Waziri wa Maliasili na utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akisikiliza maelezo ya mmoja wa wahitimu wa mafuzo ya upishi katika hoteli za kitalii wakati wa mahafali ya sita ya Chuo cha Hoteli na Utalii Njuweni kilichopo Kibaha, mkoani Pwani hivi karibuni.
_______________________________
_______________________________
Waziri wa Maliasili na utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema ili Tanzania iendelelee kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii inahitaji wafanyakazi wa kada hiyo wawe na sifa zinazostahili ikiwemo nidhamu na uaminifu.
Ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 6 ya Chuo cha Hotel na Utalii cha Njuweni kilichoko Kibaha mkoani Pwani ambayo yalifanyika kwenye viwanja vya Chuo hicho.
Alisema kuwa pamoja na vyanzo mbalimbali vya mapato vinavyokuza uchumi wa taifa taifa, Wizara ya Maliasili na Utalii ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi huo hivyo kinachotakiwa ni kuhakikisha watu wanaopewa dhamana ya kufanyakazi kwenye Wizara hiyo wanafanya kazi kwa weledi.
"Napenda kuwakumbusha kuwa nidhamu na uaminifu ndiyo siri itakayowawezesha ninyi kufika mbali katika utendaji wenu wa kazi, lakini mkiingiza tamaa na udokozi hamtafika mbali na badala yake mtalitia taifa kwenye sifa mbaya" alisema
Alisema kuwa Serikali imekuwa ikikuza uchumi wa nchi kila mwaka kupitia Sekta ya utalii ambapo idadi ya watalii imekuwa ikiongezeka kwa asilimia 23.7 kutoka watalii 867,994 mwaka 2011 hadi kufikia watalii 1,137,182 mwaka 2015. Aidha sekta hiyo inachangia asilimia 17 ya pato la taifa.
"Mapato yatokanayo na shughuli za utalii yaliongezeka kwa asilimia 28.8 kutoka dola za Marekani mil. 1,353.29 mwaka 2011 hadi kufikia dola za Marekani mil. 1,901.1 mwaka 2015" alisema
kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Nditi Rashid alisema kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana kwa miaka kadhaa tangu kuanzishwa kwa chuo hicho lakini bado kuna changamoto kadhaa zinazowakabili ikiwemo upungufu wa vifaa vya kisasa vya kuendeshea masomo ya TEHAMA
"kutokana na ufinyu wa bajeti tulionao tunakuomba mheshimiwa mgeni rasmi utusaidie kupata msaada wa vifaa vipya vitakavyotusaidia kuendesha masomo ya TEHAMA kwa ufanisi zaidi" alisema
Mahafari hayo ambayo ni ya sita tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 200o yalihusisha jumla ya wanafunzi 350 waliohitimu kwa ngazi ya stashahada ambao walipata vyeti na zawadi mbalimbali .
No comments:
Post a Comment