
slider gif
kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ
Thursday, December 8, 2016
PROF. MAGHEMBE - MOUNT KILIMANJARO CAN ONLY BE CLIMBED FROM ITS HOME, TANZANIA

Wednesday, December 7, 2016
RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO YA MAKATIBU WAKUU, NAIBU KATIBU WAKUU NA WAKUU WA MIKOA - MABADILIKO HAYO YAIGUSA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Desemba, 2016
amefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja na Mkuu wa Mkoa mmoja na pia amefanya
mabadiliko madogo katika Wizara na Mikoa kama ifuatavyo;
Dkt. Magufuli amemteua
Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.Kabla ya uteuzi
huo, Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu Mawasiliano.
Rais Magufuli
amemteua Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi
na Mifugo anayeshughulikia Kilimo. Mhandisi Mathew Mtigumwe anachukua nafasi ya
Dkt. Frolence Turuka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa.
Kabla ya uteuzi
huo Dkt. Frolence Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe.
Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Rais Magufuli
amemteua Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano na atakuwa akishughulikia Mawasiliano. Dkt. Maria Sasabo anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Faustin Kamuzora ambaye ameteuliwa Katibu Mkuu
Ofisi ya Makamu wa Rais.
Pia Rais Magufuli
amemteua Mhandisi Angelina Madete kuwa Naibu Katibu Mkuu Katika Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Mhandisi Angelina Madete anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na Dkt. Maria Sasabo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano.
Aidha, Rais
Magufuli amemteua Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii.
Wakati
huo huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Christopher Ole
Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.Bw. Christopher
Ole Sendeka anachukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo
cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Dkt. Rehema
Nchimbi anajaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye ameteuliwa
kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo.Katika
hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Dkt. Osward
J. Mashindano kuwa Msajili wa Hazina.
Dkt. Osward J.
Mashindano anachukuwa nafasi ya
Bw. Lawrence Mafuru ambaye atapangiwa kazi
nyingine
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais,
IKULU
Dar es Salaam
07 Desemba, 2016
Thursday, November 24, 2016
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUGUMZA NA VIONGOZI NA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao alichokiitisha kati yake na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Mistitu, Ofisini kwake mjini Dodoma Novemba 21, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kushoto kwake) na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akizungumza katika Mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Ofisini kwake mjiniDodoma Novemba 21, 2016.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao Ofisini kwake mjini Dodoma, Novemba 21, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) baada ya kuongoza kikao kati yake na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisini kwake mjini Dodoma Novemba 21, 2016.
____________________________
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa miezi na siku tisa kwa Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu kuhakikisha wanaweka mawe ya alama (beacons) kwenye mipaka yao ili kuepusha migogoro na wanavijiji wanaowazunguka.
Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatatu, Novemba 21, 2016) wakati akizungumza na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu nchini katika kikao alichokiitisha kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma.
“Tatizo la migogoro baina ya wafugaji, wakulima na kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya ni lazima lifanyiwe kazi. Mkitoka hapa rudini katika maeneo yenu mkawaambie wananchi mipaka yenu iko wapi. Ninyi mnatambua mipaka yenu iko wapi kwa hiyo waelewesheni wananchi kwa kuweka alama,” amesema.
“Wakati Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli akizindua bunge tarehe 20 Novemba, 2015 aliwapa maeneo makuu matatu ambayo ni kuanisha mipaka, kupambana na ujangili na kukusanya mapato. Alizungumzia suala la mipaka kwa sababu iliyopo haieleweki, mkiulizwa mnajibu kuna buffer zone. Hivi mwananchi wa kawaida anajua buffer zone ni nini?,” alihoji.
“Sasa ninawapa muda hadi Januari 31, 2017 kazi ya kuweka beacons kwenye hifadhi zote za misitu iwe imekamilika. Kila pori nenda mkatengeneze alama zenu kama TANROADS walivyofanya. Kaeni mpige hesabu ni kiasi gani cha saruji na kokoto kinahitajika. Tutarudi hapa Dodoma kupeana taarifa ya utekelezaji. Katibu Mkuu niletee taarifa ya kila mkoa na wilaya kuna mapori mangapi tutakutana hapahapa kupeana mrejesho,” alisisitiza.
Alisema kama TANROADS waliweza kuweka alama za barabarani kwa nchi nzima ni kwa nini Wizara ya Maliasili na Utalii imeshindwa kuchukua hatua kama hizo. “Ni lazima tuweke hizo alama kila katika pori lake, tusipofanya hivyo, migogoro hii itaendelea,” alisema.
“Nendeni mkaweke alama za mipaka mkishamaliza sasa muwaeleze wananchi ni umbali wanapaswa waache kutoka kwenye hizo alama zenu na muwaelimishe kwamba hiyo ndiyo buffer zone. Suala la beacons ni serious na ninatarajia nikute hizo beacons kwenye maeneo yenu”
“Kila mmoja anayo fursa ya kuitisha mkutano na wananchi na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kuwa na mapori ya akiba. Pandeni kwenye majukwaa, muelezee mipaka hiyo mipya na wananchi watawaelewa kwa sababu mwenye dhamana ya kwanza katika kutoa elimu hii ni wewe Mkuu wa Pori,” alisistiza.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema kuanzia leo Ofisi ya Rais TAMISEMI haina budi kusitisha usajili wa vijiji hadi zoezi la kuweka alama kwenye mipaka mapori ya hifadhi za misitu litakapokalimika.
“Kuanzia leo ninasimamisha zoezi la usajili wa vijiji unaofanywa na TAMISEMI hadi wizara ya Maliasili na Utalii ikamilikshe zoezi la kuainisha na kuweka alama kwenye mipaka mapori ya hifadhi za misitu. Tusipofanya hivyo tutaendelea kuwa na Taifa la walalamikaji,” alisema huku akishangiliwa na watendaji hao.
“Wakuu wa mapori tambueni ni vijiji vingapi ambavyo Serikali ilifanya makosa na kuvisajili wakati viko ndani ya hifadhi na vijiji vingapi bado havijasajiliwa. Pia onyesheni ni vijiji vingapi ambavyo ni hatarishi,” alisema.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu amemtaka Mkurugenzi wa Idara ya Utalii katika wizara hiyo, Bw. Zahoro Kimwaga pamoja na Bodi ya Utalii nchini wabadilike na kuanza kufanya kazi kibiashara zaidi.
“Mkurugenzi wa Utalii na Bodi yako ya Utalii bado hamjajitangaza vya kutosha. Promosheni ya utalii hapa nchini bado haitoshi na mgeweza kuoata mapato makubwa zaidi kwa kujitangaza. Mabango ya barabarani yamejaa matangazo ya Vodacom na Airtel badala ya kuwa na picha za wanyama ili kila mtu akiona atamani kwenda mbugani,” alisema.
“Tumieni mabango ya kieletroniki (electronic screens) kurusha picha za wanyama. Mfano pale nje ya uwanja wa Taifa, au uwanja wa ndege hata kwenye njia kuu za mikoani wekeni mabango ya iana hiyo. Ombeni vipindi kwenye televisheni nyingine, kile cha TBC1 peke yake hakitoshi,” alisisitiza.
KUKUZA UCHUMI KUPITIA SEKTA YA UTALII KUNAHITAJI WAFANYAKAZI WENYE SIFA - MAGHEMBE
Waziri wa Maliasili na utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akisikiliza maelezo ya mmoja wa wahitimu wa mafuzo ya upishi katika hoteli za kitalii wakati wa mahafali ya sita ya Chuo cha Hoteli na Utalii Njuweni kilichopo Kibaha, mkoani Pwani hivi karibuni.
_______________________________
_______________________________
Waziri wa Maliasili na utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema ili Tanzania iendelelee kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii inahitaji wafanyakazi wa kada hiyo wawe na sifa zinazostahili ikiwemo nidhamu na uaminifu.
Ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 6 ya Chuo cha Hotel na Utalii cha Njuweni kilichoko Kibaha mkoani Pwani ambayo yalifanyika kwenye viwanja vya Chuo hicho.
Alisema kuwa pamoja na vyanzo mbalimbali vya mapato vinavyokuza uchumi wa taifa taifa, Wizara ya Maliasili na Utalii ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi huo hivyo kinachotakiwa ni kuhakikisha watu wanaopewa dhamana ya kufanyakazi kwenye Wizara hiyo wanafanya kazi kwa weledi.
"Napenda kuwakumbusha kuwa nidhamu na uaminifu ndiyo siri itakayowawezesha ninyi kufika mbali katika utendaji wenu wa kazi, lakini mkiingiza tamaa na udokozi hamtafika mbali na badala yake mtalitia taifa kwenye sifa mbaya" alisema
Alisema kuwa Serikali imekuwa ikikuza uchumi wa nchi kila mwaka kupitia Sekta ya utalii ambapo idadi ya watalii imekuwa ikiongezeka kwa asilimia 23.7 kutoka watalii 867,994 mwaka 2011 hadi kufikia watalii 1,137,182 mwaka 2015. Aidha sekta hiyo inachangia asilimia 17 ya pato la taifa.
"Mapato yatokanayo na shughuli za utalii yaliongezeka kwa asilimia 28.8 kutoka dola za Marekani mil. 1,353.29 mwaka 2011 hadi kufikia dola za Marekani mil. 1,901.1 mwaka 2015" alisema
kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Nditi Rashid alisema kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana kwa miaka kadhaa tangu kuanzishwa kwa chuo hicho lakini bado kuna changamoto kadhaa zinazowakabili ikiwemo upungufu wa vifaa vya kisasa vya kuendeshea masomo ya TEHAMA
"kutokana na ufinyu wa bajeti tulionao tunakuomba mheshimiwa mgeni rasmi utusaidie kupata msaada wa vifaa vipya vitakavyotusaidia kuendesha masomo ya TEHAMA kwa ufanisi zaidi" alisema
Mahafari hayo ambayo ni ya sita tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 200o yalihusisha jumla ya wanafunzi 350 waliohitimu kwa ngazi ya stashahada ambao walipata vyeti na zawadi mbalimbali .
Wednesday, November 23, 2016
HAKUNA KIONGOZI WA JUU WA SERIKALI ANAYEPINGA ZOEZI LA UHIFADHI NCHINI – MAJALIWA
NA HAMZA TEMBA - WMU
......................................................................
Kufuatia malalamiko ya wahifadhi juu ya kauli na vitendo mbalimbali za baadhi ya wananchi na viongozi wa kisiasa vyenye lengo la kukwamisha shughuli za uhifadhi nchini kwa maslahi yao binafsi kwa visingizio kuwa ni maagizo kutoka juu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa tamko na kusema kuwa hakuna kiongozi wa juu wa Serikali anayepinga zoezi la uhifadhi wa maliasili nchini.
Majaliwa
ameyasema hayo juzi wakati akizungumza na viongozi na watendaji wakuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii, wakuu wa taasisi za uhifadhi zilizopo chini ya wizara
hiyo na wakuu wa hifadhi za taifa pamoja na mapori ya akiba katika kikao
alichokiitisha kwenye ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma.
“Wapo watu
wanaotumia majina ya viongozi wakuu kukwamisha mazoezi yanayoendeshwa na
wahifadhi nchini. Hakuna kiongozi wa juu anaeweza kuzuia zoezi muhimu kama
hili. Na Kama kuna mtu anakuja kukuambia wewe fulani kasema, mwambie
niunganishe na yeye mwenyewe. Tumeona maeneo mengi sana, watu wanafanya
madudu wanasema huyu kaagizwa kutoka juu, juu ni wapi, kwa Mkurugenzi wako? kwa
Katibu Mkuu? Naibu Waziri au Waziri? Au huku kwa Waziri mkuu? Makamu wa
Rais au Rais?,” alihoji.
“Fanyeni,
bora ukosee halafu tuseme hapo umekosea utarekebisha, kuliko kuogopa kufanya
kwa sababu mtu kakukwamisha, kwani ulivokuwa unaimplement (unafanya) alikuambia
nani? si kutokana na na sheria na taratibu, muhimu zaidi ni kuzingatia sheria
na taratibu, usije ukafanya mambo ya ajabu,” aliongeza.
Ili
kufanikisha zoezi hilo aliwaagiza pia kuhakikisha wanaweka alama za mipaka (beacons)
katika hifadhi zao hadi kufikia januari 31, 2017 ili kuepusha migogoro na
wananchi wanaovamia maeneo hayo kwa makusudi au kwa kutokujua maeneo ya mipaka
husika.
“Nendeni
mkawaambie mwisho ni hapa weka na beacon kabisa, na sheria zitachukua mkondo
wake kwa yeyote ambaye hatafata maelekezo yenu. Tatizo la migogo iliyozungumzwa
kati wa wafugaji na wahifadhi au wafugaji na kamati za ulinzi na usalama za
wilaya na mikoa ni lazma likafanyiwe kazi, lazima tuendelee kudhibiti kuingia mifugo
ndani ya mapori,” alisisitiza.
Aliwaagiza
pia kusimama kwenye majukwaa na kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi
wanaozunguka maeneo yao ya hifadhi. “Namba moja wa utoaji elimu ni wewe mkuu wa
pori, ni lazma utoe maelezo ya pori lako ni wapi linakoishia, kama mpaka huo ni
wa kisheria muwaambie, nini umuhimu wa kutoingia, wananchi wapate elimu namna
ya kuhifadhi pori na faida zake,” alisema.
Akizungumzia
changamoto iliyoibuliwa katika kikao hicho kuhusu mgongano uliopo katika
usimamizi wa misitu baina Wakala wa Huduma za misitu Tanzania na Serikali za
Mitaa alisema Serikali inaenda kuliangalia upya suala hilo ili ione namna bora
ya kutoa majukumu ya kusimamia rasilimali zote za misitu kwa chombo kimoja
tofauti na ilivyo hivi sasa, hatua ambayo inaelezwa kuwa itasaidia kwa kiasi
kikubwa kuondoa changamoto za uharibifu wa misitu nchini.
“Kama
ilivyoelezwa kuwa kuna mgongano wa majukumu kwenye kitengo cha misitu, baina ya
TFS na DFO (Ofisa misitu wa Wilaya), DFO anauza bila hata kumconsult (kumtaarifu)
TFS na anagonga na nyundo…, kwa hiyo tutaliangalia tuone majukumu yale na namna
ambavyo tunaweza tukayapa chombo kimoja ili kisimamie lakini TFS mmeperform
(mmefanya) vizuri endeleeni kufanya hivyo vizuri kwa sasa,” alisema huku akipigiwa
makofi na watendaji hao.
Changamoto
nyingine iliyoibuliwa katika kikao hicho ni matukio ya kuingizwa kwa mifugo
katika maeneo ya hifadhi yaliyoko mpakani huku asilimia kubwa ya mifugo hiyo
ikielezwa kutoka nje ya nchi, Waziri Mkuu Majaliwa amekemea kitendo hicho na
kuagiza mifugo hiyo iondolewe mara moja. “Hatutaki ng'ombe wa nje ya nchi
kuingia ndani ya nchi, mifugo ya ndani imetutosha,” alisema.
Aidha ameutaka
uongozi wa Wizara kuimarisha doria za mara kwa mara, kuongeza ajira za
makamanda (askari wa wanyamapori) na vitendea kazi muhimu vya kuimarisha doria
ikiwemo magari.
Kwa upende
wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alisema ipo
changamoto kubwa ya tishio la kutoweka kwa mvua na kukauka kwa vyanzo muhimu
vya maji nchini kutokana na uharibifu wa maeneo yaliyohifadhiwa pamoja na
mlipuko wa magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na muingiliano wa mifugo na
wanyamapori kama vile kimeta na homa ya bonde la ufa.
Naye
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Wizara hiyo, Zahoro Kimwaga alisema, umuhimu
wa uhifadhi una faida mtambuka ambapo sekta ya utalii pekee inachangia
asilimia 17 ya pato la taifa huku ikitoa ajira za moja kwa moja na zisizo za
moja kwa moja takriban milioni 1.5. Alisema sekta hiyo pia inachangia asilimia
25 ya mapato yote ya fedha za kigeni ikiwa ni sekta kiongozi kwa muda wa miaka
mitatu mfululizo.
Aliongeza
kuwa hadi kufikia Novemba 20 mwaka huu takwimu zinaonyesha kuwa maendeleo ya
sekta ya utalii yameongezeka kwa asilimia 5 licha ya malalamiko mbalimbali kuhusu
sekta hiyo baada ya Serikali kuweka kodi ya VAT katika huduma za kitalii nchini.
Tuesday, November 15, 2016
WAZIRI WA MALIASILI, PROF. JUMANNE MAGHEMBE AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA MISITU KUJADILI UHAMASISHAJI NA UENDELEZAJI WA SEKTA HIYO
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kikanda wa Wadau wa Sekta ya Misitu wa nchi ya Finland na Tanzania uliofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam. Lengo kuu la mkutano huo likiwa ni kuhamasisha uwekezaji na kukuza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika uendelezaji wa misitu nchini. Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, Taasisi ya Uongozi - UONGOZI Institute na Shirika la Maendeleo ya Kifenda la Finland - FINFUND.
Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Serikali ya Finland, Kai Mykanen akizungumza katika Mkutano huo ambapo ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Finland na Tanzania katika kuendeleza Misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho ikiwa ni pamoja na kukuza teknolojia ya uhifadhi wa mazingira ya kupunguza hewa ukaa.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Eng. Angelina Madete na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo.
Baadhi ya wajumbe katika mkutano huo wakifualia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano huo. Alieleza kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa misitu unaotokana na uvunaji wa mkaa na ukataji wa magogo, uvunaji wa miti usio endelevu jambo lililoisukuma Serikali kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ya Finland na wananchi kwa ujumla kwa ajili kuendeleza misitu kwa kupanda miti mingi zaidi iweze kukidhi mahitaji yaliyopo. Aliongeza kuwa ni marufuku kusafirisha magogo na kwamba Serikali ya awamu ya tano imelenga kukuza viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani kwenye mazao ya misitu na kuyauza kama bidhaa. Ametoa wito kwa watanzania kujishuulisha na upandaji wa miti kibiashara ili kuinua maisha yao na uchumi wa taifa kwa ujumla. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali Gaudence Milanzi na kulia kwake ni Mkurugezi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kinyago, Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Serikali ya Finland, Kai Mykanen katika hafla ya jioni iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam.
_____________________________
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kinyago, Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Serikali ya Finland, Kai Mykanen katika hafla ya jioni iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam.
_____________________________
Watanzania wametakiwa kutumia fursa ya upandaji wa miti kibiashara kuinua uchumi wa maisha yao na kuacha biashara haramu ya usafirishaji wa magogo nje ya nchi, badala yake watumie fursa hiyo kuzalisha bidhaa za misitu na kuziuza kwa faida zaidi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe aliyasema hayo jana Dar es
Salaam wakati akifungua mkutano wa uwekezaji wa misitu uliowashirikisha wadau
wa Mazingira kutoka nchi 16 ulioandaliwa kwa ushirikiano na Wizara ya Maliasili
na Utalii, Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, Taasisi ya Uongozi na Shirika la
Maendeleo ya Kifenda la Finland - FINFUND.
“Wawekezaji
wa misitu wanasema wanataka soko la mazao yao na sisi tunasema soko lipo
isipokuwa watengeneze bidhaa kama vitanda, viti na samani za ndani pamoja na
makaratasi na vifaa vyote vinavyotokana na miti na hiyo ndiyo itawasaidia ndugu
zetu kupata ajira na viwanda vitaongezeka.
“Tukiruhusu
magogo kwenda nje itakuwa kama pamba yetu inalimwa hapa na kusafirishwa halafu
inatengeneza nguo na tunaletewa, lazima Viwanda vijengwe na hiyo si kazi
ngumu.... Tunachotaka hapa teknolojia ya viwanda ije, wasafirishe bidhaa na si
magogo,” alisema Profesa Maghembe.
Aliongeza
kuwa “Tunataka kufanya uwekezaji katika hewa ukaa, ambayo italeta tija kwa
jamii na kutumia zaidi teknolojia katika upandaji wa miti ili kuongeza ubora na
soko la mazao hayo”.
Alisema
inakaridiwa kwamba hekta 30,000 za misitu zinapotea kila mwaka kutokana na
sababu mbalimbali huku zikiwa zinapadwa hekta 80,000 hadi 100,000 kila mwaka.
Alisema kuna
changamoto kubwa ya uchomaji mkaa na wengine wanasafirisha nje kupitia kwa
bandari bubu na hivyo misitu kupotea kwa sababu pia ya uvunaji wa misitu usio
endelevu.
Alisema
changamoto nyingine ni uvunaji usio endelevu wa misitu na kupungua kwa vyanzo
vya maji kutokana na ukataji wa miti hovyo na uharibifu wa misitu, hivyo Serikali
inaongeza juhudi kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa.
Mkuu wa
Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja alisema jukumu lao ni kuwaweka
viongozi na wadau mbalimbali katika kuangalia maendeleo endelevu ambapo kwa
sasa wanaangalia namna ya kukabiliana na changamoto kubwa ya mabadiliko ya
tabianchi ikiwa ni pamoja na kuboresha na kuendeleza misitu kibiashara.
Mwakilishi wa
Benki ya Dunia, Yutaka Yoshino alisema Idara ya Misitu nchini imekuwa
ikichangia ukuaji wa uchumi nchini, lakini sekta hiyo imekuwa ikikabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabianchi.
Subscribe to:
Posts (Atom)


