slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Sunday, December 30, 2018




NAIBU WAZIRI MHE.KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI

NA LUSUNGU HELELA-MWANZA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu amewataka wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani  ya Hifadhi ya misitu ya Visiwa vya  Kome  na Maisome vilivyoko wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza kulipa tozo za serikali bila kulazimishwa.



Kauli hiyo ameitoa  wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya  Msitu wa Shigala ulioko Kome Mchangani ambayo ni kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.



Mbunge wa Jimbo la Buchosa Dkt. Charles Tizeba amemueleza  Naibu Waziri hiyo kuwa kumekuwepo na changamoto ya ulipaji  tozo kubwa hata kama mtu ana eneo dogo na ndipo wananchi walilazimika kugoma kulipa tozo hiyo kwa lengo la kupata msaada zaidi.



Amefafanua kuwa mtu anayemiliki hekari moja  anatakiwa kulipa Tsh.425,000 kwa mwaka lakini hata mtu anayemikili eneo dogo la mita 20 naye anatakiwa kulipa kama wa hekari moja  kitendo kilichowafanya wananchi hao kushindwa kulipa na kusubili maelekezo ya wizara husika.



Mmoja wa wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi hiyo,Juma Ramadhani amemwomba Naibu Waziri kuangalia upya sheria hiyo ili wananchi wapate nafuu ya kulipa na serikali iweze kupata mapato yake.



Kaimu Meneja wa TFS Kanda ya Ziwa, Thomas Moshi amesema kuwa tozo hizo zipo kwa mujibu wa sheria kinachotakiwa ni wananchi kulipa na siyo kugomea kulipa tozo hizo na wanapofanya hivyo wanakwenda kinyume na matakwa ya sheria ya hifadhi ya misitu.



Kanyasu amewahakikishia wananchi hao kuwa suala hilo atalipatia majibu kwa haraka lakini amewataka watu wanaomiliki hekari moja  kulipa tozo hizo kwa wakati na wale wenye maeneo madogo madogo wajiunge katika vikundi ili waweze kuilipa pesa hiyo



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akizungumza na  wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani  ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kuwa watalipa tozo za serikali bila kulazimishwa alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akizungumza na wananchi wa Jimboni kwake  kwenye mkutano wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wa   kutatua kero za  wananchi wanaoishi ndani ya  Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya  Kome Mchangani

Mwenyekiti wa Kijiji cha Buhama kata ya Buhama, Thomas Sabuni, akizungumza  na wananchi kwenye mkutano wa hadhara kabala ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ikiwa lengo  kutatua kero za  wananchi  wa Kisiwa hicho wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya  katika eneo la Kome mchangani
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akiteta jambo na Meneja wa Shamba la Buhindi , Ayoub Kigongwira wakati wa  mkutano wa hadhara uliofanyika katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Baadhi  ya wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu ndani  ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Buhama  wakati alipowasili katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wvuvi kwa ajili ya  kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiiangalia taarifa mara baada ya kukabidhiwa taarifa Mwenyekiti wa kijiji Buhama, Thomas Sabuni  wakati alipowasili katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wvuvi kwa ajili ya  kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo




Saturday, December 8, 2018

MHE KANYASU AENDESHA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA


 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ( wa pili kushoto)  akizungumza mara baada ya ibada iliyofanyika katika ya Kanisa la Wasabato la Geita kati wakati ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita


Baadhi ya waumini ibada wa Kanisa la Wasabato la Geita kati wakifuatilia ibada kabla  ya  harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita


 Mchungaji na  Mwenyekiti wa South Nyanza Conference, Sadoki Butoke akitoa mahubiri kwa  waumini waliojumuika katika ibada ya  harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa  Kanisa la Wasabato la Geita wakisikiliza mahubiri kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita
Baadhi ya wanakwaya wakiimba wakati wa mahubiri kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akivishwa skafu na wanafunzi wa Skauti kanisa la Wasabato la Geita Kati kabla  ya Naibu Waziri huyo kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja  na kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita mara baada ya kusomewa taarifa ya hali ya uhifadhi wa misitu na wanyamapori kabala ya kushirikia harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Afya

Saturday, October 20, 2018

NAIBU WAZIRI MHE. JAPHET HASUNGA AONYA UKATAJI MITI OVYO MKOANI SONGWE

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza jana na wananchi kuhusu athari za ukataji miti ovyo  kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe





NAIBU WAZIRI MHE. JAPHET HASUNGA AONYA UKATAJI MITI OVYO MKOANI SONGWE

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amewaonya watu wenye tabia ya kukata miti ovyo kuwa Serikali hatosita kuwachukulia hatua za kisheria kutokana na kushamiri kwa uharibifu wa misitu mkoani Songwe.

Ametoa onyo hilo wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe.

Amesema kufuatia kasi ya ukataji miti ovyo unaoendelea  kwa ajili ya mbao na nishati ya mkaa katika maeneo hayo kunatishia kutoweka kwa mvua wanayoitegemea kwa ajili kilimo cha mazao ya kahawa, mahindi pamoja na mazao mengine.

Amewaeleza Wananchi hao  kuwa uharibifu huo ukiendelea utaawathiri wao wenyewe  kwa vile   mvua itakoma kunyesha katika maeneo yao.

Amewataka wakikata mti wapande miti na wale wanaokata miti kwa ajili ya Nishati ya mkaa wafuate kanuni na sheria ili kuepuka kukabiliana na Wakala wa Huduma za Misitu  Tanzania (TFS)

Aidha, Mhe. Hasunga Amewataka Wananchi hao kuwa  hata pale inapotokea wanataka kukata mti wa mwembe uliopo katika nyumba zao wanatakiwa kuomba kibali kutoka TFS.

Pia,  Waziri Hasunga amewaagiza TFS itoe miche 10,000 kwa Kata ya Wasa msimu wa mvua utakapokaribia kufuatia ombi la mwanakijji Kasian Mwanjala alilowasilisha kwa Mhe. Hasunga kuwa wanataka kupanda miti ili wanakosa miche.

"Moja ya ahadi yangu niliyoitoa kwenu ni kuhakikisha katika jimbo langu wananchi mnapata umeme, hadi sasa tayari nguzo za umeme zimeanza kuwekwa " amesema Mhe Hasunga.



 Baadhi ya Watendaji aliokuwa ameongozana nao katika mkutano huo wa hadhara katika kijiji cha Isalalo



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akimsikiliza huku akiwa anaandika swali analoulizwa na zungumza Ester Mwakanja kuhusiana  athari za ukataji miti ovyo  kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe

    Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akisoma baadhi ya ujumbe katika  karatasi  mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara ulioufanya katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe









Sunday, October 14, 2018

TFS YAHAMASISHA UTALII WA KIIKOLOJIA KWA WATANZANIA

Afisa Misitu Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS),Arijanso Mlog akizungumza na Waandishi wa habari katika Onesho la Kimataifa la  Utalii (SITE)linaloendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.



Wafanyakazi wa Huduma za Misitu nchini TFS, Wakiwaonesha wadau Mazao Mbalimbali yatokanayo na misitu ambayo ni mazuri kwa ajili ya kuimarisha afya ya Mwanadamu
Meneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini, Mariam Kobelo akieleza huduma za kitalii zilizopo ndani ya Hifadhi za Misitu zilizo chini ya TFS

Afisa Misitu Mwandamizi , Anna Lawuo Akizungumza na Waandishi wa habari  kuhusu umuhimu wa mazao yatokanayo na misitu nchini


TFS YAHAMASISHA  UTALII WA KIIKOLOJIA KWA                                      WATALII
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetoa wito kwa watanzania kutembelea Maeneo yaliyohifadhiwa ili kuweza kujionea namna ikolojia na uhifadhi katika misitu hiyo ilivyo na faida kwa viumbe hai na Wanadamu.



Akizungumza na Waandishi wa Habari,  Afisa Misitu Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS),Arijanso Mlog  katika Onesho la Kimataifa la  Utalii lijulikanalo kama Swahili  International Tourism Expo (SITE) linaloendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mlog amesema kuwa watu wanapaswa kutemblea misitu hii ili waweze kujionea na kujifunza umuhimu wa ikolojia katika hifadhi.




