slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Tuesday, July 17, 2018

DK. KIGWANGALLA AAGIZA KATIBU WA UVCCM TARIME KUKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA YA KUIKASHIFU SERIKALI

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima mtego wa misumari uliotegwa na watu wasiojulikana kwa lengo la kuzuia msafara wake wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.

Tarime - Mara
.......................................................
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameliagiza Jeshi la Polisi wilaya ya Tarime mkoani Mara kumkamata na kumfungulia mashtaka Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya hiyo, Newton Mongi na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Richard Tiboche kwa tuhuma za kuikashifu Serikali na kuchochea mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi ya Serengeti na vijiji jirani.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana majira ya saa tatu usiku baada ya kuhitimisha ziara yake wilayani humo iliyolenga kutafuta suluhu ya mgogoro uliodumu kwa miongo kadhaa kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani ikiwemo kijiji cha Kegonga.

Akiwa njiani majira ya saa tatu za usiku kwenye gari la wazi baada ya kukagua eneo hilo la mpaka kwa zaidi ya masaa sita, Waziri Kigwangalla na msafara wake walikuta lundo la mawe yakiwa barabarani ndani ya eneo la hifadhi hiyo, hali iliyosababisha taharuki kubwa na msafara wake kushuka na kuanza kuondoa mawe hayo ili kupata njia ya kupita.

Wakati zoezi hilo likiwa  linaendelea, Kiongozi huyo wa UVCCM alisikika akiituhumu Serikali kwa kuweka mawe hayo na kwamba hayakuwekwa na wananchi wa eneo hilo, jambo lililozua mshangao mkubwa  kwa viongozi wa Serikali waliokuwepo katika msafara huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.

Mkuu huyo wa mkoa alisema tukio hilo sio la mara ya kwanza na kwamba limewahi kuripotiwa mara nyingi na uongozi wa hifadhi hiyo kuwa wananchi wa vijiji jirani hujaza mawe barabarani kwa ajili ya kuzuia magari ya doria ili waweze kulisha mifugo yao ndani ya hifadhi hiyo. Alisema hata msafara wa tume ya Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda iliyoundwa na CCM hivi karibuni kufuatilia mgogoro katika eneo hilo nao ulizuiliwa kwa mawe barabarani.

Imedaiwa pia kuwa kwa nyakati tofauti viongozi hao wamekuwa wakiwatolea viongozi wa Serikali maneno ya kejeli pamoja na kuwakwamisha kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi ipasavyo.

Awali, kabla ya tukio hilo la mawe barabarani moja ya gari lililokuwa likiongoza msafara huo lilipata pancha baada ya kukanyaga misumari iliyokuwa imetengwa kwenye moja ya barabara zinazoingia na kutoka ndani ya Hifadhi ya hiyo ya Serengeti.

Waziri Kigwangalla alisikitishwa na kitendo hicho ambacho alikielezea kuwa sio cha kiuungwana kwa kuwa kinalenga kudhoofisha juhudi za Serikali kumaliza mgogoro huo kwa faida ya pande zote.

"Mimi ni Muislam, nimesikia kwa masikio yangu na wala sijaambiwa na mtu yeyote na siwezi kumsingizia mtu, nimeshangazwa sana na kiongozi tena mtendaji wa chama tawala anawezaje kuitukana Serikali, na hapa sisi tumekuja kuwahudumia wananchi" alisema Dk. Kigwangalla kwa masikitiko makubwa.

Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa wananchi wote waliovamia ndani ya Hifadhi ya Serengeti na eneo la wazi (buffer zone) ambao wanaendesha shughuli zao ikiwemo kilimo, ufugaji na makazi kuachia maeneo hayo kwa hiari yao wenyewe, na kwamba muda huo ukipita wataondolewa kwa nguvu na chochote kitakachokutwa ndani ya eneo hilo kitatekezwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumzia kuhusu suluhu ya mgogoro huo wa mpaka amesema, Serikali itaunda timu ya wataalam kutoka wizarani kwake, wizara ya ardhi, uongozi wa mkoa wa Mara na wilaya ya Tarime ambao watashirikiana na watu wengine huru watakaochaguliwa na wananchi wa vjiji husika wakiongozwa na mbunge wao, John Heche ambao watakuwa na uelewa wa kusoma ramani na kutafsiri mipaka ili kushirikiana kuhakiki mipaka halisi ya eneo hilo na kufikia muafaka.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kushoto) na viongozi wengine wa mkoa huo wakiangalia mawe yaliyowekwa njiani kuzuia msafara wake kutoka ndani hifadhi ya Serengeti na watu wasiojulikana wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi hiyo na vijiji jirani jana usiku.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake  ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge wa Tarime John Heche wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa eneo lenye mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro huo mkoani Mara jana. Katikati aliyeinama ni Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake  ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake  ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisoma taarifa mbalimbali kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani vya wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wakati wa ziara yake  ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya vijiji na hifadhi hiyo jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche.

