Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kikanda wa Wadau wa Sekta ya Misitu wa nchi ya Finland na Tanzania uliofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam. Lengo kuu la mkutano huo likiwa ni kuhamasisha uwekezaji na kukuza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika uendelezaji wa misitu nchini. Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, Taasisi ya Uongozi - UONGOZI Institute na Shirika la Maendeleo ya Kifenda la Finland - FINFUND.
Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Serikali ya Finland, Kai Mykanen akizungumza katika Mkutano huo ambapo ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Finland na Tanzania katika kuendeleza Misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho ikiwa ni pamoja na kukuza teknolojia ya uhifadhi wa mazingira ya kupunguza hewa ukaa.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Eng. Angelina Madete na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo.
Baadhi ya wajumbe katika mkutano huo wakifualia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Finland ikiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo, Kai Mykanen (wa pili kushoto) muda mfupi kabla ya ufunguzi wa mkutano huo. Wengine kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mehenge, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali, Gaudence Milanzi na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano huo. Alieleza kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa misitu unaotokana na uvunaji wa mkaa na ukataji wa magogo, uvunaji wa miti usio endelevu jambo lililoisukuma Serikali kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ya Finland na wananchi kwa ujumla kwa ajili kuendeleza misitu kwa kupanda miti mingi zaidi iweze kukidhi mahitaji yaliyopo. Aliongeza kuwa ni marufuku kusafirisha magogo na kwamba Serikali ya awamu ya tano imelenga kukuza viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani kwenye mazao ya misitu na kuyauza kama bidhaa. Ametoa wito kwa watanzania kujishuulisha na upandaji wa miti kibiashara ili kuinua maisha yao na uchumi wa taifa kwa ujumla. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali Gaudence Milanzi na kulia kwake ni Mkurugezi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kinyago, Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Serikali ya Finland, Kai Mykanen katika hafla ya jioni iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam.
_____________________________
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kinyago, Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Serikali ya Finland, Kai Mykanen katika hafla ya jioni iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam.
_____________________________
Watanzania wametakiwa kutumia fursa ya upandaji wa miti kibiashara kuinua uchumi wa maisha yao na kuacha biashara haramu ya usafirishaji wa magogo nje ya nchi, badala yake watumie fursa hiyo kuzalisha bidhaa za misitu na kuziuza kwa faida zaidi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe aliyasema hayo jana Dar es
Salaam wakati akifungua mkutano wa uwekezaji wa misitu uliowashirikisha wadau
wa Mazingira kutoka nchi 16 ulioandaliwa kwa ushirikiano na Wizara ya Maliasili
na Utalii, Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, Taasisi ya Uongozi na Shirika la
Maendeleo ya Kifenda la Finland - FINFUND.
“Wawekezaji
wa misitu wanasema wanataka soko la mazao yao na sisi tunasema soko lipo
isipokuwa watengeneze bidhaa kama vitanda, viti na samani za ndani pamoja na
makaratasi na vifaa vyote vinavyotokana na miti na hiyo ndiyo itawasaidia ndugu
zetu kupata ajira na viwanda vitaongezeka.
“Tukiruhusu
magogo kwenda nje itakuwa kama pamba yetu inalimwa hapa na kusafirishwa halafu
inatengeneza nguo na tunaletewa, lazima Viwanda vijengwe na hiyo si kazi
ngumu.... Tunachotaka hapa teknolojia ya viwanda ije, wasafirishe bidhaa na si
magogo,” alisema Profesa Maghembe.
Aliongeza
kuwa “Tunataka kufanya uwekezaji katika hewa ukaa, ambayo italeta tija kwa
jamii na kutumia zaidi teknolojia katika upandaji wa miti ili kuongeza ubora na
soko la mazao hayo”.
Alisema
inakaridiwa kwamba hekta 30,000 za misitu zinapotea kila mwaka kutokana na
sababu mbalimbali huku zikiwa zinapadwa hekta 80,000 hadi 100,000 kila mwaka.
Alisema kuna
changamoto kubwa ya uchomaji mkaa na wengine wanasafirisha nje kupitia kwa
bandari bubu na hivyo misitu kupotea kwa sababu pia ya uvunaji wa misitu usio
endelevu.
Alisema
changamoto nyingine ni uvunaji usio endelevu wa misitu na kupungua kwa vyanzo
vya maji kutokana na ukataji wa miti hovyo na uharibifu wa misitu, hivyo Serikali
inaongeza juhudi kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa.
Mkuu wa
Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja alisema jukumu lao ni kuwaweka
viongozi na wadau mbalimbali katika kuangalia maendeleo endelevu ambapo kwa
sasa wanaangalia namna ya kukabiliana na changamoto kubwa ya mabadiliko ya
tabianchi ikiwa ni pamoja na kuboresha na kuendeleza misitu kibiashara.
Mwakilishi wa
Benki ya Dunia, Yutaka Yoshino alisema Idara ya Misitu nchini imekuwa
ikichangia ukuaji wa uchumi nchini, lakini sekta hiyo imekuwa ikikabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabianchi.
No comments:
Post a Comment