
slider gif
kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ
Monday, May 8, 2017
Saturday, May 6, 2017
WANAHABARI WA ISRAEL WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA GOMBE, WAAHIDI KUTANGAZA VIVUTIO VYA TANZANIA NCHINI HUMO
Kundi la waandishi wa habari kumi kutoka nchini Israel wakiwa katika hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa ajili ya kurekodi vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuvitangaza nchini kwao ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na Hifadhi za Taifa (TANAPA). Kwa sasa soko la utalii la mashariki ya kati limeanza kufunguka kwa kasi ambapo hivi karibuni Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel Ehud Barak ametembelea hifadhi za Ngorongoro na Serengeti.
HAMZA TEMBA - WMU
.......................................................................
Kundi la wanahabari kumi
akiwemo muigizaji mmoja na maofisa wa kampuni ya utalii ya Safari kutoka nchini
Israel limetembelea hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyopo mkoani Kigoma na kufurahia
vivutio lukuki vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo na kuahidi
kuvitangaza watakaporudi nchini kwao ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Maliasili na
Utalii kupitia TANAPA na Bodi ya Utalii kutangaza vivutio hivyo nchini humo.
Akizungumza hivi karibuni mara
baada ya kukamilika kwa ziara hiyo ya siku mbili, Kiongozi wa kundi hilo, Ronit
Hershkovitz alisema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa ambapo wamefurahia
kuona vivutio vya kipekee katika hifadhi hiyo na kuahidi kuwa mabalozi wazuri
wa vivutio hivyo nchini Israel.
“Ni furaha kubwa kuwa hapa
Gombe, tumeona makundi ya Sokwe na fukwe nzuri za Ziwa Tanganyika, tuko hapa
kwa ajili ya kwenda kueleza kivutio hiki na vivutio vingine vya Tanzania nchini
Israel, Waisrael wanaipenda Tanzania na wanapenda kutembelea Tanzania, tumeona
ongezeko kubwa la watalii katika miaka ya hivi karibuni kutoka Israel baada ya
kazi ngumu ya muda mrefu, sasa tuna furaha kuona watalii wengi wanaongezeka na
tungependa kuona pia Watanzania wengi wakitembelea Israel,” Alisema Ronit.
Aliongeza kuwa, “Tunaenda
kueleza taarifa hizi kwenye mitandao ya kijamii, magazeti, televisheni na
popote tutakapoweza, lakini kubwa zaidi ni kuwaeleza marafiki zetu ana kwa ana
uzuri wa Tanzania kwasababu tunaipenda Tanzania, nakupenda sana”.
Walfson Noa, ambaye ni
Mwandishi wa Mitandao ya Kijamii na Meneja Masoko wa Kampuni ya Utalii ya
Safari ya Israel alisema, “Tulifanya matembezi kuwaona Sokwe wanaovutia sana huku
wakiishi katika mazingira yao ya asili, hili ziwa ni la maajabu sana (Ziwa
Tanganyika), hata nyani nao walikuwa wakijaribu kuingia kwenye mahema yetu ni
jambo la kuvutia, katika mtizamo wa kimasoko hili ni eneo ambalo nitawashauri
wateja wangu watembelee, ni kitu ambacho watu wanatakiwa kukifahamu, kugundua
siri ya uzuri wa hifadhi ya Taifa ya Gombe”
Kwa upande wake Meneja wa
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, Paschal Shelutete ambaye
alikuwa kiongozi wa msafara huo akishirikiana na Meneja Mawasiliano TTB,
Geofrey Tengeneza, Meneja Mawasiliano wa TFS, Glory Mziray na Afisa Mawasiliano
wa Wizara ya Maliasili, Hamza Temba alisema ujio wa wanahabari hao utaleta
chachu ya kuongezeka kwa watalii wengi kutoka Israel pamoja na kupanua soko la
utalii kwa hifadhi za mikoa ya magharibi mwa Tanzania ikiwemo hifadhi ya Gombe.