Sunday, July 15, 2018

DK. KIGWANGALLA AAGIZA MBINU HII MPYA ITUMIKE KUDHIBITI TEMBO WAHARIBIFU BUNDA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akijibu kero mbalimbali za wananchi katika kijiji cha Mariwanda kata ya Hunyari wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Lydia Bupilipili na Mbunge wa Bunda Vijijini, Bonafasi Mwita Getere (kulia). 

Na Hamza Temba, Bunda, Mara
.........................................................................

Kilio cha muda mrefu cha wananchi wa wilaya ya Bunda hususan katika ukanda unaopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuhusu wanyamapori waharibifu jamii ya Tembo kuvamia makazi yao na  mashamba kinaelekea kupata ufumbuzi wa kudumu.
Hatua hiyo inakuja kufuatia agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuanzisha mradi wa ufugaji nyuki kwa vijiji kumi vinavyopakana na hifadhi hiyo ili watumike kama uzio wa kudhibiti wanyamapori hao.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mariwanda, kata ya Hunyari wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani humo. 
"TANAPA wakishirikiana na TFS waje waanzishe mradi wa ufugaji nyuki wa kisasa katika vijiji vyote 10 vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa Serengeti, waje wahamasishe uundwaji wa vikundi, wafundishe namna ya kuweka mizinga ya kisasa na namna ya kufuga nyuki na kuvuna, na mwisho wa siku wananchi wapate faida ya kuzuia wanyamapori kuvamia mashamba na makazi yao pamoja na kuvuna asali itakayowatengenezea kipato mbadala" ameagiza Dk. Kigwangalla. 
Akielezea mbinu hiyo mpya inavyofanya kazi Dk. Kigwangalla amesema, wataalamu ndani ya wizara yake wameeleza kuwa mbinu hiyo ya kuweka mizinga ya nyuki kuzunguka maeneo ya mashamba na makazi ya wananchi itasaidia kudhibiti Tembo  kwakuwa huogopa sana nyuki na endapo wakisikia tu harufu yake huwa vigumu kusogelea maeneo hayo.
Awali akiwasilisha malalamiko kwa niaba ya wananchi wa vijiji hivyo, Mbunge wa Bunda Vijijini, Bonifasi Mwita Getere alisema kwa muda mrefu sasa wananchi hao wamekuwa wakipata madhara ya kuvamiwa na Tembo ambao hula mazao yao mashambani na hata majumbani, kuwajeruhi wananchi na wengine kupoteza kabisa maisha.
Baraka Abdul ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mariwanda wilayni humo alisema, mbinu zinazotumika kufukuza Tembo hivi sasa ikiwemo kupiga makelele na madebe na kutumia tochi za mwanga mkali zimekua hazisaidii, hivyo ameiomba Serikali kuongeza idadi ya askari na vituo katika maeneo yanayoathirika zaidi na matukio hayo.
Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ametoa onyo kali kwa wananchi wanaofanya vitendo vya ujangili na uingizaji mifugo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuwataka kuacha mara moja kwakuwa wakikamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kutaifishwa mifugo yao kwa mijibu wa kifungu cha 111 Na. 5 cha Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 2009.
Katika hatua nyingine, ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kupitia eneo la mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Bufer Zone) kuanzia Ghuba ya Speke hadi kwenye mpaka na nchi ya Kenya, wabaini mipaka halisi na ramani na kuainisha mahitaji ya wananchi na changamoto zilizopo na hatimaye kuwasilisha kwake mapendekezo ya kuondoa changamoto zilizopo.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na uongozi wa wilaya ya Bunda alipowasili wilayani hapo jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza uongozi wa wilaya ya Bunda ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Lydia Bupilipili (kulia kwake) wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kutatua changamoto za uhifadhi wilayani humo jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kata Nyatwali wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za uhifadhi katika wilaya ya Bunda mkoani Mara jana. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Martin Loibooki na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili (wa pili kulia). 
Mwananchi wa kata Nyantwali akitoa maoni yake kwa Waziri Kigwangalla.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bukore wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za uhifadhi katika wilaya ya Bunda mkoani Mara jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini, Bonifasi Mwita Getere muda mfupi baada ya kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Bukore wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za uhifadhi katika wilaya ya Bunda mkoani Mara jana.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mariwanda  wakati ziara ya Waziri Kigwangalla wilayani humo.
Baraka Abdul, mkazi wa kijiji cha Mariwanda akiwasilisha maoni yake kwa waziri Kigwangalla katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.
Dk. Kigwangalla akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mariwanda.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akijibu akifafanua jambo katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Mariwanda kata ya Hunyari wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dk. James Wakibara akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mariwanda wakimasikiliza Waziri Kigwangalla (hayuko pichani) wakati wa mkutano wa hadhara kijijini hapo.

Wednesday, July 11, 2018

DK. KIGWANGALLA AAGIZA POLISI KUMKAMATA MKUU WA KANDA, PORI LA AKIBA RUKWA, AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA MISITU TFS

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishiriki na viongozi wengine wa mkoa wa Katavi kuzima moto uliokutwa ukiwaka ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Inyonga wakati wa ziara yake katika wilaya ya Mlele mkoani humo jana.

Na Mwandishi Maalum, Mlele Katavi
....................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani Katavi kumkamata na kumfungulia mashtaka Mkuu wa Kanda - Pori la Akiba Rukwa, Emannuel Barabara kufuatia tuhuma za uhujumu uchumi zinazomkabili.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni miezi mitatu tangu alipomsimamisha kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo ambazo amesema tayari zimethibitishwa kupitia taarifa mbalimbali za kiuchunguzi.

Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo jana muda mfupi baada ya kupokea taarifa ya Wilaya ya Mlele iliyowasilishwa kwake na Mkuu wa Wilaya hiyo, Rachel Kasanda  wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani humo.

Amesema Barabara anatuhumiwa kwa vitendo vya uhujumu uchumi kwa kushindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo pamoja na kushirikiana na majangili kuruhusu uvunaji holela wa raslilimali za misitu ndani ya pori hilo kwa maslahi yao binafsi. 

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rachel Kasanda alisema katika kipindi cha mwezi Desemba 2017 hadi Februari 2018 kamati yake ya ulinzi na usalama ilipata taarifa za uvamizi mkubwa katika Pori la Akiba Rukwa ambapo iliamua kufanya operesheni maalum iliyosaidia kukamata watu 22 waliokuwa wakichana mbao na kukamata mbao 5,122, slipa 924 na magogo 188.

Alisema kwa kiasi kikubwa uhalifu huo ulichangiwa na ndugu Barabara ambaye hakutaka kuweka wazi uhalifu uliokuwa ukifanyika ndani ya pori hilo kwa kamati yake ya ulinzi na usalama na badala yake aliiaminisha kuwa mambo ni shwari ndani ya pori hilo.

Halikadhalika, Dk. Kigwangalla ameagiza maofisa na askari wote 34 wa Pori la Akiba Rukwa kurudishwa makao makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ili kupangiwa kazi nyingine, ambapo kabla ya zoezi hilo ameagiza wahojiwe na TAKUKURU kuhusu mwenendo wa vitendo vya Mkuu wa Kanda hiyo, Emmanuel barabara na endapo nao watathibitika kuhusika wafunguliwe mashtaka ya kushirikiana nae katika tuhuma zinazomkabili.

Wakati huohuo Waziri Kigwangalla amemsimamisha kazi, Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu wa wilaya ya Mlele, Ezeckiel Mbilinyi na  watumishi wengine watatu kwa kile alichokieleza kuwa ni uzembe wa kushindwa kusimamia vizuri rasilimali za misitu wilayani humo sambamba na tuhuma za kushirikiana na ndugu Emmanuel Barabara kuhujumu rasilimali za misitu kwa kutoa vibali na kugonga nyundo (mihuri) rasilimali hizo zilizokuwa zikivunwa kinyume cha sheria kwenye maeneo ya hifadhi. 

Kufuatia uamuzi huo, Dk. Kigwangalla ametangaza kusimamisha zoezi la utoaji wa vibali vipya vya uvunaji na usafirishaji wa mbao na magogo kwa mikoa ya kanda ya magharibi ikiwemo Katavi na Tabora kwa kipindi cha miezi mitatu mpaka hapo utaratibu mzuri utakapowekwa wa kudhibiti uvunaji wa rasilimali hiyo kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria. 

