Watu wanaodaiwa kuwa ni majangili na wawindaji haramu wameitungua kwa risasi helkopta ya doria ya wanyamapori katika pori la akiba la maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu kusini mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kumuua rubani wa helkopita na kumjeruhi askari mmoja wa wanyamapori.
Kufuatia tukio hilo, waziri wa maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe amefika katika eneo la tukio na kusisitiza kwamba serikali kwa kushirikiana na vyombo vyote vya dola na vyombo vya ulinzi na usalama inaanzisha mkakati mpya wa kupambana na ujangili na uwindaji haramu wa maliasili ikiwemo Tembo ambao ni rasilimali muhimu kwa taifa.
Waziri Maghembe amefika kwenye eneo husika na kushuhudia tukio hilo la kihalifu lililosababishwa na Majangili ambapo amesema tukio hilo limewakera wadau wote wa uhifadhi na serikali kwa ujumla na kamwe haliwezi kuachwa lipite bila hatua madhubuti kuchukuliwa.
Nae kamanda wa upelelezi wa mkoa wa Simiyu Jonathan Shana amesema tukio hilo lilitokea jana jioni wakati helkopita hiyo ikiwa katika doria baada ya kusikika milio ya risasi ya majangili katika pori hilo ambapo ulionekana Mzoga waTembo mmoja uliosemakana kuuwawa na Majangili hao.
Hili ni tukio la kwanza katika historia ya uhifadhi hapa nchini kwa Majangili kushambulia helkopta ya doria na kusababisha mauaji ya Rubani.
Kapteni Roger Gower raia wa Uingereza alikuwa akienda kuongeza nguvu ya askari wa uhifadhi waliokuwa wakipambana na majangili hatari wilayani Meatu, Simiyu katika ranchi ya wanyamapori ya Mwiba.
No comments:
Post a Comment