slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Tuesday, October 17, 2017

TANZANIA NA OMAN ZAFANYA MAZUNGUMZO YA KUANZISHA SOKO LA PAMOJA LA KUKUZA SEKTA YA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt.Hamisi Kigwangalla amesema  Tanzania na Oman zimefanya mazungumzo ya pamoja ya namna ya kukuza sekta ya Utalii baina ya nchi hizo mbili ambapo zitashirikiana katika muingiliano wa Watalii watakaokuwa wakitokea moja kwa moja Oman na kuja Tanzania.

“Tumeweza kuzungumzia ushirikiano wa sekta ya Utalii. Hii ni pamoja na kuanzisha soko la pamoja  kati ya Oman na Tanzania. Watalii wanaokwenda Oman wanaotaka kuja nchi za Afrika basi waunganishwe moja kwa moja kutoka Oman na kuja Tanzania kwani wenzetu wana watalii wengi kuliko sisi. Hivyo ujio wao hapa nchini ni faida kubwa kabisa na tumejifunza mengi katika sekta hii.

"Pia tumeweza kujifunza namna wenzetu wanavyoitangaza nchi yao  na sisi tutatumia uzoefu huo kuboresha sekta hii ya Utalii kama dhamana tuliyopewa” alieleza Dk. Kigwangalla.

Awali Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ iliyofika mapema juzi Jijini Dar e Salaam ikiwa katika msafara wa kitaifa kati ya Serikali ya Oman na Tanzania.

Katika tukio hilo Mhe. Kigwangalla aliungana na msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan katika chakula cha mchana ndani ya Meli hiyo ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said  ijulinakanyo kama ‘Fulk Al Salamah’.

Meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman ipo nchini hadi Oktoba 21.2017 kwa ajili ya kusambaza ujumbe wa ‘Amani na Upendo’ duniani, ambapo  baadaye itaelekea Mombasa nchini Kenya kwa madhumuni hayo hayo.Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt.Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Bi.Maitha bint Saif Al Mahrouqi wakati alipotembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman Jijini Dar es Salaam jana.
Moja ya alama za kuvutia za Taifa la Oman katika meli hiyo.
Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Bi.Maitha bint Saif Al Mahrouqi (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Maliasili Dkt. Hamisi Kigwangalla alipotembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman Jijini Dar es Salaam jana.
Picha ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ambayo ipo ndani ya meli hiyo ya kifahari.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akizungumza baada ya hafla ya chakula cha mchana ndani ya meli ya Mfalme wa Oman, jana Jijini Dar e Salaam.
Waziri Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla ya chakula cha mchana ndani ya Meli ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ijulinakanyo kama ‘Fulk Al Salamah’ Jijini Dar es Salaam jana.
Waziri Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari katika ziara hiyo.
Meli ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ijulinakanyo kama ‘Fulk Al Salamah.

No comments:

Post a Comment