Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo
Makani (wa kwanza kulia) akizungumza na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Massana
Mwishawa (wa pili kulia) alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21 Julai, 2016 kwa
ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto
aliyesimama na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa
jina la Msukuma.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Massana
Mwishawa (wa pili kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng.
Ramo Makani (wa kwanza kulia) sehemu ya fukwe za hifadhi hiyo ambazo ni makazi
ya Mamba na Ndege wa aina mbali mbali alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21
Julai, 2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto
aliyesimama na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa
jina la Msukuma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo
Makani (wa pili kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mwl.
Herman Kapufi (kulia) katika fukwe ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo
alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21 Julai, 2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto anaesaini
kitabu cha wageni ni Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa
jina la Msukuma.
Picha ya pamoja kati ya Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (katikati waliokaa), Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mwl. Herman Kapufi
(wa tatu kushoto waliokaa), Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku
maarufu kwa jina la Msukuma (wa tatu kulia waliokaa), Kaimu Mkurugenzi Mkuu
TANAPA, Ibrahim Mussa (wa pili kushoto waliokaa) na baadhi ya Watumishi wa
Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Rubondo hifadhini hapo tarehe 21 Julai, 2016.
Mamba katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Moja ya Fukwe katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Huduma za malazi katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Huduma bora ya vyumba inapatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Huduma za usafiri wa boti zinapatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.
____________________________________________________________
Mamba katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Moja ya Fukwe katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Huduma za malazi katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Huduma bora ya vyumba inapatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Huduma za usafiri wa boti zinapatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.
____________________________________________________________
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani ameitaka Mamlaka ya Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA) kuzishirikisha jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi hapa
nchini kutambua umuhimu wa kuhifadhi maeneo hayo ili kutoa ulinzi shirikishi
katika kupambana na Ujangili.
Eng. Makani amesema
hayo jana wakati akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka hiyo
akiwa ziarani Mkoani Geita katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
“Wananchi waoishi
jirani na maeneo haya ya hifadhi ni muhimu wakaelimishwa juu ya faida za
uhifadhi kiikolojia na kiuchumi kwenye maisha yao ambapo itawapa msukumo wa
kuyatunza na kuyalinda” Alisema Eng. Makani.
Aliongeza kuwa vita
dhidi ya Ujangili hapa nchini haiwezi kufanikiwa kirahisi iwapo jamii
inayozunguka maeneo ya Hifadhi haitatoa ushirikiano kwa Serikali katika kulinda
na kuhifadhi Maliasili zilizopo.
“Pamoja na mbinu
nyingine, washirikisheni wananchi watusaidie kupambana na ujangili ili fedha
ambayo ingetumiwa na Serikali kwa kazi hiyo itumike kuendeleza hifadhi zetu pamoja
na kutoa huduma nyingine za kijamii” Alisema Eng. Makani.
Akizungumzia faida za
uhifadhi kiuchumi hapa nchini alisema kuwa, Sekta ya utalii ndio sekta pekee
inayoongoza kwa kuliingizia taifa mapato mengi ya nje (foreign currency) ambayo
ni asilimia 25 ya mapato yote. Sekta hiyo pia inachangia pato la taifa kwa
asilimia 17.2.
Eng. Makani aliongeza
kuwa “Serikali ya awamu ya tano ina mpango wa kuboresha sekta ya utalii ili iweze
kuiingizia zaidi mapato, katika kufanikisha hilo tumeweka mkakati wa kuboresha
ofisi zetu za utalii za Kanda ili ziweze kutangaza na kukuza zaidi utalii wa
ndani”.
Kwa upande wa hoteli
zinazotoa huduma ya kitalii hapa nchini alisema kuwa ifikapo mwezi Septemba
mwaka huu, Serikali itaanza rasmi zoezi la kuorodhesha hoteli zote zinazotoa
huduma hiyo na kuzipanga kwenye makundi ya ubora ambapo zile zitakazoonekana
hazina hadhi kabisa zitaondolewa katika mtandao wa kutoa huduma hiyo. Alisema
zoezi hilo litaboresha huduma za kitalii nchini na kusaidia watalii kufikia
hoteli wanazozihitaji na kupata huduma stahiki .
Katika kushirikisha
sekta binafsi kwenye kukuza utalii nchini, amewaomba watoa huduma za ndege
kuangalia upya viwango vya gharama zao za usafiri ili wananchi wengi zaidi
waweze kumudu na kunufaika na huduma hiyo.
Wakati huo huo aliwaasa
watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo kufanya kazi kwa bidii, kuwa na maadili
mema na uadilifu kazini. Aliwataka pia kuwa mstari wa mbele kupiga vita
ujangili, kuboresha ukusanyaji wa mapato na kushirikisha wananchi kwenye
uhifadhi.
Hapo awali
akiwasilisha taarifa ya hifadhi hiyo kwa Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo
Makani, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Massana Mwishawa alisema kuwa
changamoto kubwa inayoikabili hifadhi hiyo ni ujangili na upatikanaji mdogo wa
mapato ambao hauwiani na mahitaji ya hifadhi hiyo.
Kwa upande wake
Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Luiza Kasheku maarufu kama Msukuma,
alimuomba Naibu Waziri huyo wa Maliasili kuboresha Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha
Rubondo ambayo ipo Jimboni kwake iweze kupata mapato ya kutosha na kujiendesha
yenyewe. Hifadhi hiyo kwa sasa inategemea mapato kutoka kwenye hifadhi nyingine
kujiendesha.
Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha
Rubondo iliyopo Mkoani Geita ni moja ya sehemu pekee na muhimu katika
uzalishaji wa mazalia ya samaki katika ziwa Victoria. Sehemu nyingine ni
Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane iliyopo Mkoani Mwanza. Hifadhi hizi zina umuhimu mkubwa
katika upatikanaji wa samaki katika Ziwa Victoria.
No comments:
Post a Comment