Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amewaonya watu wenye tabia ya kukata
miti ovyo kuwa Serikali hatosita kuwachukulia hatua za kisheria kutokana na
kushamiri kwa uharibifu wa misitu mkoani Songwe.
Ametoa onyo hilo
wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha
Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe.
Amesema kufuatia kasi
ya ukataji miti ovyo unaoendelea kwa ajili ya mbao na nishati ya mkaa
katika maeneo hayo kunatishia kutoweka kwa mvua wanayoitegemea kwa ajili kilimo
cha mazao ya kahawa, mahindi pamoja na mazao mengine.
Amewaeleza Wananchi
hao kuwa uharibifu huo ukiendelea utaawathiri wao wenyewe kwa
vile mvua itakoma kunyesha katika maeneo yao.
Amewataka wakikata mti
wapande miti na wale wanaokata miti kwa ajili ya Nishati ya mkaa wafuate kanuni
na sheria ili kuepuka kukabiliana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS)
Aidha, Mhe. Hasunga
Amewataka Wananchi hao kuwa hata pale inapotokea wanataka kukata mti wa
mwembe uliopo katika nyumba zao wanatakiwa kuomba kibali kutoka TFS.
Pia, Waziri
Hasunga amewaagiza TFS itoe miche 10,000 kwa Kata ya Wasa msimu wa mvua
utakapokaribia kufuatia ombi la mwanakijji Kasian Mwanjala alilowasilisha kwa
Mhe. Hasunga kuwa wanataka kupanda miti ili wanakosa miche.
"Moja ya ahadi
yangu niliyoitoa kwenu ni kuhakikisha katika jimbo langu wananchi mnapata
umeme, hadi sasa tayari nguzo za umeme zimeanza kuwekwa " amesema Mhe
Hasunga.