slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Tuesday, January 9, 2018

DK. KIGWANGALLA ATEUA KAMATI YA UCHUNGUZI WA CHANGAMOTO ZA BONDE LA MTO KILOMBERO


Na Mwandishi Maalum
...........................................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) ameteua Kamati maalum ya kuishauri Serikali hatua za kuchukua katika kutatua changamoto zinazolikabili bonde la mto Kilombero lililopo Mkoani Morogoro.

Waziri Kigwangalla amesema, Kamati hiyo aliyoiteua,  ndio itakayomshauri juu ya usimamizi wa bonde hilo ikiwemo hatua za kuchukua ili kulinda bonde hilo ambalo lina umuhimu mkubwa ikiwemo chanzo kikubwa  cha maji yanayotengeneza Stiegler’s Gorge ambako Serikali imeamua kuweka mikakati ya utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa megawatts 2100 huku pia bonde hilo likiwa na utajiri wa kuwepo na aina zaidi ya 400 ya ndege pamoja na mnyama aina ya Puku ama Sheshe ambaye hapatiani kwengineko duniani zaidi ya Tanzania pekee.

"Hii ndio Kamati yangu, itakayonishahuri juu ya bonde ili litasimamiwa vipi. Hii ndio Kamati ambayo itanishahuri mimi na kwamaana hiyo Serikali kwa ujumla wake juu ya namna bora ya uhifadhi hususani katika eneo lile la Pori tengefu.

Hapa kuna vitu viwili vya kuzingatia: Ardhi Oevu (Ramsar site) ambalo lina eneo lake huku pia eneo la pori tengefu nalo kichukua nafasi kubwa zaidi" Amesem Waziri Dk Kigwangalla wakati wa kuteua Kamati hiyo.

Kamati hiyo inaundwa na  wajumbe mbalimbali ambao wataongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Ndugu Andrew Napacho, Pia wajumbe ni  Brig. Gen. (Mst.) Edmund Mndolwa, Aliyekuwa Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Mstaafu, Suleiman Kova, Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha wafugaji Bwana  Semkae Kilonzo (Policy Forum).

Wengine ni  Dk. Simon Mduma, Prof. Jaffar Kideghesho, Ruzika Muheto, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, MKuu wa Wilaya ya Kilombero na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi.

Wengine ni Mwenyekiti Halmashauri Ulanga, M/Halmashauri Kilombero, M/Halmashauri Malinyi  na M/Halmashauri Ifakara.
Pia yupo  Mtendaji Mkuu wa KPL, Mtendaji MKuu wa Illovo, Mkuu Kikosi JKT Chita. Wengine ni  Dk. Aggrey Mlimuka, Mwakilishi kutoka mamlaka ya maji Bonde la Kilombero, Mwakilishi kutoka Wizara ya ardhi.

Wajumbe wengine ni Ndugu Innocent Kylogeris, Dk. James Wakibara, Mkurugenzi Mkuu TAWA ambaye atakuwa Katibu wa Kamati hiyo.

Hatua hiyo inafuatia Waziri Dk Kigwangalla kufanya ziara maalum kwenye bonde hilo la kilombero ambapo ameweza kushuhudia athari kubwa zaidi zilizofanywa na wavamizi wakiwemo wakulima na wafugaji ambao wameonekana kuvamia maeneo makubwa  ndani ya pori tengefu la bonde pamoja na Kwenye eneo ohevu ndani ya bonde hilo.

No comments:

Post a Comment