“Tumekuja na kundi hili la wanahabari
ambao wameamua kama mlivowasikia kwa dhati kabisa kwamba watakaporudi nyumbani
watatumia mitandao ya kijamii, radio mbalimbali, Televisheni lakini kubwa zaidi
magazeti, wataandaa makala na vipindi mbalimbali hivyo tunaamini kwa dhati
kabisa watakaporudi nyumbani na kuzifanyia kazi taarifa zote walizozipata
katika hifadhi ya Taifa ya Gombe ama kwa hakika tutashuhudia ongezeko kubwa la
watalii kutoka nchini Israel katika siku chache zijazo,” Alisema Shelutete.
Aliongeza kuwa, “Ni wajibu
wa kila Mtanzania kuhakikisha rasilimali hizi za hifadhi zinazopatikana katika
hifadhi za taifa zinaendelea kutunzwa kwa ajili ya kizazi hiki na vizazi
vijavyo, watalii hawaji kuangalia ng’ombe kwenye hifadhi zetu, nasisitiza kuwa mifugo
haikubaliki kwenye hifadhi zetu”.
Msafara huo ulikuwa na
wanahabari kutoka vyombo maarufu nchini humo ikiwemo kituo cha Televisheni cha Channel
2, Jarida la Atmosphere, Jarida la National Geographic, Jaria la wiki la Yediot
Acharanot -7 Yamim na waandishi wawili wa mitandao ya kijamii. Wengine ni
maofisa wawili wa kampuni ya Utalii ya Safari ya nchini humo.
Hifadhi ya Taifa ya Gombe ilianzishwa
mwaka 1968 kwa ajili ya tafiti za kisayansi, hususani katika kuwalinda na
kuwahifadhi wanyamapori adimu wa jamii ya Sokwe Mtu (chimpanzees) ambao wapo
hatarini kutoweka. Hifadhi hii inaelezwa kuwa na Sokwe wasiopungua mia moja
ambao huishi kwa makundi na kuwa kivutio kikubwa na adimu katika hifadhi hiyo ambayo
ina ukubwa wa kilomita za mraba 52.
Timu maalum ya wanahabari kutoka nchini Israel ikiwa na wajumbe kumi ilipowasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma tayari kwa ajili ya ziara ya kitalii ya siku mbili katika hifadhi ya Taifa ya Gombe. Ziaza hiyo iliandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na Shirika ya Hifadhi za Taifa Tanzani (TANAPA) kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Israel ikiwa ni mkakati maamlum wa kukamata soko la Mashariki ya Kati. Kutoka kulia wanaongoza msafara huo ni Meneja Mawasiliano TANAPA, Paschal Shelutete na Meneja Mahusiano wa TTB, Geofrey Tengeneza.
Wanahabari kutoka Israel wakipanda kwenye boti kwa ajili kunza safari kuelekea hifadhi ya Taifa ya Gombe. Msafara huo ulikuwa na wanahabari kutoka vyombo maarufu nchini humo ikiwemo kituo cha Televisheni cha Channel 2, Jarida la Atmosphere, Jarida la National Geographic, Jaria la wiki la Yediot Acharanot -7 Yamim na waandishi wawili wa mitandao ya kijamii. Wengine ni maofisa wawili wa kampuni ya Utalii ya Safari ya nchini humo.
Msafara wa Wanahabari wa Israel wakiwa kwenye boti tayari kwa safari ya kuelekea hifadhi ya Taifa ya Gombe ambapo kutoka Kigoma mjini hadi kwenye hifadhi hiyo ni mwendo wa saa moja na nusu hadi masaa mawili.
Mhifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Gombe, Elihuruma Wilson (kushoto) akitoa maelezo mafupi kwa wanahabari kutoka nchini Israel kuhusu hifadhi hiyo kabla ya kuanza ziara ya kutembelea vivutio vilivyopo. Alieleza kuwa hifadhi hiyo ina vivutio vingi wakiwemo Sokwe zaidi 100, Nyani, Kima, maporomoko ya maji, ndege aina mbalimbali na fukwe nzuri za kuogelea za ziwa Tanganyika.
Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Paschal Shelutete (kulia), Meneja Mahusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania (Geofrey Tengeneza) na Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Glory Mziray) wakiongoza msafara wa wanahabari wa Israel kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Timu ya wanahabari wa Israel wakianza safari ya kuingia ndani ya msitu wa hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa ajili ya kuona makundi mbalimbali ya Sokwe. Lengo kuu la ziara hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na TANAPA ni kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Israel.
Wanahabari kutoka Israel wakipata maelezo kutoka kwa mhifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Gombe kuhusu utarartibu wa kuzingatia wawapo ndani ya hifadhi hiyo ikiwemo kutokupiga kelele na kuepuka matumizi ya mwanga wa kamera (Flash Lights).
Mmoja ya wanahabari wa Israel, Gerald Eddie wa Jarida la National Geographic akiwa katika harakati za kupata taswira mwanana ya picha za Sokwe ndani hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Wanahabari wa Israel wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Sokwe akirukia matawi ya miti akiwa na mtoto wake ndani ya hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati wa ziara ya wanahabari wa Israel kwenye hifadhi hiyo.
Taswira mwanana ya Sokwe Mtu ndani ya hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati wa ziara hiyo.
Mtoto wa Sokwe akila matunda yanayopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati wa ziara ya wanahabari wa Israel katika hifadhi hiyo. Lengo kuu la ziara hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na TANAPA ni kutangaza vivutio vilivyopo Tanzania nchini Israel.
Sokwe akiwa kapumzika kwenye maeneo yake ya kujidai ndani ya hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati wa zaira ya wanahabari wa Israel katika hifadhi hiyo. Wanahabari hao walifurahia kuwaona sokwe hao wanaoelezewa na wanasayansi kuwa wanakaribiana na binaadamu kwa takribani asilimia 80.
Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Paschal Shelutete (wa pili kulia) akionesha kifaa maalum cha kupigia picha za angani (drone) kilichorushwa na mmoja wa mwanahabari ambaye ni mpigapicha kutoka Israel katika fukwe za Ziwa Tanganyika pembezoni mwa hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati wa zaiara ya wanahabari hao hifadhini hapo.
Kifaa hicho maalum cha kupiga picha za angani kijulikancho kama 'drone' kikiwa angani kupata taswira pana ya hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Wanahabari hao wakipiga picha za mwanahabari mwenzao na nyani wanaopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Gombe katika fukwe za Ziwa Tanganyika.
Mpiga picha wa Jarida la National Geographic la nchini Israel, Gerald Eddie akipiga picha nyani wanaopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Gombe ambao pia ni kivutio cha utalii katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuvitangaza katika jarida hilo.
Nyani akiwa kambeba mtoto wake katika hifadhi ya Taifa ya Gombe tukio ambalo pia sehemu ya vivutio vinavyopatikana katika hifadhi hiyo.
Wanahabari hao hawakutaka kupitwa na tukio lolote katika ziara yao hiyo, hapo wakipiga picha boti ambayo hufanya safari za kawaida kwa wananchi wa vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika na Manispaa ya Kigoma.
Mwanahabari maarufu nchini Israel, Dana Spector, wa Jarida la Yediot Acharonot (wa pili kushoto) na Mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni nchini humo, Ran Sarig wakiigiliza mkao wa nyani dume na jike katika fukwe za ziwa Tanganyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Mwanahabari maarufu nchini Israel, Dana Spector, wa Jarida la Yediot Acharonot (wa pili kushoto) na Mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni nchini humo, Ran Sarig wakifurahia matukio mbali mbali yaliyokuwa yakifanywa na nyani wa hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Wanahabari hao pia walipata fursa ya kuogolea katika fukwe za kitalii za ziwa Tanganyika pembezoni mwa Hifadhi hiyo ya Taifa ya Gombe, Fukwe hiyo ni kivutio kikubwa cha utalii katika hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Wanahabari hao wakiwa wanaogelea katika fukwe za kuvutia za ziwa Tanganyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Gombe huku wakipiga picha za tukio hilo kwa ajili kutangaza kivutio hicho nchini Israel.
