoza kodi ya utalii kwa watu wanaotumia barabara hiyo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazosabishwa na barabara hiyo kwenye uhifadhi.
Hayo yamesemwa mkoani Morogoro na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kufuatia ombi la uongozi wa hifadhi hiyo la kuiomba Serikali kuchepusha barabara hiyo kutokana na athari mbalimbali za kimazingira zinazosabishwa na uwepo wa barabara hiyo ndani ya hifadhi hususan vifo vya mara kwa mara vya wanyamapori, ujangili na ukosefu wa mapato ya Serikali.
Awali akiwasilisha taarifa ya hifadhi
hiyo mbele ya Waziri Kigwangalla, Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Gerald
Mono alisema licha ya barabara hiyo kuwa na fursa nyingi za kimaendeleo imekuwa
na changamoto nyingi kwenye uendeshaji wa shughuli za uhifadhi.
Alisema wastani wa mnyamapori mmoja
hugongwa na gari kila siku katika barabara hiyo ambapo takwimu zinaonyesha kuwa
mwaka 2014 idadi ya wanyamapori waliogongwa walikuwa 351, mwaka 2015 walikuwa 361
na mwaka 2016 walikuwa 218.
Alisema changamoto nyingine ni
uchafuzi wa mazingira ambapo wastani wa taka ngumu zisizopungua kilo 138.3
huzalishwa kila siku na watumiaji wa barabara hiyo.
Mbali na changamoto hizo alisema nyingine
ni ukosefu wa mapato ya Serikali kufuatia kukosekana kwa mageti ya kulipia tozo
za utalii kwa watumiaji wa barabara hiyo ambao hufaidi utalii wa bure na
kuikosesha Serikali mapato.
Alisema Changamoto nyingine ni
ujangili ambao huchochewa na uwepo wa barabara hiyo ambayo hutoa fursa kwa
majangili kuingia katika hifadhi hiyo kiurahisi kwa njia mbalimbali ikiwemo
magari na pikipiki.
“Hifadhi inaiomba Serikali kuchepusha
barabara hii ili kupunguza changamoto hizi zinazotokana na uwepo wa barabara
husika na kuongeza mapato ya Hifadhi kwa kuzuia utalii a bure unaofanywa na
watumiaji wa barabara wa ndani na nje,”. Alisema Kaimu Mhifadhi Mkuu huyo wa
Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema changamoto kubwa aliyoiona katika
hifadhi hiyo ni namna ya watalii kufika na kufanya shughuli za utalii katika
hifadhi hiyo.
Alisema licha ya uwepo wa barabara ya
lami inayokatiza hifadhini hapo, barabara hiyo sio rafiki kwenye uhifadhi. “Kuna
hiyo barabara ambayo inaleta watalii hapa, ni barabara ambayo iko bize sana, ni
barabara ya kitaifa na kwa vyovyote vile hii sio barabara mahsusi kwa ajili ya
shughuli za utalii.
“Sisi (Serikali) tunatafakari namna ya aidha
kuiondoa hiyo barabara au namna ya kuwachaji watu wanaokatiza hizi kilometa
hamsini ambazo zipo ndani ya hifadhi ya Mikumi,” alisema Dk. Kigwangalla.
Katika hatua nyingine Dk. Kigwangalla
amemtaka muwekezaji aliyepewa hoteli ya kitalii ya Mikumi Wildlife Lodge
iliyopo ndani ya hifadhi hiyo kwa ajili ukarabati na uendelezaji kuhakikisha anakamilisha
makubaliano hayo ndani ya muda aliyopewa kwa mujibu wa mkataba aliosaini na TANAPA
ama sivyo atanyang’anywa kibali hicho.
Akizungumzia jitihada za kuimarisha
ulinzi wa hifadhi hiyo, Dk. Kigwangalla amesema Serikali inakusudia kuharakisha
mchakato wa kuanzishwa kwa jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Kidoma
itakayojumuisha vijiji vya Kilangali, Doma na Maharaka ili kutengeneza buffer
na hatimaye kuimarisha uhifadhi shirikishi.
