Waziri
wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Muwakilishi
wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi
wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa
Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo
mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji.
Na Hamza Temba-WMU
.......................................................
Na Hamza Temba-WMU
.......................................................
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla leo Februari 6, 2018 ofisini kwake mjini Dodoma
amekutana na kufanya mazungumzo na Muwakilishi wa Benki ya Dunia, Daniel
Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa Kusimamia Maliasili na Kuendeleza
Utalii wa Ukanda wa Kusini -REGROW unaofadhiliwa kwa mkopo na benki hiyo ambapo
wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji.
Miongoni mwa mambo waliyojadili ni kuboresha
miundombinu ya barabara kuunganisha maeneo ya vivutio na miji ya ukanda huo pamoja
na viwanja vya ndege ndani ya hifadhi viwe na hadhi na ubora wa kutua ndege
kubwa ikiwemo za Air Tanzania.
"Nawapongeza kwa mradi huu ambao ni mzuri sana kwenye uhifadhi lakini una
mapungufu kidogo kwenye biashara ya utalii jambo ambalo ni muhimu kuangaliwa
ili uwe na tija zaidi kwa jamii na taifa kwa ujumla" alisema Dk.
Kigwangalla.
Alimuomba mratibu huyo kuona namna ya kubadilisha vipengele vya utekelezaji wa
mradi huo ili uweze kuwa na tija zaidi hususan suala la miundombinu ya
kuunganisha hifadhi mbalimbali za ukanda huo na miji ili kurahisisha usafiri wa
kufikia vivutio hivyo kwa muda mfupi na kwa wakati.
Kwa upande wake mratibu huyo alisema jambo hilo linajadilika na kwamba
uendelezaji wa maeneo hayo ni mtambuka ukihusisha Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
ambazo nazo zimeahidi kuboresha miundombinu ya maeneo hayo.
Mradi wa REGROW unatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 12 Februari mwaka huu
Mjini Iringa na Mhe. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. Mwezi Agosti mwaka
jana Serikali ya Tanzania ilisaini mkopo wa masharti nafuu wa Dola za
Kimarekani Milioni 150 sawa na takriban bilioni 340 za Tanzania kwa ajili ya
kuendeleza mradi huo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisisitiza jambo wakati
wa mazungumzo na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel
Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili
na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari
06, 2018 ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa
utekelezaji. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikiliza Muwakilishi
wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi
wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa
Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo
mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiagana na Muwakilishi
wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi
wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa
Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 baada ya kujadili mambo
kadhaa ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. Katikati ni Mratibu wa mradi
huo kutoka Tanzania, Someni Mteleka. (PICHA NA HAMZA TEMBA-WMU)
No comments:
Post a Comment