slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Thursday, March 2, 2017

MTI MREFU ZAIDI BARANI AFRIKA WAGUNDULIKA KATIKA HIFADHI YA MLIMA KILIMANJARO

Mti mrefu Afrika wagunduliwa katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania
Wanasayansi wanasema kuwa wamegundua kile wanachoamini kuwa ni mti mrefu zaidi barani Afrika. Mti huo uko bonde moja lililo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika eneo la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Wanasayansi kutoka chuo cha Bayreuth nchini Ujerumani, wanasema wanaamini kuwa mti huo unaopatikana karibu na mlima Kilimanjaro ndio mrefu zaidi barani Afrika.
Mmoja wa wanasayansi hao alisema kuwa aliona mtu huo miaka 20 iliyopita, lakini ni hadi hivi majuzi wakitumia vifaa maalum walifaulu kupima urefu wake.
Mti huo kutoka familia ya 'Entandrophragma excelsum' una urefu wa mita 81.
Wanasayansi nchini Tanzania bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu ugunduzi huo.
Wanasayansi waliogundua mti huo sasa wanataka ujumuishwe kwenye kumbukumbu ya miti isiyo ya kawaida duniani. (SOURCE: BBC SWAHILI)

1 comment:

  1. kwanini wana sayansi wa tz hawajajibu kituchocote ..binafsi nimefurahishwa na hizi taarifa maana naona kivutitio kipya so inazidi kuiweka nchi yangu pahala pazuri.taarifa nzuri.

    ReplyDelete