slider gif
kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ
Saturday, November 18, 2017
Tuesday, November 14, 2017
TUTAWEKA MIKAKATI MIPYA WA KUNADI VIVUTIO VYA UTALII NCHINI CHINA - DK. KIGWANGALLA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke ofisini kwake mjini Dodoma jana Novemba, 14 ambapo walijadili mikakati ya kuongeza idadi watalii na wawekezaji katika sekta hiyo kutoka nchini China.
Na Hamza Temba - WMU
................................................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali kupitia Wizara yake inakusudia kuandaa mkakati maalum wa kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini China ili kuongeza idadi ya watalii na mapato ya Serikali.
Dk. Kigwangalla amesema hayo jana ofisini kwake mjini Dodoma akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke ambaye alimtembelea kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya Uhifadhi na Utalii.
“Moja ya mkakati wangu kama Waziri mpya wa Wizara hii kukuza utalii ni kuweka mkakati wa kuleta watalii wengi kutoka China, China ni Taifa Kubwa lenye watu wengi, tunalenga zaidi kuwafikia watu wanaoishi maisha ya kati ambao ndio wanaopenda kutumia fedha zao kufurahia maisha” alisema Dk. Kigwangalla.
Katika mazungumzo hayo alimuomba Balozi huyo kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa njia ya ushauri wa kitaalamu au wa kifedha kwa ajili ya kuandaa mkakati mahususi wa kulifikia soko la utalii la China kwa kuainisha vivutio na aina ya huduma ikiwemo hoteli ambazo zitakuwa kivutio kwa watalii kutoka China kuweza kutembelea Tanzania.
Miongoni mwa mikakati waliojadiliana ni uwezekano wa kutumia fursa ya uwepo wa wawakilishi wa Televisheni ya CCTV ya China nchini Tanzania ambao wanaweza kutumika kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini ikiwemo kuambatana na Waziri Kigwangalla kwenye ziara zake za kikazi kwenye maeneo ya vivutio na baadaye kuvitangaza nchini China na Duniani kote.
Walijadili pia uwezekano wa kuanzisha safari za moja kwa moja za ndege baina ya nchi hizo mbili kwa lengo la kurahisisha Safari za Utalii pamoja na kuanzisha mtandao wa pamoja wa watoa huduma za utalii wa mataifa hayo mawili.
Aidha, Dk. Kigwangalla alimuomba balozi huyo kuleta wawekezaji katika sekta ya Hoteli za kitalii na kuahidi kuwapa maeneo ya kujenga hoteli hizo ili kukuza huduma na soko la utalii nchini kwa kurahisisha upatikanaji wa watalii wa China kutembelea Tanzania.
Kwa upande wake Balozi Wang Ke alimueleza Waziri Kigwangalla kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali ambapo mwezi Februari mwakani (2018) itaandaa Maonyesho ya Kimataifa ya Kuuza Nje na Kuingiza Bidhaa na Huduma (International Export and Import Fair) ambapo watu mashuhuri kutoka China watashiriki akiwemo mcheza Filamu mashuhuri kwenye filamu ya kichina kwa Lugha ya Kiswahili maarufu kama Maododo.
Alisema kupitia Maonyesho hayo Tanzania itaweza kujenga mtandao wa utalii na China kwa kunadi vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini kwa watu maarufu watakaoshiriki maonyesho hayo wakiwemo wafanyabiashara na watoa huduma za utalii na ukarimu.
Monday, November 13, 2017
DK. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WAWILI (UJERUMANI NA CHINA) OFISINI KWAKE MJINI DODOMA LEO KUHUSU MAENDELEO YA UHIFADHI NA UTALII NCHINI
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla (kulia) akisalimiana na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Wächter ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo
wamejadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na
Ujerumani katika kuendeleza Uhifadhi na Utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla (kulia) akizungumza na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef
Wächter (kushoto) ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamejadili mambo
mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani katika
kuendeleza Uhifadhi na Utalii nchini.
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) na Balozi wa Ujerumani nchini,
Dk. Detlef Wächter (katikati) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yaliyofanyika
ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuimarisha
ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani katika kuendeleza Uhifadhi na Utalii
nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akizungumza na Balozi wa China nchini, Bi. Wang Ke ofisini kwake
mjini Dodoma leo ambapo amemuomba kushirikiana na Wizara yake kuweka mkakati wa
pamoja wa kuongeza idadi watalii na wawekezaji katika sekta hiyo kutoka nchini China.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla (kulia) akipokea zawadi ya taswira la Ua la Taifa la China kutoka kwa
Balozi wa nchi hiyo nchini, Bi. Wang Ke ofisini kwake mjini Dodoma leo. Amemuomba
balozi huyo kushirikiana na Wizara yake kuweka mkakati wa pamoja wa kuongeza
idadi watalii na wawekezaji katika sekta hiyo kutoka nchini China.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akimsikiliza Balozi wa China nchini, Bi. Wang Ke alipotembelewa na
balozi huyo ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo amemuomba kushirikiana na
Wizara yake kuweka mkakati wa pamoja wa kuongeza idadi watalii na wawekezaji katika
sekta hiyo kutoka nchini China. (Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii).
