slider gif
kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ
Wednesday, July 5, 2017
Tuesday, July 4, 2017
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, PROF. JUMANNE MAGHEMBE AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA HIFADHI YA NGORONGORO NA SERENGETI
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amefanya ziara ya kushtukiza tarehe 02 Julai, 2017 katika Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuona maendeleo ya shughuli za utalii na changamoto zilizopo. HAYA NI MATUKIO YA ZIARA HIYO KATIKA PICHA.
Monday, July 3, 2017
TANZANIA IS THE HOME OF KILIMANJARO MOUNTAIN

Dubbed the 'Rooftop of Africa'. The snowy peak of Mt. Kilimanjaro rises above the gently rolling hills and plateaux of northern Tanzania, towering 5,896 metres above sea level, it’s slopes and glaciers shimmering above the rising clouds. If paced well, everyone from seasoned trekkers to first-time enthusiasts can scale the snowy peak.
Enjoy the Climb.
Karibu! #VisitTanzania
http:// www.tanzaniatourism.go.tz/ en/destination/ mount-kilimanjaro-national- park
Enjoy the Climb.
Karibu! #VisitTanzania
http://
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KATIKA KIPENGELE CHA MAUZO YA BIDHAA NJE YA NCHI KATIKA MAONESHO YA 41 YA SABA SABA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi tuzo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi, baada ya Wizara hiyo kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha Uuzaji bora wa Bidhaa Nje ya Nchi (Best Exhibitor Export Products), katika Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28. Kulia anayepiga makofi ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Tofauti na miaka mingine, mwaka huu maonyesho hayo badala ya kumalizika Julai 8, yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13.
SHIRIKA LA KIJAMII LA UHIFADHI WA WANYAMAPORI (WCS) LATOA MSAADA WA VITENDEA KAZI KATIKA PORI LA AKIBA LA LUKWATI/ PITI.
Na: Chifuno Crispo Jembe
.......................................................................
Mapori ya akiba Lukwati na Piti yapo katika Wilaya ya Songwe mkoani Songwe, awali kabla ya kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Songwe yalikuwa katika eneo la Mkoa wa Mbeya katika Wilaya ya Chunya, pori la akiba la Lukwati lilianzishwa tarehe 08/08/1997 (G.N Na 459) na lina kilometa za mraba 3,146.7 na pori la akiba Piti lilianzishwa tarehe 19/04/2013 (G.N Na 75) na lina jumla ya Km za mraba 2,972.93. Mapori yote mawili yana jumla ya km za mraba 6,119.63.
Hifadhi ya mapori ya akiba ya Lukwati/Piti yanasisimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) na ni moja ya mapori ya akiba yaliyohifadhiwa na kuwa na wanyamapori wengi kama Tembo, Simba, Chui, Mamba, Viboko, Nyati, Palahala, Kongoni, Pundamilia na wengineo.
Hifadhi ya wanyamapori ya Lukwati/Piti ni moja ya mapori ya akiba ambayo yamefanikiwa kwa asilimia kubwa kuzuia uvamizi wa mifugo na shughuli zingine za kibinamu kama uvamizi wa kilimo na uvuvi katika ufukwe wa ziwa Rukwa ambao umepakana na pori la akiba la Lukwati.
Sababu hizi zinapelekea kuwa moja ya maeneo yaliyohifadhiwa na TAWA yenye thamani kubwa za kiikolojia na kiuchumi. Shughuli za uwindaji wa kitalii zinazofanyika kila msimu wa mwaka katika maeneo haya zinaonekana kuchangia kiasi kikubwa cha pato katika makusanyo ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Pamoja na udogo wake ukilinganisha na mapori ya akiba mengine kama Selous na Rungwa utaona Lukwati/Piti ina kamata nafasi ya nne kwa makusanyo yatokanayo uwindaji wa kitalii na kuendelea kuwa moja sehemu muhimu ya kivutio cha utalii kutoka nje chini ya TAWA.