Wanahabari hao pia walipata fursa kutembelea jamii ya kijiji cha Mwamgongo ambacho kinapakana na hifadhi ya Taifa ya Gombe, hapo wakimpiga picha mtoto aliyekuwa na mpira wa makaratasi ambao ni sehemu ya utalii wa kiutamaduni.
Mwandishi wa habari kutoka Israel ambaye ni mpiga picha wa kituo cha Televisheni cha Chanel 2, Roni Dahabari Kuban akiwapiga picha watoto katika kijiji cha Mwamgongo jirani na hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni nchini Israel, Ran Sarig akifungwa shuka aliyoinunua na wananchi wa Kigoma katika ziara hiyo. Shuka hizo zinazofumwa kwa mikono ni maarufu Mkoani Kigoma na sehemu ya utalii wa Kiutamaduni unaopatikana katika Mkoa huo.
Wanahabari hao walipotembelea kijiji cha Mwamgongo kilichopo jirani na hifadhi hiyo ya Taifa ya Gombe walipata kujionea na kushiriki katika ngoma za asili ambazo pia ni sehemu ya utalii wa kiutamaduni.
Mwanahabari maarufu nchini Israel, Dana Spector, wa Jarida la Yediot Acharonot akijaribu kuwasiliana na wanakikundi cha ngoma za asili wa kijiji cha Mwamgongo kinachopakana na hifadhi ya Taifa ya Gombe na kushudia kazi zao za mikono na ngoma ambazo ni sehemu ya utalii wa kiutamaduni.
Mwandishi wa habari wa mitandao ya kijamii nchini Israel, Walfson Noa akifurahia michezo na jamii ya watoto wa kijiji cha Mwamgongo wakati wa ziara hiyo.
Watalii wa ndani nao pia walikuwemo kufurahia vivutio vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo na kutoa wito kwa watanzania wengi zaidi kuvitembelea. Meneja wa Shirika la Hifadhi za Taifa, Paschal Shelutete (wa pili kushoto waliosimama) akiongoza mahojiano na watalii hao wa ndani.
Picha ya pamoja ya wanahabari wa Israel, wahifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Gombe na waongoza msafara huo ambao ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA, Paschal Shelutete (wa pili kulia), Meneja Mahusiano wa TTB, Geofrey Tengeneza (katikati waliosimama), Meneja Mawasiliano TFS, Glory Mziray (wa tatu kulia) na Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Hamza Temba (wa nne kulia).
Baada ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Gombe msafara wa wanahabari hao ulipanda boti kwa ajili ya safari ya kurudi Kigoma Mjini.
Monday, May 1, 2017
WAZIRI MAGHEMBE AZIPA HADHI YA NYOTA HOTELI ZA DAR ES SALAAM
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti vya kutambua hadhi za Hotel zilizopo jijini Dar es Salaam na kwa kuzipa madaraja mpaka nyota tano katika soko la utali hapa nchin, katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Serena Hoteli, Seraphin Lusala baada ya Hoteli hiyo kutambuliwa kuwa na hadhi ya Nyota tano katika mkoa wa Dar es Salaam, katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Majaji ambao waliokuwa wakitoa maksi ya hadhi za hoteli hapa nchini wakisimama kujitambulisha kwa wageni waliofika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali Gaudence Milanzi akizungumza na Wamiliki wa Mhoteli jijini Dar es Salaam leo kabla ya kukabidhi vyeti vya madaraja ya hotel zao.
Afisa utalii kutoka bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Irene Mville akitoa maelekezo kwa wadau wa mahoteli ambao walifika katika hafla ya ugawaji wa madarajana viwango katika Hoteli zilizopo jijini Dar es Salaam .
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa Hotel jijini Dar es Salaam.
.........................................
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema soko la utalii nchini linakua kwa haraka zaidi, ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki kutokana na vivutio na huduma.
Profesa Maghembe alisema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo za nyota katika hoteli zinazotoa huduma katika Mkoa wa Dar es Salaam. “Tanzania imekuwa na soko kubwa la utalii katika jumuiya ya Afrika Mashariki…Kwa maana ya kukua kwa utalii katika soko, sisi tuna nafasi kubwa sana na kwa mwaka jana tulipata watalii milioni 1,218,000 na Wakenya walipata 1.3 na nchi zingine zilipata wachache,” alisema Profesa Maghembe.
Alisema “pamoja na kwamba wakenya walipata wengi juu yetu lakini sisi tunakua kwa utalii kwa haraka zaidi ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki na hata yule aliyeko mbele yetu yeye anashuka, alikuwa milioni mbili na nsasa ameshuka hivyo sisi tunakua zaidi.” Akizungumzia kuhusu tuzo hizo, alisema zimetolewa kwa hoteli zenye ubora wa huduma na zimepewa nyota kulingana na madaraja yao kuanzia nyota moja hadi tano.
“Nyota hizi zimetolewa kwa hoteli ambazo zimekuwa katika Jiji la Dar es Salaam baada ya mwaka 2009, zipo ambazo zilikuwa zimepewa nyota kuanzia 2009 kurudi nyuma… Biashara ya hoteli ni sehemu ya biashara nzima ya utalii ambayo inachangia fedha za kigeni na pato la Taifa,” alifafanua.
Aliongeza kuwa huduma bora ndizo zinawafanya wataalii kuwa mabalozi wazuri, wanaporudi kwao na kueleza wamekutana na huduma nzuri na malazi mazuri hivyo kuwavutia wenzao. Katika tuzo hizo, Hoteli ya Serena imepewa hadhi ya kuwa na nyota tano, huku hoteli za Double Tree na Ramada Resort zikipewa hadhi ya nyota nne ambapo pia hoteli nyingine 13 zilipewa hadhi ya nyota tatu, hoteli 31 zilipewa hadhi ya nyota mbili na hoteli sita zilipewa hadhi ya nyota moja.
Alisema baada ya kukamilisha tathmini hiyo Dar es Salaam, watakwenda mikoa ya Arusha, Manyara, Mwanza, Kilimanjaro na Mara. Baada ya kumaliza mikoa yote, wataangalia upya hoteli zote zilizopewa nyota na zile za 2009. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Utalii (TCT), Abdulkadir Mohamed alisema wamefanya tathmini hiyo ili kuhakikisha kila mtu anapata huduma kulingana na uwezo wake sambamba na kuwapatia watalii huduma bora.
Friday, April 28, 2017
Saturday, April 22, 2017
VOTE for Mt Kilimanjaro #Tanzania as Africa's Leading Tourist Attraction in World Travel Awards 2017.
DID YOU KNOW? Mount Kilimanjaro is the 2016 Africa's Leading Tourist Attraction.
HOW TO VOTE? Click link below, register&vote
Pigia kura Mt Kilimanjaro katika Tuzo za World Travel Awards 2017 kama Kivutio Bora Afrika.
JE WAJUA? Mlima Kilimanjaro ndio kivutio bora Afrika mwaka 2016.
Jinsi ya kupiga kura: bonyeza link hapa chini, jisajili (register), nenda kwenye majina (Africa nominees) kisha piga kura kwa kubonyeza kiduara pembeni mwa jina.
LINK
LINK
Sunday, April 16, 2017
360 YA CLOUDS TV KWENDA MUBASHARA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI KESHO
Thursday, April 13, 2017
KIPINDI CHA 360 KURUSHWA MUBASHARA KUTOKA KATIKA HIFADHI ZA SERENGETI NA NGORONGORO
Watangazaji wa kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds Tv wamewasili mkoani Arusha jana kwa ajili ya ziara katika hifadhi za taifa za Serengeti na Ngorongoro kwa lengo la kutangaza utalii wa ndani.
Kipindi hicho kinachoendelea kujizolea umaarufu cha 360 kinataraji kurushwa moja kwa moja kutoka katika hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na Serengeti kikiongozwa na watangazaji wake Baby Kabaye, Sam Sasali, Hassan Ngoma na James Tupa tupa.
Leo Ijumaa na Jumamosi kitarushwa LIVE kutokea hifadhi ya Ngorongoro na Jumatatu kutokea hifadhi ya Serengeti.
Subscribe to:
Posts (Atom)







