Serikali
imesema kuwa itaendelea kuweka mazingira rafiki, kuwahamasisha na kuwavutia
Wawekezaji watakaosaidia kuwapeleka watalii katika maeneo ya Kanda ya Ziwa ili
kukuza Sekta ya Utalii Katika maeneo hayo.
Hatua hiyo
inakuja baada ya kuyapandisha hadhi Mapori ya Akiba ya ya
Burigi, Biharamulo, Kimisi,Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi ya Taifa.
Akizungumza
kwenye mkutano uliohusisha Wizara
Maliasili na Utalii na Wawekezaji kutoka
maeneo mbalimbali nchini, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine
Kanyasu amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Sekta binafsi kwa kuwa
sekta hiyo ni injini ya Utalii nchini.
Amesema kuwa
mkutano huo una umuhimu mkubwa Katika maendeleo ya sekta hiyo kwa kuwa
Serikali inapata nafasi ya kuwaelezea Wawekezaji fursa
mbalimbali zinazopatika katika Ukanda
huo pamoja na kusikia changamoto zao.
Amesema
kufuatia kufanyika kwa mkutano huo Sekta Binafsi itakuwa na kila sababu ya
kuwekeza katika Ukanda huo baada ya Serikali kuendelea kuweka mazingira rafiki
kwa Uwekezaji
Amesema
Serikali imeendelea kuweka Miundombinu wezeshi ambayo imekuwa chachu ya
kurahisisha watalii na wageni mbalimbali kutembelea maeneo ya hifadhi.
Mhe.Kanyasu
ameyataja maeneo yaliyoboreshwa
kuwa ni Barabara,
Uwanja wa ndege wa Mwanza pamoja na
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Chato ambao umefunguliwa.
Hata hivyo,
Mhe.Kanyasu amesema kuwa licha ya kuwa
Tanzania imekuwa ikifanya vizuri kwenye shughuli za Uhifadhi, lakini katika
Uendelezaji Utalii bado jitihada za makusudi zinahitajika.
"Tuna
vivutio vingi vya utalii lakini idadi ya watalii wanaotembelea vivutio hivyo
hairidhishi, tunahitaji kuongeza juhudi katika kuwahamasisha watalii wa ndani
na nje ya nchi kutembelea maeneo hayo" Amesisitiza
Kwa upande
wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye alikua mwenyeji wa mkutano huo,
Prof.Adolf Mkenda amesema kupitia mkutano huo kutasaidia kuchagiza idadi ya
watalii kuongezeka kwa kutembelea vivutio vya utalii vinavyopatikana katika
ukanda huo.
Amesema
kufanyika kwa mkutano huo ni muendelezo wa kutawanya fursa za uwekezaji wa
sekta ya utalii nchi nzima.
Akichangia
hoja kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Watalii (
TATO)Wilbard Chamburo ameiomba Serikali iangalie uwezekano wa kutobadili mara kwa mara sera na mipango ya kukuza
masuala ya Utalii kwa kuwa kuwa hali hiyo inayochangia kuwakatisha tamaa
Wawekezaji.
Amesema
Wawekezaji wanataka kuwekeza mahali ambako wana uhakika wa kupata faida itayowasaidia kujiendesha kibiashara
pamoja na kulipa kodi stahiki za serikali.
Katika
mkutano huo, Wakuu wa mikoa yote ya Kanda ya Ziwa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza,Mhe.John Mongela walikua miongoni mwa Washiriki.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa siku moja
uliofanyika jana jijini Mwanza baina ya
Wizara ya Maliasili na Utalii na
Wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuhamasisha Utalii
Ukanda wa Ziwa
Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (wa kwanza kushoto) akiteta jambo na
Mkurugenzi Mkuu wa Hifdadhi za Taifa.Alllan Kijazi (kulia) kabla ya Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine
(wa pili kushoto) Kanyasu
kufungua mkutano baina ya Wizara hiyo na Wawekezaji uliofanyika jijini Mwanza.
Baadhi ya
washiriki wa mkutano baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii hiyo na Wawekezaji uliofanyika jijini Mwanza'
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza kwenye
mkutano wa siku moja uliofanyika jana jijini Mwanza baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali nchini
ka lengo la kuhamasisha Utalii Ukanda wa Ziwa
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (mbele) akiwa
ameongozana na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu
(wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John
Mongela(katikati)
No comments:
Post a Comment