Baada ya kuona umuhimu huu wa kiikolojia basi Shirika La Kijamii La Uhifadhi Wa Wanyamapori (WCS) limeona umuhimu wa kusaidia baadhi ya vitendea kazi katika kituo cha Mapori ya Akiba ya Lukwati na Piti.
WCS kupitia programu yao ya uhifadhi wa ikolojia ya Ruaha-Katavi wametoa msaada wa vifaa vifuatavyo;
Mosi wamefanikisha ujenzi wa jengo la utawala wa zaidi ya milioni 227 na samani zake katika mapori ya Akiba ya Lukwati na Piti ambalo awali Msimamizi Mkuu (Meneja) wa mapori hayo hakuwa na ofisi za utawala ambazo angeweza kufanya baadhi ya shughuli za kiutawala kituoni hapo lakini kwa sasa tunaamini kupitia msaada huu wa WCS usisimamizi wa hifadhi hizi za Wanyamapori zitaimarika na kuwa zenye ufanisi mkubwa zaidi katika kulinda Wanyamapori.
Shirika La Kijamii La Uhifadhi Wa Wanyamapori (WCS) wametoa msaada wa magari maalam kwa ajili ya shughuli za doria pamoja na spidi boti kwa ajili ya kuimarisha shughuli za doria katika sehemu ya ziwa Rukwa ambayo ni eneo la hifadhi hiyo ya Mapori ya Akiba ya Lukwati na Piti.
Sambamba na hayo WCS imetoa mafunzo ya utayari kwa kikosi maalum (RRT) na kwa tafrisi isiyo rasmi ni kwamba Lukwati/ Piti ina kikosi maalum kama cha F.F.U ambacho kimepewa mafunzo ya kupambana na ujangili katika eneo na muda wowote.
Wametoa vifaa kama GPS na SMART ili kusaidia doria za miguu na vifaa maalum vya kubebea maji wakati wa doria ndefu za miguu ikiwemo pia mavazi maalum wakati wa doria za masika.
WCS wamewafungia mfumo wa mawasiliano ya simu za upepo za kidigitali katika mapori haya ya Akiba katika magari yao yote kituoni hapo, vituo vidogo vyote mradini hapo pamoja na simu za upepo za mkononi ili kuleta mawasiliano ya uhakika ukizingatiwa karibu eneo lote la mapori hayo hayafikiwi na mtandao wa aina yoyote wa mawasiliano ya simu za mkononi.
Kumekuwa na changamoto ya maji ya uhakika katika vituo vidogo vya doria lakini WCS katika mipango yao ya baadae wameshaahidi kuchimba kisima kimoja kirefu cha maji katika moja ya vituo vidogo (game post) ili kurahisisha kupatikana kwa maji ya kutosha kwa askari wa ulinzi wa wanyamapori katika Mapori haya ya Lukwati na Piti.
Kama mdau wa masuala ya uhifadhi nawapongeza WCS kwa misaada hii kwani itasaidia kupunguza changamoto katika vita ya mapambano dhidi ya ujangili wa aina yoyote katika maeneo hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj Gen. Gaudence Milanzi akikata utepe kuashia uzinduzi na mapokezi ya magari hayo yaliyotolewa na WCS kwa ajili ya pori la Lukwati/Piti, Rukwa na Rungwa. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Martin Loibooki.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj Gen. Gaudence Milanzi (wa tatu kulia) akikagua kikosi cha RRT kutoka Lukwati/Piti kilichopewa mafunzo na jeshi la marekani kupitia ubalozi wa marekani nchini kwa ufadhili wa WCS.
Magari hayo 3 ya doria yalikabidhiwa kwa ajili ya pori la Lukwati/Piti, Rukwa na Rungwa.
Mkurugenzi wa WCS, Aaron Nicholas (kushoto) akikabidhi jengo la milioni 227 kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kulia) kwa ajili ya shughuli za utawala kwa Mapori ya akiba ya Lukwati/Piti. Wa tatu kulia anaeshuhudia ni Kaimu kurugenzi Mkuu wa TAWA, Martin Loibooki.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Askari wa Lukwati/Piti juu ya ukusanyaji wa taarifa katika eneo la tukio "Crime Scene Management".