Aidha ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Mlele kufanya uhakiki wa vibali vya uvunaji wa mbao na magogo ambavyo vimeshatolewa ili kujiridhisha juu ya uhalali wake kabla ya kutoa vibali vya usafirishaji. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishiriki na viongozi wengine wa mkoa wa Katavi kuzima moto uliokutwa ukiwaka ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Inyonga wakati wa ziara yake katika wilaya ya Mlele mkoani humo jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mapori ya Akiba ya Rukwa na Lwafi, Pasko Mrina kuhusu namna bora ya kuimarisha ulinzi wa rasilimali za misitu na wanyamapori katika mapori hayo wakati wa ziara yake kwenye wilaya ya Mlele mkoani Katavi jana. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rachel Kasanda.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu, Kanda ya Magharibi, Valentino Msusa kufuatia uharibifu uliofanywa kwenye Hifadhi ya Msitu wa Inyonga uliopo wilaya ya Mlele mkoani Katavi wakati wa ziara yake wilayani humo jana. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Rachel Kasanda. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu, Kanda ya Magharibi, Valentino Msusa kuhusu magogo yaliyokamatwa baada ya kuvunwa kinyume cha Sheria ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Inyonga wakati wa ziara yake wilayani hapo jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mapori ya Akiba ya Rukwa na Lwafi, Pasko Mrina kuhusu namna bora ya kuimarisha ulinzi wa rasilimali za misitu na wanyamapori katika mapori hayo wakati wa ziara yake kwenye wilaya ya Mlele mkoani Katavi jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rachel Kasanda.

Monday, July 9, 2018

WAZIRI KIGWANGALLA ATEMBELEA HIFADHI YA MSITU WA NORTH EAST MPANDA, TONGWE NA MAPOROMOKO YA NKONDWE MKOANI KATAVI

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa wilaya ya Tanganyika alipotembelea wilaya hiyo jana wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhifadhi mkoani Katavi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Salehe Mbwana Mhando.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa ramani ya Hifadhi ya Msitu wa North East Mpanda alipotembelea msitu huo jana kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Kigwangalla akikagua moja ya eneo la chanzo cha maji yanayozalisha Maporomoko ya Nkondwe katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi jana, maji hayo yanapita chini ya miamba (mawe) inayoonekana. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Salehe Mhando. 
Waziri Kigwangalla akivuka kigingi alipokua akienda kuangalia maporomoko ya Nkondwe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wakikagua eneo la Msitu wa Hifadhi wa North East Mpanda ambao pia una kivutio cha utalii cha Maporomoko ya Nkondwe wilayani humo.
Muonekano wa Maporomoko ya Nkondwe jana ambayo ni moja ya kivutio cha utalii, katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu Maporomoko ya Nkondwe na fursa za utalii zinazopatikana katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi jana. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Salehe Mbwana Mhando.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wakifurahia maporomoko ya Nkondwe ambayo ni miongoni mwa vivutio vya asili mkoani humo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia maumbo ya asili kwenye miamba iliyopo karibu na Maporomoko ya Nkondwe ambayo ni miongoni mwa kivutio cha utalii katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi jana.  Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Salehe Mhando.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya Tanganyika akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo, Selehe Mhando (wa pili kulia) wakikagua Msitu wa Hifadhi wa North East Ugala baada ya kutembelea maporomoko ya Nkondwe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya Tanganyika akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo, Selehe Mhando (kulia kwake) wakiwa wamepumzika kidogo baada ya kupanda mlima uliopo ndani ya Msitu wa Hifadhi wa North East Ugala baada ya kutembelea maporomo ya Nkondwe jana.
Msitu wa Tongwe ni moja ya misitu michache ya asili iliyohifadhiwa vizuri mkoani Katavi.

DK. KIGWANGALLA ATEMBELEA MAPOROMOKO YA KALAMBO, AMBAYO NI YA PILI KWA UREFU AFRIKA

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa wakifurahia kufika karibu na  kina cha Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, maporomoko haya ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kuelekea karibu na kina cha Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, maporomoko haya ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipanda mlima baada ya kuona Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, maporomoko haya ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa wakishuka kwenda kuona Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa wakinawa mikono kwenye mto kalambo ambao unatengeneza Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika katika kijiji cha Kapozwa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kapozwa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa muda mfupi baada ya kutembelea Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mandhari ya Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika katika kijiji cha Kapozwa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika katika kijiji cha Kapozwa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa Serikali wakishuka kwenda kuona Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, maporomoko haya ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa wakipanda ngazi baada ya kuona Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, maporomoko haya ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
 Muonekano wa eneo la kuingilia kuelekea kwenye mporomoko ya mto Kalambo.
Muonekano mwanana wa Maporomoko ya Mto Kalambo.