Thursday, November 9, 2017
BENKI YA DUNIA YAIPATIA TANZANIA MKOPO NAFUU WA BILIONI 340 KUENDELEZA UTALII UKANDA WA KUSINI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kulia), akitoa neno la shukurani wakati wa kusainiwa kwa Mkataba wa Mkopo Nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbiji Bi. Bella Bird.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa-TANAPA, Bw. Allan Kijazi na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Makubaliano ya utekelezaji wa Mkataba wa Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania utakao gharimu Shilingi bilioni 340 zilizotolewa kama mkopo wenye masharti nafuu na Benki hiyo kwa Tanzania, Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, (wa pili kulia waliosimama akifuatiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Jijini Dar es Salaam................................................................................
BENKI ya Dunia imeipatia Tanzania Mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 150, sawa na takriban Shilingi bilioni 340 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa kufungua fursa za utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania.
Mkataba wa mkopo huo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi, Bi. Bella Bird.
Bw. James alisema kuwa mkopo huo umelenga kuimarisha miundombinu ya utalii katika ukanda huo wa kusini ikiwemo ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, madaraja pamoja na kuibua fursa nyingi za utalii ili kuvutia watalii wengi zaidi.
Alisema pia kwamba mradi huo umelenga kuwajengea uwezo wananchi wanaozunguka maeneo ya utalii kwa kuanzisha miradi itakayo chochea maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi pamoja na kuendeleza uhifadhi katika maeneo yao.
Aidha, mkopo huo utatumika katika kampeni ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko katika ukanda huo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania ili kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea maeneo hayo badala ya hali ilivyo sasa ambapo watalii wengi wanatembelea vivutio vilivyoko ukanda wa Kaskazini.
Monday, November 6, 2017
"SIWEZI KUJARIBIWA NA SIWEZI KUCHEZEWA, SIKO HAPA KWA BAHATI MBAYA". DK. KIGWANGALLA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akikagua maeneo ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo
lenye mgogoro la Pori Tengefu Loliondo jana mkoani Arusha jana.
Dk. Kigwangalla (kulia) akimuhoji mmoja ya wananchi jamii ya wafugaji alipotembelea Pori Tengefu Loliondo jana.
Waziri Kigwangalla (kushoto) akioneshwa mpaka wa Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Pori Tegefu Loliondo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Hamdun Mansuri wakati wa ziara yake ya kukagua iwapo mifugo inaingizwa katika hifadhi ya Serengeti kama ilivyoripotiwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari.
Saturday, November 4, 2017
DK. KIGWANGALLA ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA ZIWA MANYARA NA KUKAGUA SHUGHULI MBALIMBALI ZA UHIFADHI NA UTALII
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
(kushoto) akisalimiana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Manyara, Noelia
Myonga alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua
shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi
endelevu na utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
(kushoto) akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara,
Noelia Myonga (wa pili kushoto) kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za
uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
(kushoto) akizungumza na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Noelia
Myonga alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua
shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi
endelevu na utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Noelia Myonga alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
(kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya
Ziwa Manyara, Noelia Myonga kuhusu hifadhi hiyo alipoitembelea jana mkoani
Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa
lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
akigusa maji ya moto ya asili ambayo ni kivutio cha kipekee cha utalii
kilichopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo
jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na
utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. Maji hayo
yanakadiriwa kuwa na nyuzi joto 80 ambapo imeelezwa kuwa baadhi ya watalii
huweza kuchemsha mayai katika maji hayo. Nyuma yake anayeshuhudia ni Mhifadhi
Mkuu wa hifadhi hiyo, Noelia Myonga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
(kushoto) akionyeshwa maeneo ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara na Mhifadhi
Mkuu wa hifadhi hiyo, Noelia Myonga alipoitembelea hifadhi hiyo jana mkoani
Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa
lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
(wa pili kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa ‘Lodge’ ya AndBeyond
Lake Manyara Tree, Mei Saimon (kulia) kuhusu ‘lodge’ hiyo ambayo ipo ndani ya
Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha
kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo
la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
(wa pili kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa ‘Lodge’ ya AndBeyond
Lake Manyara Tree, Mei Saimon (kulia) kuhusu mazingira ya nje ya ‘lodge’ hiyo
ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo
jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na
utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini.