Saturday, July 1, 2017
KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI AWATAKA WADAU WA UHIFADHI KUUNGA MKONO MPANGO WA SERIKALI WA KUZALISHA UMEME KATIKA MRADI WA STIEGLER'S GORGE ULIOPO SELOUS
Na Mwandishi wetu, Katavi
..............................................................
Wizara ya Maliasili na utalii imewataka wadau wa uhifadhi kote nchini kuunga mkono mpango wa Serikali wa kujenga mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme wa Stiegler's Gorge katika mto Rufiji kwenye pori la akiba la Selous ambao ukikamilika unatarajiwa kuzalisha zaidi ya megawati 2,100.
Katibu Mkuu wizara ya Maliasili na utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi amesema utekelezaji wa mradi huo wa umeme ni wa muhimu kwa taifa kwani utasaidia kuharakisha maendeleo ya taifa kuelekea azima yake ya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati.
Akiongea wakati akifunga mafunzo ya askari wa wanyamapaori kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanayamapori Tanzania -TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili, Meja Jenerali Gudance Milanzi amesema mradi huo wa umeme pamoja na mradi wa bwawa la maji la Kidunda utachukua eneo dogo la pori la akiba la Selous (takriban asilimia 3) lenye ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba elfu 50.
Amesema pori hilo ndilo kubwa miongoni mwa mapori ya aina hiyo ulimwenguni na ukubwa wake ni zaidi ya nchi za Rwanda na Burundi zikiunganishwa kwa pamoja.
Katibu Mkuu amesema ujenzi wa miradi hiyo hauna tafsiri kwamba Tanzania haithamini masuala ya uhifadhi bali unazingatia uhifadhi wenye manufaa kwa jamii na maendeleo ya taifa na hasa dhamira ya serikali ya rais Dkt. John Pombe Magufuli kuelekea Tanzania ya viwanda ambayo inahitaji nishati ya umeme itakayoyotosheleza mahitaji ya taifa.
Amesema Tanzania inatambua umuhimu wa uhifadhi ndiyo maana imetenga eneo la zaidi ya asilimia 28 ya eneo lote la nchi kavu Tanzania bara kwa ajili ya uhifadhi wa aina mbalimbali ukiwemo wa wanayamapori, malikale, misitu na vyanzo vya maji ambayo ni muhimu kwa shughuli za kijamii na kiuchumi, “ ni nchi chache sana duniani zenye eneo kubwa la uhifadhi kama Tanzania” alisisitiza katibu mkuu.
Katibu mkuu huyo amewataka wafanyakazi wa wizara na watanzania kwa ujumla kutokuwa kikwazo katika utekelezaji wa mradi huo na kwamba wadau wanaotaka kuisaidia Tanzania wasaidie kuhakikisha inatumia maliasili zake kupiga hatua ya kimaendeleo ikiwemo misaada ya teknolojia za kisasa na rafiki wa mazingira kusaidia kufikia malengo yake kimaendeleo.
“Mtakumbuka mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli hivi karibuni alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Pwani amezungumzia kwa kirefu sana umuhimu wa miradi hiyo ukiwemo wa bwawa la Kidunda na wa umeme wa Stieglars Gorge, sasa sisi kama wahifadhi na kama watumishi lazima tumuunge mkono na tusiwe kikwazo katika dhamira hii njema” alisema Jenerali Milanzi.
Ametoa mfano wa nchi ya Qatar ambayo amesema ilikuwa na eneo la uhifadhi lililokuwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia kutokana na uwepo wa baadhi ya viumbe adimu lakini walipogundua mafuta, waliamua kujitoa kwenye urithi wa dunia ili wachimbe mafuta na kuinufaisha nchi hiyo na maendeleo ya wananchi wake.
Akizungumzia kuhusu tatizo la mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa, Katibu mkuu amewataka wahifadhi kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hiyo na kusimamia sheria zilizotungwa na Bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zinakataza mifugo kuingia hifadhini kinyume cha sheria.