"Ni vyema watu wakaja wakatembelea hifadhi ya misitu ya Amani waweze kujionea namna Misitu iliyopakana na makazi ya watu na maporoko ya maji ambayo hayakauki muda wote na kujionea maua ambayo yanaaminika katika imani kuwa ndio yalitumika wakati wa kristo na watu husafiri kutoka sehemu mbalimbali  kuyafuata kutoka maeneo ya mbali"amesema Mlog.




Kwa upande wake, Meneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini, Mariam Kobelo amewataka wdau mbalimbali  kutembelea banda lao lililopo katika   Onesho La Kimataifa la Utalii la SITE linaloendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam ili kujionea huduma zitolewazo na TFS na kujua wapi wanaweza kutembelea kwa ajili ya mapumziko yao.


Mariamu amesema kuwa Misitu inayohifadhiwa na TFS ina upekee sana , Hivyo ametoa wito kwa wanafunzi, wanasayansi na wanataaluma mbalimbali kuwa wanaweza kwenda ili kuweza  kufanyia tafiti, Mapumziko kwa wana ndoa pia wanaweza kwenda kutembea na  familia zao .




Thursday, October 11, 2018

NAIBU WAZIRI, MHE.JAPHET HASUNGA AFANYA ZIARA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII

Add caption1.       Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (katikati) akiwa  na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Sedoyeka  wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Chuo mara katika Kampasi ya Bustanini   jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga(wa pili kushoto)  akizungumza na watumishi wa chuo hicho katika Kampasi ya Bustanini , jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Sedoyeka



 Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga(wa pili kushoto)  akizungumza na watumishi wa chuo hicho katika Kampasi ya Bustanini , jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Sedoyeka


1Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga(kulia) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Sedoyeka(kushoto)  mara baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara katika chuo ambapo alizungumza na watumishi wa chuo hicho katika Kampasi ya Temeke, jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga(kulia) akiwa ameongoza na  Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Sedoyeka(kushoto)  mara baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara katika chuo  hicho katika Kampasi ya Temeke, jijini Dar es Salaam.



 1.       Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga(katikati) akipewa maelezo na  Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Sedoyeka(kushoto) kuhusiana na vyumba vipya vya kulala wageni  vilianzishwa katika chuo hicho  mara baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara katika chuo  hicho katika Kampasi ya Bustanini  jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga(katikati) akipewa maelezo na  Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Sedoyeka(kushoto) kuhusiana na vyumba vipya vya kulala wageni  vilianzishwa katika chuo hicho  mara baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara katika chuo  hicho katika Kampasi ya Bustanini  jijini Dar es Salaam.






Tuesday, July 31, 2018

SERIKALI KUKUZA UTALII KUPITIA MCHEZO WA GOLF – DK. KIGWANGALLA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni zawadi ya kinyago cha Makonde walipoagana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.

Na Hamza Temba-WMU
........................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali itatumia fursa ya ujio wa Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus kutoka nchini Marekeni kubuni viwanja vya mchezo huo karibu na maeneo ya vivutio vya utalii nchini ili kuvutia watalii wengi wa kimataifa na hivyo kukuza pato la sekta hiyo.

Dk. Kigwangalla amesema hayo jana mara baada ya kumuaga mchezaji huyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam alipokuwa akirudi nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku kumi yeye na familia yake katika vivutio mbali mbali vya utalii hapa nchini.

“Tutatumia utaalamu na uzoefu wake kwenye mchezo wa Golf kwa kumtaka aje na kampuni yake atusaidie kutengeneza plan (mpango) ya kujenga viwanja vya golf.

“Amedesign viwanja zaidi ya 300 kwenye nchi zaidi ya 50 duniani na nchi hizo zimefaidika, amesema katika project zake zaidi ya asilimia 90 zinafanya vizuri pamoja na kwamba ni uwekezaji wa gharama kubwa bado imelipa kwa kiasi kikubwa na hakuna hata kiwanja kimoja kimepata hasara na vimekuwa vinasaidia kukuza utalii katika nchi hizo.