Waziri, Dk. Kigwangalla akikagua miundombinu ya lodge hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
(wa pili kulia) akikagua mazingira ya Lodge’ ya AndBeyond Lake Manyara Tree
ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo
jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na
utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. Kulia kwake ni
Meneja wa hoteli hiyo, Mei Saimon.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
akikagua baadhi ya miundombinu ya kupumzikia wageni katika Lodge’ ya AndBeyond
Lake Manyara Tree ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli
mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. Kulia kwake ni Meneja wa hoteli hiyo, Mei Saimon.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya miundombinu ya kupumzikia wageni katika Lodge’ hiyo ya AndBeyond Lake Manyara Tree ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara. Kulia ni Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Noelia Myonga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
(wa tatu kulia waliosimama) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya
wafanyakazi wa Nyumba ya Kulala Wageni ya AndBeyond Lake Manyara Tree Lodge
ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara wakati alipotembelea
hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na
utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini.
Simba katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Baadhi ya miundombinu ya daraja katika hifadhi hiyo ambayo huwarahisishia watalii kuona wanyamapori mbalimbali.
Pundamilimilia
Ndege na nyati katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Ndege aina mbalimbali wanapatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Mtoto wa Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Baadhi ya Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)
Friday, November 3, 2017
DK. KIGWANGALLA AAGIZA RASIMU YA SERA MPYA YA TAIFA YA MISITU IKAMILIKE NDANI YA MWEZI HUU WA NOVEMBA KUWEZESHA UPATIKANAJI WA SHERIA NA KUNUNI MPYA ZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA SEKTA HIYO
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasili katika ukumbi wa Hoteli ya Morena mjini Dodoma jana kwa ajili ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera
mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha
sekta hiyo.
Na Hamza Temba - WMU
............................................................
“Natoa agizo mchakato
huu ukamilike ndani ya mwezi huu wa 11, tarehe moja mwezi wa 12 mlete rasimu
ambayo nyie wataalamu mmeridhika nayo, muiwasilishe kwangu mimi na Mhe. Naibu
Waziri, na siku hiyo mtakayoiwasilisha kwetu mniletee timu ya wataalamu watakaonishauri
kwenye maeneo mbalimbali.
Na Hamza Temba - WMU
............................................................
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza kukamilishwa haraka kwa rasimu mpya ya
Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 2016 ili kuwezesha upatikanaji wa Sera, Sheria
na Kanuni mpya za usimamizi wa rasilimali za misitu nchini kwa ufanisi zaidi.
Ameagiza wataalamu wa
Wizara hiyo kukamilisha rasimu hiyo mwezi huu wa Novemba na iwasilishwe kwake mapema
mwezi ujao (Desemba) ili aweze kupata ushauri zaidi wa wataalamu wengine huru kabla ya kuwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri na baadaye kutungiwa Sheria na Kanuni za
utekelezaji.
Dk. Kigwangalla ametoa
agizo hilo jana mjini Dodoma wakati akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa
misitu iliyolenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki,
pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
“Pamoja na hao wataalamu
washauri nataka watu wengine huru wahusike kwenye kunishauri, ili nipate picha
ya watu wengine huru kabla hatujatengeneza andiko ambalo tutalipeleka kwenye kikao
cha baraza la Mawaziri, waje wanishauri maeneo yanayotaji maboresho, kuongeza ubunifufu
au kukazia zaidi”. Aliagiza Dk. Kigwangalla.
Alisema amelazimika
kuharakisha zoezi hilo ili Sera hiyo ikamilike haraka iweze kushughulikia changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo ongezeko la watu linalosababisha misitu
mingi kuteketezwa kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kupitia
shughuli za kilimo na uanzishwaji wa makazi mapya.
Alisema pamoja na
misitu kuonekana inachangia kidogo kwa asilimia 3.5 kwenye pato la taifa, bado mchango
wake ni mkubwa kuliko inavyochukuliwa hivi sasa. Alisema tafiti zilizofanywa
awali hazikuzingatia mambo muhimu ikiwemo mchango halisi wa misitu kwenye
upatikanaji wa maji ambayo huzalisha umeme, hunywesha mifugo na wanyamapori,
matumizi ya majumbani na kilimo cha umwagiliaji.
Alisema ili kupata
mchango halisi wa misitu kwenye uchumi mpana wa taifa letu, Wizara yake imeshaandaa
andiko maalum kwa ajili ya kuendesha utafiti mkubwa wa kubaini mchango huo na kazi
inayofanyika hivi sasa ni ya utafutaji wa fedha kutoka kwa wadau mbalimbali
kufanikisha utafiti huo.
