slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Wednesday, January 10, 2018

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla azindua Kamati ya Kitaifa ya Kuandaa Mwezi Maalum wa Maadhimisho ya Urithi wa Tanzania

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala akizungumza katika mkutano na  Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania uliofanyika leo kwenye Chuo cha Taifa cha Utalii Posta jijini Dar es salaam leo. 
Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam
................................................................................................
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangala amezindua kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania.
 Kamati hiyo inahusisha Wakuu wa Mikoa ambao pia ni wajumbe wateule wa Kamati ya kitaifa ya kuratibu shughuli za maandalizi ya Mwezi Maalum wa Maadhimisho ya urithi wa Tanzania.
 Akizungumza Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo, Dk.Kigwangala amesema anawapongeza  wajumbe wote wa Kamati ya Maadhimisho wa Mwezi wa Urithi wa Tanzania kwa kuteuliwa kwao kwa ajili ya shughuli hii muhimu katika kuhimiza urithi wa Tanzania kwa maendeleo ya sekta ya utalii katika Taifa letu.
Amesema sekta ya utalii imekuwa mhimili muhimu katika ukuaji wa uchumi  wa Tanzania ambapo kwa mwaka 2017 sekta ya  utalii imechangia dola za kimarekani Bilioni 2.1 takriban asilimia 25  ya  fedha za kigeni.
Amesema takwimu zinaonesha mwaka 2016 idadi ya watalii waliotembelea nchi yetu walifikia 1,284,279. Katika taarifa yake ya 6 ya maendeleo ya uchumi, inayoitwa “Unlocking the Potential of the Tourism Industry for Tanzanians” Benki ya Dunia inaonesha kuwa mapato ya utalii yatakua kila mwaka na kufikia Dola za Marekani 16 bilioni ifikapo 2025. 
“Hata hivyo, mpaka sasa sekta ya utalii Tanzania imekua ikijikita zaidi katika utalii wa wanyamapori ili kuvutia watalii ambapo takriban asilimia zaidi ya 80 ya watalii wa kimataifa wanaotembelea Tanzania bara huja kuona wanyamapori.
“Nchi yetu imejaliwa kwa kuwa na rasilimali mbalimbali za urithi wa Taifa nje ya zile za wanyamapori. Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizojaliwa kuwa na rasilimali za kipekee duniani zinazobainisha harakati za maendeleo ya binadamu kama vile chimbuko lake, teknolojia alizotumia.
”Na namna ambavyo binadamu amekuwa akitumia mazingira yake ili kumwezesha kuishi kwa zaidi ya miaka milioni tatu iliyopita. Mfano wa rasilimali hizo ni masalia ya Binadamu wa Kale (Zamadamu) walioishi Bonde la Olduvai zaidi ya miaka milioni 1.7 iliyopita na nyayo za Zamadamu aitwaye Australopithecus afarensis aliyeishi Laetol miaka milioni 3.6   iliyopita”amesema.
Pia miji ya kihistoria kama vile Bagamoyo na Kilwa, michoro ya miambani, Kondoa na mapango ya Amboni.Aidha Tanzania ikiwa na zaidi ya makabila 120 imejaliwa kuwa na anuaia za mila, desturi, vyakula, misemo, imani, mavazi, nyimbo, ngoma za aina mbali mbali na matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kuunganisha Watazania. 
Dk.Kigwangala amesema kutokana na kuona hayo yote wizara yake imeamua kuwepo na mwezi maalumu kwa ajili ya kusheherekea Urithi wa Taifa la Tanzania.
 Amesema Urithi huo wa Taifa ni miongoni mwa vivutio vya utalii kwa kuwa ni  vielelezo vya historia,  utamaduni na ustaarabu wa jamii katika hatua mbalimbali za maisha.
Ameongeza urithi huo huonesha na kuikumbusha jamii husika chimbuko la tabia, mila na desturi ambazo inazitumia katika nyanja za uchumi, siasa, teknolojia na elimu.
“Jamii yoyote ile inatambuliwa, kuthaminiwa na kuheshimiwa kutokana na urithi wake. Kwa sababu hiyo, tuna kila sababu ya kuendeleza urithi huu tuliojaliwa na mwenyezi Mungu.
” Kwa kutambua umuhimu huo,kuuenzi, kuutangaza na kuutumia urithi wa Taifa la Tanzania kama kivutio cha utalii na kumbukumbu za Taifa, Wizara yangu imeona ni vema kukwepo na mwezi maalum wa kusherehekea Urithi wa Taifa la Tanzania (Tanzania National Heritage Month).Tumekubaliana mwezi huo utakuwa ukiadhimishwa kila ifikapo Septemba ya kila mwaka,”amesema.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala akizungumza katika mkutano na  Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania uliofanyika leo kwenye Chuo cha Taifa cha Utalii Posta jijini Dar es salaam leo. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki akizungumza katika mkutano huo.
Imani Kajula Mjumbe wa Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania akizungumza kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye chuo cha Utalii cha Taifa Posta jijini Dar es salaam kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo na katikati ni Jokate Mwegelo mjumbe pia.
 Kutoka kulia ni Wajumbe wa kamati hiyo WEma Sepetu, Dkt. Sebastian Ndege, Dk. James Wakibara na Dk. Fredy Manongi na Devotha Mdachi
 Mjumbe wa kamati hiyo Ritha Paulsen akichangia mada katika mkutano huo uliofanyika kwenye chuo cha Utalii cha Taifa jijini Dar es salaam.
 Mjumbe wa Kamati hiyo Jokate Mwegelo akitoa mchango wake wa mawazo katika mkutano huo kulia ni Mjumbe Imani Kajula na kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo. 
 Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati), Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. John Mtaka (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki (kulia)
 Picha ya pamoja
  Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla na wajumbe wa kamati hiyo.
Baada ya kuhitimisha uzinduzi na picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment