slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Monday, May 1, 2017

WAZIRI MAGHEMBE AZIPA HADHI YA NYOTA HOTELI ZA DAR ES SALAAM


 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti vya kutambua hadhi za Hotel zilizopo jijini Dar es Salaam na kwa kuzipa madaraja mpaka nyota tano  katika soko la utali hapa nchin, katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe  akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi wa  Masoko na Mauzo wa Serena Hoteli, Seraphin Lusala baada ya Hoteli hiyo kutambuliwa kuwa na hadhi ya Nyota tano katika mkoa wa Dar es Salaam, katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

 Majaji ambao waliokuwa wakitoa maksi ya hadhi za hoteli hapa nchini wakisimama kujitambulisha kwa wageni waliofika.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali Gaudence Milanzi akizungumza na Wamiliki wa Mhoteli jijini Dar es Salaam leo kabla ya kukabidhi vyeti vya madaraja ya hotel zao.

Afisa utalii kutoka bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Irene Mville akitoa maelekezo kwa wadau wa mahoteli ambao walifika katika hafla ya ugawaji wa madarajana viwango katika Hoteli zilizopo jijini Dar es Salaam . 

  Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa Hotel jijini Dar es Salaam.

.........................................

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema soko la utalii nchini linakua kwa haraka zaidi, ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki kutokana na vivutio na huduma.
Profesa Maghembe alisema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo za nyota katika hoteli zinazotoa huduma katika Mkoa wa Dar es Salaam. “Tanzania imekuwa na soko kubwa la utalii katika jumuiya ya Afrika Mashariki…Kwa maana ya kukua kwa utalii katika soko, sisi tuna nafasi kubwa sana na kwa mwaka jana tulipata watalii milioni 1,218,000 na Wakenya walipata 1.3 na nchi zingine zilipata wachache,” alisema Profesa Maghembe.
Alisema “pamoja na kwamba wakenya walipata wengi juu yetu lakini sisi tunakua kwa utalii kwa haraka zaidi ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki na hata yule aliyeko mbele yetu yeye anashuka, alikuwa milioni mbili na nsasa ameshuka hivyo sisi tunakua zaidi.” Akizungumzia kuhusu tuzo hizo, alisema zimetolewa kwa hoteli zenye ubora wa huduma na zimepewa nyota kulingana na madaraja yao kuanzia nyota moja hadi tano.
“Nyota hizi zimetolewa kwa hoteli ambazo zimekuwa katika Jiji la Dar es Salaam baada ya mwaka 2009, zipo ambazo zilikuwa zimepewa nyota kuanzia 2009 kurudi nyuma… Biashara ya hoteli ni sehemu ya biashara nzima ya utalii ambayo inachangia fedha za kigeni na pato la Taifa,” alifafanua.
Aliongeza kuwa huduma bora ndizo zinawafanya wataalii kuwa mabalozi wazuri, wanaporudi kwao na kueleza wamekutana na huduma nzuri na malazi mazuri hivyo kuwavutia wenzao. Katika tuzo hizo, Hoteli ya Serena imepewa hadhi ya kuwa na nyota tano, huku hoteli za Double Tree na Ramada Resort zikipewa hadhi ya nyota nne ambapo pia hoteli nyingine 13 zilipewa hadhi ya nyota tatu, hoteli 31 zilipewa hadhi ya nyota mbili na hoteli sita zilipewa hadhi ya nyota moja.

Alisema baada ya kukamilisha tathmini hiyo Dar es Salaam, watakwenda mikoa ya Arusha, Manyara, Mwanza, Kilimanjaro na Mara. Baada ya kumaliza mikoa yote, wataangalia upya hoteli zote zilizopewa nyota na zile za 2009. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Utalii (TCT), Abdulkadir Mohamed alisema wamefanya tathmini hiyo ili kuhakikisha kila mtu anapata huduma kulingana na uwezo wake sambamba na kuwapatia watalii huduma bora.

No comments:

Post a Comment