Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Wazara ya Maliasili na Utalii kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 .
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza katika Mkutano huo.
Baadhi ya Watumishi wa Wizar ya Maliasili na Utalii wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 .
Baadhi ya Waandishi wa Habari na Watumishi wa Wizara ya Maliasi na Utalii katika Mkutano huo.
Picha ya pamoja kati wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa (katikati waliokaa) na Viongozi pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
____________________________________
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa
Wizara ya Maliasili na Utalii kubadilisha mfumo wa uvunaji wa vitalu vya miti kwenye mashamba
ya Serikali ili kuweka uwazi kwenye biashara hiyo na kuipatia zaidi Serikali
mapato.
Mhe. Majaliwa alisema
hayo jana kwenye Mkutano na Viongozi pamoja na Watumishi wa Wizara ya Maliasili
na Utalii uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga uliopo
Kijitonayama Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia mabadiliko
hayo, Mhe. Majaliwa alisema kuwa utaratibu uliokuwa ukitumika hapo awali wa
kuuza miti kwenye mashamba ya Serikali kwa njia ya vibali hauna tija kwakuwa
umekuwa ukiikosesha Serikali mapato na kuwanufaisha wafanyabiashara wachache.
“Utaratibu wa sasa wa
kutumia vibali unatuletea migongano ndani ya Wizara na kuikosesha Serikali
mapato, hivyo ni lazima tuubadilishe” Aliongeza Majaliwa.
Aliuagiza Uongozi wa
Wizara kufanya marekebisho kwenye utaratibu huo na kuweka utaratibu wa mnada
ili kuweka uwazi zaidi na kuondoa manung’uniko kwenye biashara hiyo. “vibali visitishwe,
mnada uanze kama inavyofanyika kwenye
mitiki” Alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Hivi karibuni Mhe. Majaliwa
alisitisha utoaji wa vibali vya uvunaji wa miti kwenye mashamba matano
yanayomilikiwa na Serikali kutokana na kupokea malalamiko mengi kutoka kwa
wananchi.
Katika hatua nyingine,
Mhe.
Majaliwa aliagiza mabadiliko ya haraka katika vizuizi vya ukaguzi wa Maliasili ambavyo
amesema vimekuwa havina tija na kuagiza baadhi yake vifutwe kabisa. Miongoni
vya vizuizi alivyoagiza vifutwe ni Kibaha Stendi, Kimanzichana na Mbagala, pia
aliagiza kuimarishwa kwa kituo cha Vikindu, Kibiti na Vigwaza.
Mhe. Majaliwa aliwaagiza
wataalamu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana na Tamisemi kwa ajili
ya kuweka mfumo mzuri wa kuhifadhi na kuvuna mazao ya misitu yaliyopo katika
Halmashauri na kutenga Misitu ya Asili tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo
kumekuwepo muingiliano katika kutekeleza majukumu hayo jambo linalopelekea uharibifu
wa misitu.
Hapo awali Mhe.
Majaliwa alieleza lengo kuu la Mkutano huo kuwa ni katika utaratibu wake wa
kawaida aliojiwekea wa kutembelea Wizara na kuzungumza na watumishi kwa ajili
kukumbushana majukumu yao, kuangalia changamoto mbalimbali na kuzitafutia
ufumbuzi. Aliwaasa watumishi wa Wizara ya Maliasili kuwa wazalendo, waadilifu, waaminifu
na kuongeza uwajibikaji ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake ya
kuwahudumia vizuri wananchi.
“Ninyi ni watu muhimu
sana katika utoaji wa huduma kwa wananchi, tekelezeni majukumu yenu kwa
uadilifu wa hali ya juu. Kamilisheni malengo yenu kulingana na mpangokazi wenu
mliojiwekea” Alisema Mhe. Majaliwa.
Kwa upande wake
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alisisitiza watumishi wa
Wizara hiyo kuhakikisha kuwa wanalinda misitu kule iliko na sio kusubiri katika
vituo na kukamata rasilimali zake ambazo zimevunwa isivyo halali na kuzitoza
faini, kinyume chake rasilimali hizo zilipiwe kihalali kabla ya kuvunwa.
Aliahidi pia kuisuka upya Idara ya Misitu.
No comments:
Post a Comment