JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUWASILISHA MAOMBI YA LESENI
YA BIASHARA YA NYARA (TROPHY DEALER’S LICENCE - TDL) KWA MWAKA 2017
Wizara ya Maliasili na Utalii inawajulisha wananchi
wanaotaka kufanya Biashara ya Nyara kuwasilisha maombi yao kwa Mkurugenzi kwa
kujaza Fomu za Maombi ya Leseni zinazopatikana na kupitishwa na Maafisa
Wanyamapori wa Wilaya husika. Fomu hizo
pia zinapatikana kwenye Ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori zilizopo
Morogoro (Jengo la TAFORI), Dar Es Salaam, na Arusha.
Hakuna Leseni za Daraja lolote au Mnyama yeyote,
kwa Mwaka 2017 zitakazotolewa kwa madhumuni ya ukamataji na usafirishaji wa
Wanyamapori hai nje ya nchi. Aidha,
Tangazo hili linafuta Tangazo lililotolewa tarehe 06/12/2016 katika vyombo
mbalimbali vya habari.
Fomu za mwombaji zinatakiwa kujazwa na kuwasilishwa
kwa Maafisa Wanyamapori wa Wilaya ndani ya siku 45 tangu tarehe ya Tangazo
hili.
Meombi ya Leseni kwa Mwaka 2017 ni kwa Daraja
zifuatazo:-
DARAJA
|
MAELEZO
|
1.
|
Biashara ya Meno ya Kiboko
au Ngiri ambayo hayajatengenezwa, nzima au kipande
|
2.
|
Biashara ya ngozi za
wanyamapori isipokuwa ngozi za Pimbi na Mbega
|
3.
|
Biashara ya ngozi ya Pimbi
|
5.
|
Biashara ya kukata na
kutengeneza ngozi za Chui, Simba, Mondo au ngozi nyingine za wanyamapori
jamii ya Paka.
|
6.
|
Biashara ya kukata na
kutengeneza ngozi za wanyamapori isipokuwa za Pimbi na Mbega pamoja na
kutengeneza vitu kutokana na nyara hizo.
|
7.
|
Biashara ya nyara
zilizotengenezwa
|
8.
|
Biashara ya kuhifadhi
nyara mbalimbali ili zisiharibike mapema
|
10.
|
Biashara ya mikia ya
wanyamapori isipokuwa ya Tembo, Faru, na Mbega na vitu vinavyotokana na nyara
hizo.
|
11.
|
Wakala wa kusafirisha
nyara kwa ujumla isipokuwa Wanyama hai.
|
17.
|
Bustani ya Wanyamapori
|
18.
|
Mashamba ya kufuga
wanayamapori (isipokuwa kwa nia ya kusafirisha Wanyamapori hai nje ya nchi).
|
19.
|
Vituo vya Karantini
(isipokuwa kwa nia ya kusafirisha wanyama hai nje ya nchi).
|
20.
|
Ranchi za wanyamapori
(isipokuwa kwa ajili ya kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi)
|
21.
|
Aina yoyote ya biashara ya
nyara ambayo haikutajwa kwenye daraja la 1-20 isipokuwa kusafirisha wadudu na
viumbe wengine hai nje ya nchi.
|
Mwombaji
anatakiwa kuwasilisha fomu ya maombi ya leseni pamoja na uthibitisho wa
yafuatayo:-
1.
Endapo mwombaji ni mtu binafsi anatakiwa awasilishe
hati ya usajili wa jina la biashara
(Certificate of Registration of Business name) au iwapo mwombaji ni Kampuni
awasilishe Katiba ya Kampuni (Memorandum and Articles of Association) na Hati
ya utambulisho wa mlipa kodi (Tax payer Identification Number).
2.
Uthibitisho wa kuwa na Wakamataji wenye elimu ya
Uhifadhi wa Wanyamapori kutoka kwenye Chuo kinachotambulika na Serikali.
3.
Uthibitisho kwamba biashara ina leseni kutoka
kwenye Mamlaka husika.
4.
Mpango wa biashara (business plan) unaoruhusu
biashara inayotarajiwa kufanywa na uthibitisho wa mtoaji.
5.
Uthibitisho wa malipo ya Ada ya maombi ya leseni ya
(TZS. 5,000/=) ambayo haitarudishwa (Non-Refundable). Fedha hizo zilipwe kupitia Benki ya NBC
Samora Avenue, Akaunti Na. 012103011903 ya “SELOUS GAME RESERVE au CRDB
Tanzania Wildlife Management Authority Akaunti Na. 0150319566100 TAWA”
6.
Mwombaji asiwe na rekodi ya kupatikana na hatia ya
kuvunja Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 na
7.
Kwa mwombaji wa shughuli za ufugaji wa Wanyamapori,
Ada ya Maombi ya Leseni ya Ufugaji itategemea aina ya ufugaji kama ifuatavyo:-
i)
Bustani ya Wanyamapori; Ada ya Maombi ni Dola za
Kimarekani 150 kwa mzawa, mzawa kwa kushirikiana na Mgeni Dola za Kimarekani
250.
ii)
Mashamba ya Ufugaji Wanyamapori; Ada ya Maombi ni
Dola za Kimarekani 200 kwa mzawa na kwa mzawa akishirikiana na mgani ni Dola za
Kimarekani 500.
iii)
Ranchi za Wanyamapori Ada ya Maombi ni Dola za
Kimarekani 500 kwa mzawa na kwa kushirikiana na mgeni ni Dola za Kimarekani
1000.
KATIBU MKUU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
23 JANUARI, 2017
No comments:
Post a Comment