“Lengo letu ni kutengeneza ukanda maalum wa viwanja vya golf ambao utakuwa na viwango vya kimataifa na utavutia wacheza Golf kutoka nchi mbalimbali duniani, kwahiyo hii ni aina nyingine ya utalii wa watu wenye uwezo ambao wataleta pesa nyingi kwa wakati mmoja.

 “Tutaendelea kuwa na mawasiliano nae na kampuni yake ili tuweze kuona anawezaje kutusaidia na sisi walau tuwe na hiyo plan (mpango) lakini pia tukapata wawekezaji wakaja kuwekeza kwenye viwanja vya golf vitakavyojengwa karibu na fukwe, karibu na mito au hifadhi za Taifa ambapo tutavutia sio tu watalii ambao wanaokuja  kufanya utalii wa wanyamapori au beach lakini tutavutia watalii wanaokuja mahsusi kwa kwa ajili ya utalii wa golf” alisema Dk. Kigwangalla.

Wakati huo huo Dk. Kigwangalla amesema Serikali itaendelea kuheshimu na kujali maslahi ya wageni mashuhuri wanaokuja nchini ikiwemo ya usiri wa safari zao na kwamba atakayetaka aje kimya kimya na aondoke kimya kimya atapata heshma hiyo na atakayekubali kuwa wazi naye pia atapata heshma hiyo.

Kwa upande wake Jack Nicklaus alisema amefurahishwa sana na vivutio mbalimbali vya utalii alivyovishuhudia katika safari yake hapa nchini pamoja na ushirikiano na ukarimu mzuri kutoka kwa watanzania na ameahidi kuwa balozi wa utalii wa Tanzania huo aendako.

Jack Nicklaus ndiye mchezaji mwenye tuzo nyingi kuliko wachezaji wengine wa mchezo huo hapa duniani kwa sasa, ameweka rekodi ya kushinda mashindano ya kulipwa 117 na mashindano makubwa 18 (major champions). 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuondoka kurudia kwao baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni wakitumbuizwa na kikundi cha ngoma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuondoka kurudia kwao baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
  Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni na familia yake na uongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Jaji Mst. Thomas Mihayo muda mfupi kabla ya ugeni huo kuondoka na kurudi kwao.

Sunday, July 29, 2018

WAZIRI KIGWANGALLA AMETOA SIKU 7 KWA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI YA TANZAM 2000 KUONDOKA KATIKA PORI LA AKIBA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua mazingira ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe ilani ya siku 7 kwa kampuni ya Tanzam 2000 iliyokuwa ikifanya utafiti wa madini ya dhahabu ndani ya pori hilo iondoe mali zake zote na endapo itakaidi zitaifishwe kuwa mali ya Serikali. Kushoto kwake ni Meneja wa Pori hilo, Benjamin Kijika na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAWA, Mabula Misungwi.

Na Mwandishi Wetu
..........................................................
Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 iliyokuwa ikifanya utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Luahika ndani ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi imetakiwa kuondoa vifaa na mitambo yake katika eneo la hilo ndani ya siku saba kwa amri ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kutoa ilani ya siku saba kwa kampuni hiyo iondoe vifaa na mitambo yake katika eneo hilo na endapo muda huo utapita bila kufanya hivyo mali hizo zitataifishwa na kuwa mali ya Serikali kwa kuwa wao ni wavamizi kwa mujibu wa sheria.

Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo juzi alipotembelea pori hilo katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo alihitimisha ziara yake ya siku 25 aliyoipa jina la Pori Kwa Pori kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi nchini na kutatua changomoto zake.

Alisema uwepo wa vifaa na mitambo ya muwekezaji huyo ndani ya hifadhi hiyo imekuwa kishawishi kikubwa kwa wachimbaji wadogo wa madini kuvamia maeneo hayo wakiamini kuwa eneo hilo lina dhahabu na kwamba bado linaruhusiwa kwa shughuli za uchimbaji.

Awali Meneja wa Pori hilo, Benjamin Kijika alisema kampuni hiyo ilipewa kibali na Wizara ya Malisili na Utalii kwa ajili ya kufanya utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo hilo kwa mwaka 2005 hadi 2010 na kuongezewa muda hadi 2012.

