Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesema Wizara ya Maliasili na
Utalii inatarajia kuja na mkakati maalum
wa kutangaza utalii ndani na nje ya nchi kwa kunadi maeneo ya vivutio vya utalii badala ya
kuinadi nchi kwa ujumla na vivutio vyake
Pia,Amesema maeneo hayo yatakuwa yakinadiwa kwa mfumo wa vifurushi (Packages) hali
itakayopelekea mtalii akija nchini ataweza kutembelea maeneo ya Hifadhi,
Misitu ya Mazingira asilia pamoja na
maeneo ya utalii wa kiutamaduni.
Amesema
lengo la kuja na mkakati huo ni kusaidia maeneo hayo kuweza kujulikana pamoja
na kumuwezesha mtalii kuweza kuvifahamu vivutio vinavyopatikana katika eneo
hilo kwa undani badala ya kuitangaza nchi kwa kujumuisha vivutio vya utalii
vilivyopo kwa ujumla wake.
Amesema
mkakati huo utasaidia kuongeza idadi ya
watalii katika maeneo yenye vivutio ya utalii lakini kwa sasa yamekuwa yakipata
idadi ndodgo ya watalii kwa vile yamekuwa hayafahamiki ipasavyo.
Amesema
mkakati huo utalenga zaidi katika maeneo yenye utalii wa kiutamaduni pamoja na
maeneo ya Misitu asilia, Ni utalii mpya ambao kwa Tanzania haufahamiki sana
unaojikita kuangaliia viumbe ambao wapo hatarini kutoweka.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri huyo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea
Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi pamoja na Msitu Asilia wa Chome katika wilaya ya
Same mkoani Kilimanjaro.
Ameeleza
kuwa aina hiyo ya kutangza vivutio vya utalii katika eneo fulani badala ya nchi
italeta manufaa makubwa kwa Hifadhi na maeneo yale ambayo kwa sasa yamekuwa
yakipokea idadi ndogo ya watalii hasa katika ukanda wa Kusini na Magharibi.
Amesema
ukizungumzia utalii kwa sasa unalenga mikoa ya Kaskazini ambako zaidi ya
asilimia 80 unafanyika ukanda huko huku kanda nyingine kama vile kanda ya ziwa,
Magharibi pamoja na Kusini zikiwa bado idadi ya watalii wanaotembelea ni ndogo
ukilinganisha na uwingi wa vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo hayo.
Kwa upande
wake Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Shabani Shekilindi amesema Tanzania
imejaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii lakini mapato yatokanayo na utalii
hayaakisi ualisia wa vivutio vilivyopo nchini hivyo mikakati mipya ya kutangaza
vivutio inahitajika.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akipigiwa saluti na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi wakati alipokuwa ameongozana na Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea eneo hilo kwa ajili yamradi wa kuzalisha faru weusi na mbwa mwitu
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii kutembelea eneo la maradi wa kuzalisha faru weusi na mwitu katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi mkoani Kilimanjaro. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki.
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania iliyopo katika wilaya ya Same
No comments:
Post a Comment