Akizungumzia Uhifadhi Shirikishi
Jamii, Dk. Kigwangalla alisema kwa zaidi ya asilimia 32 ya maeneo yote nchini yamehifadhiwa
kisheria, hivyo njia rahisi ya kuyalinda ni kupitia ushirikishwaji wa wananchi.
“Bila kufanya hivyo hatuwezi kusema tuna askari wa kutosha kulinda misitu yote,
mbuga zote za wanyama au mapori yote tengefu nchini.
“Lakini nje ya maeneo hayo
kuna maeneo ya vijiji ambayo pia yamehifadhiwa, yote haya huwezi kusema
utayalinda kirahisi sana bila ushiriki wa wananchi, kuwaleta wananchi kwenye
uelewa wa pamoja, kwamba tunahifadhi kwa faida yao.
“Tuwaelimishe, kwa mfano
usipohifadhi misitu kiwango cha mvua kitashuka, usalama wa chakula utaathirika,
upatikanaji wa maji safi na salama utaathirika, upatikanaji wa umeme nao pia utaathirika,
hivyo tunahifadhi kwa faida ya jamii kwa ujumla”. alisema Dk. Kigwangalla.
Awali akiwasilisha mada
kuhusu hali ya sekta ya misitu nchini, Prof. Romanus Ishengoma wa Chuo Kikuu cha
Sokoine - SUA alisema changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo ni ukataji
holela wa miti ambapo takwimu za NAFORMA zinaonyesha kuwa Tanzania inapoteza
hekta 372,000 za misitu kwa mwaka.
Alisema changamoto
nyingine ni uchomaji moto misitu, uvunaji wa mkaa, uingizaji mifugo kwenye
maeneo ya hifadhi, kukosekana kwa mpango bora wa matumizi ya ardhi, utegemezi
uliokithiri kwenye mazao ya misitu, uanzishwaji wa makazi mapya na utegemezi wa
nishati ya kuni. Alisema changamoto hizo zinahitaji Sera madhubuti za kukabiliana
nazo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa alisema, Rasimu hiyo ya Sera mpya ya Misitu itakamilika kwa wakati kama alivyoelekeza Waziri Kigwangalla na kwamba maoni yote ya wadau yatazingatiwa katika Rasimu hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa alisema, Rasimu hiyo ya Sera mpya ya Misitu itakamilika kwa wakati kama alivyoelekeza Waziri Kigwangalla na kwamba maoni yote ya wadau yatazingatiwa katika Rasimu hiyo.
Warsha hiyo ya siku moja
iliyofanyika mjini Dodoma iliandaliwa kwa ushirikiano wa Mtandao wa Jamii wa
Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Shirika la Uendelezaji wa Nishati
Endelevu za Kisasa Tanzania (TATEDO), Kundi la Uhifadhi wa Misitu Tanzania (TFCG),
Wizara ya Maliasili na Utalii na Ubalozi wa Switzerland nchini.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia)
akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha
ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga
kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto
na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto)
akiteta jambo na Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli muda mfupi
baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini
Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya
Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta
hiyo.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki warsha hiyo wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa
pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal
Briquettes ltd, Abdala Seushi kuhusu nishati mbadala ya mkaa mkombozi wa afya
na mazingira muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu
iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu
ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya
kuboresha sekta hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia)
akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal Briquettes ltd,
Abdala Seushi kuhusu majiko banifu ya mkaa muda mfupi baada ya kufungua warsha
ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga
kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto
na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara
hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza katika warsha hiyo.
Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli akizungumza katika warsha hiyo.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa
pili kushoto) akipokea zawadi ya nishati mbadala ya mkaa mkombozi wa afya na mazingira
kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Charcoal Briquettes ltd, Abdala Seushi (wa
tatu kushoto) muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu
iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu
ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya
kuboresha sekta hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa
Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa.
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia)
akizungumza na Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli muda mfupi
baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau sekta misitu iliyofanyika mjini
Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho ya Rasimu ya Sera mpya ya
Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta
hiyo.
Prof. Romanus Ishengoma wa Chuo Kikuu cha Sokoine - SUA akiwasilisha mada kuhusu hali ya sekta ya misitu nchini katika warsha hiyo.
Picha ya pamoja.
Meza kuu, Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Uhifadhi wa Misitu Tanzania, Charles Meshak (wa pili kushoto), Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Matli (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Doto Biteko (kulia).
Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza
na waandhishi wa habari muda mfupi baada ya ufunguzi wa warsha ya siku moja ya wadau
sekta misitu iliyofanyika mjini Dodoma jana. Warsha hiyo ililenga kujadili maboresho
ya Rasimu ya Sera mpya ya Misitu na Nyuki, pamoja na changamoto na mikakati
mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)