Alisema wakati kibali hicho kinatolewa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 ambayo inazuia tafiti kama hizo na shughuli nyingine za kibinaadamu kwenye maeneo ya hifadhi ilikua bado haijatoka.

Alisema baada ya hapo wizara haikutoa tena kibali kwa kampuni hiyo licha ya wizara ya madini kuipa kibali cha kuchimba dhahabu katika eneo hilo mwaka 2013. Aliongeza kuwa kwa nyakati tofauti Wizara ya Maliasili imeitaka kampuni hiyo iondoe mali zake zote ndani ya eneo hilo, agizo ambalo bado halijatekelezwa mpaka sasa.

Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Josephat Paulo Maganga alisema atasimamia utekelezaji agizo hilo la Waziri Kigwangalla ili eneo hilo liendelee kuhifadhiwa kwa mujibu wa sheria.

Alisema hifadhi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uvamizi wa mara kwa mara wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu hususan katika eneo la Kigosi Kaskazini na hivyo kupelekea uharibu mkubwa wa mazingira katika hifadhi hiyo.

Alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo pori hilo limeanzisha kambi mbili za ulinzi katika eneo hilo kwa ajili ya kudhibiti uharibifu huo ambapo mpaka sasa kesi 24 zenye wachimbaji haramu 52 zimeshafikishwa mahakamani huku kukiwa na vielelezo kadhaa ambavyo ni pamoja na baiskeli 102, viroba vya mchanga unaosadikika kuwa na madini ya dhahabu na vifaa vya uchimbaji.

Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi ni muunganiko wa mapori mawili yenye ukubwa wa kilometa za mraba 21,060. Pori la Moyowosi lipo katika wilaya za Kibondo na Kakonko (Kigoma) na Pori la Kigosi katika wilaya ya Biharamulo (Kagera), Bukombe na Mbogwe (Geita), Kahama (Shinyanga) na Kaliua (Tabora).

Pori hili lina umuhimu mkubwa kiikolojia na kiuchumi kwakuwa pia ni ardhi oevu ambayo ni chanzo kikubwa cha maji ya ziwa Nyamagoma na Sagara ambayo huingiza maji mto Malagarasi na hatimaye ziwa Tanganyika, maji hayo hutumika kwa matumizi mbalimbali ya majumbani na kilimo. Pia hifadhi hiyo ni  makazi muhimu ya wanyamapori adimu kama Nzohe ambao huliingizia Taifa fedha za kigeni.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akimuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Mabula Misungwi (Kulia) kutoa ilani ya siku 7 kwa kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 ili itoe mali zake zote katika eneo la Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita na endapo muda huo utapita zitaifishwe kuwa mali na Serikali.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa na mitambo ya kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 katika eneo la Luahika ndani ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe ilani ya siku 7 kwa kampuni hiyo iondoe mali zake zote na endapo itakaidi zitaifishwe kuwa mali ya Serikali,  Nyuma yake ni Meneja wa Pori hilo, Benjamin Kijika.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa na mitambo ya kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 katika eneo la Luahika ndani ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe ilani ya siku 7 kwa kampuni hiyo iondoe mali zake zote na endapo itakaidi zitaifishwe kuwa mali ya Serikali,  Kulia ni Meneja wa Pori hilo, Benjamin Kijika.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akioneshwa vielelezo (mchanga wa madini ya dhahabu na baiskeli) walivyokamatwa navyo wachimbaji wadogo wa madini katika eneo Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi na Meneja wa Sekta ya Kigosi Kaskazini, Salum Kulunge alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe ilani ya siku 7 kwa kampuni ya Tanzam 2000 iliyokuwa ikifanya utafiti wa madini ya dhahabu ndani ya pori hilo iondoe mali zake zote na endapo itakaidi zitaifishwe kuwa mali ya Serikali.

Thursday, July 26, 2018

DK. KIGWANGALLA AAGIZA WAVAMIZI MAENEO YA HIFADHI MKOANI KIGOMA WAHAME MARA MOJA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifuatilia Sokwe Mtu kwenye mapito yao ndani ya Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.

Na Hamza Temba-Kigoma
........................................................