Hifadhi ya Taifa ya Mikumi
ilianzishwa mwaka 1964 kwa Tangazo la Serikali Na. 465 ikiwa na ukubwa wa
kilometa za mraba 1,070. Mwaka 1975 Serikali iliona umuhimu wa kuongeza eneo
upande wa kusini na kaskazini mwa Hifadhi na kufikia ukubwa wa kilometa za
mraba 3,230 kwa tangazo la Serikali Na. 121.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiongea na Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi,
Gerald Mono wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi hiyo jana mkoani
Morogoro. Uongozi wa hifadhi hiyo umeiomba Serikali kuchepusha barabara ya lami
inayopita ndani ya hifadhi hiyo kutokana na athari mbalimbali za kimazingira
zinazosabishwa na barabara hiyo ikiwemo vifo vya wanyamapori, ujangili na
ukosefu wa mapato ya Serikali unaotokana na watu kufaidi utalii wa bure.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akikagua maziringira ya jengo lililoungua moto la Mikumi Wildlife
Lodge ambalo linalofanyiwa ukarabati wakati wa ziara yake ya kikazi katika Hifadhi
ya Taifa ya Mikumi jana mkoani Morogoro ambapo amemtaka muwekezaji aliyepewa
hoteli hiyo kuikarabati ndani ya muda aliopewa ama sivyo atanyang’anywa kibali alichepewa.
Kushoto kwake ni Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Gerald Mono.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiongozwa na Kaimu Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Gerald Mono kukagua mazingira ya hifadhi
hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi hiyo jana mkoani Morogoro.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Gerald Mono wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi hiyo jana mkoani Morogoro.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mazingira mwanana ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi hiyo jana mkoani Morogoro.
Picha ya pamoja.
Monday, February 12, 2018
MAKAMU WA RAIS AZINDUA MRADI WA KUSIMAMIA MALIASILI NA KUENDELEZA UTALII KANDA YA KUSINI (REGROW)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kabrasha lenye mkataba na andiko la mradi wa Kusimamia Maliasili na Kuendeleza Utalii Kanda ya Kusini (REGROW) kuashiria uzinduzi wa mradi huo katika eneo la Kihesa Kilolo mkoani Iringa leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla kabrasha lenye Andiko la mradi wa REGROW na Mikataba ya Fedha na utekelezaji wa mradi mara baada ya kuuzindua mradi huo katika eneo la Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bi. Bella Bird muda mfupi kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa mradi huo. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Japhet Hasunga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo katika banda la Wizara ya Maliasili muda mfupi kabla ya uzinduzi wa mradi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa uwekezaji katika miundo mbinu ya mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua mradi wa REGROW.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya washiriki katika uzinduzi huo.
Baadhi ya washiriki katika uzinduzi huo.
HOTUBA YA MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN
HOTUBA YA WAZIRI WA MALIASILI, DK. HAMISI KIGWANGALLA
HOTUBA YA KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI, MAJ. GEN. GAUDENCE MILANZI
Saturday, February 10, 2018
Friday, February 9, 2018
MKUTANO WA MAWAZIRI WA SEKTA YA MALIASILI NA MAZINGIRA WA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI WAFANYIKA LEO JIJINI ARUSHA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,
Muungano na Mazingira, January Makamba wakati wa mkutano wa tano wa Baraza la
Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mkutano huo
ulilenga kujadili na kusaini makubaliano mbalimbali ya namna bora ya kusimamia sekta
hizo katika nchi wanachama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano
na Mazingira, January Makamba (kulia) akisaini baadhi ya makubaliano yaliyofikiwa
katika mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na
Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa leo katika
ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mkutano huo ulilenga kujadili na kusaini makubaliano
mbalimbali ya namna bora ya kusimamia sekta hizo katika nchi wanachama. Wanaoshuhudia
ni Mawaziri wa Mazingira kutoka Uganda na Kenya.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla (kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira, January Makamba (wa pili kulia) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania,
Bi. Katerina Rangnitt wakiangalia baadhi ya michoro ya katuni za kuhamasisha
uhifadhi wa mazingira muda mfupi baada mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la
Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa
leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mradi huo ya katuni unafadhiliwa na Serikali ya Sweden kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira, January Makamba wakimsikiliza mmoja ya wachora katuni za kuhamasisha
uhifadhi wa mazingira muda mfupi baada mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la
Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa
leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mkutano huo ulilenga kujadili na kusaini
makubaliano mbalimbali ya namna bora ya kusimamia sekta hizo katika nchi
wanachama.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
(PICHA ZOTE NA HAMZA TEMBA-WMU)
Thursday, February 8, 2018
WIZARA YA MALIASILI, ARDHI NA TAMISEMI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO – DK. KIGWANGALLA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi aliyekuwa akimunesha mpaka wa kijiji hicho na Pori la Akiba Mkungunero wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Na Hamza Temba - Kondoa, Dodoma
..........................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla jana tarehe 7 februari, 2018 ametembelea Pori la Akiba Mkungunero katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma na kuwataka wananchi wanaozunguka pori hilo kusubiri uamuzi wa Serikali utakaoshirikisha Wizara yake, Wizara ya Ardhi na Tamisemi katika kujibu maombi yao ya kutaka kupewa sehemu ya ardhi katika pori hilo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kibinadamu.