Amesema ndiyo maana serikali inatumia fedha nyingi kugharamia mafunzo ya askari wa wanyamapori na wahifadhi ili kuwaongezea ujuzi na weledi wa kulinda maliasili za taifa kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Katibu Mkuu Meja Jenerali Gaudance Milanzi amezungumzia pia umuhimu wa kuhakikisha mapori ya uhifadhi yanatumiwa kwa uhifadhi badala ya kutumika kwa mambo mengine ikiwemo kilimo cha bangi na maficho ya majambazi na majangili na amewataka wahifadhi na askari kushirikiana na vyombo vingene vya ulinzi na usalama kuwafichua wahalifu wanaojificha kwenye mapori hayo na kufanya ujangili na uhalifu mwingine.
Mapema katika taarifa yake kwa katibu mkuu, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania -TAWA Martin Loibooki alieleza kuwa mafunzo hayo yamesaidia kuimarisha uhifadhi kwenye mapori mbalimbali ya akiba nchini na maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori.
Aliwashukuru wadau mbalimbali wa uhifadhi wa ndani na nje ya nchi wanaofadhili mafunzo hayo na vitendea kazi juhudi ambazo amesema zimeanza kuzaa matunda ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya tembo na wanyamapori wengine kwenye mapori mengi nchini.
Mfunzo hayo yaliyowashirikisha askari wa wanyamapori wapatao 98 kutoka Mamlaka ya wanayamapori Tanzania TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Maliasili na utalii kwa askari wa wanyamapori na watumishi wengine wa wizara hiyo katika hatua za kuelekea mfumo wa jeshi usu.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akiwasilisha hotuba yake kwa wahitimu hao.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Martin Loibooki akiwasilisha hotuba yake katika mafunzo hayo.
Wahitimu wa mafunzo hayo wakitoa heshima mbele ya mgeni rasmi, Katibu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (hayuko pichani)
Wahitimu wa mafunzo hayo wakifanya onesho la mafunzo kwa vitendo mbele ya mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (hayuko pichani).
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akiwa kwenye picha ya
pamoja na wahitimu wa mafunzo hayo.
Tuesday, June 27, 2017
WANAWAKE WAWEKA REKODI YA KUCHEZA SOKA KATIKA KILELE CHA UHURU,MLIMA KILIMANJARO
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii-Kanda ya Kaskazini.
.........................................................................................................................
Wachezaji 30 wa timu za soka za mataifa mbalimbali wameshiriki kuweka rekodi ya kwanza Duniani kwa kucheza mchezo wa kirafiki katika mlima Kilimanjaro ,umbali mita 5731 kutoka usawa wa bahari.
Rekodi nyingine iliyowekwa ni ile ya mwamuzi wa kike wa Tanzania anayetambulika na Shirikiho la Soka Duniani (FIFA) Jonesia Rukyaa kuchezesha mchezo huo wa dakika 90 uliomalizika kwa sare ya bila kufungana .
Kundi la Wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa zaidi ya 20 walioshiriki kuweka rekodi ya kucheza soka katika eneo la kreta lililopo katika kilele cha Uhuru.
Baadhi ya wachezaji walioshiriki mchezo wa soka katika Kilele cha uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrta Loibook akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini ,Devota Mdachi walipowapokea wachezaji wa timu za taifa za wanawake wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Mwika.
Mhifadhi Mkuu KINAPA,Betrita Loibook pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii,Geofrey Tengeneza wakifurahia mara baada ya wachezaji wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani kuweka rekodi ya kucheza mpira katika kilele cha Uhuru .
Wachezaji wa timu za Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya utalii pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Timu za Gracier fc na Volcano fc zikijiandaa kwa mchezo wa kirafiki katika eneo la Kreta,kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakiweka pozi la picha katika Kreta ya Uhuru katika kilele cha Uhuru juu ya Mlima Kilimanjaro.
Subscribe to:
Posts (Atom)
