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ameagiza wavamizi wote waliopo ndani ya Pori la Akiba Kigosi/Moyowosi na Hifadhi ya Msitu wa Makere mkoani Kigoma waondoke mara moja kupisha maeneo hayo yaendelee kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na uongozi wa mkoa wa Kigoma, ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani humo. 

Alisema taarifa za kiitelijensia zinaonyesha kuwa wengi wa wavamizi hao ambao wameanzisha makazi, kilimo na ufugaji ni raia kutoka nchi jirani ambao pia wamekuwa wakijihusisha na uharibifu wa mazingira na vitendo vya ujangili.

"Haivumiliki kwa kiongozi yeyote mzalendo kwa nchi yake ambaye anajua kabisa maeneo yetu yamewekwa akiba kwa ajili ya uhifadhi na tunawazuia hata wananchi raia kuyatumia alafu wanakuja raia wa nchi nyingine wanaachiwa wafanye wanavyotaka, hapana hili halikubaliki" alisisitiza Dk. Kigwangalla huku akiutaka uongozi wa Mkoa huo usaidie kusimamia Sheria na wavamizi hao waondoke mara moja. 

Aidha, ametoa kipindi cha miezi mitatu kwa watu wote waliovamia maeneo ya kinga za hifadhi (bafa) ambayo ni mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi na vijiji waondoke kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Katika hatua nyingine, Waziri Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA  kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Kigoma na Halmashauri husika pamoja na Wakala wa Huduma za Barabara TANROADS katika ujenzi wa barabara inayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Gombe na Mkoa huo na maeneo mengine.

Alisema, Serikali ya awamu ya tano imepanga kufungua Sakiti mpya za utalii ikiwemo ya Kanda ya Magharibi ambayo inaujumuisha mkoa wa Kigoma, hivyo ni lazima miundombinu ya barabara ijengwe na kuimarishwa ipitike muda wote ili hifadhi hizo zitumike zaidi kibiashara na ziweze kuchangia ipasavyo kwenye pato la Taifa kuliko ilivyo hivi sasa.

Ameuagiza pia uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu TFS kupima maeneo ya misitu ya vijiji jirani na Hifadhi ya Taifa ya Gombe ili kuona uwezekano wa kuyahifadhi kwa kutumia sheria za misitu na hivyo kutengeneza mapito muhimu ya Sokwe Mtu yatakayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Gombe na Mahale na hifadhi za Misitu ya Tongwe East, Tongwe West, Masito East na Masito West. 

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Donatus Bayona alisema changamoto kubwa iliyopo katika hifadhi hiyo ni miundombinu ya barabara ya kuunganisha hifadhi hiyo na maeneo mengine ikiwemo mji wa Kigoma ambapo amesema kwa sasa hifadhi hiyo inafikika kiurahisi kwa kutumia usafiri wa boti.

Akiwa katika hifadhi hiyo, Waziri Kigwangalla alizindua tukio la kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa Hifadhi hiyo na kuzindua rasmi kituo cha utafiti wa Sokwe Mtu ambacho kimefadhiliwa na Taasisi ya Jane Goodal, pia alitembelea Maporomoko ya Maji ya Kakombe ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii ndani ya hifadhi hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa, Muongoza Watalii wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe, Iddi Kaluse kuhusu Maporomoko ya Maji ya Kakombe ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii ndani ya  Hifadhi ya Taifa ya Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma.
Baadhi ya Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipanda mlima kwa ajili ya kuwaona Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.
 Msafara wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ukielekea Hifadhi ya Taifa Gombe kwa kutumia usafiri wa boti.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye boti alipotembelea Hifadhi ya Taifa Gombe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma jana.
 Mandari ya Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akicheza ngoma na kikundi cha Mwamgongo alipotembelea Hifadhi ya Taifa Gombe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akizindua rasmi kituo cha utafiti wa Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe ambacho kimefadhiliwa na Taasisi ya Jane Goodal, alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake mkoani Kigoma.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikata keki kama ishara ya kuzindua hafla fupi ya kuadhimisha miaka 50 toka kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake mkoani Kigoma. Anaeshudia kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu, TANAPA, Nyamakumbati Mafuru na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Donatus Bayona.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Gombe katika Maporomoko ya Maji ya Kakombe alipotembelea hifadhi hiyo janawakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma jana.