Dk. Kigwangalla ambaye aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, alitembelea vijiji vinne vya Ikengwa, Keikei Tangini, Keikei na Kisondoko na kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kujiridhisha na kujifunza juu ya mgogoro uliopo baina ya vijiji hivyo na Pori la Akiba Mkungunero.
"Nimefika hapa leo kujifunza juu ya mgogoro huu, nimejionea hali halisi lakini pia nina maelezo ya wataalamu ambayo yapo kwenye maandishi naomba niende nikayasome, niyatafakari ili niweze kushauriana na wenzangu na mwisho wa siku tuweze kuja na suluhu ya namna ya kuondokana na changamoto ambazo zimekuwepo.
"Niwaombe sana wakati Serikali inaendelea kutafuta suluhu ya mgogoro huu ni vema tukafuata sheria zilizopo, tuzingatie mipaka iliyowekwa ili tusiingie kwenye migogoro, lakini kwa sasa siwezi kwa namna yeyote ile kutamka neno la kujibu maombi ya mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji na wananchi yaliyotolewa hapa leo.
"Kama Serikali tutakaa, Wizara yangu, Wizara ya Ardhi na Tamisemi ili tujue kiini cha mgogoro huu tufanye uamuzi kuwa ni maeneo gani yaongezwe katika hifadhi kwa ajili ya wananchi au ni vitongoji vipi vifutwe, tutaleta majibu, na jambo hili tutalifanya kwa uadilifu mkubwa bila kumuonea mtu ili kumaliza mgogoro huu," alisisitiza Dk. Kigwangalla.
Awali akimkaribisha Waziri huyo kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Ikengwa, Mbunge wa jimbo hilo, Dk. Ashatu Kijaji alisema kutokana na ukweli kuwa Serikali ya awamu ya tano inasikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi, ni vema Waziri huyo akatumia hekima na kuangalia uwezekano wa kuwapa wananchi hao Kilomita 12 za mraba kutoka kwenye hifadhi hiyo kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kibinadamu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi alisema mgogoro baina ya vijiji hivyo na Pori la Akiba Mkungunero ulinza mwaka 2006 kufuatia zoezi la kuanzishwa kwake pamoja na lile na uwekagi wa vigingi vya mpaka na vijiji jirani kutoshirikisha wananchi na viongozi wa halmashauri za vijiji hoja ambayo ilipigwa na Meneja wa Pori hilo, Emannuel Bilaso.
Aidha alisema wananchi wa vijiji hivyo wanakabiliwa na uhaba wa maeneo ya kilimo na ufugaji, hivyo akamuomba Waziri huyo pamoja na Serikali kwa ujumla kutumia busara kuwamegea wananchi wa vijiji hivyo eneo la Kilomita 12 za mraba kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.
Naye Meneja wa Pori hilo, Emannuel Bilaso alisema Pori la Akiba Mkungunero lilianzishwa kwa tangazo la Serikali Na. 307 la mwaka 1996 baada ya kupandishwa hadhi kutoka Pori Tengefu. Alisema mchakato wa kupandisha hadhi pori hilo ulishirikisha wananchi na viongozi wa vijiji na wilaya ambapo mihutasari mbalimbali ilisainiwa.
Alisema pori hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazochochea mgororo huo ikiwemo kijiji kimoja cha Kisondoko kusajiliwa kimakosa ndani ya hifadhi hiyo pamoja na malalamiko mbalimbali ya wananchi kuwa hawakushirikishwa kwenye uanzishwaji wa pori pamoja na madai mengine kuwa pori hilo limeingilia mipaka ya vijiji hivyo.
Pori la Akiba Mkungunero ambalo lina ukubwa wa Kilimita za Mraba 557.9 lina umuhimu mkubwa kiuchumi na kiikolojia kwa kuwa ni chanzo muhimu cha mto Tarangire ambao ni uhai wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire na ikolojia nzima ya ziwa Manyara. Pori hilo pia ni sehemu ya mapito na mazalia ya wanyamapori pamoja na makazi ya wanyamapori adimu duniani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kondoa muda mfupi baada ya kuwasili wilayana humo jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa ramani ya Pori la Akiba Mkungunero na Mrasimu Ramani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Peter Nyange (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya Pori la Akiba Mkungunero na Mrasimu Ramani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Peter Nyange (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia) akiteja jambo na Meneja wa Pori la Akiba Mkungunero, Emannuel Bilaso wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi wakati wa ziara yake ya kikazi jana katika Pori la Akiba Mkungunero Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea mabango ya malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kisondoko kuhusu Pori la Akiba Mkungunero na vijiji jirani wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisondoko wilayani Kondoa jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya Pori la Akiba Mkungunero na mmoja wa wahifadhi wa Pori hilo wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Subscribe to:
Posts (Atom)


