Serikali imeahidi kuendelea kutatua
changamoto mbalimbali zinazoukabili mchezo wa wavu ambao ni miongoni mwa michezo iliyosahaulika licha ya kuwa ni
mchezo wenye kuvutia watu wengi na unaweza kutumika kama sehemu ya watu
kujiajiri
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati alipokuwa akifungua
mashindano ya wavu ya Afrika Mashariki katika viwanja vya Milongo yajulikakanayo kwa jina la Jembe Mirjan East
Africa Volleyball Championship yanayofanyika jijini Mwanza.
Mashindano hayo yana shirikisha timu
sita na yatafanyika ndani ya muda nne
ambapo mashindano hayo yameanza kati ya timu ya MTC Nyegezi dhidi ya Polisi
Zanzibar ambapo mchezo umemalizika huku
Zanzibar Polisi wakiongoza kwa goli 39 kwa 30
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mashindano hayo, Mhe.Kanyasu amewataka wachezaji wawe wavumilivu kutokana na
changamoto wanazozipitia kwa vile mchezo wa wavu mbali na mchezo wa mpira wa
miguu ni mchezo ambao umekuwa ukikosa Wadhamini kwa sababu haujaweza kufahamika
kiasi cha kuwashawishi Wadhamini kuweza kuweka pesa zao.
Amewaeleza wachezaji hao kuwa lazima wakubali kuumia kwanza kwa hiki kipindi cha mwanzo ili
baadaye wadhamini waweze kujitokeza.
Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu
amewahakikishia waandalizi wa mchezo huo kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
itadhamini mchezo huo kama ilivyokuwa imeahidi mwanzo
Naye,
Meneja wa Jembe FM, Fredy Kikoti amesema mchezo huo umekuwa ukikabiliwa
na changamoto nyingi ikiwa pamoja na kukosekana kwa wadhamini hali iliyopelekea
baadhi ya timu kushindwa kushiriki katika mashindano hayo.
Amesema mashindano hayo tangu
yalipoanzishwa mwaka jana yamekuwa chanzo cha
kuibua vipaji kwa vijana wa Kanda ya ziwa pamoja na Tanzania kwa
Ujumla
Mashindano hayo ya Afrika Mashariki
yameanza Juni 12 mwaka huu yanatarajia kumalizika Juni 16 mwaka huu katika
viwanja vya Milongo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu akisalimiana na kocha wa timu ya Polisi ya Zanzibar,
Zuberi Ahmad mara baada ya kuzindua mashindano ya Kikapu ya Afrika Mashariki
yanayofanyika jijini Mwanza kabla ya mchuano kuanza kati ya timu hiyo ya Polisi
na MTC ya Mwanza
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu (wa pili kushoto)
akisitiza jambo wakati akiangalia mpira wa kikapu kati ya timu ya Polisi
Zanzibar na MTC ya Mwanza ambapo timu ya Polisi Zanzibar waliibuka washindi. Wa
kwanza kushoto ni Meneja Masoko wa Jembe Fm, Domina Erasto na kulia ni Meneja
wa Jembe FM , Fredy Kikoti.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa mpira wa
wavu ya MTC Mwanza kabla ya kufungua
mashindano ya wavu ya Afrika mashariki yanayofanyika jijini Mwanza
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa mpira wa
wavu ya Polisi Zanzibar kabla ya kufungua mashindano ya wavu ya Afrika
mashariki yanayofanyika jijini Mwanza
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia mtanange kati ya timu ya Polisi ya Zanzibar na MTC ya Mwanza mara
baada ya mashindano hayo ya wavu ya Afrika Mashariki kufunguliwa na Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu katika viwanha vya
Milongo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya MTC ya
Mwanza wakati wa kufungua Mashindano ya wavu ya Afrika Mashariki kabla ya mechi kuanza kati ya timu ya MTC ya
Mwanza na Polisi Zanzibar.
Baadhi ya wananchi na wapenzi wa mpira
wa wavu wakiwa wameshika bango wakiwa wanaelekea kwenye viwanja vya Milongo kwa
ajili ya ufunguzi wa Mashindano ya wavu ya Afrika Mashariki yanayofanyika
jijini Mwanza.